Wakati wa mdororo wa kiuchumi mtu wa mauzo
kwenye duka moja alipunguzwa kazi. Baada ya kutafuta kazi katika uchumi ambapo
kazi zilikuwa adimu, alichagua kuanzisha biashara yake mwenyewe. Alikuwa na
uzoefu kidogo wa utunzaji wa mahesabu ya biashara, alichukua kozi maalumu ya
uhasibu, akajizoesha mwenyewe mbinu za kisasa za utunzaji wa hesabu za biashara pamoja na vifaa vya ofisini.
Akianza na duka ambalo alikuwa akifanya kazi
zamani, alifanya mikataba na zaidi ya wafanyabiashara wadogo 100 kuwatunzia vitabu vyao kwa ada ya
chini kabisa ya mwezi. Wazo lake lilikuwa linatekelezeka kiasi kwamba kwa muda
mfupi tu aliona umuhimu wa kutengeneza ofisi inayohamishika katika gari jepesi
la kutolea huduma, ambalo aliweka vifaa vya kisasa vya ofisi.
Sasa alikuwa na msururu wa hizi ofisi za
utunzaji vitabu vya mahesabu
“zinazotembea” na kuajiri wafanyakazi wengi hivyo kuwapa wafanyabiashara
wadogo huduma za uhasibu za kiwango cha juu kwa gharama ya chini kabisa.
Ujuzi maalumu, pamoja na ubunifu vilikuwa ni
viungo vilivyowekwa katika biashara hii ya kipekee na yenye mafaikio. Mwaka
uliopita mmiliki wa biashara ile alilipa kodi ya mapato karibu mara kumi zaidi
ya kiasi alichokuwa akilipwa na mfanyabiashara aliyekuwa wakati mmoja akifanya
kazi kwake. Kupoteza kazi kulilazimisha taabu ya muda juu yake iliyothibitika
kuwa neema iliyojificha.
Mwanzo wa biashara hii yenye mafanikio
ilikuwa ni wazo, kwa kiasi kilekile
kama nilivyokuwa na upendeleo wa kumpa wazo muuzaji asiyekuwa na ajira, sasa
nachukulia upendeleo zaidi wa kupendekeza wazo jingine ambalo ndani yake lina
uwezekano wa hata mapato makubwa, pamoja na uwezekano wa kutoa huduma zenye
manufaa kwa maelfu ya watu wanaohitaji sana huduma hiyo.
Wazo lilipendekezwa kwa mtu wa mauzo ambaye
aliachana na kazi ya mauzo na kwenda kwenye biashara yakutunza vitabu vya hesabu
kwa jumla. Mpango ulipopendekezwa kama suluhisho la tatizo lake la ukosefu wa
ajira, mara moja alitoa mshangao, “Napenda wazo hilo lakini sijui jinsi ya
kuligeuza kuwa pesa”. Kwa maneno mengine alilalamika asingeweza kujua namna ya
kutafuta soko la utaalamu wake wa kutunza vitabu vya biashara baada ya kuupata.
Hivyo hilo liliibua tatizo jingine la
kutatua. Kwa msaada wa mwanamke kijana mjuzi wa maandishi ya mkono, na mwenye
kuweza kuweka habari pamoja, kitabu cha kuvutia sana kilitayarishwa kikielezea
faida za mfumo mpya wa kutunza vitabu vya hesabu.
Kurasa zilichapwa kwa unadhifu na kubandikwa
katika kitabu cha kawaida ambacho kilitumika kama zana ya kuuzia. Habari za
biashara hii mpya zilisambazwa vizuri kiasi kwamba mmiliki wake alipata vitabu
vingi kuliko vile alivyoweza kuvihudumia.
Maelfu ya watu wanahitaji huduma za mtaalamu
wa biashara mwenye uwezo wa kuandaa muhtasari wa kuvutia kwa ajili ya kutumia
katika kutafuta soko la huduma zao.
Akichochewa kutenda na mafanikio ya haraka ya
“mpango wake wa kwanza ulioandaliwa wa kutafuta soko la huduma”. Mwanamke huyu
mwenye bidii alihamia kwenye suluhisho la tatizo linalofanana kwa kijana wake
wa kiume ambaye ndiyo kwanza alikuwa ametoka kumaliza chuo lakini ambaye
alikuwa ameshindwa kabisa kutafuta soko la huduma zake. Mpango alioanzisha kwa
ajili ya matumizi yake ulikuwa ni mfano bora zaidi wa kutafuta soko la huduma
niliowahi kuona.
