Leo hii kwenye kipengele cha ongea na mshauri
wako kuna msomaji wetu mmoja kutoka Dar es salaam, yeye anataka kujua ikiwa
kama anaweza akaanzisha biashara ya kuuza vocha za simu za jumla kwa mtaji wa
shilingi million mbili. Swali lake alilotuma
ni hili hapa chini’
Ndugu
mshauri naomba ushauri wako, mimi naishi maeneo ya uwanja wa ndege jijini Dar
es salaam nimepata sehemu(fremu ya duka) maeneo ya stendi ya njia panda ya
kuelekea segerea na ninao mtaji wa shilingi milioni mbili, kwa mtaji huo je,
naweza nikafungua biashara ya kuuza vocha za simu za mkononi? Au mshauri
ningeomba kama haiwezekani basi unishauri biashara za kufanya nyingine
ninazoweza kuanza kwa mtaji huo,
Natanguliza
shukrani zangu za dhati kwako.
Majibu ya swali hilo ni haya yafuatayo.
Kulingana na swali uliloniuliza, kwanza mimi
nitalijibu kwa mtazamo wa namna ya kuanzisha biashara kwa ujumla pasipo kujali
kama ni biashara ya kuuza vocha za simu jumla au ni biashara nyingine yeyote
ile na kisha ndipo tutakapokuja kwenye biashara yenyewe ya vocha za simu.
SOMA: Natengeneza sabuni, shampoo, batiki na unga wa lishe lakini sioni unafuu wowote kimaisha, naomba ushauri.
SOMA: Natengeneza sabuni, shampoo, batiki na unga wa lishe lakini sioni unafuu wowote kimaisha, naomba ushauri.
Unapotaka kuanzisha biashara yeyote ile kuna
hatua mtu unazotakiwa uzipitie na wakati mwingine hatua hizo wala siyo lazima
uwe umezisomea ila unajikuta tu wewe mwenyewe umezifanya kama ni mdadisi. Moja
ya hatua hizo ni kufanya utafiti wa biashara ile unayokusudia kuianzisha.
Utafiti wa biashara au utafiti wa masoko unakuwezesha kufahamu kwa kina mambo
mbalimbali yanayohusiana na biashara husika ambayo ndiyo yanayohitajika kuja
kutekelezwa ndipo biashara yenyewe iweze kupata mafanikio.
Utafiti au upembuzi wa biashara unakuwezesha
kutambua vikwazo au matatizo kama vile ya mtaji yanayoweza kuja kujitokeza
baadae hivyo kuchukua tahadhari ya kuyapunguza mapema kuliko kuja kuyashitukiza
ghafla na kuanza kuhangaika huku na kule pasipokujua ufanye nini.
Moja ya majukumu hayo kwenye utafiti ni kujua
ikiwa biashara tarajiwa itahitaji mtaji kiasi gani ili kuweza kuanza. Mahitaji
ya kuanzisha biashara ni rahisi kujua kwani baada ya kupita katika maduka
kadhaa yanayosambaza bidhaa au kile wewe utakachouza na kuuliza bei zao, bila
shaka kwa haraka haraka utafahamu bei ya malighafi au bidhaa utakazouza utaweza
kuzipata kwa gharama kiasi gani na utakapokwenda kuuza utapata faida ghafi
kiasi gani.
SOMA: Biashara ya vocha za simu, je ulikuwa unalijua hili?
SOMA: Biashara ya vocha za simu, je ulikuwa unalijua hili?
Huishii hapo tu, bali utauliza kila kitu
kingingine kinachohusiana na biashara hiyo ikiwa utakipata kwa gharama kiasi
gani, vitu kwa mfano eneo la kufanyia biashara husika, vifaa na vyombo
utakavyotumia wakati ukifanya biashara, Gharama mbalimbali wakati wa kusajili
biashara, vitu kama umeme, maji, simu nk. kama biashara yenyewe itavihitaji,
pamoja hata na gharama za kumuajiri mtu kwenye hiyo biashara ikiwa labda
utalazimika kwenda kumtafuta kutoka vituo vya ajira.
Baada ya kumaliza kazi hiyo ya utafiti sasa
chukua kalamu yako na karatasi na kisha uchore jedwali kama hili lifuatala
JEDWALI LA MAHITAJI YA KUANZISHA BIASHARA.
Kisha utajaza kila hitaji kiasi cha fedha unazokadiria kutegemeana na mtaji wako uliokuwa nao. Utakuwa umeshafahamu kwani katika utafiti wako ni lazima uulize watu mbalimbali wanaouza bidhaa au huduma kama za kwako kwamba unaweza ukaanza na bidhaa kiasi gani halafu bidhaa hizo utazidisha mara bei ya kununulia uliyokwisha ifahamu pia baada ya kutafiti kwa wauzaji au wasambazaji wakubwa wa bidhaa hiyo kwa jumla.
MAHITAJI MBALIMBALI YA KUANZA BIASHARA
|
Tsh.
|
1. Kusajili biashara
|
|
2. Leseni
|
|
3. Kodi ya chumba/eneo la biashara
|
|
4. Maboresho ya eneo/chumba
|
|
5. Mtaji wa kununulia bidhaa/malighafi
|
|
Jumla ya mahitaji yote ya kuanzia
|
Y
|
Kisha utajaza kila hitaji kiasi cha fedha unazokadiria kutegemeana na mtaji wako uliokuwa nao. Utakuwa umeshafahamu kwani katika utafiti wako ni lazima uulize watu mbalimbali wanaouza bidhaa au huduma kama za kwako kwamba unaweza ukaanza na bidhaa kiasi gani halafu bidhaa hizo utazidisha mara bei ya kununulia uliyokwisha ifahamu pia baada ya kutafiti kwa wauzaji au wasambazaji wakubwa wa bidhaa hiyo kwa jumla.
