Mawazo ya biashara kama kazi zingine zozote zile zinazotumia akili katika kubuni, zina thamani na zinaweza zikauzwa sawasawa kama vile huduma na bidhaa za kawaida zinavyoweza kuuzwa.
Wazo la biashara laweza kuwa ni biashara
yeyote ile lakini pia hapa tunatazama wazo la biashara kwa muktadha mpana zaidi
tukijumuisha pia na ubunifu wa aina nyinginezo kama vile wa kazi za kisanii
pamoja na ugunduzi mbalimbali kwa mfano hata ubunifu wa kisayansi, majina ya
biashara, nembo mbalimbali za biashara nk.
Sababu zinazoweza kukufanya uuze wazo lako la
biashara au ubunifu ni hizi zifuatazo,
1. Kubuni
na kuliendeleza wazo la biashara kunagharimu rasilimali nyingi ukiwemo muda
pesa na hata kujitoa kikamilifu. Changamoto hizo zote zinaweza zikamfanya mtu
akaamua ni bora akamuuzia mtu mwingine yeyote yule aliyekuwa tayari kwenda
kuliendeleza wazo hilo.
SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara unayoipenda.
SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara unayoipenda.
2. Kuanzisha
biashara mpya kutokana na wazo jipya ulilolibuni kunaambatana na hatari
mbalimbali kama vile, kushindwa kutimiza malengo ya biashara, kufilisika na
hata kukosa muda wa kutosha. Hivyo kuepukana na hatari hizo unaweza ukaamua
kuliuza wazo lako.
3. Unaweza
pia ukauza ubunifu au wazo lako la biashara kutokana na kukosa maarifa ya kijasiriamali,
ujuzi pamoja na nguvu za kiushindani kwenye biashara.
4. Lakini
pia unaweza kuuza wazo lako la biashara ikiwa lengo lako kubwa wakati wa
kulibuni lilikuwa ni kupata faida ya haraka na katika muda mfupi.
5. Ikiwa
wewe shughuli yako rasmi ni ya
kuchunguza fursa mbalimbali zilizoko kwenye jamii na kuwaandalia watu,
makampuni na wawekezaji mawazo ya biashara, bila shaka ni lazima ubadilishane
nao mawazo hayo kwa pesa.
Ili sasa uweze kuuza wazo lako la biashara au
ubunifu katika jambo lolote lile ni lazima ufuate hatua hizi zifuatazo.
1. Tafuta mwanasheria.
Hatua
ya awali kabisa ni kumtafuta mwanasheria anayefahamu masuala ya mikataba ya
kibiashara na sheria ya hakimiliki, hii ni hatua muhimu sana ikiwa hutaki kuja
kujutia hapo baadae. Mwanasheria atakuwa na wewe wakati wa kusaini mikataba, na
pia kukusaidia kuchunguza kitaalamu makubaliano yenu ikiwa kama kuna hila
zozote na hivyo kukufanya wewe uweze kuwa upande salama zaidi na wenye faida.
2. Wekea ulinzi wazo/ubunifu wako.
Hatua
nyingine ya kufuata hata kabla hujaingia kwenye meza na wawekezaji wako
watarajiwa ni ya wewe kuhakikisha kwamba sheria za nchi zinakutambua wewe kama
mmiliki halali wa wazo au ugunduzi husika.
SOMA: Kwanini kubuni kitu ni hatari?
SOMA: Kwanini kubuni kitu ni hatari?
Kwa
mujibu wa kitabu cha MICHANGANUO YA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI, vyombo vinavyohusika na ulinzi wa hakimiliki ya
ubunifu wa kiakili kwa hapa Tanzania ni kama vile COSOTA, BRELA na BASATA,
vyombo hivi hulinda, hakimiliki ya ubunifu wa kazi za kisanaa, ugunduzi, hatimiliki,
majina ya biashara na alama za biashara.
3. Tathmini na kutambua thamani halisi ya
wazo lako.
Ukishatambua
wazo lako lina thamani kiasi gani, sasa panga bei utakayoliuza. Thamani ya pesa
ya wazo hilo katika soko ni kiasi gani? Na ni jinsi gani utakavyokokotoa
thamani hiyo. Unaweza ukamtafuta mtaalamu wa biashara na makadirio au hata wewe
mwenyewe unaweza ukathaminisha tu kwa kuangalia fursa ya soko iliyokuwepo
kutokana na wazo hilo.
4. Weka kiwango cha chini cha thamani
utakachouza wazo lako.