Kitabu cha mpango kilipokamilika, kilikuwa na
karibu kurasa 50 zilizochapwa vizuri kwa taarifa iliyopangwa kwa ustadi,
akielezea habari ya uwezo wa asili wa kijana wake, elimu, uzoefu binafsi na
aina nyingine nyingi za habari, ambazo nyingine ni ndefu mno kuzielezea. Kitabu
cha mpango pia kilibeba maelezo kamili ya nafasi kijana wake aliyotamani pamoja
na picha ya maneno ya mpango kamili ambao angeweza kutumia katika kujaza nafasi
hiyo.
Matayarisho ya kitabu cha mpango yalihitaji
kazi ya wiki kadhaa, muda ambao mtengenezaji wake alimpeleka kijana wake kwenye
maktaba ya umma karibu kila siku kupata taarifa zilizohitajika katika kuuza
huduma zake kwa faida nzuri zaidi. Alimtuma pia kwa washindani wote wa mwajiri
wake mtarajiwa na kukusanya kutoka kwao taarifa muhimu kuhusiana na njia zao za
kufanya biashara ambazo zilikuwa ni zenye thamani kubwa katika kuunda mpango
aliokusudia kuutumia katika kujaza nafasi aliyokuwa akiitafuta.
Wakati mpango ulipokuwa umekamilika, ulikuwa
umebeba zaidi ya nusu dazeni ya mapendekezo mazuri sana kwa matumizi na faida
ya mwajiri mtarajiwa, ambayo yangewekwa katika matumizi na kampuni baada ya
yeye kuajiriwa. Mtu anaweza akaamua kuuliza, “Kwanini upate shida yote hiyo
kutafuta kazi?” Jibu lipo wazi. Pia linavutia kwasababu linahusika na jambo
linalochukua sehemu ya janga la mamilioni ya wanaume na wanawake ambao chanzo
chao pekee cha kipato ni huduma zao.
Jibu ni, KUFANYA JAMBO VIZURI SIYO TATIZO!
MPANGO ULIOTAYARISHWA NA MAMA HUYU KWA MANUFAA YA KIJANA WAKE ULIMSAIDIA KUPATA KAZI ALIYOOMBA KATIKA
USAILI WA KWANZA, KWA MSHAHARA ALIOPANGA YEYE MWENYEWE.
Zaidi ya hapo,- na hili pia ni muhimu –
NAFASI HII HAIKUMTAKA KIJANA KUANZA CHINI. ALIANZA KAMA BOSI MDOGO KWA MSHAHARA
MKUBWA
“Kwanii kusumbuka kote huko?” Unajiuliza .
Vizuri, ni kwa kitu kimoja, wasilisho lililoandaliwa la maombi ya kazi ya
kijana huyu lilikata siyo chini ya miaka 10 ya muda ambao angelihitaji ili
kufikia pale alipoanzia ikiwa angeanzia kazi chini na kupanda juu.
Wazo hili la mtu kuanzia kazi chini na
kupanda juu linaweza kuonekana zuri, lakini kikwazo kikubwa kwako ni hiki-
wengi wa wale wanaoanzia chini kamwe hawawezi kuinua vichwa vyao juu kiasi cha
kutosha ili kuonekana na fursa. Hivyo
hubakia kuwa chini.
Ikumbukwe pia kwamba mtazamo kutoka chini siyo mzuri sana au wa kuvutia. Una tabia ya kuua malengo, tunaiita “kuingia kwenye mazoea”, maana yake tunakubali majaaliwa yetu kwasababu tumejenga mazoea ya desturi za kila siku, tabia ambayo mwishowe huja kuwa na nguvu kiasi ambacho tunashindwa kujaribu kuiacha. Na hiyo ni sababu nyingine kwanini inalipa mtu kuanza hatua moja au mbili kutoka chini. Kwa kufanya hivyo mtu hujenga tabia ya kuangalia, ya kuchunguza jinsi wengine wanavyosonga mbele, ya kuona fursa, na ya kuikumbatia pasipo kusita.