Kwa suala lako itakubidi hata uende mpaka kwa
watoa huduma wa makampuni ya simu za mkononi kama vile Vodacom, Tigo, Airtel,
Zantel, Smart, Halotel, TTCL NK. kwenye vituo vyao kama vile kule mlimani city
na kuwauliza wale maafisa masoko namna unavyoweza kupata vocha kwa ajili ya
kwenda kuuza jumla na bei ya kuuziwa kwa wewe mtu unayekwenda kuuza jumla.
Ukisha maliza zoezi hilo hapo kwenye hilo
jedwali la mahitaji ya fedha za kuanzishia biashara sasa jumla ya kiasi hicho
cha fedha “Y” ndiyo mtaji utakaotosha kuanzisha mradi au kampuni yako
ndogo.
Kumbuka kwamba idadi ya mahitaji hayo
itategemea ukubwa wa biashara au kampuni unayotaka kuianzisha yakwangu hapo ni
mfano tu, wewe kama mjasiriamali ni lazima ujiongeze kujua jinsi ya kufanya
biashara uliyochagua kuifanya, kuwa mbunifu, siyo lazima biashara yako ihusishe
ununuzi wa bidhaa au malighafi, pengine wewe utaanzisha biashara ya kutoa
huduma, itakubidi pale badala ya kuorodhesha bidhaa au malighafi basi
utaorodhesha posho za siku za wafanyakazi watakaotoa huduma ukiwemo wewe
mwenyewe kama utahusika pamoja na gharama labda za steshenari nk.
Inawezekana pia labda wewe biashara yako ni
ya kuanzisha kiwanda cha kuzalisha bidhaa, kwenye mahitaji yako ni lazima
uhakikishe vitu muhimu vya kuanzisha kiwanda kama mashine, ujuzi na malighafi
unavitaja na gharama zake zote.
Baada ya majibu hayo ya jumla hebu sasa tuje
kwenye swali lako la msingi,
NATAKA KUFUNGUA DUKA LA KUUZA KADI ZA SIMU ZA
KIGANJANI KWA BEI YA JUMLA KWA MTAJI WA SHILINGI 2,000,000/= (MILIONI 2), JE
MTAJI HUO UTATOSHA?
Ndugu msomaji wangu kulingana na majibu ya
jumla niliyokupa hapo juu, nadhani utakuwa umekwisha pata mwangaza kuhusiana na
swali lako hili. Lakini pia sijafahamu ikiwa hiyo fremu ya duka au eneo unalosema
umepata njia panda ya Segerea kama umeshalilipia kodi ya pango au umepewa na
mhisani au ndiyo unategemea mtaji huo huo uliokuwa nao wa shilingi milioni
mbili ndio utakaotumia hapo kiasi kulipia pango.
SOMA: Kuanzisha biashara ningali bado chuoni nasoma je, inawezekana?
SOMA: Kuanzisha biashara ningali bado chuoni nasoma je, inawezekana?
Hata hivyo, vyovyote vile iwavyo, ni lazima
ufanye zoezi kama nililoonyesha hapo juu na kama ukigundua kiasi cha fedha
ulichokuwa nacho kitabakia kidogo sana kiasi cha kushindwa kununua mzigo au
vocha idadi watu waliokushauri kuanza nazo, basi nakushauri biashara hiyo hebu
iache kwanza na utafute biashara nyingine itakayoendana na mtaji uliokuwa nao.
Ikiwa inatosha basi ruksa endelea.
Ikiwa itatosha na una moyo wa kutosha wa
kuifanya biashara ya kuuza vocha za jumla basi ni vizuri hapo hakuna kitu
kingine tena kitakachoweza kukuzuiak kuanzisha biashara uliyoichagua . Mtaji wa
kutosha ni kigezo nyeti sana kwenye kufanikiwa au kufeli kwa biashara mpya
inayoanza.
………………………………………………………………..
Mpenzi msomaji wa Jifunzeujasiriamali, kama
unapenda kelewa maswala mbalimbali yahusuyo ujasiriamali na biashara kwa kina
kabisa kama vile,
· Namna ya kuanzisha biashara au kampuni
· Kufanya utafiti wa biashara yeyote ile
· Kuandika au kuandaa kichwani mpango wa
biashara
· Kusoma michanganuo halisi na
iliyokamilika ya biashara mbalimbali zinazolipa hapa Tanzania
· Kujua ikiwa biashara unayotaka kuanzisha
italipa au kutengeneza hasara badala ya faida
· Kutafuta soko la bidhaa/huduma zako
· Utunzaji wa mahesabu na kumbukumbu za
biashara yako
· Namna ya kufanya mauzo kitaalamu
· Jinsi ya kumhudumia mteja arudi tena na
tena kwenye biashara yako.
· Mbinu za kusimamia biashara kitaalamu
· Matumizi ya teknolojia na mawasiliano
katika kuboresha biashara.
· Mbinu zinazotumiwa na matajiri wkubwa
kutajirika na kuendelea kubakia kileleni muda wote.nk.
Yajue mambo hayo yote ndani ya KITABU CHA MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALIkwa bei ya shilingi elfu 10 tu kama ni softcopy na shilingi elfu 20 tu ikiwa
utahitaji hardcopy. Kwa mawasiliano piga simu, 0712 202244 au 0765 553030
Ukinunua kitabu hiki unapata ofa ya kujiunga
bure na blogu hii hapa ya SEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA
Picha ni kwa hisani ya Swahiba Media.
0 Response to "MTAJI WA KUANZISHA BIASHARA YA VOCHA ZA SIMU JUMLA, MILIONI MBILI 2 INATOSHA?"
Post a Comment