Kabla
hujakaa mezani na mnunuzi wa wazo lako la biashara, na tayari umekwishafahamu
thamani ya wazo lako, sasa weka kiwango cha chini cha bei utakayouza, chini ya
bei hiyo ni kwamba hautauza kabisa.
Hii
itafanya kazi ya kuliuza wazo lako kuwa rahisi kwani unafahamu kwa uhakika ni
kitu gani unachokitaka. Kwa mfano tuseme umejiwekeamalemgo kwamba, albamu yako
ya nyimbo za injili au nyingine zozote zile kiwango chake cha chini cha kuuza
ni shilingi milioni ishirini(20,000,000/=). Ikiwa promota atakupa milioni 18,
katu huwezi kukubali, ni lazima iwe ni kuanzia milioni 20 au juu ya hapo.
5. Chagua ni mfumo upi mauzo yatafanyika
Mfumo
au njia ya mauzo maana yake ni kwamba, utataka ulipwe kupitia mtindo upi?,
utapokea pesa taslimu au kwa cheki?, je ni kwa malipo ya papo kwa hapo au ni
kwa kupitia mfumo wa mrahaba?. Hilo litategemea zaidi wewe na mnunuzi wako
mtakavyokubaliana.
6. Tambua malengo yako.
Unaweza
kujikuta unaingia katika majadiliano ya mkataba na watu wajanja watakaokupa
ahadi tamu tamu zisizoweza kuja kutekelezwa kamwe kusudi tuwewe uweze kukubali
kuuza wazo lako na hili limewahi kuwakuta watu wengi hapa Tanzania hasa watunzi
wa kazi za kisanii kama muziki na filamu. Kabla hujaingia kwenye meza ya
majadiliano, fahamu kabisa malengo yako ni nini, jua kile unachokihitaji na
usiyumbeyumbe.
7. Watambue kabla wanunuzi wako watarajiwa.
Hatua
ya saba ya kuuza wazo la biashara au ubunifu wako ni kuwatambua kwanza wanunuzi
wako watarajiwa, makampuni, wawekezaji, au hata watu binafsi waliokuwa na
uwezekano wa kununua wazo hilo. Kisha waorodheshe wote katika karatasi.
SOMA: Kufanya utafiti wa soko la biashara yako.
SOMA: Kufanya utafiti wa soko la biashara yako.
8. Andika na utume kwa kila mteja mtarajiwa
andiko la biashara la mapendekezo yako.
Ukisisitiza
zaidi faida na mambo ya kimsingi ya wazo hilo, kikubwa hapa ni wewe kuuza faida
za wazo lako kuamsha hisia za mvuto wa wazo lako kwa wanunuzi watarajiwa.
9. Kutana na wanunuzi watarajiwa
walioonyesha kuvutiwa.
Ikiwa
wazo lako linaonekana lina fursa ndani yake wanunuzi watarajiwa watakaovutiwa
nalo watawasiliana na wewe na kufanya majadiliano ya biashara na wewe lakini
kumbuka usisahau kufanya hivyo chini ya mwanasheria wako. Pia usionyeshe papara
yeyote na kama unaona hutaweza kujadiliana vizuri unaweza hata ukamchukua mtu
mwingine mwenye ujuzi zaidi.
10.
Uza
wazo lako au hamia kwa mnunuzi mwingine aliyevutiwa.
Ikiwa
mambo yatakwenda kama yalivyo tokea hatua ya kwanza mpaka ya 9, basi unaweza
ukauza wazo lako. Ikiwa siyo, usipoteze muda wako nenda tena kwa mnunuzi
mwingine aliyeonyesha dalili za kutaka kununua, kumbuka hapa una orodha ya wale
wanunuzi watarajiwa ulioandika kwenye karatasi.
……………………………………………………………………......
Ndugu
msomaji wa blogu hii, ikiwa unapenda kujifunza kwa kina kabisa kuhusiana na
kuanzisha na kuendeleza biashara yeyote ile, jipatie kitabu hiki cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa bei ya shilingi 20,000/=
hardcopy au shilingi, 10,000/= softcopy
Pia
tuna vitabu vingine 2, vifuatavyo,
MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA Tsh. 10,000/=hardcopy na sh. 5,000/=softcopy
MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA Tsh. 5,000/=hardcopy na sh. 3,000/=softcopy.
Wasiliana
nasi kwa namba za simu 0712 202244 au
0765 553030
Tunayo pia MASOMO YA SEMINA ya jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara kwa njia ya
e-mail na blogu maalumu, kiingilio ni Tsh. 10,000/=
0 Response to "JINSI YA KUUZA WAZO LAKO LA BIASHARA AU BUNIFU KWA WAWEKEZAJI NA WATU WENGINE"
Post a Comment