Lakini hii imetokana na kazi kubwa ya kuhakikisha ile
semina yetu ya Michanganuo ya biashara tuliyotangaza wiki chache zilizopita
inakamilika katika ubora wake na kwa kiwango cha hali ya juu kabisa kusudi
kutimiza dhamira yetu ya kuwafanya washiriki waliojiunga na wanaoendelea
kujiunga na semina hii kuhitimu semina wakiwa na cheti chao mkononi ambacho ni “document”
ya mchanganuo wa biashara watakayoandika wenyewe kwa usaidizi wa karibu wa
wakufunzi wa semina.
Sasa hivi tulichogundua ni kwamba Watu hususani
Watanzania hawako tayari tena kulipia bidhaa ama huduma zisizoshikika au
kuonekana dhahiri kwa macho kutokana na gharama za maisha kuwa juu na fedha kupatikana
kwa jasho jingi.Hivyo watu wanapenda thamani ya kutosha kwa kila senti yao
wanayoitoa. Kwa maana nyingine watu hawapendi longolongo linapokuja suala la
kutoa fedha yao mifukoni, wanahitaji vitu vya ukweli
Sababu hii ndiyo iliyotufanya Self Help tuhakikishe semina hii kwanza inakuwa ya hali ya juu sana
na washiriki mbali ya kushiriki semina lakini mwishoni watoke na kitu wanachoweza
kukiona ambacho ni ujuzi wa kuandaa mpango wa biashara.
Tumefanya hivyo kwa karibu kila bidhaa ama huduma
tunazozitooa, kwa mfano sasa hivi pale juu ya blogu ya jifunzeujasiriamali
utaona page ya, HUDUMA ZETU, ambayo
tumeorodhesha huduma mbalimbali tunazozitoa. Huduma kama ya ushauri, mtu akishalipia shilingi elfu
5 atapata huduma nyingi ndani ya miezi 6 kulingana na yeye atakavyohitaji, kuna
usaidizi katika kuanzisha na kuendeleza blogu, zawadi ya kitabu kipya kinachokaribia
kutoka hivi karibuni, ushauri mbalimbali wa biashara ndogo atakaohitaji nk.
vyote kwa sh. elfu 5 tu. Hapo utaona kwamba tunatoa thamani kubwa kwa fedha
mteja anayoitoa.
Kingine ni vitabu vyetu ambavyo tumekuwa tukiviuza kila
siku, gharama ya kitabu kwa mfano MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI,
unapolinganisha wingi na umuhimu wa masomo yaliyopo ndani yake na bei ya kitabu
kwa kweli utasema, “mbona wanapata
hasara?” Na sasa hivi tena unaweza kukipata kitabu hicho mpaka bure kikiwa
softcopy baada ya kulipia semina ambapo hii ni ofa ya muda mfupi tu.
Ndugu msomaji wangu, ninaamini sana katika kushughulika
kwa kina na jambo moja kwanza(concentration/focus) kabla ya kwenda kwenye jambo
jingine kwa ajili ya matokeo mazuri zaidi, hivyo nitawaombeni radhi sana
wasomaji ikiwa ratiba zetu za kawaida zitakiukwa kwa muda. Kwa kipindi kama cha
wiki 2 hivi mpapa 6 kwa kweli nitakuwa nikishughulika zaidi na semina hii ya
michanganuo, hata makala nyingi zitakazoandikwa zitahusiana na semina hiyo
kusudi kutimiza ahadi niliyoitoa kwa washiriki.
Washiriki ambao bado hawajajiunga nafasi bado ipo, mfumo
wa semina hii haubagui mtu kwa muda anaoingia ingawa ukichelewa sana utakuja
kukuta kile kipindi ambacho wakufunzi tulichojitolea kwa hali na mali huku hata
tukiacha majukumu mengine muhimu kimemalizika, ni sawa na mtu kuingia ukumbi wa
harusi muda wa saa 6 za usiku. Unakuta mambo mazuri yanakaribiaa kuisha na DJ
keshaanza kuchoka. Hivyo nakusihi kama Semina hii unaona kuna kitu cha manufaa
kwako usisite tuma ada yalo shilingi elfu 10 kwenye namba 0712 202244 au 0765 553030 jina Peter Augustino Tarimo
pamoja na anuani yako ya Gmail. Nitakupa link haraka uanze kusoma masomo yako.
………………………………………………………………..................
0 Response to "MASOMO YOTE 11 YA SEMINA YAMEKAMILIKA, LINGANISHA THAMANI, UBORA NA BEI"
Post a Comment