Kitu kikubwa kabisa unapotaka kuandika mpango wa biashara
ni kujua kwanza ni mahitaji gani au matatizo gani wateja wanayotaka bidhaa au
huduma zao ziyatatue; “Business plan, It’s all about finding what
is the problem a customer needs to be solved by your service or product” Ulisha lifahamu hilo pamoja na kujua
namna utakavyowatatulia wateja shida hiyo kwa ufanisi zaidi kuwashinda watu
wengine wanaotatua shida za wateja kama wewe, basi biashara hiyo utakuwa
umeibuka kidedea.
Kwa hiyo mchanganuo wa biashara kama maelezo mengi
kuhusiana na biashara wakati mwingine yanaweza yasiwe na umuhimu mkubwa sana
kama mtu utakuwa na haraka au kutojua namna ya kuandika mchanganuo wenyewe.
Kama nilivyoandika jana juu ya njia 3 mtu anazoweza akazitumia kuifanya kazi ya
kuandika mpango wa biashara kuwa nyepesi, leo hii nimeamua kuendelezea
nilipoacha jana kwani njia moja niliyoahidi sikuwa bado nimeiweka rasmi katika ile Blogu
yetu ya SEMINA kwa ajili ya washiriki kuipakua.
SOMA: Kuku ni utajiri. soma mchanganuo wa kuku 1000 wa mayai
SOMA: Kuku ni utajiri. soma mchanganuo wa kuku 1000 wa mayai
Hata washiriki wengi wakaanza kunitania, “Vipi mkufunzi mbona unaaza kuleta usanii?” lakini
sasa nawajibu semina hii nimeamua kujitolea na nipo ‘serious’ kwelikweli siwezi
kuwaangusha hata kidogo. Kwanza niseme tu kwamba washiriki ambao bado
hawajaanza kuweka msingi wa mipango ya biashara zao za mazoezi nawaomba
watafute daftari zuri au kama ni kompyuta basi wafungue ‘document’ watakayoanza
kujaza vitu ndani kusudi baada ya muda waje waunganishe mipango yao kuwa
mchanganuo kamili.
Unaanza kuifikiria biashara unayoiandikia mpango, kila hatua ni vitu gani utavifanya na kisha unaandika kwenye hilo daftari au kompyuta. Mambo yako hayo utakayokuwa ukiyaandika ni lazima yatokane na utafiti kusudi yaweze kuwa na ukweli na siyo vitu vya kutunga au hadithi. Kama ni bei za bidhaa basi zioane kweli na bei za bidhaa hiyo au huduma iliyopo sokoni.
Unaanza kuifikiria biashara unayoiandikia mpango, kila hatua ni vitu gani utavifanya na kisha unaandika kwenye hilo daftari au kompyuta. Mambo yako hayo utakayokuwa ukiyaandika ni lazima yatokane na utafiti kusudi yaweze kuwa na ukweli na siyo vitu vya kutunga au hadithi. Kama ni bei za bidhaa basi zioane kweli na bei za bidhaa hiyo au huduma iliyopo sokoni.
Nirudie tena kwani kauli hii nimeisema mahali pengi hasa
kwenye masomo yetu yaliyopo kwenye blogu ya MICHANGANUO, “Unaposikia aina mbali
mbali za michanganuo ya biashara,sijui mpango mkakati, sijui mpango wa masoko,
upembuzi yakinifu, andiko la biashara, mpango wa utekelezaji na hata “UKURASA
MMOJA WA MCHANGANUO” kama huu nitakaouzungumzia leo hii na ambao nimeweka
mfano(sample) wake mzima kwenye blogu ya MICHANGANUO, aina zote hizo wala
zisikuchanganye akili ukadhani labda kila moja ni aina ya kipekee sana ya
mchanganuo. Zote ni mchanganuo wa biashara uleule ila katika sura na maumbile
tofautitofauti
Utakuta kila aina ina vipengele vilevile lakini
hutofautiana katika wingi wa vipengele au wingi au uchache wa maelezo tu, kwa
mfano unaposema Ukurasa mmoja wa mchanganuo ni mchanganuo lakini ulioshindiliwa
ili uweze kuenea katika ukursa mmoja, ni jinsi gani unavyoshindiliwa sasa
inabidi uutazame ukurasa huo mmoja ukiwa kamili ndani ya blogu yako ya
michanganuo.
