Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusiana na ikiwa
mpango wa biashara unaweza kusaidia katika mafanikio ya biashara au la, watu
wengi kwa muda mrefu wamekuwa na dhana kwamba mchanganuo au mpango wa biashara
ni kwa ajili ya kuombea pesa (mkopo) tu na baada ya hapo basi ni kuuweka
kabatini uendelee kuliwa na wadudu.
Zipo sababu nyingi zinazoweza kuwafanya
wajasiriamali wengi kutokuandika mpango wa biashara lakini iliyokuwa kubwa
zaidi ni hii ya kufikiri kwamba, kuandika mpango wa biashara ni jukumu zito
linalohitaji muda mwingi na utaalamu katika tasnia ya biashara na fedha. Lakini
kumbe ni kinyume chake kabisa.
SOMA: SABA(5) KWANII UANDIKE MPANGO WA BIASHARA YAKO
Kwanza mpango wa biashara siyo kwa ajili ya
kuombea fedha tu peke yake, isitoshe siyo kweli kwamba kuandika mpango wa
biashara mtu anatakiwa kuwa amesomea masomo ya biashara ndipo aweze kuandika.
Kama unao uwezo wa kufikiria wazo la
biashara, ukatafuta mtaji wa kuanzisha biashara yenyewe pamoja na kuiendesha,
basi wewe tayari unao uwezo wa kuandika au kuandaa mpango wa biashara yako
kuliko hata mtu mwenye digirii ya biashara. Kila siku, kila mahali duniani na
karibu kila binadamu katika wakati fulani wa maisha yake ni lazima aandae
mpango/mchanganuo wa biashara, penda asipende. Haiwezekani kabisa mtu ufanye
biashara yeyote ile hata kama ni ya kuuza karanga mitaani pasipo kwanza kufanya
mchanganuo wa biashara hiyo akilini kwake.
SOMA: Kwanini mpango wa biashara wa kuandikiwa siyo mzuri kwako?
Kitendo tu cha kujua utapata faida kiasi gani
kwenye kilo moja ya karanga utakazokaanga, tayari hiyo ni hatua mojawapo ya
mchanganuo wa biashara hiyo ya kuuza karanga. Sasa iweje useme huwezi
kutengeneza mpango wa biashara? Siku hizi mambo yamerahisishwa mno siyo kama
zamani, Mpango wa biashara wa kukuwezesha kuendesha biashara yako kwa ufanisi
mkubwa siyo lazima tena uandike kurasa 20 au 50 kama unapeleka benki kuomba
pesa. Lakini pia unaweza kuandika haikatazwi na ni faida zaidi ikiwa unaweza
kufanya hivyo.
Pointi yangu hapa ni kwamba, ikiwa unaona
uvivu kuandika mchanganuo wa biashara wenye kila kitu kama michanganuo
iliyokuwepo katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, basi
zipo njia fupi zinazoweza kukufanya ufurahie kufanya mchanganuo wa biashara
yako pasipo kutumia muda mwingi wala utaalamu mkubwa sana.
Njia mojawapo mimi binafsi ninayoikubali
sana, ni ya kujifunza namna ya kufanya michanganuo ya biashara kupitia usomaji wa michanganuo kama ile tunayotoa OFFA katika group la Michanganuo. Ukishajua mbinu
zinazotumika wakati wa kuandaa mpango wa biashara, hiyo ni nusu ya kuandika
mpango wenyewe wa biashara kwani sasa unaweza tu kufanya biashara yako kwa
kutegemea mpango unaouweka kichwani(akilini) mithili ya matajiri wa zamani
ambao hawakuwa wamesoma hata darasa moja lakini ulikuwa huwezi kuwaeleza kitu
chochote kwenye usimamizi na uendeshaji wa biashara zao.
Njia nyingine maarufu sana siku hizi ni
kutengeneza kitu kinachoitwa Mpango wa biashara Ukurasa mmoja (Ope Page Business Plan). Hii ni aina ya
mpango wa biashara ambao haihitaji muda mwingi kuandaa lakini vipengele vyote
muhimu vya biashara hujumuishwa ndani. Mfano na Template ya namna ya kuandika
mpango huo upo kwenye kitabu (E-book) ambayo ni miongoni mwa vitabu vilivyoko kwenye Offa yetu ya semina ya mwaka huu 2022
Sasa
basi ni kwa jinsi gani unavyoweza ukatumia mchanganuo au mpango wako wa biashara
kuiendesha biashara yako ikakuletea mafanikio?
