Awamu ya kwanza ya masomo ya semina ya jinsi ya kuandika
mchanganuo wa biashara ilijumuisha vitu hivi vifuatavyo,
· Utambulisho
wa semina,
· Masomo
ya msingi 11 katika mifumo ya PDF na
mp3,
· Violezo(Templates)
· vitabu
vya michanganuo ya biashara, kile cha kiswahili cha “MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI” pamoja na kitabu kingine maarufu sana duniani cha namna ya
kuandika mpango wa biashara katika lugha ya kiingerera kimoja.
· Pamoja
na masomo mengine kadhaa ya ziada.
Masomo hayo yalikuwa yakitolewa kwa njia ya BLOGU HII MAALUMU(kuingia ni kwa aliyelipia tu)
ambayo wasomaji wake huingia baada ya kulipa kiingilio cha Tsh. 10,000/=.
Masomo yote katika PDF na mp3 hutumwa pia kwa njia ya email kusudi mshiriki aweze
kudumu nayo muda wote hata ikiwa hatadownload ama kusoma masomo yaliyopo katika
blogu hiyo.
SOMA: Jinsi ya kujiunga na Semina ya michanganuo ya biashara.
SOMA: Jinsi ya kujiunga na Semina ya michanganuo ya biashara.
Katika kipindi kisichopungua miezi mitatu, semina hii
walijiunga watu wengi na waliweza kujifunza masomo ya semina huku wengi wakitoa
mirejesho mbalimbali kama vile kuuliza maswali kwa mambo ambayo hawakuyaelewa
vizuri, kutoa maoni mbalimbali ya namna ya kuboresha semina na hata wengine
kuchangia mada mbalimbali kwa njia za email, meseji na kisanduku cha maoni.
Baada ya awamu hiyo wadau wengi walipendekeza kuwa
ikiwezekana tuanze awamu nyingine ambayo ‘itadili’ zaidi na uandishi wa moja
kwa moja(kwa vitendo zaidi) wa
michanganuo ya biashara huku msisitizo ukiwa katika kipengele au sehemu ya
fedha ambayo kwa mujibu wa wadau wengi wanasema ndiyo kipengele kigumu kuliko
vingine vyote.
Mwanzoni tulikuwa tumepanga kwamba mshiriki wa semina
atahesabu amehitimu semina hii baada ya kuweza yeye mwenyewe kuandika mpango wa
biashara yake atakayoipenda, na tulifikiri kuwa kila mshiriki aliyeanza semina
siku zile za mwanzo mpaka kufikia mwezi huu wa nne tayari angekuwa ameshamaliza
kuandika mchanganuo huo. Hata hivyo washiriki asilimia kubwa wameshakamilisha
lakini bado wapo baadhi ambao hawajakamilisha.
SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara?
SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara?
Kutokana na maoni ya washiriki hata na wale walioweza tayari
kuandika michanganuo yao, tumeona umuhimu wa kuwa na awamu ya pili ya semina
hiyo itakayozingatia zaidi maeneo hayo mawili lakini pia hata na maeneo yale
ambayo mshiriki mmoja mmoja atakuwa hajayaelewa vizuri.
Tutaanza kuchambua na kuandika michanganuo ya biashara
mbalimbali kuanzia mwazo mpaka mwisho huku tukionyesha hatua kwa hatua jinsi
kila kipengele kinavyoandikwa. Sambamba na hilo pia tutaweka msisitizo zaidi
katika kipengele au sehemu ya makisio ya fedha. Masomo yatawekwa asubuhi au jioni na mchanganuo mmoja utachukua siku tatu kumalizika.
Tutaanza awamu ya pili ya semina kwa kuchanganua mpango wa biashara ya saluni sehemu za biashara, bidhaa/huduma, uongozi,
na mikakati siku ya kwanza, kisha soko siku ya pili na kumalizia na sehemu ya
fedha siku ya 3. Hata hivyo katika michanganuo mingine kwenye awamu zitakazofuata, tutaanza na kipengele chochote ili kuthibitisha kuwa unapoandika mpango wako wa biashara hulazimiki kufuata mlolongo wa vipengele/sehemu jinsi ulivyokuwa rasmi bali unaanza popote isipokuwa muhtasari tu unaokuwa wa mwisho mara zote.
Kwa
washiriki wanaoendelea kujiunga kuanzia sasa wasiwe na
wasiwasi wowote kwamba wamechelewa kwani watajifunza kila kitu ambacho wenzao
waliotangulia walijifunza kutokana na mfumo wa semina yenyewe kuw ni ule wenye kunyumbulika(flexible)
Mfumo wa semina hii ni ule ambao masomo yake yote na kila
kitu kinachofundishwa hurekodiwa katika hii BLOGU MAALUMU YA MASOMO YA SEMINA YA MICHANGANUO, ambayo ipo muda wote kwa mshiriki yeyote aliyetoa kiingilio cha
shilingi elfu 10 pamoja na kututumia anuani yake ya baruapepe(email) aina ya
GMAIL ambayo ndiyo tunayoitumia kumtumia mwaliko wa kujiunga na blogu hiyo.
Kisha yeye hubonyeza kiungo(link)
itakayotumwa kwenye email yake na tayari sasa atakuwa akiingia katika BLOGU
hiyo kila anapohitaji bila kikwazo.
Kwa
washiriki wale wa zamani waliotangulia kujiunga, nao
wasiwe na hofu hata kidogo kwani watakwenda sambamba na hao wapya huku wakijifunza kwa
undani zaidi kivitendo pamoja na kujipiga msasa katika maeneo yale ambayo
hawakuyamudu vyema, lengo likiwa ni “kumaster” kabisa uandaaji wa mpango wa
biashara.
……………………………………………………………….......
KWA MAWASILIANO NA MRATIBU WA SEMINA AU KUJIUNGA NA
SEMINA HII, TUMIA NAMBA ZA SIMU ZIFUATAZO,
0712
202244 AU 0765 553030
Jina:
Peter Augustino Tarimo
0 Response to "BAADA YA MASOMO 11 SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA SASA INAINGIA AWAMU YA PILI"
Post a Comment