SOMO:MAMILIONEA VIJANA 10 WAKISIMULIA SIRI ZA UTAJIRI WAO WALIVYOFANIKIWA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SOMO:MAMILIONEA VIJANA 10 WAKISIMULIA SIRI ZA UTAJIRI WAO WALIVYOFANIKIWA

Vijana Wajasiriamali waliofanikiwa


Tumeanzisha kipengele ama ‘segment’ maalumu kwa ajili ya wajasiriamali au watu waliofanikiwa ambapo tutakuwa tukielezea stori na safari zao za mafanikio, walikopita milima na mabonde ili na sisi tuweze kuhamasika na mwishowe tuwe kama wao. Segment hiyo itaitwa SUCCESS STORIES.

Leo hapa kuna wajasiriamali matajiri vijana wapatao 10 kutoka Afrika ya kusini ambao wanasimulia kila mmoja uzoefu wake na namna alivyoweza kuvuka vikwazo mbalimbali katika safari yake ya ujasiriamali wakitumia uunifu na mbinu mbalimbali za kijasiriamali. Hebu bila ya kupoteza muda mwingi tuanze kuwasikiliza.

1. THABO KHUMALO - ToVch
Thabo Khumalo
“Nilijifunza kudizaini na kushona wakati nikimsaidia mama yangu ambaye alikuwa fundi-nguo na hapo ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa na kipaji cha ubunifu” Anaelezea Khumalo.  “Lakini sikuwa najua kama nilikuwa mjasiriamali. Thabo Khumalo alianzisha kampuni yake iitwayoToVch mwaka 2010 na tangu hapo amekuwa akionekana katika Wiki ya Mitindo Afrika Kusini, Wiki ya Mitindo Soweto na ile ya Mpumalanga.

SOMA: Gundua siri ya kufanikisha biashara yako sasa.

Khumalo ana mashabiki wachache lakini wanaojituma ambao huwasiliana nao moja kwa moja. “Nembo(Brand) ina mashabiki wanaojitolea, na uwepo wa mitandao ya kijamii pia unaniruhusu kuendelea kuchambua mazingira ya mitindo ili kukabiliana na ushindani kutoka nje”.

SOMO TUNALOLIPATA
Moja ya changamoto kubwa aliyokumbana nayo wakati akianzisha biashara yake ilikuwa ni kutafuta soko la brandi yake huku akiwa hana mtaji wa kutosha. Alilazimika kutumia mitandao ya kijamii na maneno ya mdomo kwa mdomo kutafuta soko. “Kwenye mitandao ya kijamii watu hushea nembo yako na watu wengine basi tu kwa kuwa wanapenda kufanya hivyo” anasema Khumalo. “Ni jukwaa lenye nguvu na haligharimu chochote” Khumalo alijenga kampuni yake akitumia msaada kutoka mtandao imara wa kijamii, ambao ndio uliokuwa mkakati wake wa masoko.


2. LUVUYO RANI – Silulo Ulutho Technologies
Luvuyo Rani
Anasema hivi, “Tulifikiri ya kwamba tumegundua soko lakini soko lenyewe kumbe lilikuwa halijajitambua lenyewe” anaeleza Rani, “Watu wanahitaji teknolojia, lakini tulikuwa tukilihubiria soko ambalo halikuwa linafahamu jinsi ya kukitumia kile tulichokuwa tukiwauzia.

Katika harakati za kulifundisha soko lake jinsi ya kutumia kompyuta, alibuni wazo lenye kuuzika lililokuwa na uhitaji mkubwa mno katika soko, “Teknolojia ya Silulo Ulutho” ambayo mpaka sasa hivi ana matawi zaidi ya 40  kote nchini Afrika ya kusini.

