Katika mlolongo wa sehemu au vipengele vya
mpango rasmi wa biashara, Muhtasari au unaweza ukauita Muhtasari Tendaji,
unahesabika kama sehemu ya kwanza ya mchanganuo wa biashara yako baada ya Jaladala nje, Jina la mchanganuo na yaliyomo. Hii ndiyo sehemu muhimu kuliko nyingine zote katika mpango wa biashara kwani ndiyo msomaji anapoanza kusoma na atapata hamasa ya kuendelea kusoma sehemu nyingine za mpango wa biashara endapo sehemu hii itamvutia. Ikiwa muhtasari wako hauwezi kumshawishi msomaji basi ujue atautupa kapuni, hivyo ni sehemu inayotakiwa umakini wa hali ya juu.
Sehemu hii hukaa mwanzoni lakini huandikwa
baada ya kukamilisha sehemu nyingine zote. Aya zinazounda Muhtasari ni
ufupisho kutoka katika sehemu/vipengele vingine vyote 7. Kumbuka wakati
unapoanza kuandika vipengele/sehemu nyingine zote unapaswa kila sehemu uanze na
ufupisho mdogo wa sehemu husika, mihutasari hiyo midogomidogo ndiyo hatimaye
huja kuunda muhtasari.
Au unaweza tu ukachagua kutoka katika kila
kipengele zile sentensi muhimu zilizobeba vitu muhimu ukaziunganisha pamoja na
kupata Muhtasari wako ama ufupisho wa andiko lako zima la biashara.
Kama unavyoweza kuona, MUHTASARI unaweza
ukabeba vitu muhimu kwa ufupi kama vile;
· Historia
ya biashara
· Malengo
ya biashara
· Mahitaji
ya wateja unayotaka kuyakidhi
· Upekee
wa biashara yako
· Uchambuzi
wa mazingira ya biashara, nguvu, udhaifi, fursa na hatari(vikwazo).
· Utawala
na wafanyakazi
· Kiasi
cha makadirio ya mtaji unaohitaji
· Chanzo/vyanzo
vya mtaji.
· Mikakati
ya kufanikisha malengo
· Makisio
ya mapato na matumizi
· Jinsi
utakavyolipa deni ikiwa utakopa.
Hata hivyo siyo sheria kwamba katika
muhtasari wako ni lazima pointi zilizotajwa hapo juu ziwe ndizo zitakazounda
Muhtasari wako hapana. Katika Muhtasari unaweka vile vitu ambavyo katika
mchanganuo wako unaona ndivyo vyenye uzito zaidi kwasababu kila mchanganuo au
tuseme kila biashara ina malengo na vipaumbele tofauti na nyingine na hivyo
kusababisha hata vipengele navyo kuweza kuwa tofauti au kuwa na uzito
usiolingana.
Mpenzi
msomaji huu ni utangulizi tu wa somo letu la nne 4 katika semina yetu ya Darasa
la Michanganuo ya biashara. Pata somo zima ndani ya blogu maalumu ya
Michanganuo hapa, pamoja na kutumiwa somo hilo (PDF) katika email yako.
…………………………………………………………………….
Masomo yanawekwa kila siku somo moja, huku washiriki
wakifuatilia na kuuliza maswali. Kila mshiriki anahudumiwa kikamilifu kulingana
na mahitaji na uelewa wake, ni lazima kila anayeshiriki mafunzo haya mwisho wa
semina aweze kuandika mpango wa biashara na ataamua yeye mwenyewe wazo la
biashara atakayoiandikia mchanganuo kisha kupewa usaidizi wowote atakaohitaji
hatua kwa hatua hata ikiwezekana mkufunzi kuja mpaka eneo la biashara na
kufanya naye utafiti wa baadhi ya vipengele mpaka mchanganuo umekamilika.
Ada ya semina ni shilingi elfu 10. Ukishalipa
kupitia namba 0712 202244 au 0765 553030 , unatuma na email yako pia lakini iwe (GMAIL),
utaunganishwa na blogu ya michanganuo ambayo 'link' yake ipo kwenye blogu hii ya
jifunzeujasiriamali pale juu katika MENU, baada ya kuactivate email tutakayokutumia utaweza kusoma masomo kwenye blogu hiyo lakini pia masomo hayohayo utatumiwa kwenye email yako moja kwa moja. Unapatiwa pia na kitabu cha Michanganuo ya Biashara na
Ujasiriamali(softcopy) bure.
Kwa yule atakayehitaji kitabu cha karatasi
hardcopy, basi atalipia semina sh. 10,000/= na kitabu atapewa kwa punguzo la
shilingi 10,000/= badala ya bei yake ya kawaida ya shilingi elfu 20.
Nafasi
zinazotarajiwa zikishatimia darasa litafungwa mpaka waliojiunga wamalize
kwanza kutokana nafasi na rasilimali za
mkufunzi, dhamira yetu kubwa ni kuhakikisha tunaandikisha idadi ya washiriki
tutakaokuwa na uwezo wa kuwafundisha barabara ili na wao wakawatangazie wengine
huduma zetu.
Kwa hiyo ni vizuri kama unahitaji semina hii ukawahi mapema kabla muda haujakwisha. Zoezi la kujiunga litaenda sambamba na semina mpaka pale idadi tarajiwa itakapotimia.
Kwa hiyo ni vizuri kama unahitaji semina hii ukawahi mapema kabla muda haujakwisha. Zoezi la kujiunga litaenda sambamba na semina mpaka pale idadi tarajiwa itakapotimia.
0 Response to "SEHEMU YA 4: DARASA LA SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA(MUHTASARI)"
Post a Comment