Katika ulimwengu wa kazi, ajira na biashara kitu hiki makubaliano ni swala nyeti sana. Na makubaliano au mkataba hutumika katika kila nyanja ya ujasiriamali na biashara duniani kama ilivyoonyeshwa pia katika makala nyingine ya hivi karibuni iliyosema, jinsi ya kuuza wazo lako la biashara au ubunifu kwa wawekezaji na watu wengine.
Kwa kifupi kabisa makubaliano yana maanisha mapatano
baina ya pande mbili tofauti kila upande
ukiwa na matakwa yake(Malengo). Na katika makubaliano hayo kila upande kabla
haujaja mezani inatakiwa kwanza kujiandaa kwa kujua ni vitu au malengo gani
unaoyahitaji. Mfano mzuri sana ni pale mtu anapokwenda kuomba ajira.
Wote mwajiri na mwajiriwa kila mmoja anamhitaji mwenzake
na huo ndiyo msingi hasa wa kusema kwamba kila mmoja anatakiwa kujua ni kitu
gani anachokihitaji kutoka kwa mwenzake na matakwa hayo ni sharti yawekwe wazi
wakati wa makubaliano au mkataba ikiezekana hata kwa maandishi.
Huwezi tu kwenda na kusema kwa mfano, “natafuta kazi ya
hoteli” halafu ukishaambiwa “njoo uanze kesho” kesho yake unaibuka kuja kuanza
kazi pasipo hata kwanza kuweka wazi unataka nini kwenye hiyo kazi. Ni kweli
nafasi za kazi Tanzania siku hizi ni dili lakini isije ikawa ni kwa gharama za kutokukupata
hata kile unachostahili. Unapodai mkataba, wengine watakukebehi, “kazi bongo…toka
lini bongo kukawa na kazi, hapa ni kibarua tu..…kazi labda serikalini kwa wenye
madigirii”
Kutokuweka wazi matakwa ya kila mmoja kabla ya ajira
husababisha matatizo makubwa baina ya waajiri na waajiriwa, siyo ajira rasmi tu
bali hata unapoangalia katika zile ajira zisizokuwa rasmi kama vile kazi za
ndani, ajira ndogo ndogo katika biashara za watu binafsi na katika makampuni
madogomadogo yasiyokuwa rasmi. Utakuta mwajiri anakubaliana tu juu juu na
mfanyakazi na kwa kuwa mwajiriwa mwenyewe yeye ana shida na kazi amekaa muda
mrefu bila ya kuipata sasa anashindwa kusisitiza kile anachokitaka katika
makubaliano hayo.
Matokeo yake mbele ya safari, kunakuja kuibuka
sintofahamu au mgogoro mkubwa. Yule mfanyakazi anashindwa kumudu mahitaji yake
kutokana na maslahi ya kazi yenyewe kuwa duni. Anaanza kufanya hujuma
mbalimbali kama udokozi, uvivu na kukosa morali wa kazi huku akiwaza ni vipi
atamudu kuitunza pengine familia yake au hata yeye mwenyewe maisha yake hatima
yake itakuwaje huko mbele.
Shilingi ina pande mbili kichwa na mwenge, hali kadhalika na kwenye makubaliano ya pande mbili mfano ajira kama tulivyotangulia kusema, mwajiri naye ana matakwa yake ambayo ni lazima anapoingia kwenye meza ya makubaliano atataka yawekwe wazi. Mwajiri naye kama alivyokuwa mwajiriwa au mfanyakazi asipofahamu ni kitu gani anachokitaka kutoka kwa yule anayetaka kumpa kazi basi ujue baadaye yataibuka matatizo. mwajiriwa anaweza kuja kuhisi anaonewa kwa kupewa majukumu ambayo tokea mwanzoni hayakuwekwa wazi. Weka mezani kila kitu unachotarajia yule unayetaka kumpa kazi aje afanye kabla ya mkataba kusudi na yeye aweze kulinganisha ikiwa vitaoana na kile anachokitaka kutoka kwako.
Shilingi ina pande mbili kichwa na mwenge, hali kadhalika na kwenye makubaliano ya pande mbili mfano ajira kama tulivyotangulia kusema, mwajiri naye ana matakwa yake ambayo ni lazima anapoingia kwenye meza ya makubaliano atataka yawekwe wazi. Mwajiri naye kama alivyokuwa mwajiriwa au mfanyakazi asipofahamu ni kitu gani anachokitaka kutoka kwa yule anayetaka kumpa kazi basi ujue baadaye yataibuka matatizo. mwajiriwa anaweza kuja kuhisi anaonewa kwa kupewa majukumu ambayo tokea mwanzoni hayakuwekwa wazi. Weka mezani kila kitu unachotarajia yule unayetaka kumpa kazi aje afanye kabla ya mkataba kusudi na yeye aweze kulinganisha ikiwa vitaoana na kile anachokitaka kutoka kwako.
Hata katika makubaliano baina ya ndugu wawili kwa mfano
mtu na kaka, mtu na dada yake, mjomba, shangazi nk. Usije ukakubali kuingia
katika mkataba wa jambo lolote lile bila kwanza kujua kila mmoja, upande
unahitaji kitu gani. Mmepeana kazi basi mapema kabisa, mwambie, “Mjomba, kaka,
shangazi, mimi nitapata nini baada ya kukutimizia kazi hii?” Kumbuka hakuna
kazi yeyote ile isiyokuwa na malipo duniani. Hata ikiwa ni chakula, basi
mwanzoni kabisa ijulikane bayana kuwa wewe malipo yako ni ‘msosi’ utakaokuwa
ukila pale kwa baba mdogo au shangazi. Vinginevyo ni kuja kulaumiana baadaye au
undugu kufa pasipokuwa na sababu zozote za msingi.
Usipoweka wazi kile unachokitaka mapema ukachukulia tu
upande wa pili utajua wenyewe ni makosa makubwa. Upande huo baadaye utajiona
kuwa wewe ndiye unayenufaika zaidi ili hali hata kumbe siyo hivyo ni kinyume
chake, kwa mfano unakaa kwa mjomba na pale unasaidia kazi zote za pale nyumbani
huku na wewe ukiwa unapata milo yote ya siku kama watoto wa mjomba. Ikifika
siku ukaumwa labda malaria, mjomba anaweza kujisikia ugumu wa kukupa hela ya
matibabu kwa kuwa hamkukubaliana toka mwanzo afanye hivyo, na isitoshe anaweza
akaona kama vile ni mzigo kwake kwakuwa tena unakula pale kwake kila siku.
Hawezi kufikiria na wewe unatoa mchango mkubwa katika kazi za pale nyumbani
hata pengine kuwazidi watoto wake mwenyewe.
Mifano ipo mingi karibu kila mahali katika jamii zetu
tunamoishi. Makubaliano hata ikiwa siyo ya kuandikiana kwenye karatasi, hata ya
mdomo yanasaidia. Kikubwa ni kila upande kujua ni nini hasa unachokitaka katika
makubaliano hayo.
......................................................................................
Kwa vitabu bora kabisa vya Ujasiriamali, Biashara na Maendeleo binafsi pata vitabu hivi hapa chini;
......................................................................................
Kwa vitabu bora kabisa vya Ujasiriamali, Biashara na Maendeleo binafsi pata vitabu hivi hapa chini;
Tuwasiliane kwa namba, 0712 202244 au
0765 553030
0 Response to "UNAPOAJIRI AU KUAJIRIWA, ZINGATIA UMUHIMU WA KUJUA NI NINI UNACHOTAKA"
Post a Comment