Tumeanzisha kipengele ama ‘segment’ maalumu kwa ajili ya wajasiriamali au watu waliofanikiwa ambapo tutakuwa tukielezea stori na safari zao za mafanikio, walikopita milima na mabonde ili na sisi tuweze kuhamasika na mwishowe tuwe kama wao. Segment hiyo itaitwa SUCCESS STORIES.
Leo hapa kuna wajasiriamali matajiri vijana wapatao 10
kutoka Afrika ya kusini ambao wanasimulia kila mmoja uzoefu wake na namna
alivyoweza kuvuka vikwazo mbalimbali katika safari yake ya ujasiriamali
wakitumia uunifu na mbinu mbalimbali za kijasiriamali. Hebu bila ya kupoteza
muda mwingi tuanze kuwasikiliza.
1. THABO
KHUMALO - ToVch
Thabo Khumalo |
SOMA: Gundua siri ya kufanikisha biashara yako sasa.
Khumalo ana mashabiki wachache lakini
wanaojituma ambao huwasiliana nao moja kwa moja. “Nembo(Brand) ina mashabiki
wanaojitolea, na uwepo wa mitandao ya kijamii pia unaniruhusu kuendelea
kuchambua mazingira ya mitindo ili kukabiliana na ushindani kutoka nje”.
SOMO
TUNALOLIPATA
Moja ya changamoto kubwa aliyokumbana
nayo wakati akianzisha biashara yake ilikuwa ni kutafuta soko la brandi yake
huku akiwa hana mtaji wa kutosha. Alilazimika kutumia mitandao ya kijamii na
maneno ya mdomo kwa mdomo kutafuta soko. “Kwenye mitandao ya kijamii watu
hushea nembo yako na watu wengine basi tu kwa kuwa wanapenda kufanya hivyo”
anasema Khumalo. “Ni jukwaa lenye nguvu na haligharimu chochote” Khumalo
alijenga kampuni yake akitumia msaada kutoka mtandao imara wa kijamii, ambao
ndio uliokuwa mkakati wake wa masoko.
2. LUVUYO RANI – Silulo Ulutho Technologies
Luvuyo Rani |
Katika harakati za kulifundisha soko lake
jinsi ya kutumia kompyuta, alibuni wazo lenye kuuzika lililokuwa na uhitaji mkubwa
mno katika soko, “Teknolojia ya Silulo Ulutho” ambayo mpaka sasa hivi ana
matawi zaidi ya 40 kote nchini Afrika ya
kusini.
SOMA: Teknolojia inavyoweza kuwakomboa wasanii Tanzania
SOMA: Teknolojia inavyoweza kuwakomboa wasanii Tanzania
SOMO
TUNALOPATA
“Usiling’ang’anie sana wazo ama mfumo
wako wa biashara” anasema Rani. “Wakati mwingine unatakiwa ubadilike ili
uendane na soko linavyotaka, huwezi kutegemea soko ndilo libadilike kufuata
matakwa yako wewe, basi tu kwa kuwa unawauzia huduma au bidhaa fulani. Tafuta
kile wanachohitaji au wanachokitaka na kisha wapatie suluhisho” Katika kukidhi
matakwa hayo ya wateja Rani aliweza kupata wazo lake la biashara lenye
mafanikio.
3. ALEX FOURIE - weFix
Alex Fourie. |
SOMA: Kutafuta soko la bidhaa zako kunahitaji ubunifu mkubwa.
Biashara ya Fourie, weFIX sasa inayo matawi
11 nchini kote na huuza bidhaa zake yenyewe za ndani na bima kwa baadhi ya
bidhaa.
“Tunakadiria kuwa na wateja wapatao 10,000
kwa mwezi, na asilimia 75% hutokana na matangazo ya mdomo kwa mdomo.