SOMA: Teknolojia inavyoweza kuwakomboa wasanii Tanzania

SOMO TUNALOPATA
“Usiling’ang’anie sana wazo ama mfumo wako wa biashara” anasema Rani. “Wakati mwingine unatakiwa ubadilike ili uendane na soko linavyotaka, huwezi kutegemea soko ndilo libadilike kufuata matakwa yako wewe, basi tu kwa kuwa unawauzia huduma au bidhaa fulani. Tafuta kile wanachohitaji au wanachokitaka na kisha wapatie suluhisho” Katika kukidhi matakwa hayo ya wateja Rani aliweza kupata wazo lake la biashara lenye mafanikio.


3. ALEX FOURIE - weFix
Alex Fourie.
Alex Fourie anaeleza, “Mwanzoni nilikuwa natatua matatizo yangu mwenyewe. Kisha ilikuwa ni pale nilipo post tangazo langu la kofia na simu yangu ikalia mara 15 katika siku ya kwanza pekee. Nilifikiria kwamba pale pangeliweza kuwa na biashara”

SOMA: Kutafuta soko la bidhaa zako kunahitaji ubunifu mkubwa.

Biashara ya Fourie, weFIX sasa inayo matawi 11 nchini kote na huuza bidhaa zake yenyewe za ndani na bima kwa baadhi ya bidhaa.

“Tunakadiria kuwa na wateja wapatao 10,000 kwa mwezi, na asilimia 75% hutokana na matangazo ya mdomo kwa mdomo.

SOMO TUNALOLIPATA
“Ubora siyo matokeo ya uamuzi mmoja au maamuzi 2, ni matokeo ya maelfu ya maamuzi madogomadogo mengi. Kila unachokifanya kifanye vizuri katika ubora wake na yaliyobakia yatajipanga yenyewe mbele ya safari”


4. REPELANG RABANA – Rekindle Learning
Repelang Rabana
“Nilichokuwa nikiwaza tu ni kwamba, nilihitaji kutafuta njia ya kujinasua kutokana na kile nilichokuwa nikikichukulia kama mfumo wa maisha uliokuwa ukishinikiza sheria na majukumu ambayo sikuwa naelewa lengo lake”

Wazo la kuendelea kufanya kazi kupitia mifumo zaidi na zaidi, kutoka high school mpaka chuo kikuu mpaka ulimwengu wa makampuni makubwa ulinielemea. Lakini sikuwa na wazo kwamba hii ingeweza kuwa na maana kwamba nataka kuwa mjasiriamali”.

SOMA: Hatua7 rahisi za kuanzisha biashara yako ukiwa bado kazini umeajiriwa.

Repelang Rabana alianzisha kampuni iitwayo Rekindle Learning, ambayo hutoa mafunzo na maendeleo kupitia simu za mkononi na kompyuta. Mafunzo haya humsaidia mhusika kupata ujuzi wa kazi na mazingira ya kujifunza.

SOMO TUNALOLIPATA
“Karibu miaka 10 nyuma nilikuwa nimefanya uamuzi  wa kuanzisha biashara yangu licha ya mkanganyiko wa mawazo na fikra, kutokujua maisha yatakuwaje” alisema. “Sasa kujiamini nilikojiwekea mwenyewe kufuata njia yangu mwenyewe ilikuwa inazaa matunda ambayo sikuwa nimeyawazia, yote ni kutokana kuthubutu kujisikiliza mwenyewe. Nikitambua thamani ya uchaguzi huo wa miaka 10 najisikia amani kubwa”.

5. SIZWE NZIMA -  Iyeza Express
Sizwe Nzima.
“Iyeza Expess ni mradi wa maendeleo wa kijamii” Nzima anaamini, “ Lengo pia ni kuajiri wanajamii kuwa waendeshaji, kutoa huduma na kuwa viongozi, kuufanya siyo tu kuwa kwa ajili ya huduma za kiafya bali pia kuwa chanzo cha ajira”

SOMA: Ubunifu!, Maktaba ya vitabu inayotembea huko mwwanza.

