PATA 90,000: FURAHIA OFA KUBWA BEI YA VITABU NA SEMINA ZA ELIMU YA MAFANIKIO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PATA 90,000: FURAHIA OFA KUBWA BEI YA VITABU NA SEMINA ZA ELIMU YA MAFANIKIO


Ni wiki moja sasa imepita tangu makala ya mwisho kuhusiana na semina ya michanganuo ya biashara hapa katika blogu ya jifunzeujasiriamali. Si kwamba semina ilisimama, hapana ila tulitoa fursa kwa washiriki ambao tayari walikuwa wameshajiunga na semina kupata muda wa kutosha kuweza kumengenya au kutafakari kwa kina masomo ambayo yalikuwa yamewekwa mengi mfululizo katika kipindi kifupi. Kumbuka ndani ya siku mbili tu ama tatu tulikuwa tumeweka zaidi ya masomo matano.

SOMA: Sikiliza ni kwanini semina hii ni ya kipekee?

Sasa baada ya washiriki kuyapitia masomo hayo 11 ya msingi, kudownload vielezo(templates) mbalimbali, michanganuo kamili isiyokuwa ndani ya kitabu, pamoja na masomo ya sauti sasa tutaanza tena kuweka masomo mengine, hayatoki nje ya hayo 11 lakini pia hayafanani moja kwa moja na hayo 11, ni masomo yanayosaidia kuboresha uelewa wa hayo masomo ya msingi au kuweka msisitizo pale ambapo panaonekana kuwa na ugumu mtu kuelewa. Masomo mengine yatakuwa yanatokana na maswali ya washiriki watakayokuwa wakiuliza au ambayo tayari wamekwisha uliza.

Vile vile tutaendelea kuweka vitu(resources) mbalimbali ambavyo humsaidia mtu kuelewa au kujifunza michanganuo ya biashara kwa kina zaidi. Kwa mfano leo tumeweka Kitabu maarufu sana cha jinsi ya kujifunza kuandika michanganuo ya biashara kilichoandikwa kwa lugha ya kiingereza(HOW TO WRITTE BUSINESS PLAN), ni kitabu kinachosadikiwa kuwa namba moja duniani kwa Mipango ya biashara. Kipo pale bure kabisa huchajiwi hata senti tano zaidi ya kujiunga na darasa hili. Pia tumeongeza vielezo(template) za kiingereza mbili pamoja na mchanganuo kamili kwa kiingereza, lengo kubwa likiwa ni kuzidi kupanua uelewa kwa washiriki wa jinsi ya kuandika mpango wa biashara katika lugha zote yaani kiswahili na kiingereza.


Ndiyo maana nilitangulia kusema kwamba masomo mapya na hata mawazo mbalimbali nitakayoyaweka kwenye semina mengine yatatokana na washiriki wenyewe kwani hata hili la kuweka vitabu, vielezo na baadhi ya masomo katika lugha ya kiingereza lilitokana na mshiriki mmoja, yeye ni mzee mstaafu lakini anafanya kazi kama meneja katika  kampuni moja ya Wachina pale kariakoo na alinieleza kuwa siyo kwamba hajui kuandika michanganuo ya biashara, hapana, hiyo ndiyo kazi hasa anayowafanyia Wachina.

Aliona umuhimu wa kununua kitabu cha michanganuo, kwanza, ili kulinganisha wakati ule alipojifunza yeye na sasa, mambo mengi yeye alijifunza miaka kadhaa iliyopita hivyo ni vizuri akaona na kwa miaka hii kuna vitu gani vimebadilika ama kuongezeka. Pili aliniambia kwamba yeye amezowea kuandika michanganuo kwa lugha ya kiingereza tu na angefurahi kuona michanganuo kwa lugha ya kiswahili pia. Mzee huyo hata hivyo aliniomba kama ninaweza kuwa na kitabu cha miaka hii cha michanganuo ya biashara kilichoandikwa kwa lugha ya kiingereza pamoja na ‘material’ nyingine mbalimbali anazoweza kupitia ili kujinoa zaidi.

Nilimwambia vitu vyote hivyo anaweza akavipata na nikampa kitabu hicho maarufu sana duniani, ‘templates’ kadhaa pamoja na michanganuo iliyoandikwa kwa kiingereza. Kwa hiyo alinifungua masikio nikajua kumbe kuna kundi la washiriki ambao watafurahia kujifunza michanganuo ya kiswahili sambamba na kwa lugha ya kiingereza pia kwani kuna wakati mtu unaweza ukakuta ukihitajika kuandika kwa kiingereza hasa unapotaka kuwakilisha mpango wako wa biashara wadau kama baadhi ya mabenki nk. Matokeo yake leo nikaamua kuviweka kwenye blogu yetu ya Masomo ya SEMINA ya michanganuo ya biashara vile vitu vyote nilivyompatia yule Meneja wa kampuni ya Wachina Kariakoo. Utakapoingia katika blogu hiyo kama umeshalipia semina na kupewa link ya kuingia humo basi utaweza kuvipata vitu hivyo vyote, masomo pamoja na kila kitu tulichowaandalia washiriki.

SOMA: Shindano la kuandika mpango wa biashara.

Ndugu msomaji wangu unaweza ukajiuliza, “Mbona waandaaji wa semina hii wameweka vitu vingi sana katika blogu hii kwa gharama ileile ambavyo kimsingi vilitakiwa kulipiwa fedha ?