SOMO
TUNALOLIPATA
“Ubora siyo matokeo ya uamuzi mmoja au
maamuzi 2, ni matokeo ya maelfu ya maamuzi madogomadogo mengi. Kila
unachokifanya kifanye vizuri katika ubora wake na yaliyobakia yatajipanga
yenyewe mbele ya safari”
4. REPELANG RABANA – Rekindle Learning
Repelang Rabana |
Wazo la kuendelea kufanya kazi kupitia mifumo
zaidi na zaidi, kutoka high school mpaka chuo kikuu mpaka ulimwengu wa makampuni
makubwa ulinielemea. Lakini sikuwa na wazo kwamba hii ingeweza kuwa na maana
kwamba nataka kuwa mjasiriamali”.
SOMA: Hatua7 rahisi za kuanzisha biashara yako ukiwa bado kazini umeajiriwa.
SOMA: Hatua7 rahisi za kuanzisha biashara yako ukiwa bado kazini umeajiriwa.
Repelang Rabana alianzisha kampuni iitwayo
Rekindle Learning, ambayo hutoa mafunzo na maendeleo kupitia simu za mkononi na
kompyuta. Mafunzo haya humsaidia mhusika kupata ujuzi wa kazi na mazingira ya
kujifunza.
SOMO
TUNALOLIPATA
“Karibu miaka 10 nyuma nilikuwa
nimefanya uamuzi wa kuanzisha biashara
yangu licha ya mkanganyiko wa mawazo na fikra, kutokujua maisha yatakuwaje”
alisema. “Sasa kujiamini nilikojiwekea mwenyewe kufuata njia yangu mwenyewe
ilikuwa inazaa matunda ambayo sikuwa nimeyawazia, yote ni kutokana kuthubutu
kujisikiliza mwenyewe. Nikitambua thamani ya uchaguzi huo wa miaka 10 najisikia
amani kubwa”.
5. SIZWE
NZIMA - Iyeza Express
Sizwe Nzima. |
SOMA: Ubunifu!, Maktaba ya vitabu inayotembea huko mwwanza.
Aliyemvutia Sizwe Nzima kutambua kuwa alikuwa
anahitaji kuchukua hatua ili kuifanya jamii yake mahali pazuri pa kuishi ni mtu
aitwaye Raymond Ackerman. Kampuni yake Iyeza Express, inatumia baiskeli kwa
ajili ya kubebea dawa za magonjwa sugu kutoka katika mahospitali ya umma na kuwapelekea moja kwa moja wagojwa
majumbani mwao.
SOMO
TUNALOLIPATA KUTOKANA NA KIJANA HUYU
Dhumuni la Iyeza Express ni kumfanya kila
mtu aweze kuzifikia huduma za afya kwa urahisi” anaeleze Nzima. “Watu
wanahitaji njia nzuri ya kuzifikia huduma za afya licha ya hali zao za kichumi,
bila ya kujali ni wapi wanapoishi ni haki ya kimsingi ya binadamu.”
Richard Ackerman alimhamasisha Nzima
kufanya mazuri na matokeo yake Nzima alikuza biashara nzuri. Aliendelea
kuijenga biashara yake kuisaidia jamii na anafanya kazi kutengeneza mfumo
madhubuti wa biashara utakaowezesha huduma yake ya kuwapelekea watu dawa
majumbani kusambaa nchi nzima kwa wale wanaoihitaji na wale wanaohitaji ajira
pia.
6. NAFTALY MALATJIE – South Africa Youth Project
Naftaly Malatjie |
SOMO: Kabla ya kuchukua mkopo mahali wa biashara, pambana kwanza kiume usijekuaibika bure.
Lengo la mradi ni kuwapa vijana matumaini
katika jamii kupitia mafunzo ya kijasiriamali, ushonaji, semina za upambaji wa
ndani, mafunzo ya sehemu za kazi, ushauri wa ajira, na mafunzo ya kompyuta.
