Kwenye mpango wa biashara kuna tathmini
inayofanywa wakati unapoanza kuandaa mchanganuo wako ambapo unaangalia kwa
haraka haraka hesabu na namba zako, ikiwa biashara yako kwa kipindi fulani
labda tuseme wiki, mwezi au mwaka inatakiwa iuze mauzo kiasi gani kusudi iweze kurudisha
ghara zote ulizotumia. Ukweli ni vigumu kutambua ikiwa biashara italeta faida
au haitaleta lakini tathmini hii inasaidia kwa asilimia kubwa kutabiri
uwezekano wa biashara kufanikiwa.
Ijapokuwa hiki ni kipengele kidogo kwenye
sehemu ya makisio ya pesa, lakini hufanyika mwanzoni kabla ya kuandika sehemu
yenyewe ya fedha ili kujiridhisha ikiwa biashara italipa au haitalipa. Hata
hivyo katika michanganuo mingine watu wengine huweka tathmini hii kwenye sehemu
ya fedha.
Katika ‘Break even’ unaweza kutathmini mauzo yatakayorudisha gharama
au muda biashara itakaporudisha gharama zote zilizotumika. Kwa mfano tuseme
umetumia jumla ya shilingi milioni moja kuanzisha biashara ya kuuza nguo, mauzo
yako yatakapofika shilingi milioni moja hapo unakuwa umerejesha gharama zako
zote. Ni tathmini inayotumia kanuni rahisi inayohusisha vitu vikuu vinne ambavyo
ni hivi vifuatavyo;
1. Mauzo - A
2. Gharama
za mauzo zinazobadilika - B
3. Gharama
za kudumu za uendeshaji - C
4. Kiasi
cha mauzo yatakayorudisha gharama - D
Kanuni inayotumika kukokotoa Mauzo yatakayorudisha
gharama ni hii hapa chini;
Ni sawa na kuchukua ;
Gharama za kudumu gawanya kwa (1- sehemu ya gharama
zinazobadilika kwenye mauzo
Sehemu ya gharama zinazobadilika kwenye mauzo inakuwa katika
mtindo wa sehemu au desimali, ni mauzo gawanya kwa gharama za mauzo.
Kujua
muda biashara itakaporudisha gharama zote break even time kanuni yake
unachukua
Jumla ya gharama zote ulizotumia (B + C) kisha unagawanya kwa kiasi cha faida kwa mwaka, siku au mwezi kulingana na muda wako unaotafuta. Kama unataka kujua ni miaka mingapi utatumia faida ya mwaka 1, halikadhalika na ikiwa ni siku au mwezi.
Kwa
mfano ikiwa mradi wa mandazi unagharimu shilingi 5,000/= kuanzisha, na kisha
kwa siku unapata faida ya shilingi 1,000/= ina maana kwamba mradi huo
utakuchukua siku 5 kurejesha gharama zako zote ulizotumia kuanzisha mradi wako
wa mandazi; Inamaana kuwa unachukua, 5,000/1000.
Kanuni
hizi hapa zimeonyeshwa kwa ufupi sana, ufafanuzi wake kwa kia unaweza kuuona
katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pamoja na masomo ya
SEMINA YA MICHANGANUO yaliyo kwenye BLOGU YA MICHANGANUO
Baada
ya kupata Kiasi cha mauzo yatakayorudisha gharama zote katika kipindi fulani,
sasa hapo ndipo utakapojua ikiwa utaongeza mauzo yako kwa kiasi gani ndipo uweze
kutengeneza faida nyingi zaidi.
Ikiwa
utagundua kwamba mauzo yako unayokadiria yatakuwa chini ya kiasi cha mauzo ya
kurudisha gharama, unaweza kuangalia uwezekano wa kuja kupunguza aidha gharama
za kudumu, gharama zinazobadilika au kuangalia uwezekano wa kuongeza mauzo
kusudi uweze kupita kiasi hicho na hatimaye uje upate faida.
Ila
chukua tahadhari usije ukarekebisha namba tu kusudi zikupe majibu ya
kukuridhisha binafsi, hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe, hesabu zako
zinatakiwa zioane na utafiti uliofanya, uhakikishe kweli zina uhalisia
usikadire mauzo yasiyotekelezeka.
…………………………………………………………………….
Ndugu msomaji, Semina bado inaendelea
hujachelewa kwani jinsi inavyoendeshwa siyo kama semina za kawaida, masomo
yanahifadhiwa kwenye blogu maalumu ambapo mshiriki yeyote anapojiunga huyakuta
masomo hayo yote na kila kitu walichojifunza washiriki wengine.
Ikiwa umeshalipia ada yako sh. 10,000/=
bonyeza maneno yafuatayo ukiwa umesign in kwa email yako.BLOGU YA MASOMO YA SEMINA ITAFUNGUKA.
Soma hapa utannngulizi wa masomo 11 ya msingi ya semina.
Soma hapa utannngulizi wa masomo 11 ya msingi ya semina.
0 Response to "NI LINI BIASHARA YAKO ITARUDISHA GHARAMA ZOTE ULIZOTUMIA?(BREAK EVEN POINT)"
Post a Comment