Aliyemvutia Sizwe Nzima kutambua kuwa alikuwa anahitaji kuchukua hatua ili kuifanya jamii yake mahali pazuri pa kuishi ni mtu aitwaye Raymond Ackerman. Kampuni yake Iyeza Express, inatumia baiskeli kwa ajili ya kubebea dawa za magonjwa sugu kutoka katika mahospitali ya umma  na kuwapelekea moja kwa moja wagojwa majumbani mwao.

SOMO TUNALOLIPATA KUTOKANA NA KIJANA HUYU
Dhumuni la Iyeza Express ni kumfanya kila mtu aweze kuzifikia huduma za afya kwa urahisi” anaeleze Nzima. “Watu wanahitaji njia nzuri ya kuzifikia huduma za afya licha ya hali zao za kichumi, bila ya kujali ni wapi wanapoishi ni haki ya kimsingi ya binadamu.”

Richard Ackerman alimhamasisha Nzima kufanya mazuri na matokeo yake Nzima alikuza biashara nzuri. Aliendelea kuijenga biashara yake kuisaidia jamii na anafanya kazi kutengeneza mfumo madhubuti wa biashara utakaowezesha huduma yake ya kuwapelekea watu dawa majumbani kusambaa nchi nzima kwa wale wanaoihitaji na wale wanaohitaji ajira pia.


6. NAFTALY MALATJIE – South Africa Youth Project
Naftaly Malatjie
“Nilitaka kubadilisha jinsi vijana wanavyofikiri kuhusiana na wao wenyewe,” Anasema Naftaly, mwanzilishi wa South Africa Youth Project. “Mafunzo hufanyika kwenye jamii katika eneo la Gauteng na huwapa vijana mafunzo ya kutosha ya kuwasaidia kupata kazi”

SOMO: Kabla ya kuchukua mkopo mahali wa biashara, pambana kwanza kiume usijekuaibika bure.

Lengo la mradi ni kuwapa vijana matumaini katika jamii kupitia mafunzo ya kijasiriamali, ushonaji, semina za upambaji wa ndani, mafunzo ya sehemu za kazi, ushauri wa ajira, na mafunzo ya kompyuta.

SOMO TUNALOJIFUNZA KUTOKA KWA NAFTALY NI HILI HAPA
Mwanzoni kabisa nilipata ufadhili kutoka shirika kubwa, na bila ya kufikiria nikatumia bajeti yote ya mwaka mzima kwa kipindi cha wiki moja tu” Malatjie anabainisha “Nilikuwa nimesaini mkataba na mwishowe nikaishia kulipia gharama za mradi kwa mikopo binafsi katika kipindi cha mwaka kilichokuwa kimebakia. Hili hutokea wakati mhemko kutokana na mradi wako unapoifunika mantiki”

“Kulikuwa na matatizo mengi yaliyokuwa yanahitaji kurekebishwa, ambayo nilitaka kuyarekebisha yote kwa wakati mmoja, ukosefu wa malengo nusura uharibu ndoto zangu. Chochote kile unachopanga kukifanya, kwanza elekeza bajeti na rasilimali zako, hasahasa kwa fedha za wafadhili” Anashauri Malatidje.


7. EZYLN BARENDS  -The Dreamgirls
Ezyln Barends.
Ezyln Barend ameionyesha dunia jinsi shauku yake ya kuwasaidia wengine ilivyokuwa na nguvu na namna inavyoweza kuibadilisha dunia. Dreamgirls ilianza bila ya kuwa na bajeti, lakini badala yake kutokana na matumaini yake makubwa ya kufanya mazuri pamoja na ahadi yake ya kutimiza. Sasa wazo lake linatarajia kuwa na matawi duniani kote.

SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na ni kwanini ujiwekee malengo makubwa maishani.

“Tumejijengea utamaduni wetu wenyewe, ambao tunauita 'DreamGirls'(Ndoto ya wasichana) njia ya kufanya mambo” Anasema Barends. “Kwa sababu taasisi ilijengwa juu ya seti maalumu ya maadili, taasisi hii ni zaidi ya kuwasaidia tu wasichana kupata elimu ya juu. Lengo kuu hasa ni kuhusiana na kutoa usaidizi na ushirikiano kwa kila mtu anayehusika.