SOMO
TUNALOJIFUNZA KUTOKA KWA NAFTALY NI HILI HAPA
Mwanzoni kabisa nilipata ufadhili kutoka
shirika kubwa, na bila ya kufikiria nikatumia bajeti yote ya mwaka mzima kwa
kipindi cha wiki moja tu” Malatjie anabainisha “Nilikuwa nimesaini mkataba na mwishowe
nikaishia kulipia gharama za mradi kwa mikopo binafsi katika kipindi cha mwaka kilichokuwa
kimebakia. Hili hutokea wakati mhemko kutokana na mradi wako unapoifunika
mantiki”
“Kulikuwa na matatizo mengi yaliyokuwa
yanahitaji kurekebishwa, ambayo nilitaka kuyarekebisha yote kwa wakati mmoja,
ukosefu wa malengo nusura uharibu ndoto zangu. Chochote kile unachopanga
kukifanya, kwanza elekeza bajeti na rasilimali zako, hasahasa kwa fedha za
wafadhili” Anashauri Malatidje.
7. EZYLN BARENDS -The Dreamgirls
Ezyln Barends. |
SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na ni kwanini ujiwekee malengo makubwa maishani.
“Tumejijengea utamaduni wetu wenyewe,
ambao tunauita 'DreamGirls'(Ndoto ya wasichana) njia ya kufanya mambo” Anasema
Barends. “Kwa sababu taasisi ilijengwa juu ya seti maalumu ya maadili, taasisi
hii ni zaidi ya kuwasaidia tu wasichana kupata elimu ya juu. Lengo kuu hasa ni
kuhusiana na kutoa usaidizi na ushirikiano kwa kila mtu anayehusika.
SOMO
KUBWA TUNALOLIPATA KUTOKA KWA BARENDS NI HILI HAPA.
“Moja ya kitu muhimu zaidi
nilichojifunza ni kuwaacha watu wengine katika taasisi yako kuongoza” Anaelezea
Barends. “Huo umekuwa ni utambuzi muhimu kwangu kama ninavyojihusisha katika
miradi mingi, inayosababisha muda kuwa rasilimali yenye thamani mno.
Barends anashauri, “Kufanya kazi pamoja
na watu waliokuwa na maadili na maono kama yakwako, huku ukiwapa uhuru, ambavyo
ni vitu vya kawaida miongoni mwa wajasiriamali pamoja na kuwawezesha wengine
katika taasisi yako ndiyo siri kuu ya mafanikio. Hivyo ndivyo DreamGirls
ilivyokua na kuwa biashara ya kijamii yenye mafanikio.”
8. LUDWICK MARISHANE - Headboy Industries
Ludwick Marishane |
SOMA: Uwezo wa akili ya binadamu ni wa ajabu na usiokadirika.
“Jamii zilizokuwa na uwezo zitakuta kwamba
DryBath huokoa muda na ni njia ya kubana matumizi ya maji yanayotumika kuogea
kila siku, ninaamini, ni silaha muhimu katika kupambana na janga la maji
linalozidi kuongezeka.
SOMO
TUPATALO TOKA KWA LUDWICK
Marishane Ludwick hakuwa na kianzio cha fedha cha aina yeyote
ile wala uwezekano wa matumizi ya kompyuta. “Hata hivyo niliweza kumiliki simu
ya mkononi ya kawaida ambayo ilikuwa na uwezo wa kuunganishwa na intaneti,
hivyo nikaweza kufanya utafiti. Unatakiwa ufanye kazi na kile ulichokuwa nacho
na ufanye kwa ubora wa hali ya juu kabisa pamoja na mapungufu uliyonayo.”
Anaelezea Marishane. Aliendelea kuandika mpango wa biashara wa kurasa 40 kwenye
simu ya kawaida ya Nokia.
9. DOUGLAS HOERNLE – Rethink Education
Douglas Hoernle |
SOMA: Kuanzisha biashara tokea mwanzo mpaka mwisho, mafunzo muhimu 5
“Mwanafunzi wa kawaida wa wa sekondari ya juu
hutumia teknolojia kuwasiliana. Wanatumia staili ya kuchati katika majukwaa ya
kijamii kama vile WhatsApp, Mxit, BBM, Facebook na Twitter. Jukwaa letu hulisha
katika majukwaa hayo kwa kutoa maudhui
ya elimu kupitia mitandao hiyo. Unaweza ukailinganisha na daftari la
mawasiliano” anaelezea Hoernle
SOMO
TUNALOLIPATA
Hoernle anabainisha kwamba safari ya
ujasiriamali imejaa vikwazo na haifai kwa mtu anayekata tamaa. “Kumekuwa na
changamoto nyingi ambazo imetubidi kukabiliana nazo katika kujenga mfumo wa
kibunifu wa elimu Afrika ya kusini. Kutumia njia bunifu, za kiuweledi na za ziada
katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yote tuliyokutana nayo, imetusaidia
kuvipita vikwazo vingi.”