·       SEMINA yenyewe  Sh. 10,000/=
·       Kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali   Sh. 10.000/=
·       Template(vielezo) kwa kiswahili(makadirio Sh. 10,000/=)
·       Templates(vielezo) kwa kiingereza(makadirio Sh. 10,000/=)
·       Kitabu cha michanganuo kwa kiingereza(Makadirio Sh.20,000)
·       Michanganuo mbalimbali ya biashara kama vile mchanganuo wa kuku wa mayai na mingineyo. (makadirio Sh.40,000)

Kwa haraka haraka hapo unaweza kuona kwamba, ukiondoa masomo yenyewe ya Semina ambayo gharama yake halisi ni shilingi elfu 10, vitu vingine vitano vilivyobakia na vingine vitakavyowekwa baadae kidogo ni kama vile mshiriki anapewa bure(free of charge). Ina maana kama vingelilipiwa vyote gharama yake ingelifikia shilingi laki moja kamili(100,000/=) Ni kama kuna ofa ya shilingi elfu 90 hivi.

JE, OFA HII ITAENDELEA MPAKA LINI?
Ofa au punguzo hili halitadumu milele, utafika muda itakwisha na kila kitu itabidi kilipiwe gharama zake kama kilivyo, Kwa hiyo ndugu msomaji wangu kama wewe ni mjanja na unapenda kunufaika na maarifa haya yote, basi huu ndiyo muda muafaka wa kulipia ada ya semina tu ambayo ni shilingi elfu 10 na upate bure punguzo hilo la zaidi ya shilingi elfu 90.

SOMA: Mchanganuo kamili wa biashara yaufugaji wa kuku wa mayai, kuku 1,000

Ni watu wengi wamediriki hata kunicheka kwa kutoa vitu vingi vyenye thamani namna hii kwa gharama hiyo ndogo ya shilingi elfu 10, lakini huwa nawaambia, “nataka nipate idadi fulani tu ya watu kwa ajili ya kwenda kutangaza ubora wa kazi za kampuni yetu kwa maelfu ya watu wengine kote nchini na duniani kwa ujumla.”.

Ungependa kuwa miongoni mwa watu hao wachache watakaokwenda kutangaza vizuri jina la Self Help Books kutokana na faida kubwa utakayoipata kwenye mafunzo yaliyokuwemo kwenye vitabu na semina hii? Kama jibu ni ndiyo basi wahi fursa hii kabla haijapita kwa kuchukua hatua sasa hivi na wala siyo kesho.

Kuna offer au punguzo jingine tulilotangaza wiki iliyopita, nayo ilikuwa ni ya kununua kifurushi cha vitabu 3 maarufu vya self help books vikiwa katika mfumo pepe(softcopy) kwa email kwa shilingi elfu 15 tu badala ya shilingi elfu 18 bei ya kawaida. Vitabu hivyo ni hivi hapa chini;

1.  MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI,
2.  SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NA
3.  MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA 

Mwisho wa punguzo hili ulipaswa uwe jana tarehe 19 feb. 2017 lakini tumeona tusogeze mbele muda huo kwa ajili ya wateja ambao kutokana na sababu mbalimbali hawakuweza kupata taarifa za punguzo hilo, kwanza hatukuweka tangazo hapa kwenye blogu zaidi ya kutoa tangazo katika baadhi ya magroup kwenye facebook. Ofa hii nayo itakuwa ya muda maalumu baada ya hapo ni bei ya kawaida.

Kwa hiyo ndugu msomaji wangu, ijapokuwa kukupa ujanja mimi hainiongezei faida, lakini nitakufundisha ujanja mmoja na hata ikiwa wewe mwenyewe tayari ni mjanja basi utakuwa umeshaugundua ujanja huo mwenyewe.

Kama unapenda unufaike kwa asilimia mia moja na ofa hizi mbili kwa mpigo kwa gharama ya chini kabisa ambayo haijawahi kutokea mahali pengine popote pale, lipia kifurushi cha vitabu 3, (softcopy) shilingi elfu 15, na kisha udai kushiri darasa la MICHANGANUO kwani unakuwa tayari na sifa za kushiriki kutokana na kununua kitabu cha MICHANGANUO. Kwa mantiki hiyo unakuwa umepata kila kitu kinachotolewa na kampuni ya SELF HELP BOOKS kwa gharama ya shilingi elfu 15 pekee. Kweli kama huo siyo ujanja ni kitu gani?

.............................................................................................

Ukihitaji vitabu vya biashara na ujasiriamali tembelea SMART BOOKS TANZANIA


Kufahamu huduma zetu nyingine bofya hapa, HUDUMA ZETU


Kujiunga na group la masomo ya kila siku na semina za kuandika michanganuo bunifu lipia ada ya mwaka sh. 10,000/= kisha tuma ujumbe "NATAKA OFFA YA VITU 14 NA KUJIUNGA GROUP LA MASOMO"




1 Response to "PATA 90,000: FURAHIA OFA KUBWA BEI YA VITABU NA SEMINA ZA ELIMU YA MAFANIKIO"

  1. Kwa wanaohitaj mafunzo ya mashine za kutotoleshea vifaranga..na mashine za kutumia mafuta ya taa na wanaohitaji kuku wa kienyej na chotara ..0744903557 dsm

    ReplyDelete