Unapojikuta katika hali ya kutokuwa na mtaji kabisa wa
fedha, unaweza kufikiria njia nyingi sana za ni namna gani utakavyoweza
kuendesha maisha yako ya kila siku. Ukiwa katika hali kama hiyo, mtaji wako
pekee unakuwa ni nguvu zako ulizokuwa nazo kama huna ugonjwa wowote
unaokusumbua, ujuzi, maarifa au elimu uliyo nayo pamoja na uzoefu ulioupata
siku za nyuma.
Sasa zipo biashara unazoweza
kuzifanya hata ikiwa hauna kabisa mtaji kwa maana ya fedha, ingawa hauwezi
kabisa kabisa kusema ipo biashara isiyotumia mtaji kwa kuwa hata nguvu na ujuzi
kitalamu huhesabiwa kama ni mtaji mojawapo. Orodha ile ya biashara nitakazozitaja
hapa ya biashara zisizohitaji mtaji wa pesa kabisa ni tofauti na nyingine
niliyowahi kutaja tena katika blogu hii iliyokuwa inaziorodhesha biashara zilizokuwa na faida kubwa na yaharaka mara 2 ya mtaji utakaowekeza.
Vile vile hapa sizungumzii zile biashara unazoweza
kuanzisha bila mtaji wa pesa kwa maana ya kutumia mbinu mbalimbali kama vile
kukopa mali kutoka kwa wasambazaji na wauzaji wa jumla kisha na wewe baada ya
kwenda kuuza rejareja unarudi kuja kuwalipa fedha zao, itategemea bidha hizo
unakwenda kuuzia wapi, ikiwa huuzii katika fremu au chumba cha kulipia labda
unauzia nyumbani au kutembeza mitaani sawa itakuwa ni biashara isiyotumia mtaji.
Au kutoa huduma kama vile za kiushauri wa kitaalamu
ambazo mtu ingawa unaweza usitumie mtaji wa pesa lakini unajikuta ukihitaji
pesa kwanza za kuandaa ofisi nk. Au biashara ya kwenye mtandao wa intaneti
ambayo ni lazima kwanza uhakikishe unayo kompyuta, moderm au simu ya kisasa ya mkononi kama smartphone na shilingi lfu moja, mbili za kuweka bando la intaneti . Biashara
kama hizo badala ya kusema hazihitaji kabisa mitaji tunaweza kuziita ni
biashara za mtaji kidogo au za uwekezaji mdogo kwa sababu haiwezekani kabisa
uanzishe bila senti tano mfukoni.
SOMA: Biashara ndogo za kufanya Dar bila kulipa pango
SOMA: Biashara ndogo za kufanya Dar bila kulipa pango
Katika orodha yangu hii namba moja 1, nitaifanya kuwa ndiyo
ya mwisho, ilitakiwa kuwa ya kwanza lakini kutokana na upekee wake naona
tuiache kwanza mpaka mwishoni ndipo niitaje.
1. Udalali wa vitu, nyumba, vyumba, viwanja na mashamba; Hapa nazungumzia ule udalali wa ngazi ya chini kabisa mitaani, siyo ule wa ngazi za makampuni yaliyosajiliwa kisheria ingawa kama ukishaanza chini ni lazima baada ya kupata mtaji sasa ukumbuke kwenda kujisajili kisheria serikalini. Kwa kuanza unaweza kutafuta mtaani unakoishi watu wenye vitu mbalimbali wanavyokodisha au kuuza kisha unakwenda kuwatafuta na watu wanaohitaji vitu hivyo halafu baada ya kuwaunganisha wanakupa malipo kidogo toka kila upande au upande mmoja.
Kuna
mtu mmoja yeye hakuwa na mtaji wowote ule ila alikuwa tu na aidia ya maswala ya
material na vifaa vya ujenzi vya kujengea nyumba kama vile, tofali, paving
blocks, vigae/tiles, baluster na ventilation blocks. Aliwafahamu vyema pia
wauzaji na watengenezaji wa vifaa hivyo vya ujenzi, bei za vifaa na material
hizo, na kila kitu kuhusiana navyo.
Kando
kando ya ukuta wa nyuma yake uliopakana na barabara ya Morogoro road yanakopita
magari na watu wengi alipamba ukuta huo kwa vipande vilivyovunjika vya vifaa
hivyo alivyookota wanakotengeneza pamoja na kuweka bei zake na namba yake ya
simu kama matangazo kwa wateja kwamba yeye anauza vitu hivyo.
Wateja
wanaohitaji humpigia simu wakishapatana bei huwaambia wasubiri kidogo aende
eneo anakotengenezea ili awachukulie, kumbe yeye huku anakwenda kwa
watengenezaji. Hapo hupatana kabisa na mtu wa gari wanakwenda kupakia tayari
kwa kupeleka saiti kwa mteja.
