UCHUMI UKISHUKA NA AJIRA KUWA ADIMU,UBUNIFU WA SOKO LA BIASHARA ZETU UNAHITAJIKA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UCHUMI UKISHUKA NA AJIRA KUWA ADIMU,UBUNIFU WA SOKO LA BIASHARA ZETU UNAHITAJIKA

Wakati wa mdororo wa kiuchumi mtu wa mauzo kwenye duka moja alipunguzwa kazi. Baada ya kutafuta kazi katika uchumi ambapo kazi zilikuwa adimu, alichagua kuanzisha biashara yake mwenyewe. Alikuwa na uzoefu kidogo wa utunzaji wa mahesabu ya biashara, alichukua kozi maalumu ya uhasibu, akajizoesha mwenyewe mbinu za kisasa za utunzaji wa hesabu za biashara  pamoja na vifaa vya ofisini. 

Akianza na duka ambalo alikuwa akifanya kazi zamani, alifanya mikataba na zaidi ya wafanyabiashara  wadogo 100 kuwatunzia vitabu vyao kwa ada ya chini kabisa ya mwezi. Wazo lake lilikuwa linatekelezeka kiasi kwamba kwa muda mfupi tu aliona umuhimu wa kutengeneza ofisi inayohamishika katika gari jepesi la kutolea huduma, ambalo aliweka vifaa vya kisasa vya ofisi.

Sasa alikuwa na msururu wa hizi ofisi za utunzaji vitabu vya mahesabu  “zinazotembea” na kuajiri wafanyakazi wengi hivyo kuwapa wafanyabiashara wadogo huduma za uhasibu za kiwango cha juu kwa gharama ya chini kabisa.

Ujuzi maalumu, pamoja na ubunifu vilikuwa ni viungo vilivyowekwa katika biashara hii ya kipekee na yenye mafaikio. Mwaka uliopita mmiliki wa biashara ile alilipa kodi ya mapato karibu mara kumi zaidi ya kiasi alichokuwa akilipwa na mfanyabiashara aliyekuwa wakati mmoja akifanya kazi kwake. Kupoteza kazi kulilazimisha taabu ya muda juu yake iliyothibitika kuwa neema iliyojificha.

Mwanzo wa biashara hii yenye mafanikio ilikuwa ni wazo, kwa kiasi kilekile kama nilivyokuwa na upendeleo wa kumpa wazo muuzaji asiyekuwa na ajira, sasa nachukulia upendeleo zaidi wa kupendekeza wazo jingine ambalo ndani yake lina uwezekano wa hata mapato makubwa, pamoja na uwezekano wa kutoa huduma zenye manufaa kwa maelfu ya watu wanaohitaji sana huduma hiyo.

Wazo lilipendekezwa kwa mtu wa mauzo ambaye aliachana na kazi ya mauzo na kwenda kwenye biashara yakutunza vitabu vya hesabu kwa jumla. Mpango ulipopendekezwa kama suluhisho la tatizo lake la ukosefu wa ajira, mara moja alitoa mshangao, “Napenda wazo hilo lakini sijui jinsi ya kuligeuza kuwa pesa”. Kwa maneno mengine alilalamika asingeweza kujua namna ya kutafuta soko la utaalamu wake wa kutunza vitabu vya biashara baada ya kuupata.

Hivyo hilo liliibua tatizo jingine la kutatua. Kwa msaada wa mwanamke kijana mjuzi wa maandishi ya mkono, na mwenye kuweza kuweka habari pamoja, kitabu cha kuvutia sana kilitayarishwa kikielezea faida za mfumo mpya wa kutunza vitabu vya hesabu.

Kurasa zilichapwa kwa unadhifu na kubandikwa katika kitabu cha kawaida ambacho kilitumika kama zana ya kuuzia. Habari za biashara hii mpya zilisambazwa vizuri kiasi kwamba mmiliki wake alipata vitabu vingi kuliko vile alivyoweza kuvihudumia.

Maelfu ya watu wanahitaji huduma za mtaalamu wa biashara mwenye uwezo wa kuandaa muhtasari wa kuvutia kwa ajili ya kutumia katika kutafuta soko la huduma zao.

