Wazungu husema “you can’t re-invent the wheel”
wakimaanisha kwamba huwezi ukagundua upya matairi ya gari. Usemi huu maana yake
ni kwamba ili kufanikiwa katika jambo fulani haulazimiki kufanya kitu au jambo
jipya kabisa duniani na badala yake inakupasa ufanye yaleyale waliyofanya watu
wengine kwa ubunifu na ustadi zaidi pengine hata kuwashinda.
Biashara zipo nyingi na za kila aina, ili uweze kuwa
mjasiriamali mzuri unatakiwa aidha ubuni kitu kipya kabisa, au ubuni njia mpya
ya kufanya biashara, masoko mapya, njia mpya za usimamiaji biashara, namna mpya
na bora zaidi ya kuwahudumia wateja nk.
Kinachohitajika wakati wa kutafuta wazo bora la biashara
ni mbinu za kupata wazo hilo ambazo ndizo zitakazolifanya liweze kufaa au kuwa
bora na wala siyo upya au upekee wa wazo la biashara, ingawa pia upya au upekee
ni moja kati ya njia nyingi zinazoweza kutumiwa kupata wazo linalofaa la
biashara na wajasiriamali au wafanyabiashara.
Mbinu
au njia mbalimbali za kutumia wakati wa kutafuta wazo bora linalofaa la
biashara inayolipa.
1.
Taaluma ama ujuzi uliopata
Ujuzi au taaluma uliyo nayo ndiyo mbinu ya kwanza kabisa
unayoweza kuitumia katika mchakato wako wa kupata wazo mwanana la biashara
itakayokupa faida. Madhalani unaweza ukawa wewe umeajiriwa kama mtaalamu wa
maabara katika zahanati fulani. Unaweza ukaamua baada ya kupata mtaji wa
kutosha na wewe kwenda kufungua kituo chako kwa ajili ya kuhudumia afya za watu
aidha kwa kufanya vipimo mbalimbali vya magojwa au hata kwa kufungua zahanati
yako mwenyewe huku na wewe ukiajiri wataalamu ambao wewe huna utaalamu wa kazi
zao kama manesi au madaktari.
Utakuta wajasiriamali wengi duniani wenye mafanikio makubwa
ni watu ambao zamani walikuwa wameajiriwa mahali fulani kutokana na ujuzi
waliokuwa nao na kisha baadae kuja na wao kufungua biashara zao zinazohusiana
na ujuzi waliokuwa nao.
2.
Hobby uliyokuwa nayo unaweza ukaigeuza kuwa biashara.
Kile kitu unachopendelea maishani mwako unaweza badala tu
ya kukifanya kama burudani basi ukaamua kukifanya kibiashara na kikakulipa
vizuri sana. Tuseme labda wewe hobby yako ni kutazama mpira wa miguu pamoja na
kushabikia timu za hapa na ulaya kama vile Manchester United, Liverpool, Simba,
Yanga na hata Azam FC.
Unaweza ukaamua kuwa mchambuzi wa soka katika maredio au
Tv, kazi itakayokuingizia kipato badala ya kubakia kuwa mshabiki tu peke yake.
Au hata ikiwa wewe unapendelea mchezo huo unaweza ukaanzisha banda kwa ajili ya
kuonyesha mipira mbalimbali ya nje kupitia decoda au TV na kwa kuwa watu wengi
wanapenda sana mchezo wa soka watajaa kuja kutazama kila siku kama utawawekea
chaneli nzuri za mpira wa miguu.
3. Kununua
biashara iliyokwisha anzishwa tayari
Njia ya tatu, unaweza kupata wazo lako la biashara kwa
njia ya kununua biashara ya mtu mwingine aliyekwisha ianzisha tayari lakini
akaamua kuiuza. Watu huuza biashara zao kutokana na sababu mbalimbali.
4.
Mahitaji ya watu eneo unakoishi au kufanya kazi.
Hebu jiulize maswali haya,
· Ni
kitu gani hapo unapoishi au kazini kwako kinachokupa usumbufu mkubwa kukipata
aidha kwa kuwa mbali au bei kubwa?
· Ni
bidhaa zipi au huduma ambazo katika maeneo yako hazipo kabisa lakini watu
wanazihitaji?
· Ni
vitu gani wewe na watu wengine waliokuzunguka mnavyolalamikia sana kwenye biashara
za hapo mtaani/kazini?
7.
Utalii ama kutembelea maeneo mbalimbali.
Unapotembelea sehemu nyingine ngeni kwako, ukiwa njiani
kwenye gari au hata baada ya kuwasili sehemu husika utaona na kukutana na vitu
vingi vigeni kwako ambavyo vinaweza vikawa ni fursa ya kibiashara katika sehemu
ulikotoka. Kwa mfano umeenda kutembelea mbuga za wanyama za Ngoro ngoro ukakuta kule nyama pori zikiuzwa
bei rahisi sana. Unaweza baada ya kufuatilia taratibu za vibali vya serikali na
ruksa ukaamua kuanzisha biashara ya kuuza nyama pori za swala, nyumbu na hata
pundamilia maeneo kama ya Dar ambako vitoweo vitamu kama hivyo ni adimu sana.