Ikumbukwe pia kwamba mtazamo kutoka chini siyo mzuri sana au wa kuvutia. Una tabia ya kuua malengo, tunaiita “kuingia kwenye mazoea”, maana yake tunakubali majaaliwa yetu kwasababu tumejenga mazoea ya desturi za kila siku, tabia ambayo mwishowe huja kuwa na nguvu kiasi ambacho tunashindwa kujaribu kuiacha. Na hiyo ni sababu nyingine kwanini inalipa mtu kuanza hatua moja au mbili kutoka chini. Kwa kufanya hivyo mtu hujenga tabia ya kuangalia, ya kuchunguza jinsi wengine wanavyosonga mbele, ya kuona fursa, na ya kuikumbatia pasipo kusita.
Dan Halpin ni mfano bora wa kile
ninachomaanisha. Wakati alipokuwa chuoni, alikuwa mwanafunzi, meneja wa timu
maarufu ya mpira wa miguu, Notre Dame katika mashindao ya Taifa hapo mwaka 1936 wakati ilipokuwa chini ya uongozi wa kocha mkubwa wa mpira wa miguu, Knute Rockne.
Pengine alivutiwa na Rockne kuweka malengo makubwa na siyo kufanya makosa ya kufeli kutokana na kushindwa kwa muda mfupi, ni kama tu ilivyokuwa kwa Andrew Carnegine kiongozi mkubwa kwenye viwanda
alivyowavutia wasaidizi wake kwenye biashara kuweka malengo makubwa.
Katika kiwango chochote, kijana Halpin
alimaliza chuo katika kipindi kilichokuwa kibaya sana, wakati mdororo wa uchumi
ulipokuwa umesababisha kazi kuadimika, hivyo baada ya kujaribu katika benki ya
uwekezaji na kampuni ya filamu alifuata uelekeo wa kwanza katika kazi aliyoweza
kupata – kuuza vifaa vya umeme vya kuwezesha kusikia kwa mtindo wa kamisheni.
Mtu yeyote angeweza kuanza na kazi ya aina
hiyo, na Halpin alilijua hilo, lakini ilikuwa inatosha kufungua mlango wa fursa
kwake. Kwa karibu miaka miwili aliendelea na kazi ambayo haikuwa chaguo lake,
na asingeweza kupanda juu ya hiyo kazi ikiwa asingefanya kitu kisichomridhisha.
Alilenga, kwanza kazi ya meneja mauzo msaidizi wa kampuni yake, na akaipata.
Hatua hiyo moja mbele ilimuweka juu vya kutosha kushinda watu wengine na
kumuwezesha kuona fursa kubwa bado. Kwa kuongezea ilimuweka mahali ambapo fursa ziliweza kumuona
Aliweka rekodi hiyo bora ya kuuza vifaa vya
kusikia kiasi kwamba, A.M. Andrews, mwenyekiti wa bodi ya kampuni nyingine shindani ya kutengeneza vifaa vya
kusikia(Dictograph products company) akagundua. Alitaka kufahamu kuhusiana na
huyu mtu ambaye alikuwa akiinyanganya mauzo makubwa kampuni ya Dictograph
iliyokuwa na uzoefu wa muda mrefu. Alimtumia Halpin aende. Mahojiano
yalipomalizika, Halpin alikuwa Meneja mauzo mpya wa wa kitengo cha vifaa vya
kusikia cha kampuni ya Dictograph.
Kisha, ili kujaribu ujasiri wa kijana Halpin,
Bwana Andrew alitoka kwenda Florida kwa muda wa miezi mitatu, alimuacha azame
au aogelee katika kazi yake mpya. Hakuzama. Roho ya Knute Rockne ya “Dunia yote
humpenda mshindi na haina muda na anayeshindwa” ilimtia moyo kujitahidi katika
kazi yake kiasi kwamba alichaguliwa kuwa Makamu Rais wa Kampuni na Meneja mkuu
wa kitengo cha vifaa vya kusikia na redio, kazi ambayo watu wengi wangejivunia
kuwa nayo kupitia miaka 10 ya jitihada za uaminifu. Halpin aligundua ujanja huo
chini ya miezi 6.
Ni vigumu kusema ikiwa Bwana Andrew au Bwana Halpin
ni nani anayestahili sifa, kwani wote walionyesha ushahidi wa kuwa na wingi wa
ile sifa adimu ijulikanayo kama ubunifu.
