Katika sehemu hii kuna vitu muhimu
vinavyohitaji kuelezewa baada ya Dhamira kuu, maono na malengo ambavyo ni;
· Utambulisho
kamili wa biashara(inaitwaje?)
· Umiliki
wa biashara na mfumo wake kisheria
· Historia
ya biashara /kampuni na mahesabu ya nyuma kama biashara ni ya zamani, lakini kama ni mpya basi
utaelezea mahitaji na vyanzo vya mahitaji hayo.
· Eneo
la biashara na vifaa vilivyopo pale kama vile majengo, ardhi, samani nk.
Kabla hujaanza acha nafasi kidogo kwa ajili ya aya moja
ya muhtasari wa sura nzima ambao utatakiwa kuuandika mwishoni. Kuna michanganuo mingine kwa mfano hata ile iliyopo
katika kitabu cha MICHANGANUO, utakuta vitu hivi vinne, Dhamira kuu, Malengo,
Siri za mafanikio na hata wakati mwingine Maono yanafuata baada tu ya
Muhtasari, halafu katika sehemu hii ya Maelezo ya biashara/kampuni, inabakia tu
na maelezo yanayohusu umiliki kisheria, historia ya biashara, mahitaji, vyanzo
vya mahitaji pamoja na eneo biashara ilipo. Kuweka vitu hivyo baada ya dhamira kuu
au katika sehemu hii ya biashara hakuna athari yeyote.
2.1
Dhamira kuu.
Weka dhamira yako kuu hapa, dhamira kuu ni
ile biashara unayoifanya kwa mfano biashara ya mgahawa unaweza ukasema hivi, “dhamira
yangu kuu ni kutoa huduma bora ya chakula na vinywaji baridi kwa wakazi wa mji
au eneo fulani”
2.2 Maono
Hapa weka kauli inayoelezea biashara yako
itakuwaje baada ya kipindi tuseme labda ni miaka mitatu, mitano au kipindi kingine
chochote kile ulichopanga. Kwa mfano unaweza ukasema maono ya biashara yako ya
mgahawa ni, “kuwa na mgahawa mkubwa zaidi jijini Dar es salaam”
2.3
Malengo.
Taja vitu unavyokusudia kuvipata kutokana na biashara
baada ya kutekeleza mpango wako. Vitu hivyo vinaweza vikawa, mauzo, faida,
idadi fulani ya wateja, idadi ya wafanyakazi, au kitu kingine chochote. Kwa
mfano unaweza ukasema moja kati ya malengo yako ni “kuwa na wafanyakazi watano baada
ya mwaka mmoja”, au “kufikisha mauzo ya shilingi milioni hamsini mwishoni
mwa mwaka wa tatu” nk.
2.4 Siri za mafanikio
Taja vitu vya pekee vinavyoifanya biashara
yako ifanikiwe. Kila biashara ina vitu vinavyoifanya ifanikie kwa mfano utakuta
biashara ya maduka mengi ya rejareja hufanikiwa zaidi yanapowekwa eneo zuri
lililokuwa na watu wa kutosha, hivyo utasikia watu wakisema siri ya mafanikio
ya duka ni eneo. Siri za mafanikio zaweza kuwa pia ni ubora, huduma nzuri kwa
wateja, mtaji wa kutosha au kitu kingine chochote kinachoifanya biashara yako
ishamiri zaidi ya vingine na unaweza ukataja zaidi ya kimoja.
2.5
Umiliki wa biashara
Katika kipengele hiki kidogo, taja jina la
biashara na mmiliki wake au wamiliki kama ni zaidi ya mmoja ukielezea na aina
ya usajili kisheria wa biashara hiyo kama ni ya mtu binafsi, ubia au kampuni.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Soma somo zima, kwa njia 3, PDF, Sauti MP3 na
kupitia njia ya e-mail. Unachotakiwa kufanya ili kupata masomo haya yote ni
kulipia Semina shilingi 10,000/= tu, tuma na email yako au kama umejiunga
kupitia blogu ya jifunzeujasiriamali kupata vitabu bila malipo basi huna haja
ya kutuma tena anuani yako ya email. Kwa maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba
0712 202244 au 0765 553030
0 Response to "SOMO LA 5: MAELEZO YA BIASHARA AU KAMPUNI"
Post a Comment