Akichochewa kutenda na mafanikio ya haraka ya “mpango wake wa kwanza ulioandaliwa wa kutafuta soko la huduma”. Mwanamke huyu mwenye bidii alihamia kwenye suluhisho la tatizo linalofanana kwa kijana wake wa kiume ambaye ndiyo kwanza alikuwa ametoka kumaliza chuo lakini ambaye alikuwa ameshindwa kabisa kutafuta soko la huduma zake. Mpango alioanzisha kwa ajili ya matumizi yake ulikuwa ni mfano bora zaidi wa kutafuta soko la huduma niliowahi kuona.

Kitabu cha mpango kilipokamilika, kilikuwa na karibu kurasa 50 zilizochapwa vizuri kwa taarifa iliyopangwa kwa ustadi, akielezea habari ya uwezo wa asili wa kijana wake, elimu, uzoefu binafsi na aina nyingine nyingi za habari, ambazo nyingine ni ndefu mno kuzielezea. Kitabu cha mpango pia kilibeba maelezo kamili ya nafasi kijana wake aliyotamani pamoja na picha ya maneno ya mpango kamili ambao angeweza kutumia katika kujaza nafasi hiyo.

Matayarisho ya kitabu cha mpango yalihitaji kazi ya wiki kadhaa, muda ambao mtengenezaji wake alimpeleka kijana wake kwenye maktaba ya umma karibu kila siku kupata taarifa zilizohitajika katika kuuza huduma zake kwa faida nzuri zaidi. Alimtuma pia kwa washindani wote wa mwajiri wake mtarajiwa na kukusanya kutoka kwao taarifa muhimu kuhusiana na njia zao za kufanya biashara ambazo zilikuwa ni zenye thamani kubwa katika kuunda mpango aliokusudia kuutumia katika kujaza nafasi aliyokuwa akiitafuta.

Wakati mpango ulipokuwa umekamilika, ulikuwa umebeba zaidi ya nusu dazeni ya mapendekezo mazuri sana kwa matumizi na faida ya mwajiri mtarajiwa, ambayo yangewekwa katika matumizi na kampuni baada ya yeye kuajiriwa. Mtu anaweza akaamua kuuliza, “Kwanini upate shida yote hiyo kutafuta kazi?” Jibu lipo wazi. Pia linavutia kwasababu linahusika na jambo linalochukua sehemu ya janga la mamilioni ya wanaume na wanawake ambao chanzo chao pekee cha kipato ni huduma zao.

Jibu ni, KUFANYA JAMBO VIZURI SIYO TATIZO! MPANGO ULIOTAYARISHWA NA MAMA HUYU KWA MANUFAA YA KIJANA WAKE  ULIMSAIDIA KUPATA KAZI ALIYOOMBA KATIKA USAILI WA KWANZA, KWA MSHAHARA ALIOPANGA YEYE MWENYEWE.

Zaidi ya hapo,- na hili pia ni muhimu – NAFASI HII HAIKUMTAKA KIJANA KUANZA CHINI. ALIANZA KAMA BOSI MDOGO KWA MSHAHARA MKUBWA

“Kwanii kusumbuka kote huko?” Unajiuliza . Vizuri, ni kwa kitu kimoja, wasilisho lililoandaliwa la maombi ya kazi ya kijana huyu lilikata siyo chini ya miaka 10 ya muda ambao angelihitaji ili kufikia pale alipoanzia ikiwa angeanzia kazi chini na kupanda juu.

Wazo hili la mtu kuanzia kazi chini na kupanda juu linaweza kuonekana zuri, lakini kikwazo kikubwa kwako ni hiki- wengi wa wale wanaoanzia chini kamwe hawawezi kuinua vichwa vyao juu kiasi cha kutosha ili kuonekana na fursa. Hivyo hubakia kuwa chini. 

Ikumbukwe pia kwamba mtazamo kutoka chini siyo mzuri sana au wa kuvutia. Una tabia ya kuua malengo, tunaiita “kuingia kwenye mazoea”, maana yake tunakubali majaaliwa yetu kwasababu tumejenga mazoea ya desturi za kila siku, tabia ambayo mwishowe huja kuwa na nguvu kiasi ambacho tunashindwa kujaribu kuiacha. Na hiyo ni sababu nyingine kwanini inalipa mtu kuanza hatua moja au mbili kutoka chini. Kwa kufanya hivyo mtu hujenga tabia ya kuangalia, ya kuchunguza jinsi wengine wanavyosonga mbele, ya kuona fursa, na ya kuikumbatia pasipo kusita.