Bwana Andrews anastahili pongezi kwa kuona ndani ya kijana Halpin “jitihada” za
kiwango cha juu. Halpin anastahili sifa kwa kukataa kukubaliana na maisha kwa
kukubali na kuendelea na kazi asiyoipenda. Hiyo ni moja ya pointi kubwa
ninayojaribu kusisitiza kupitia filosofia hii nzima – kwamba tunapanda kwenye
nafasi za juu au kubakia chini kwa sababu
ya hali tunazoweza kuzithibiti ikiwa tutapenda kuzithibiti.
Napenda pia kusisitiza pointi nyingine,
inayosema kwamba, vyote mafanikio na maanguko kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya tabia!. Sina shaka yeyote kwamba
uhusiano wa karibu wa Dan Halpin na kocha mashuhuri zaidi wa mpira wa miguu
Marekani iliyepata kumjua ulipandikiza ndani ya akili yake chapa ileile ya shauku ya kufanikiwa iliyoifanya timu ya
mpira wa miguu Notre Dame kuwa mashuhuri duniani. Ukweli, kuna kitu fulani
kwenye wazo kwamba kuwaheshimu Mashujaa husaidia, ikizingatiwa kwamba mtu
anamheshimu mshindi. Halpin
ananiambia kwamba Rockne alikuwa mmoja kati ya viongozi wakubwa zaidi wa watu
duniani katika historia yote.
Imani yangu katika nadharia kwamba ushirika
katika biashara ni vigezo muhimu, kote katika kuanguka na katika kufanikiwa
ilithibitika wakati kijana wangu Blair alipokuwa akipatana na Dan Halpin kwa
nafasi ya kazi. Bwana Halpin alimuahidi mshahara wa kuanzia unaofikia nusu ya
kiasi ambacho angeliweza kupata kutoka katika kampuni shindani. Niliweka
msukumo kama mzazi ili kukubali, na kumshawishi akubali nafasi kwa Bwana Halpin
kwasababu naamini kwamba kuwa na ushirikiano wa karibu na mtu anayekataa
kukubaliana na mazingira asiyoyapenda ni rasiilimali isiyoweza kupimika kwa
kipimo ch fedha.
Chini panakinaisha, panachosha, ni mahali
pasipokuwa na faida kwa mtu yeyote. Ndiyo sababu nimechukua muda kuelezea jinsi
mipango stahiki inavyoweza kuzuia mwanzo duni. Pia ndiyo maana nafasi kubwa
kiasi hicho imetengwa kwa ajili ya maelezo ya hii taaluma mpya iliyotengenezwa
na mwanamke aliyehamasika kufanya kazi nzuri ya kupanga kwa sababu alitaka kijana wake kuwa na kazi yenye maslahi
mazuri.
Wakati uchumi unapokuwa chini na kazi kuwa
adimu, njia mpya na nzuri ya kutafuta soko la huduma zetu inahitajika. Ni
vigumu kutambua kwanini hapo kabla mtu hakugundua mahitaji hayo makubwa, katika
mtazamo wa ukweli kwamba pesa nyingi zaidi hubadilishana mikono kwa malipo ya huduma kuliko kwa lengo
jingine lolote. Kiasi kinacholipwa kwa mwezi kwa watu wanaofanya kazi za
mshahara na vibarua ni kikubwa kiasi kwamba kinafikia mamia ya mamilioni na
usambazaji kwa mwaka kiasi cha mabilioni.
Labda baadhi watakuta, katika wazo hapa lililoelezwa kwa kifupi kiini
cha utajiri wanao utamani!. Mawazo
yaliyokuwa na sifa ya chini zaidi yamekuwa ndiyo mbegu utajiri mkubwa unapomea.
Wazo la Woolworth la duka la “Five and
Ten Cents”, kwa mfano halikuwa na thamani kubwa, lakini liliweza kumlimbikizia
utajiri mwanzilishi wake.
Wale wanaoona fursa iliyokuwepo katika pendekezo hili watapata msaada wenye
manufaa katika sura inayohusu mipango madhubuti. Kwa kawaida mtafutaji masoko
wa huduma mwenye ufanisi anaweza kutafuta mahitaji yanayokua kwa huduma zake
popote pale penye wanaume na wanawake wanaotafuta masoko mazuri kwa ajili ya
huduma zao. Kwa kutumia kanuni ya ushirika wa kusaidiana(Mastermind Principles)
watu wachache wenye vipaji vinavyofaa wanaweza wakatengeneza umoja, na kuwa na biashara inayolipa haraka
sana.