10. THABO KGATLHANYE NA REA NGWANE –Repurpose Schoolbags.
Thabo Kgatlhanye. |
SOMA: Njia 7 unazoweza kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako
“Kuwapata mashirika na watu binafsi wanaopenda
kuchangia katika mradi wakilenga katika elimu ya watoto ndiyo kitu kilichotuwezesha
sisi kugeuza wazo letu la mwanzo kuwa biashara endelevu ya kijamii
inayowanufaisha watoto, kuajiri watu kutoka kwenye jamii na pia kuleta faida,”
anaselezea Kgatlhanye.
Wajasiriamali hawa walitumia mashindano ya
mawazo ya kuanzisha biashara ili kukusanya kiasi cha fedha za kuwasaidia
kulitoa wazo lao chini. Mara tu walipokuwa katika hatua ya uzalishaji,
wawekezaji walikuja kugonga mlango.
SOMO TUNALOPATA
“Kila mtu hufikiri unahitaji pesa
kuanzisha biashara, jambo ambalo ni kweli, lakini tulithibitisha kwamba unaweza
ukafanya mambo tofauti ukizingatia kwamba una msukumo wa kutosha na umejiandaa
kufanya kazi kwa nguvu kuliko vile ambavyo ulidhania ingewezekana.” Alibainisha
Ngwane.
MAKALA HII NA PICHA NI KWA HISANI YA JARIDA LA "ENTREPRENEUR MAGAZINE"
...........................................................................................
Ndugu msomaji ikiwa unapenda kujifunza maswala mbalimbali ya ujasiriamali kwa kina kabisa, basi jipatie vitabu mbalimbali kutoka kwetu. Vitabu hivyo ni hivi hapa chini;
1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.
MAKALA HII NA PICHA NI KWA HISANI YA JARIDA LA "ENTREPRENEUR MAGAZINE"
...........................................................................................
Ndugu msomaji ikiwa unapenda kujifunza maswala mbalimbali ya ujasiriamali kwa kina kabisa, basi jipatie vitabu mbalimbali kutoka kwetu. Vitabu hivyo ni hivi hapa chini;
1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.
Na shilingi elfu 10 softcopy kwa njia ya email.
2. SIRI YA MAFANIKIO: BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
Na kwa kitabu cha email au softcopy ni shilingi elfu 5
2. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA
Na softcopy kwa njia ya email ni shilingi elfu 3
Pia tuna masomo ya semina kuhusiana na michanganuo ya biashara ambayo yanapatikana kwenye blogu hii MAALUMU YA MICHANGANUO. Kujiunga na masomo hayo ni shilingi elfu kumi pamoja na kupewa bure softcopy ya kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali.
Tunapatikana MBEZI KWA MSUGURI stendi ya daladala jirani na hospitali ya BOCHI,
Simu: 0712 202244 AU 0765 553030
Jina, Peter Augustino Tarimo
Kama upo mikoani na unataka vitabu vya karatasi, unaweza kumuagiza mtu anayefika Dar es salaam akakuchukulia, au tunaweza kutuma kwa njia ya Basi linalofika kule ulipo, lakini gharama za usafiri zitaongezeka kidogo.
Ukihitaji vitabu kwa njia ya e-mail ukiwa popote pale, tuma fedha pamoja na anuani yako ya email kwenye namba zetu hapo juu nasi tutakutumia kitabu/vitabu muda huohuo bila kuchelewa.
0 Response to "SOMO:MAMILIONEA VIJANA 10 WAKISIMULIA SIRI ZA UTAJIRI WAO WALIVYOFANIKIWA "
Post a Comment