Hapa chini nitaenda kuweka kwa kuorodhesha baadhi tu ya
vipengele vichache vinavyopatikana ndani ya ukurasa mmoja wa mchanganuo, kwa
kweli ni kitu kinachovutia kwani hata unaposoma ukurasa huo wote unapata picha
vizuri sana ya biashara nzima itakavyokuwa au ilivyo.
SOMA: Utambulisho rasmi wa semina hii.
SOMA: Utambulisho rasmi wa semina hii.
Kuna vile vitu vya msingi sana katika biashara kama
ulivyoona kwenye kichwa cha makala hii nilivyoandika, JIBU HITAJI AU TATIZO LA MSINGI WATEJA WAKO
WATARAJIWA LINALOWASUMBUA. Vitu vya msingi kama hivyo huwezi ukavikosa katika
kila aina ya michanganuo tofauti niliyoitaja nau aina zingine zozote zile hata
ikiwa vitaandikwa kwa namna tofauti, Soko halikadhalika, washindani na
rasilimali au nguvukazi. Nataka uanze kufahamu kwamba mpango wa biashara siyo
kitu cha ajabu bali ni yaleyale mambo unayoyafanya kila siku katika mchakato
mzima wa biashara yako.
UKURASA MMOJA WA MCHANGANUO
UTAMBULISHO
Ielezee
biashara yako katika sentensi moja ni kitu gani unachokifanya. Kwa mfano
utambulisho wa duka la nguo za wanawake unaweza kuwa hivi; “Tunauza nguo zinazomfanya mwanamke kujiamini muda wote na siyo
ilimradi nguo tu”. Utambulisho wako ni kile kitu kinachokutofautisha na
washindani wako.
TATIZO UNALOTATUA
Eleza
hitaji au tatizo lile ambalo wateja wako watarajiwa linawasumbua. Ni kwanini wanahitaji
bidhaa ama huduma zako?
SULUHISHO LAKO
Bidhaa
au huduma yako ni nini? Ielezee hapa na jinsi itakavyotatua shida ya mteja.
USHINDANI
Ni bidhaa
au huduma utakavyowahudumia kwa ufanisi zaidi kuwashinda washindani wako.gani
wateja wako watarajiwa wanaitumia kwa sasa kukidhi mahitaji yao? Eleza……………
Nakuomba ukadownload template ya UKURASA HUO MMOJA WA
MCHANGANUO uone jinsi unavyotakiwa kuwa, ni kitu gani hasa huwa ndani yake na
kisha wewe mwenyewe kwa dakika 15 uandike wa kwako mwenyewe kwa ajili ya
uendeshaji kwa ufanisi wa biashara yako. Lakini mpango kamili wa biashara usiache
kujifunza kwani kwa kujifunza michanganuo unapanua zaidi uwezo wako wa kufikiri
kibiashara na hatimaye uwezo mkubwa zaidi wa kufanya biashara yeyote ile kwa
weledi kama walivyo kina Bill Gates, Warren Buffet, Donald Trump, kina Rostam
Aziz, MO, Mzee Mengi na Bakhresa.
...........................................................................
TEMBELEA UKURASA WA VITABU VYAKO VYA UJASIRIAMALI NA MAENDELEO BINAFSI HAPA
...........................................................................
TEMBELEA UKURASA WA VITABU VYAKO VYA UJASIRIAMALI NA MAENDELEO BINAFSI HAPA
0 Response to "JIBU HITAJI AU TATIZO LA MSINGI WATEJA WAKO WATARAJIWA LINALOWASUMBUA"
Post a Comment