2. Biashara ya utoaji wa huduma mbali mbali
kama vile biashara ya huduma ya kuangalia watoto wadogo wakati wazazi wao
wakiwa kazini(babysitting au home daycare), hii unaweza ukaifanyia nyumbani
kwako lakini katika kiwango cha watoto wachache tu kuanzia labda mmoja mpaka
watatu ukitumia vifaa na eneo la nyumba unayoishi, kisha baadae unaweza ukatafuta vibali na
leseni kwa ajili ya kuanzisha kituo kamili cha kuangalia watoto wengi zaidi.
Huduma
nyingine unayoweza kutoa bila kuwa na mtaji wa pesa ni, biashara ya udobi,
kufua na kupiga pasi nguo za watu ukiwa majumbani mwa watu hao, unakwenda wewe
mwenyewe na vifaa vyote ni vya kwao. Au hata unaweza kwa kutumia vifaa vyako
vya nyumbani ukawatangazia majirani na watu wanaohitaji huduma hiyo wakaleta
nguo zao hapo nyumbani unapoishi.
Huduma
ya kufundisha na ushauri, yanaweza kuwa masomo ya ziada ya shule(tuition) ama
ujuzi wowote uliokuwa nao na ambao kuna watu wengine wanaohitaji kujifunza kama
vile muziki, ujasiriamali, mapishi, kutarizi, utengenezaji wa vitu kama
mishumaa, batiki, sabuni, unga wa lishe nk. Unaweza kuwafundisha wateja wako
mmojammoja majumbani mwao au ukawaita eneo unaloishi na kuwapa masomo kisha
wakakulipa. Vifaa kwa mfano malighafi za kutengenezea vitu ni mteja mwenyewe atakayenunua.
3. Biashara ya kuokota na kuuza vitu
chakavu kama vile chupa
za plastiki, vyuma chakavu, chupa na mikebe ya kuwekea vitu iliyotupwa
pamoja na vifusi kutoka majengo yaliyobomolewa. Kuna biashara pia ya kuzoa na
kuuza mchanga kutoka kwenye mifereji ya barabara au maeneo yanayoruhusiwa. Usije ukaaona waokota makopo na chupabarabarani ukadhani wote ni machizi, wapo wajanja hata kukushinda wewe uliyeko
ofisini.
4. Kuuza mbolea na mifupa ya ngombe au kuku.
Sehemu za machinjio ya wanyama kama kuku, ngombe na mbuzi. Kile wanachotupa
kama uchafu, wapo watu wanaokihitaji kwa mfano mbolea kwa ajili ya kuoteshea
mbogamboga na mimea, mifupa na damu kwa ajili ya kulishia wanyama kama kuku,
samaki nk. Unaweza kutafuta kwanza oda kutoka kwa watu wanaohitaji kisha na
wewe unakwenda kuchukua na kuwapelekea, wakakulipa pesa.
5. Biashara ya kuuza mabaki ya vyakula mahotelini na kwenye migahawa. Tafuta kwanza watu wanaohitaji mabaki hayo ya
vyakula na wengi ni wale wanaofuga wanyama kama mbwa, paka, kuku, bata na
nguruwe, halafu kazi yako inakuwa ni kupita maeneo mbalimbali wanakopika na
kuuza vyakula kama kwa akina baba na mama lishe, migahawa, baa na mahoteli
mbalimbali. Waombe wawe wanakupa yale mabaki ya vyakula vinavyobaki na kama
hawana kazi navyo watakupa na wewe ukaviuze kwa wateja uliokwishawapata.
6. Utengenezaji wa mapambo na bidhaa
ndogondogo kwa kutumia malighafi zitokanazo na vitu vilivyotupwa majalalani
kama vile maua, midoli, vyungu vya maua kwa kutumia udongo nk. Biashara ya
kuuza miche ya maua na miti mbalimbali, hii unaweza kuotesha miche ya mimea ya
maua na miti mbalimbali ambayo mbegu zake unaweza kuzipata bure au kuokota
kwenye miti, na kwa kutumia karatasi za nailoni zilizotupwa na makopo au chupa
unapanda miche na kuiuza kandokando ya barabara ambako huchajiwi kodi na mtu
yeyote ilimradi tu umepanga kwa unadhifu pasipo kuharibu au kuchafua mazingira.
7.
*AJIRA.
Biashara
ya mwisho unayoeza kuifanya wakati hauna kitu chochote kile mfukoni na ambayo
nilisema ilipaswa kuwa ya kwanza lakini kutokana na kwamba ni biashara iliyo
katika mjadala mzito ikiwa ni biashara kweli ama siyo biashara ni biashara ya
ajira.
Kwa
upande wangu mimi nafikiri pengine na kuna watu wengine wanaoamini hivyo, ajira
au kazi nayo ni biashara kama zilivyokuwa biashara zingine kutokana na sababu
kubwa kwamba, mwajiriwa anauza nguvu au ujuzi wake kwa mwajiri. Ili biashara
iitwe biashara ni lazima kuwe na bidhaa au huduma halafu muuzaji na mnunuzi.
SOMA: Ajira siyo laana, bali chanzo kizuri zaidi cha mtaji wa biashara.