SOMO KUBWA TUNALOLIPATA KUTOKA KWA BARENDS NI HILI HAPA.
“Moja ya kitu muhimu zaidi nilichojifunza ni kuwaacha watu wengine katika taasisi yako kuongoza” Anaelezea Barends. “Huo umekuwa ni utambuzi muhimu kwangu kama ninavyojihusisha katika miradi mingi, inayosababisha muda kuwa rasilimali yenye thamani mno.

Barends anashauri, “Kufanya kazi pamoja na watu waliokuwa na maadili na maono kama yakwako, huku ukiwapa uhuru, ambavyo ni vitu vya kawaida miongoni mwa wajasiriamali pamoja na kuwawezesha wengine katika taasisi yako ndiyo siri kuu ya mafanikio. Hivyo ndivyo DreamGirls ilivyokua na kuwa biashara ya kijamii yenye mafanikio.”  


8. LUDWICK MARISHANE  - Headboy Industries 
Ludwick Marishane
Akiwa na umri wa miaka 17, Ludwick Marishane aligundua DryBath, ambacho ni chombo kinachomsaidia mtu kukaa katika hali ya usafi pasipo kutumia maji. Aliutoa ugunduzi wake kupitia kampuni yake iitwayo, Headboy Industries Inc. “Nilikusudia DryBath kuwasaidia masikini, jamii zenye shida ya maji kote duniani” Anaelezea Marishale.

SOMA: Uwezo wa akili ya binadamu ni wa ajabu na usiokadirika.

“Jamii zilizokuwa na uwezo zitakuta kwamba DryBath huokoa muda na ni njia ya kubana matumizi ya maji yanayotumika kuogea kila siku, ninaamini, ni silaha muhimu katika kupambana na janga la maji linalozidi kuongezeka.

SOMO TUPATALO TOKA KWA LUDWICK
Marishane Ludwick  hakuwa na kianzio cha fedha cha aina yeyote ile wala uwezekano wa matumizi ya kompyuta. “Hata hivyo niliweza kumiliki simu ya mkononi ya kawaida ambayo ilikuwa na uwezo wa kuunganishwa na intaneti, hivyo nikaweza kufanya utafiti. Unatakiwa ufanye kazi na kile ulichokuwa nacho na ufanye kwa ubora wa hali ya juu kabisa pamoja na mapungufu uliyonayo.” Anaelezea Marishane. Aliendelea kuandika mpango wa biashara wa kurasa 40 kwenye simu ya kawaida ya Nokia.


9. DOUGLAS HOERNLE – Rethink Education
Douglas Hoernle
Rethink Education iliyoanzishwa na Douglas Hoernle ilibuni jukwaa la elimu la kidigitali linalowasaidia wanafunzi wa elimu ya juu kujifunza hesabu na sayansi kupitia simu zao za mkononi.

SOMA: Kuanzisha biashara tokea mwanzo mpaka mwisho, mafunzo muhimu 5

“Mwanafunzi wa kawaida wa wa sekondari ya juu hutumia teknolojia kuwasiliana. Wanatumia staili ya kuchati katika majukwaa ya kijamii kama vile WhatsApp, Mxit, BBM, Facebook na Twitter. Jukwaa letu hulisha katika majukwaa hayo kwa  kutoa maudhui ya elimu kupitia mitandao hiyo. Unaweza ukailinganisha na daftari la mawasiliano” anaelezea Hoernle

SOMO TUNALOLIPATA
Hoernle anabainisha kwamba safari ya ujasiriamali imejaa vikwazo na haifai kwa mtu anayekata tamaa. “Kumekuwa na changamoto nyingi ambazo imetubidi kukabiliana nazo katika kujenga mfumo wa kibunifu wa elimu Afrika ya kusini. Kutumia njia bunifu, za kiuweledi na za ziada katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yote tuliyokutana nayo, imetusaidia kuvipita vikwazo vingi.”