Hakuna mtu asiyefahamu kuwa kwenye biashara
yale tunayoyapanga hayawezi kuja kuwa sawasawa na matokeo yenyewe wakati
wa kufanya biashara yenyewe halisi. Mambo mara nyingi huja kwenda tofauti.
Lakini hauwezi ukasema kuwa mpango wa biashara hauna maana kwa sababu hata
ikiwa hujafanya mpango rasmi wa biashara kama nilivyotangulia kusema hapo juu
ni lazima tu ulipanga kichwani, hilo halina ubishi, ukisema hukupanga basi wewe
siyo binadamu ni roboti.
Ingawa tunapanga lakini vilevile tunahitaji
kujiandaa na mabadiliko yatakayojitokeza kwa kasi katika hali halisi mbele ya
safari. Na hivyo ndivyo binadamu tunavyofanya kila mara tunapopanga kufanya
jambo lolote lile katika maisha yetu ya kila siku. Sasa kwa faida zaidi ya
kupanga ndipo utakuta watu wakipanga “simple”
na katika kutafuta urahisi huo ndiyo maana mimi huwa nashauri kila wakati mtu ujue …ABCD…. kuhusiana na mipango
ya biashara na kisha kwenye kuandika uandike mpango 'simple' utakaokusaidia
katika kusimamia biashara yako kwa uhakika na kisasa, pasipo hata kuandika
mamia ya kurasa.
Kuna vitu kwa mfano kama;
· Malengo
ya biashara, maono
· Mikakati
· Vitendo
halisi
· Vipimo
katika utekelezaji
· Hesabu
na namba za msingi kama vile mauzo, bajeti ya gharama mbalimbali na mahitaji.
Ukishaandika vitu hivyo kwa ufupi sasa
unatakiwa wakati wa utekelezaji wa biashara ufanye mapitio mara kwa mara,
unaweza ukaamua kujipangia ratiba ufanye mapitio ya mpango wako vs
hali halisi katika kipindi fulani, kwa mfano unaweza kufanya kila siku, kwa
wiki au kwa mwezi. Unaangalia tofauti iliyokuwepo kati ya mpango na matokeo
halisi. Hapa huhitaji kuwa mtaalamu wa biashara bali unatumia akili ya kawaida
tu ya kuifahamu vizuri biashara yako na kufuatilia kujua ni kitu gani
kilichotokea ukilinganisha na kile ulichopanga.
SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya michanganuo ya biashara awamu ya kwanza 1
Katika ulinganisho huo ni lazima utagundua kwamba,
mpango wa biashara mara nyingi hauwezi kwenda sawasawa kwa asilimia 100% kama
ulivyopanga. Lakini kuna umuhimu mkubwa na faida kiutendaji kwani kunakuwezesha
kufahamu ni kwa nini hali haikwenda sawa na ulivyopanga. Kumbuka hali halisi
siyo mara zote huwa tofauti kwa maana ya mambo kwenda mrama hapana, kuna wakati
mwingine hata pengine katika mpango ulikisia mauzo kuwa Sh. 1,000,000/= lakini
katika hali halisi unashangaa mauzo yanakuja kuwa 1,300,000/=. Kwa hiyo zoezi
hili litakusaidia kuamua ufanye mabadiliko gani, na utegemee matokeo gani kwa wakati
ujao.
Zoezi hili la kufanya marekebisho ya mpango
pamoja na kulinganisha mpango na matokeo halisi ni jambo muhimu sana na katika
hali ya kawaida kabisa ni zoezi linalofanyika katika maeneo mengi ya kazi na
biashara. Kwa mfano unapoingia katika nyumba nyingi za habari (News rooms) iwe ni
katika magazeti, redio au Televisheni, utakuta kila siku wana mikutano, wengine
huiita “postmortem” Mhariri mkuu hukaa na wafanyakazi wote na kuanza kufuatilia
kile walichofanya jana yake ikiwa walifikia malengo waliyojiwekea jana kwa
kiwango gani. Kisha siku hiyo mhariri huandaa mpango mwingine wa siku, nani aende wapi, akafanye nini, na kwa gharama gani nk.
