Duka la rejareja au duka la vyakula, mara
nyingi aina ya maduka haya huwa tunayaona huko mitaani, huwezi ukatembea hatua
20 mpaka 30 pasipo kukutana nalo hata moja. Bidhaa utakazokutana nazo huko mara
nyingi ni zile ambazo zinahitajika katika matumizi ya binadamu ya kila siku
kuanzia vyakula mpaka dawa za maumivu kama panado na asprin.(mahitaji
ya msingi kabisa ya binadamu)
Zipo bidhaa ambazo mteja yeyote anapokwenda
katika duka la rejareja hutegemea kwa asilimia kubwa kuzikuta na anapofika
dukani na kukuta vitu hivyo havipo basi hukata tamaa hata ya kurudi tena katika
duka hilo siku nyingine. Na kwa bahati mbaya bidhaa nyingi za namna hiyo
utakuta faida yake siyo kubwa sana katika kila bidhaa moja unayouza. “low gross profit goods”.
Kwa upande mwingine wa shilingi, uzuri wa
bidhaa za namna hiyo ni kwamba hutoka haraka haraka sana(high turn over ). Faida ghafi tunayoizungumzia hapa ni ile baada ya
kuchukua bei ya bidhaa uliyonunulia na kutoa bei ya kuuzia. Kwa mfano umenunua
sukari kilo moja shilingi 2,000/= na kwenda kuiuza shilingi 2,400/= kwa kilo,
faida ghafi yake hapo ni shilingi 400 katika kilo moja ya sukari.
Kama mmiliki wa duka au muuza duka la
rejareja unatakiwa uzifahamu bidhaa hizo
na hata ikiwezekana uhakikishe hazikosekani dukani kwako hata siku moja, Zipo
bidhaa ambazo kutokana na eneo na mazingia ya eneo husika bidhaa za namna fulani
hutoka harakaharaka lakini pia kuna bidhaa zingine, zenyewe bila kujali eneo
wala mazingira mahitaji yale popote pale ni muhimu mno kwa binadamu kiasi
kwamba zinauzika chap chap ijapokuwa faida yake siyo kubwa sana.
Kwanini
bidhaa zinazotoka haraka haraka lakini zilizokuwa na faida kidogo ni nzuri
kwenye duka lako?
Kuna ule usemi usemao, “kidogo dogo hujaza
kibaba” na “bandu bandu hatimaye humaliza gogo” misemo hii naihusisha na dhana
hii kwa mantiki kwamba, ile faida unayo iona kidogo kidogo lakini unaipata kila
baada ya muda mfupi inao uwezo mkubwa wa kujilimbikiza na kuwa kubwa kwa haraka
kiasi cha kushangaza.
Duka lako unahitaji wateja wanaojirudia tena
na tena kusudi uweze kufanya biashara endelevu, hivyo unapokuwa na bidhaa hata
zile zilizokuwa na faida kidogo lakini wateja wanazotaka, unawafanya wateja wasikauke
katika duka lako hata siku moja na wanapokuwa wanaridhika zaidi na huduma zako
ndipo huwavuta na wateja wengine wenye mahitaji kama ya kwao nao kuja dukani
kwako kukuunga mkono.
Aina
za bidhaa zenye faida kidogo dukani kwako lakini zinazotoka upesi upesi na
hivyo kukuingizia faida ‘fasta fasta’(haraka haraka)
Bidhaa zenyewe zilizokuwa na uwezo wa kuuzika
haraka haraka ijapokuwa faida ghafi yake siyo kubwa sana ni hizi hapa;
v Vocha
za simu za mkononi
v Sukari
v Chumvi,
v Unga
wa sembe
v Maharage
v Majani
ya chai,
v Unga
wa ngano
v Kiberiti
v Dona
v Mafuta
ya kula
v Majani
ya chai
v Dawa
za mswaki
v Sabuni
ya mche
v Sabuni
za vipande
v Sabuni
za kuogea
v Sabuni
ya kufulia
v Sabuni
ya unga
v Vitu
vya kutafuna watoto kama vile, pipi, karanga, biskuti, chama, bazoka, big ghee,
peremende, ubuyu, bublish, nk.
v Mafutaya
taa na
v Soda.
