Hivi ni vitabu vya pesa na mafanikio vya wakati wote(SELF
DEVELOPMENT BOOKS OF ALL TIMES), Hii ni safu mpya ambayo inaanza hapa katika
blogu yako ya jifunzeujasiriamali, na safu hii itakuwa kila siku tukiangazia
kwa ufupi vitabu mashuhuri zaidi duniani vinavyohusiana na maendeleo binafsi ya
mtu, vitabu ambavyo vilitamba, bado vinatamba na vitaendelea kutamba kwa miaka
mingi ijayo. Tutazungumzia pia waandishi wake, wasifu wao na nakala walizowahi kuuza
mpaka sasa.
Kumbuka ndugu msomaji, duniani kumejaa vitabu mamilioni
kwa mamilioni lakini vile vinavyofanikiwa kuwa maarufu au kuuza nakala nyingi
ni vichache, hata hivyo uchache wake hatuwezi tukasema labda ni vitabu mia au
elfu kadhaa tu hapana, navyo ni maelfu kwa maelfu.
Hata useme leo unaamua kila kitabu utakisoma basi itabidi
labda uishi miaka elfu moja. Lakini kama kitabu cha KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMUYA PESA NA MAFANIKIO kinavyopendekeza, unaweza ukachagua baadhi ya vitabu
utakavyovisoma na ukapata maarifa makubwa kwa kile unachokihitaji katika muda fulani
tu huku masuala mengine ya kimaisha nayo yakipata muda wa kuyafanya.
“Countdown” hii nitakayokwenda kukuletea hapa, siyo kama
ni sheria kwamba mtu ni lazima avisome hapana, ni pendekezo linalotokana na
utafiti uliofanyika juu ya umashuhuri wa vitabu hivyo
Bila ya kupoteza muda mwingi leo hii tutaanza moja kwa
moja na kitabu namba moja cha elimu ya pesa na mafanikio kutoka katika listi
yangu ambacho siyo kingine bali ni kitabu cha Mwandishi Napoleon Hill, Think
and Grow Rich(Fikiri Utajirike) au kwa jina jingine MSAHAFU WA MAFANIKIO kama
kilivyopewa jina hilo kwa mara ya kwanza kabisa na Blogu hii.
Napoleon Hill anajulikana kuwa ndiye mwandishi rasmi wa
kwanza kabisa kuandika vitabu vya maendeleo binafsi ya watu. Vitabu vyake kama
vilivyopata kuwa muhimu miaka takribani 80 iliyopita, ndivyo hivyohivyo na leo
vilivyokuwa muhimu. Kamwe havijapitwa na wakati.
Fikiri utajirike |
Kitabu chake, THINK AND GROW RICH ni mkusanyiko au
ufupisho wa kitabu kingine kiitwacho, Sheria za Mafanikio(Laws of Success) Mkusanyiko
huo ukazaa kanuni 13 za mafanikio binafsi ya mtu na maudhui yake makubwa ni
kwamba, mtu yeyote mwenye Shauku ya jambo/kitu, akiwa na Imani na Uvumilivu
vikiambatana na kuondoa aina zote za mawazo hasi akilini, huku akiwa na Malengo
makubwa, mtu huyo hakuna kitu chochote kile kitakachoweza kumzuia kufikia
MAFANIKIO MAKUBWA KABISA MAISHANI MWAKE.
Kitabu hiki kwakweli nasema katika Blogu hii ndipo mahali
pake kwani tangu imeanza, tumekuwa tukikitafsiri kitabu hicho katika lugha ya
kiswahili, kitabu kizima kama kilivyo pamoja na Ufupisho wake au uchambuzi kwa kifupi. Kusoma tafsiri hiyo na ufupisho
wake fungua maandishi yafuatayo, FIKIRI UTAJIRIKE(Think & Grow Rich)
Usikose mfululizo wa orodha ya vitabu hivi 300
nilivyokuandalia kila siku. Asante.
..............................................................................................
Ile SEMINA ya Michanganuo ya Biashara bado inaendelea, soma Masomo yatakayofundishwa hapa, RATIBA YA MASOMO YA SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA
Kwa vitabu vyako bora kabisa vya biashara na ujasiriamali katika lugha ya kiswahili, ingia kwenye ukurasa wa SMARTBOOKSTZ
Nice
ReplyDelete