Dan Halpin ni mfano bora wa kile ninachomaanisha. Wakati alipokuwa chuoni, alikuwa mwanafunzi, meneja wa timu maarufu ya mpira wa miguu, Notre Dame katika mashindao ya Taifa hapo mwaka 1936 wakati ilipokuwa chini ya uongozi wa kocha mkubwa wa mpira wa miguu, Knute Rockne. Pengine alivutiwa na Rockne kuweka malengo makubwa na siyo kufanya makosa ya kufeli kutokana na kushindwa kwa muda mfupi, ni kama tu ilivyokuwa kwa Andrew Carnegine kiongozi mkubwa kwenye viwanda alivyowavutia wasaidizi wake kwenye biashara kuweka malengo makubwa.

Katika kiwango chochote, kijana Halpin alimaliza chuo katika kipindi kilichokuwa kibaya sana, wakati mdororo wa uchumi ulipokuwa umesababisha kazi kuadimika, hivyo baada ya kujaribu katika benki ya uwekezaji na kampuni ya filamu alifuata uelekeo wa kwanza katika kazi aliyoweza kupata – kuuza vifaa vya umeme vya kuwezesha kusikia kwa mtindo wa kamisheni.

Mtu yeyote angeweza kuanza na kazi ya aina hiyo, na Halpin alilijua hilo, lakini ilikuwa inatosha kufungua mlango wa fursa kwake. Kwa karibu miaka miwili aliendelea na kazi ambayo haikuwa chaguo lake, na asingeweza kupanda juu ya hiyo kazi ikiwa asingefanya kitu kisichomridhisha. Alilenga, kwanza kazi ya meneja mauzo msaidizi wa kampuni yake, na akaipata. Hatua hiyo moja mbele ilimuweka juu vya kutosha kushinda watu wengine na kumuwezesha kuona fursa kubwa bado. Kwa kuongezea ilimuweka mahali ambapo fursa ziliweza kumuona  

Aliweka rekodi hiyo bora ya kuuza vifaa vya kusikia kiasi kwamba, A.M. Andrews, mwenyekiti wa bodi ya kampuni  nyingine shindani ya kutengeneza vifaa vya kusikia(Dictograph products company) akagundua. Alitaka kufahamu kuhusiana na huyu mtu ambaye alikuwa akiinyanganya mauzo makubwa kampuni ya Dictograph iliyokuwa na uzoefu wa muda mrefu. Alimtumia Halpin aende. Mahojiano yalipomalizika, Halpin alikuwa Meneja mauzo mpya wa wa kitengo cha vifaa vya kusikia  cha kampuni ya Dictograph.

Kisha, ili kujaribu ujasiri wa kijana Halpin, Bwana Andrew alitoka kwenda Florida kwa muda wa miezi mitatu, alimuacha azame au aogelee katika kazi yake mpya. Hakuzama. Roho ya Knute Rockne ya “Dunia yote humpenda mshindi na haina muda na anayeshindwa” ilimtia moyo kujitahidi katika kazi yake kiasi kwamba alichaguliwa kuwa Makamu Rais wa Kampuni na Meneja mkuu wa kitengo cha vifaa vya kusikia na redio, kazi ambayo watu wengi wangejivunia kuwa nayo kupitia miaka 10 ya jitihada za uaminifu. Halpin aligundua ujanja huo chini ya miezi 6.

Ni vigumu kusema ikiwa Bwana Andrew au Bwana Halpin ni nani anayestahili sifa, kwani wote walionyesha ushahidi wa kuwa na wingi wa ile sifa adimu ijulikanayo kama ubunifu. Bwana Andrews anastahili pongezi kwa kuona ndani ya kijana Halpin “jitihada” za kiwango cha juu. Halpin anastahili sifa kwa kukataa kukubaliana na maisha kwa kukubali na kuendelea na kazi asiyoipenda. Hiyo ni moja ya pointi kubwa ninayojaribu kusisitiza kupitia filosofia hii nzima – kwamba tunapanda kwenye nafasi za juu au kubakia chini kwa sababu ya hali tunazoweza kuzithibiti ikiwa tutapenda kuzithibiti.