SOMA: Ajira siyo laana, bali chanzo kizuri zaidi cha mtaji wa biashara.
Kwa
mantiki hiyo basi, ikiwa hauna mtaji wowote ule mfukoni hiyo ndiyo fursa nzuri
zaidi ya kutafuta ajira yeyote ile unayoweza kuifanya kulingana na uzoefu,
ujuzi au taaluma uliyokuwa nayo. Hata kama ikiwa huna vitu vyote hivyo, basi
uza nguvu zako kwa kutafuta zile kazi ambazo ni nguvu zako tu ndizo
zinazotakiwa kama vile kubeba mizigo(ukuli), kulima, shughuli za ujenzi kama
kubeba zege, kuwasaidia mafundi, kufagia barabara, kupiga debe, kazi za
ndani(housegirl & houseboy) kazi ya kufyatua matofali, kazi ya uuzaji na
kutangaza bidhaa(sales and marketing) maarufu kama kazi za promosheni, kazi ya
kuuza, kazi ya kuuza mgahawani nk.
Halafu
sasa kitu kimoja cha kuvutia zaidi ni kwamba ajira ni chanzo kizuri sana cha
mtaji wa kuanzisha biashara zingine za kawaida kama za uuzaji wa bidhaa au
utoaji wa huduma kwani kwa kutumia akiba ya mshahara utakaoupata unaweza
ukaanza biashara yako.
Kwa ufupi sana nimejaribu kuorodhesha zile biashara
ambazo mtu anaweza akazianzisha pasipokuwa na shilingi hata moja mfukoni. Hata
hii ya 7 ambayo nimesema ipo katika mjadala nayo nimejitahidi sana kutaja zile
kazi ama ajira ambazo kwa kweli hata hazihitaji utaalamu au ujuzi wa kuzifanya
bali nguvu za mtu mwenyewe tu au akili ya kuzaliwa.
......................................................................................................
Ndugu msomaji wa blogu hii, ninaamini katika makala tunazokuletea mara kwa mara humu hukosi kitu cha kujifunza chenye manufaa kwako. Nakuomba endelea kusoma makala zetu kila wakati lakini pia jitahidi uweze kupata na moja ya vitabu vyetu hivi au semina na mafunzo mbalimbali tunayoyatoa, zijue huduma hizo kwa kubonyeza hayo maandishi au katika menu pale juu bonyeza palipoandikwa HUDUMA ZETU.
Hata ikiwa hujawa tayari kununua kitabu au kulipia semina na mafunzo basi pata angalao kitabu chetu tunachotoa bure bila malipo yeyote kwa kubonyeza maandishi yafuatayo, JIUNGE NA BLOGU HII kupata vitabu vizuri bila malipo kwa kuweka jina, email na namba yako ya simu katika kisanduku.
Kitabu rahisi kabisa unachoweza ukakinunua na ambacho kwa kweli ni kitabu kila mtu aliyewahi kukisoma hushindwa kuelewa ni kwanini tukiuze bei rahisi kiasi hicho ukilinganisha na yale yaliyokuwemo ndani yake ni MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA, kitabu hiki unakipata kwa shilingi elfu 3 tu ndani ya email yako. Jaribu leo kusoma kitabu hiki usipoona tofauti na vitabu ulivyowahi kusoma vya ujasiriamali na maendeleo binafsi hakika nitakurudishia pesa yako.
......................................................................................................
Ndugu msomaji wa blogu hii, ninaamini katika makala tunazokuletea mara kwa mara humu hukosi kitu cha kujifunza chenye manufaa kwako. Nakuomba endelea kusoma makala zetu kila wakati lakini pia jitahidi uweze kupata na moja ya vitabu vyetu hivi au semina na mafunzo mbalimbali tunayoyatoa, zijue huduma hizo kwa kubonyeza hayo maandishi au katika menu pale juu bonyeza palipoandikwa HUDUMA ZETU.
Hata ikiwa hujawa tayari kununua kitabu au kulipia semina na mafunzo basi pata angalao kitabu chetu tunachotoa bure bila malipo yeyote kwa kubonyeza maandishi yafuatayo, JIUNGE NA BLOGU HII kupata vitabu vizuri bila malipo kwa kuweka jina, email na namba yako ya simu katika kisanduku.
Kitabu rahisi kabisa unachoweza ukakinunua na ambacho kwa kweli ni kitabu kila mtu aliyewahi kukisoma hushindwa kuelewa ni kwanini tukiuze bei rahisi kiasi hicho ukilinganisha na yale yaliyokuwemo ndani yake ni MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA, kitabu hiki unakipata kwa shilingi elfu 3 tu ndani ya email yako. Jaribu leo kusoma kitabu hiki usipoona tofauti na vitabu ulivyowahi kusoma vya ujasiriamali na maendeleo binafsi hakika nitakurudishia pesa yako.
Nimependa huduma yenu aiseehh mungu awabariki
ReplyDeleteNa wewe pia ubarikiwe
Delete