10. THABO KGATLHANYE NA REA NGWANE –Repurpose Schoolbags.
Thabo Kgatlhanye.
Thabo Kgatlhanye na Rea Ngwane walianzisha Repurpose Schoolbags kwa kurudisha tena upya kiwandani plastiki zilizokwishatumika na kuunda mabegi ya shule kwa ajili ya watoto waishio katika mazingira magumu. Mabegi hayo pia yana taa inayotumia umeme wa jua ambayo huwawezesha watoto kumalizia homework zao wakati wa usiku wanapokuwa hawana umeme.

SOMA: Njia 7 unazoweza kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako

“Kuwapata mashirika na watu binafsi wanaopenda kuchangia katika mradi wakilenga katika elimu ya watoto ndiyo kitu kilichotuwezesha sisi kugeuza wazo letu la mwanzo kuwa biashara endelevu ya kijamii inayowanufaisha watoto, kuajiri watu kutoka kwenye jamii na pia kuleta faida,” anaselezea Kgatlhanye.

Wajasiriamali hawa walitumia mashindano ya mawazo ya kuanzisha biashara ili kukusanya kiasi cha fedha za kuwasaidia kulitoa wazo lao chini. Mara tu walipokuwa katika hatua ya uzalishaji, wawekezaji walikuja kugonga mlango.

SOMO TUNALOPATA
“Kila mtu hufikiri unahitaji pesa kuanzisha biashara, jambo ambalo ni kweli, lakini tulithibitisha kwamba unaweza ukafanya mambo tofauti ukizingatia kwamba una msukumo wa kutosha na umejiandaa kufanya kazi kwa nguvu kuliko vile ambavyo ulidhania ingewezekana.” Alibainisha Ngwane.


MAKALA HII NA PICHA NI KWA HISANI YA JARIDA LA "ENTREPRENEUR MAGAZINE"

...........................................................................................

Ndugu msomaji ikiwa unapenda kujifunza maswala mbalimbali ya ujasiriamali kwa kina kabisa, basi jipatie vitabu mbalimbali kutoka kwetu. Vitabu hivyo ni hivi hapa chini;

1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.

Bei yake ni shilingi elfu 20 kitabu cha kawaida cha karatasi
Na shilingi elfu 10 softcopy kwa njia ya email.

2. SIRI YA MAFANIKIO: BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA



Bei ya kitabu cha kawaida cha karatasi ni shilingi elfu 10
Na kwa kitabu cha email au softcopy ni shilingi elfu 5

2. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA



Bei ya kitabu cha karatasi ni shilingi elfu 5
Na softcopy kwa njia ya email ni shilingi elfu 3

Pia tuna masomo ya semina kuhusiana na michanganuo ya biashara ambayo yanapatikana kwenye blogu hii MAALUMU YA MICHANGANUO. Kujiunga na masomo hayo ni shilingi elfu kumi pamoja na kupewa bure softcopy ya kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali.

Tunapatikana MBEZI KWA MSUGURI stendi ya daladala jirani na hospitali ya BOCHI,

Simu: 0712 202244  AU  0765 553030
Jina, Peter Augustino Tarimo

Kama upo mikoani na unataka vitabu vya karatasi, unaweza kumuagiza mtu anayefika Dar es salaam akakuchukulia, au tunaweza kutuma kwa njia ya Basi linalofika kule ulipo, lakini gharama za usafiri zitaongezeka kidogo.

Ukihitaji vitabu kwa njia ya e-mail ukiwa popote pale, tuma fedha pamoja na anuani yako ya email kwenye namba zetu hapo juu nasi tutakutumia kitabu/vitabu muda huohuo bila kuchelewa.  

0 Response to "SOMO:MAMILIONEA VIJANA 10 WAKISIMULIA SIRI ZA UTAJIRI WAO WALIVYOFANIKIWA "

Post a Comment