Napenda pia kusisitiza pointi nyingine, inayosema kwamba, vyote mafanikio na maanguko kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya tabia!. Sina shaka yeyote kwamba uhusiano wa karibu wa Dan Halpin na kocha mashuhuri zaidi wa mpira wa miguu Marekani iliyepata kumjua ulipandikiza ndani ya akili yake chapa ileile ya shauku ya kufanikiwa iliyoifanya timu ya mpira wa miguu Notre Dame kuwa mashuhuri duniani. Ukweli, kuna kitu fulani kwenye wazo kwamba kuwaheshimu Mashujaa husaidia, ikizingatiwa kwamba mtu anamheshimu mshindi. Halpin ananiambia kwamba Rockne alikuwa mmoja kati ya viongozi wakubwa zaidi wa watu duniani katika historia yote.

Imani yangu katika nadharia kwamba ushirika katika biashara ni vigezo muhimu, kote katika kuanguka na katika kufanikiwa ilithibitika wakati kijana wangu Blair alipokuwa akipatana na Dan Halpin kwa nafasi ya kazi. Bwana Halpin alimuahidi mshahara wa kuanzia unaofikia nusu ya kiasi ambacho angeliweza kupata kutoka katika kampuni shindani. Niliweka msukumo kama mzazi ili kukubali, na kumshawishi akubali nafasi kwa Bwana Halpin kwasababu naamini kwamba kuwa na ushirikiano wa karibu na mtu anayekataa kukubaliana na mazingira asiyoyapenda ni rasiilimali isiyoweza kupimika kwa kipimo ch fedha.

Chini panakinaisha, panachosha, ni mahali pasipokuwa na faida kwa mtu yeyote. Ndiyo sababu nimechukua muda kuelezea jinsi mipango stahiki inavyoweza kuzuia mwanzo duni. Pia ndiyo maana nafasi kubwa kiasi hicho imetengwa kwa ajili ya maelezo ya hii taaluma mpya iliyotengenezwa na mwanamke aliyehamasika kufanya kazi nzuri ya kupanga kwa sababu alitaka kijana wake kuwa na kazi yenye maslahi mazuri.

Wakati uchumi unapokuwa chini na kazi kuwa adimu, njia mpya na nzuri ya kutafuta soko la huduma zetu inahitajika. Ni vigumu kutambua kwanini hapo kabla mtu hakugundua mahitaji hayo makubwa, katika mtazamo wa ukweli kwamba pesa nyingi zaidi hubadilishana  mikono kwa malipo ya huduma kuliko kwa lengo jingine lolote. Kiasi kinacholipwa kwa mwezi kwa watu wanaofanya kazi za mshahara na vibarua ni kikubwa kiasi kwamba kinafikia mamia ya mamilioni na usambazaji kwa mwaka kiasi cha mabilioni.

Labda baadhi watakuta, katika wazo hapa lililoelezwa kwa kifupi kiini cha utajiri wanao utamani!. Mawazo yaliyokuwa na sifa ya chini zaidi yamekuwa ndiyo mbegu utajiri mkubwa unapomea. Wazo la Woolworth la duka la  “Five and Ten Cents”, kwa mfano halikuwa na thamani kubwa, lakini liliweza kumlimbikizia utajiri mwanzilishi wake.

Wale wanaoona fursa iliyokuwepo katika pendekezo hili watapata msaada wenye manufaa katika sura inayohusu mipango madhubuti. Kwa kawaida mtafutaji masoko wa huduma mwenye ufanisi anaweza kutafuta mahitaji yanayokua kwa huduma zake popote pale penye wanaume na wanawake wanaotafuta masoko mazuri kwa ajili ya huduma zao. Kwa kutumia kanuni ya ushirika wa kusaidiana(Mastermind Principles) watu wachache wenye vipaji vinavyofaa wanaweza wakatengeneza  umoja, na kuwa na biashara inayolipa haraka sana.