8.
Teknolojia inaweza ikakupa wazo la biashara.
Chunguza ni teknolojia ipi inayoenda na wakati uliopo kwa
mfano sasa hivi kuna teknolojia ya huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu
za mkononi kama Maxmalipo, tigo pesa, mpesa, airtelmoney, halopesa, ezy pesa na
nyinginezo. Kutokana na teknolojia hizo unaweza ukaanzisha biashara nzuri tu
kama wakala wa kampuni hizo kuuza miamala, muda wa maongezi, pamoja na bandle
za intaneti.
9.
Haiba, urembo na utanashati wako.
Haiba yako inaweza ikatumika kama wazo la biashara.
Tumeshuhudia hata hapa Tanzania achilia mbali nchi za nje wasichana wengi
wakitengeneza pesa kupitia tasnia ya urembo, basi tu kwasababu ni warembo,
wanapata mikataba minono ya pesa nyingi kwenye matangazo ya biashara na hata
katika mashindano ya urembo. Wanaume watanashati nao hupata pesa kupitia
mashindano ya watunisha misuli pamoja na kuingia katika mikataba minono kama
walivyokuwa wenzao wasichana.
10.
Mahitaji katika makampuni makubwa na taasisi mbalimbali
Kuna makampuni na taasisi nyingi kama mashule,
mahospitali, mahoteli, vyuo, viwanda, taasisi za dini, serikali nk. wote hawa
wana mahitaji mbalimbali yanayosubiri kutimizwa kama vile kusambaziwa bidhaa au
huduma mbalimbali.
11.
Kununua haki ya kufanya biashara ya kampuni nyingine(FRANCHISE)
Njia hii mtu unanunua haki ya kutumia jina (BRAND) la
kampuni au biashara ya mtu mwingine ambaye tayari anajulikana na wewe ukafanya
biashara kwa masharti ya kutoa huduma au bidhaa zinazofanana na kwa ubora wa
kiwango kilekile cha mmiliki wa hilo jina. Kuna mifano hata hapa ya biashara
kama hizo kama vile makampuni ya soda za cocacola na pepsi, migahawa kama ya
mackdonald iliyosambaa duniani kote nk.
12.
Kuangalia na kusikiliza vyombo vya habari.
Magazeti, televisheni, redio, kusika kutoka mazungumzo ya
watu ya mdomoni, majarida na siku hizi mtandao wa intaneti ni njia nzuri sana
za mtu kuweza kupata wazo la biashara kwa kusikiliza au kuona ni fursa zipi
zilizopo mahali fulani zinazohitaji kutimizwa.
13.
Ugunduzi.
Kama unaweza kugundua ama kuvumbua kitu fulani nayo ni
fursa nzuri ya kibiashara. Kuna watu waliokuwa na uwezo wa kugundua dawa za
asili au hata dawa za kisasa, kugundua mitambo au mashine ya kurahisisha jambo
fulani, kugundua mbinu mbalimbali zinazoweza kuleta unafuu wa maisha ya
binadamu nk. ni moja kati ya njia za kupata mawazo bora ya biashara itakayokupatia
pesa.
14.
Kuiga mawazo ya biashara za watu wengine waliofanikiwa.
Hii japo unaweza kuiona siyo njia nzuri sana lakini ndiyo
moja kati ya njia zinazotumiwa zaidi na watu wengi ijapokuwa baadhi yao huwa
hawawezi kufanikiwa kwa kiwango kile waanzilishi wa mawazo hayo
walivyofanikiwa.
…………………………………………………………………….
Ndugu
msomaji wa blogu hii, kwa elimu ya kina zaidi kuhusiana na Ujasiriamali,
kuanzisha biashara za aina mbalimbali, kuziendeleza, kuzisimamia na hata njia
wanazotumia matajiri kutajirika, jipatie vitabu vyako kutoka Self Help Books
Tanzania ltd.
Unaweza kununua kitabu kimoja kimoja lakini pia ukitaka
kifurushi(bundle) la vitabu vyote vitatu(3pack) unapata.
Kifurushi
cha vitabu halisi vya karatasi hardcopy ni Tsh. 35,000/=
Na kifurushi
cha vitabupepe kwa njia ya e-mail softcopy ni Tsh. 18,000/=
Kwa
bei ya kitabu kimoja kimoja bonyeza maandishi yafuatayo, PATA VITABU VYA UJASIRIAMALI PDF NA HARSCOPY HAPA
Usisahau
pia lile DARASA LA SEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA linaendelea.
0 Response to "WAZO BORA LA BIASHARA INAYOLIPA SIYO LAZIMA LIWE JIPYA SANA "
Post a Comment