TUNATOA HUDUMA ZA USHAURI WA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WANAOANZA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TUNATOA HUDUMA ZA USHAURI WA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WANAOANZA

Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukitoa ushauri au kuzungumza na wajasiriamali wenye maswali mbalimbali na changamoto zinazohitaji ufumbuzi na mara chache tumekuwa tukishea majibu hayo katika blogu yetu hii ya jifunzeujasiriamali na wakati mwingine katika tovuti ya jifunzeujasiriamli.com kama ushauri wa Katarina(siyo jina lake halisi lakini) kuhusiana na utengenezaji wa sabuni shampoo, batiki na unga wa lishe.

Huduma hii ya kuzungumza na wajasiramali huwa tunaifanya bure kabisa bila ya kutoza kiasi chochote kile cha fedha na tutaendelea kufanya hivyo siku zote bila kudai pesa kutoka kwa wale wenye shida na changamoto mbalimbali za kibiashara hususani biashara ndogondogo. Najua ni kiasi gani mfanyabiashara mdogo hata shilingi mia moja ilivyokuwa muhimu kwake na hata wakati mwingine huwa anaipata kwa shida sana hivyo kwa kweli siyo busara kumchaji kila huduma anayopewa.


Lakini pia kuna wajasiriamali wengine ambao wangependa baada ya kupata huduma ya bure ya mara moja basi waweze tena hata kurudi kesho yake na kuuliza jambo jingine au hata jambo lilelile alilouliza mara ya kwanza kwa ufafanuzi wa kina zaidi. Wajasiriamali wa namna hiyo tumewawekea utaratibu mzuri wa kuchangia huduma hiyo kiasi cha shilingi elfu 5 tu, na atapata fursa  ya kupata ushauri wa karibu kila atakapohitaji ndani ya kipindi cha miezi 6.

Pia ikiwa atahitaji kufanyiwa vitu kama tathmini ya kiasi cha mahitaji ya kuanzisha biashara fulani atafanyiwa bure na kutumia kwa njia ya meseji au email. Huduma hii pia itakwenda sambamba na kupewa ushauri kuhusiana na maswala ya kuanzisha blogu na kuiendeleza, ni kwa namna gani aongeze watembeleaji nk. Haya yote yatafanyika bure ikiwa yeye ataomba baada ya kujiunga na huduma hii.

  
Narudia tena kusema kwamba huduma hii ya kulipia haitaathiri kwa vyovyote vile ile huduma ya kawaida ya bure ya kuuliza jambo lolote kwa mara moja. Ukitaka kujiunga na huduma hii tuma kiingilio shilingi 5,500/= kwa namba 0712 202244  au  0765 553030 jina litokee Peter Augustino Tarimo, halafu tuma na meseji inayojulisha kuwa unataka kujiunga na huduma za ushauri pamoja na maelezo ya ushauri unaohitaji au changamoto unayotaka majibu. 

Utampa mshauri kama muda wa masaa 4-6 hivi akitafakari changamoto yako na kuitafutia majibu kisha sasa mtaongea ukiwa mahali palipotulia kwa dk. 15-20.

...........................................................................................
Kwa vitabu vyako vvya biashara na maendeleo binafsi tembelea SMARTBOOKSTZ


Pakua hapa KITABU CHA KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU ya pesa na mafanikio bure pamoja na vitabu vingine vizuri 25


0 Response to "TUNATOA HUDUMA ZA USHAURI WA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WANAOANZA"

Post a Comment