Mmoja anaweza akahitaji kuwa mwandishi mzuri mwenye kipaji cha kufanya matangazo na kuuza, mwingine katika kubuni michoro na mwingine anatakiwa kuwa mfanyabiashara wa daraja la kwanza ambaye ataweza kuifanya dunia ifahamu kuhusiana na huduma hiyo. Ikiwa mtu mmoja anazo sifa zote hizi, basi anaweza akaendesha biashara mwenyewe mpaka itakapokuwa kubwa sana kwa mtu mmoja kuimudu.

Mwanamke aliyetayarisha mpango wa mauzo kwa ajili ya mwanaye alipokea maombi kutoka sehemu zote za nchi kwa ajili ya ushirikiano wake katika kuandaa mipango inayofanana kwa wengine ambao walitamani kutafuta soko la huduma zao ili kupata pesa zaidi. Mwishowe alisimamia wafanyakazi waliokuwa na ujuzi wa kutaipu, wasanii na waandishi waliokuwa na uwezo wa kutia chumvi jambo kikamilifu kiasi kwamba biashara ya mtu ingeliweza kuuzwa kwa fedha nyingi zaidi kuliko mishahara iliyopo katika biashara kama hizo. Alikuwa anauamini uwezo wake kiasi kwamba alikubali sehemu kubwa ya ada aliyolipwa itokane na asilimia ya ongezeko lililotokana na mapato aliyowasaidia wateja wake kupata.

Ni lazima isichukuliwe kwamba mpango wake ulijumuisha tu kuuza kwa werevu ambapo aliwasaidia wanaume na wanawake kudai na kupata fedha nyingi kwa hu4duma zilezile ambazo mwanzoni ziliuzwa kwa fedha kidogo. Aliangalia maslahi ya wanunuzi kama alivyoangalia ya wauzaji wa huduma, na hivyo kuandaa mipango yake ambapo mwajiri angeweza kupata thamani nzima kwa malipo ya ziada aliyoyatoa.

Njia ambayo alikamilisha matokeo haya ya kushangaza, ni siri ya kitaaluma ambayo hakumwambia mtu yeyote isipokuwa wateja wake. Ikiwa unao ubunifu na unatafuta njia yenye faida zaidi kwa ajili ya kuuza huduma zako, pendekezo hili linaweza kuwa kichocheo ambacho umekuwa ukikitafuta. Wazo hili linao uwezo wa kuzalisha mapato makubwa zaidi kushinda yale ya daktari wa “kawaida”, mwanasheria au mhandisi ambaye elimu yake ilihitaji miaka kadhaa chuoni. Wazo linauzika kwa wale wanaotafuta nafasi mpya katika karibu nafasi zote za kazi za utendaji au uwezo wa usimamiaji, na wale wanaotamani kurekebisha vipato vyao katika nafasi walizokuwepo sasa.

Hakuna bei moja kwa mawazo mazuri! Kinachoyapa nguvu mawazo yote ni ujuzi maalumu. Kwa wale wasiopata utajiri mwingi, ujuzi maalumu upo mwingi na unaweza kupatikana kirahisi kuliko mawazo. Kutokana na ukweli huu, yapo mahitaji ya pamoja na fursa inayoongezeka daima kwa mtu aliyekuwa na uwezo wa kuwasaidia wanaume na wanawake kuuza huduma zao kwa faida. Uwezo maana yake ni ubunifu, sifa moja inayohitajika kuunganisha ujuzi maalumu na mawazo katika hali ya mipango madhubuti iliyotengenezwa kuleta utajiri.


Ikiwa unao ubunifu, sura hii inaweza kukupa wazo linalotosha kuwa kama chanzo cha utajiri unaoutamani. Kumbuka wazo ndiyo kitu muhimu, ujuzi maalumu unaweza ukapatikana tu mahali – mahali popote.


Na huo mpenzi msomaji ndio mwisho wa Sura ye 5 ya kitabu Fikiri Utajirike, Usikose sehe ya kwanza ya Sura ya 6.












0 Response to "UCHUMI UKISHUKA NA AJIRA KUWA ADIMU,UBUNIFU WA SOKO LA BIASHARA ZETU UNAHITAJIKA"

Post a Comment