Ingawa utakuta kuna vitu havikuenda sawa kama
mpango ulivyosema, lakini hapa kumbuka mhariri hamtafuti mchawi wala kumlaumu
mtu, bali yeye anachotafuta ni kwa nini mambo hayakwenda sawa au kwanini
yalikwenda vizuri zaidi kushinda ilivyokisiwa, kusudi mbinu hizo ziweze
kutumiwa zaidi wakati ujao.
Kwa hiyo matokeo ya mchakato wa kupanga au
mpango mzuri wa biashara siyo maandishi bali ni utekelezaji wake(execution),
jinsi unavyopanga vipaumbele vya biashara yako na kufuatilia utekelezaji wake
kujua ni kipi kimeenda sawa au ni kipi kimeenda mrama kwa ajili ya kufanya
marekebisho kwa ajili ya wakati ujao.
Kusimamia biashara ni sawa na mtu
unavyoendesha gari, unatakiwa uelewe ni uelekeo upi unaokwenda na uwe na maono
ya kule uendako, picha ya hatma ya safari yako. Ukichanganya vitu hivyo na
marekebisho ya hapa na pale njiani kama vile kuruka matuta, kukwepa vitu
barabarani nk. hata kama ikiwa ni barabara kubwa kama Morogoro road,
hakukosekani matuta na vizuizi vya hapa na pale. Lakini muda wote unatakiwa
kushikilia usukani wako pasipo kutetereka kwa kuwa tayari unao mpango na maono
kichwani ni wapi unakokwenda.
………………………………………………………………….
Ndugu msomaji, ikiwa wewe unahitaji kujifunza kwa kina jinsi ya kuandika mpango wa biashara yeyote ile pamoja na kupata ‘materials’ zote
zinazohusiana na michanganuo ya biashara kama vile vitabu kwa kiswahili na kiingereza, Templates za kiswahili na kiingereza na Sample za Michanganuo kamili ya biashara mbalimbali, basi hapa ndiyo mahali pake.
Tunayo Semina inayoendelea sasa kwenye Group la Michanganuo-online kila siku usiku yenye masomo 11 na leo ni siku ya pili. Ada ni Tsh. 10,000/= na ukiwahi kujiunga kabla ya tarehe 10/4/2022 unapewa papo hapo Offa ya Vitabu, michanganuo na templates jumla ni vitu 20 kama ilivyoonyeshwa hapo chini;
Namba zetu ni: 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo. Baada ya kulipia tuma ujumbe usemao, "NATAKA SEMINA NA OFFA YA VITU 20"
OFFA YA VITU 20 ITAKAYOISHA RASMI TAREHE 10/04/2022
1.
KITABU cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha
kiswahili
2.
KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa
biashara (One Page Business Plan) -cha
kiswahili
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili
4.
KITABU
mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN
ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza
5.
KITABU
cha
mwandishi Tim Berry cha JINSI YA
KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza
6.
Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha
kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili
7.
Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara
ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili
8.
Mchanganuo
kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili
9.
Mchanganuo
Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama-
kwa kiswahili
10. Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku
wa nyama- kwa
kiingereza
11. Mchanganuo
Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai -
kwa kiswahili
12. Mchanganuo
Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili
13. Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji
(KIBADA
WATERMELON)-kwa kiswahili
14. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa kiswahili
15. Mchanganuo
wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa
kiingereza
16. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
17. Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
18. Kielezo cha mchanganuo
wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili
19. Kielezo
cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa
kiingereza
20. Somo
maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili
21. Kunganishwa
group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima
Habari! Nahitaji kuandika andiko la ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa na ujenzi wa madarasa matatu ya wanafunzi wenye mahitaji Maalum. Naweza kusaidiwa juu ya hilo?
ReplyDeleteInawezekaka kabisa, tuwasiliane namba zangu ni 0765553030
Delete