Mmoja anaweza akahitaji kuwa mwandishi mzuri
mwenye kipaji cha kufanya matangazo na kuuza, mwingine katika kubuni michoro na
mwingine anatakiwa kuwa mfanyabiashara wa daraja la kwanza ambaye ataweza
kuifanya dunia ifahamu kuhusiana na huduma hiyo. Ikiwa mtu mmoja anazo sifa
zote hizi, basi anaweza akaendesha biashara mwenyewe mpaka itakapokuwa kubwa
sana kwa mtu mmoja kuimudu.
Mwanamke aliyetayarisha mpango wa mauzo kwa
ajili ya mwanaye alipokea maombi kutoka sehemu zote za nchi kwa ajili ya
ushirikiano wake katika kuandaa mipango inayofanana kwa wengine ambao
walitamani kutafuta soko la huduma zao ili kupata pesa zaidi. Mwishowe
alisimamia wafanyakazi waliokuwa na ujuzi wa kutaipu, wasanii na waandishi
waliokuwa na uwezo wa kutia chumvi jambo kikamilifu kiasi kwamba biashara ya
mtu ingeliweza kuuzwa kwa fedha nyingi zaidi kuliko mishahara iliyopo katika
biashara kama hizo. Alikuwa anauamini uwezo wake kiasi kwamba alikubali sehemu
kubwa ya ada aliyolipwa itokane na asilimia ya ongezeko lililotokana na mapato
aliyowasaidia wateja wake kupata.
Ni lazima isichukuliwe kwamba mpango wake
ulijumuisha tu kuuza kwa werevu ambapo aliwasaidia wanaume na wanawake kudai na
kupata fedha nyingi kwa hu4duma zilezile ambazo mwanzoni ziliuzwa kwa fedha
kidogo. Aliangalia maslahi ya wanunuzi kama alivyoangalia ya wauzaji wa huduma,
na hivyo kuandaa mipango yake ambapo mwajiri angeweza kupata thamani nzima kwa
malipo ya ziada aliyoyatoa.
Njia ambayo alikamilisha matokeo haya ya
kushangaza, ni siri ya kitaaluma ambayo hakumwambia mtu yeyote isipokuwa wateja
wake. Ikiwa unao ubunifu na unatafuta njia yenye faida zaidi kwa ajili ya kuuza
huduma zako, pendekezo hili linaweza kuwa kichocheo ambacho umekuwa ukikitafuta.
Wazo hili linao uwezo wa kuzalisha
mapato makubwa zaidi kushinda yale ya daktari wa “kawaida”, mwanasheria au
mhandisi ambaye elimu yake ilihitaji miaka kadhaa chuoni. Wazo linauzika kwa
wale wanaotafuta nafasi mpya katika karibu nafasi zote za kazi za utendaji au
uwezo wa usimamiaji, na wale wanaotamani kurekebisha vipato vyao katika nafasi
walizokuwepo sasa.
Hakuna bei moja kwa mawazo mazuri!
Kinachoyapa nguvu mawazo yote ni ujuzi maalumu. Kwa wale wasiopata utajiri
mwingi, ujuzi maalumu upo mwingi na unaweza kupatikana kirahisi kuliko mawazo.
Kutokana na ukweli huu, yapo mahitaji ya pamoja na fursa inayoongezeka daima
kwa mtu aliyekuwa na uwezo wa kuwasaidia wanaume na wanawake kuuza huduma zao
kwa faida. Uwezo maana yake ni ubunifu, sifa moja inayohitajika kuunganisha
ujuzi maalumu na mawazo katika hali ya mipango madhubuti iliyotengenezwa kuleta
utajiri.
Ikiwa unao ubunifu, sura hii inaweza kukupa
wazo linalotosha kuwa kama chanzo cha utajiri unaoutamani. Kumbuka wazo ndiyo
kitu muhimu, ujuzi maalumu unaweza ukapatikana tu mahali – mahali popote.
Na huo mpenzi msomaji ndio mwisho wa Sura ye 5 ya kitabu Fikiri Utajirike, Usikose sehe ya kwanza ya Sura ya 6.
0 Response to "UCHUMI UKISHUKA NA AJIRA KUWA ADIMU,UBUNIFU WA SOKO LA BIASHARA ZETU UNAHITAJIKA"
Post a Comment