Katika mfululizo wa vitabu vyetu 300 mashuhuri vya elimu ya pesa na mafanikio, leo tunakiangalia kitabu cha Mwanamama Louise L. Hays, You can Heal your life au kwa kiswahili, unaweza ukayaponya maisha yako. Kitabu hiki kilichapishwa hapo mwaka 1984 na kupewa promosheni ya nguvu katika show ya televisheni inayoendeshwa na mwanamama mwenzake Oprah Winfrey.
Louise alifanikiwa kuuza nakala za kitabu hicho nyingi
sana, zaidi ya nakala milioni 50 na kumfanya awe miongoni mwa wanawake wachache
waliouza vitabu nakala nyingi zaidi duniani.
Kwa ufupi maudhui ya kitabu hiki, ‘Unaweza ukayaponya
maisha yako’, yamejikita zaidi katika elimu ya uhusiano baina ya akili na mwili
wa mwanadamu. Anasema vitu hivyo viwili akili na mwili vinategemeana kiasi
kwamba mawazo hasi ndiyo chanzo cha karibu magonjwa yote yanayompata binadamu
kuanzia mafua mpaka kansa.
Hivyo anapendekeza kwamba ili kuponya magonjwa mbalimbali basi mtu hana budi kuhakikisha anakuwa na
fikra chanya muda wote, upendo pamoja na moyo wa kujisamehe yeye binafsi. Kwa
ujumla mtu anapaswa kubadilisha kabisa namna anavyofikiri kutoka ile ya msongo
wa kimawazo kwenda ile isiyokuwa na msongo wa mawazo.
0 Response to "UNAWEZA KUPONYA MAISHA YAKO(YOU CAN HEAL YOUR LIFE)"
Post a Comment