Kama nilivyotangulia kusema, kulingana na
mazingira ya eneo lilipo duka lako la rejareja, bidhaa zinazotoka haraka lakini
faida yake kidogo zinaweza kuwa tofauti na hizi au zaidi ya hizi lakini hapa
nimejaribu kutaja tu zile ambazo ndiyo mara nyingi hukuta karibu kila eneo iwe
ni kijijini ama mjini basi utakuta ndizo zinazoongoza kwa kuwa na mahitaji
makubwa sana na ya kila wakati hivyo faida yake kufanywa kuwa kidogo sana kwa
kila kipimo cha bidhaa moja inayouzwa.
Kama hujui unaweza ukazidharau bidhaa za
namna hiyo na kujisemea, “niweke za nini, zinanimalizia nafasi ya bure
tu, bidhaa zenyewe kwanza faida yake ni kidogo kama nini” Kumbe hujui
nguvu yake ni nini katika kasi ya kutoka. Ili mradi kitu kinahitajika na wateja
wewe wawekee hata kama faida yake siyo kubwa sana, kuna faida nyingi
utakazozipata kama nilivyokwisha kueleza katika aya zilizopita.
Kwa leo naona niishie hapa, ila nakuahidi
kukuletea makala za mara kwa mara kuhusiana na jinsi ya kuboresha biashara yako
ya duka hususani kama ni la rejareja pamoja na biashara nyingine zozote zile za
rejareja, kwani biashara za rejareja kanuni yake ni ile ile, uwe unauza nyanya,
vifaa vya ujenzi, chakula au supermarket.
Usisahau siri kubwa katika biashara hii ni
mahusiano yako mazuri na wateja ambayo huhusisha vipengele vingi, Hivi
unafahamu hata kitendo cha kumwambia mteja, sina chenchi katafute, ni kosa
kubwa?
Asante, ila kama unahitaji mbinu hizi kwa
ukamilifu zaidi ujifunze umetulia, basi nakushauri ununue kitabu cha, MAFANIKIO
YA BIASHARA: DUKA LA REJAREJA, bei yake ni Tsh. 10,000/= kitabu halisi cha
karatasi na Shilingi 5,000/= softcopy kwa email. Tupo MBEZI KWA MSUGURI stendi
ya daladala, au tuwasiliane kwa simu: 0712 202244 au 0765 553030
Karibu, tunatoa huduma ya kuandika mpango wa biashara yeyote ile unayotaka kwa ajili ya mahitaji mbalimbali kama vile kuombea mkopo, kuwasilisha kwa wabia, wawekezaji au kwa ajili tu ya uendeshaji wa biashara yako. Bei zetu ni nafuu sana, unachagua mwenyewe lugha ya kuandikia kati ya kiswahili na kiingereza.
Vilevile tunatoa mafunzo(course) nzima ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara yeyote ile. Package nzima ya mafunzo hayo ni pamoja na vitabu 2 cha kiingereza na cha kiswahili, templates au vielezo, Samples au Michanganuo kamili katika lugha ya kiingereza na kiswahili pamoja na semina mbalimbali kuhusu uandishi wa michanganuo ya biashara.
Kupata moja kati ya huduma hizi wasiliana na sisi kwa namba;
whatsapp/simu: 0765553030
SMS/Simu: 0712202244
BUSINESS PLANS / MICHANGANUO YA BIASHARA
Karibu, tunatoa huduma ya kuandika mpango wa biashara yeyote ile unayotaka kwa ajili ya mahitaji mbalimbali kama vile kuombea mkopo, kuwasilisha kwa wabia, wawekezaji au kwa ajili tu ya uendeshaji wa biashara yako. Bei zetu ni nafuu sana, unachagua mwenyewe lugha ya kuandikia kati ya kiswahili na kiingereza.
Vilevile tunatoa mafunzo(course) nzima ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara yeyote ile. Package nzima ya mafunzo hayo ni pamoja na vitabu 2 cha kiingereza na cha kiswahili, templates au vielezo, Samples au Michanganuo kamili katika lugha ya kiingereza na kiswahili pamoja na semina mbalimbali kuhusu uandishi wa michanganuo ya biashara.
Kupata moja kati ya huduma hizi wasiliana na sisi kwa namba;
whatsapp/simu: 0765553030
SMS/Simu: 0712202244
Well said
ReplyDeleteSafi
ReplyDelete