Utajua vipi kama biashara yako itaweza kudumu
miaka mingi ijayo, tuseme labda miaka hata mia moja(100) na zaidi? Kuna watu na
hasa wa asili ya Bara la Asia utakuta biashara zao walirithi tangu enzi za
mababu na mpaka leo hii bado zipo na zitaendelea kuwepo. Siri yao kubwa ni kitu
gani?
Mtu yeyote yule anapoanzisha biashara,
kichwani mwake ni lazima awe na vitu hivi muhimu vitatu, Dhamira kuu, Malengo
na Dira. Vitu hivi ndiyo humuongoza katika mchakato wake huo wa kuanzisha
biashara hata ikiwa yeye mwenyewe haelewi kama anavyo kichwani. Na vitu vyote
hivi vitatu ni sehemu ya kitu kingine kikubwa zaidi kinachoitwa, MPANGO WA BIASHARA.
SOMA: Mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.
SOMA: Mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.
Unapokuwa na maono au picha halisi ya
biashara yako kwamba unataka baada ya miaka, hamsini, mia nk.iwe vipi, hautayumbishwa
na vikwazo vya kupita utakavyokutana navyo njiani. Kuna baadhi ya vipengele
vingine katika mpango wako wa biashara vinavyoweza kubadilika kulingana na muda
na hiyo ndiyo tabia ya mipango, inabidi uifanyie marekebisho kila baada ya muda
mfupi kulingana na hali halisi inavyojitokeza lakini pia kuna vitu vingine kama
hivyo vitatu nilivyokutajia vinavyodumu kwa muda mrefu biashara yako utakaotaka
idumu.
Kinacho ua biasharayingi siyo tukio moja
linalotokea ghafla, hapana bali muunganiko wa matukio na makosa madogomadogo
mengi ambayo kama utayawekea mpango mapema wa kukabiliana nayo basi unakuwa na
uwezo wa kuyazuia kabla hayajatokea. Mpango wa biashara hukulazimisha
kuifikiria biashara yako na kuielewa vizuri kwa undani kabla hata haujaanza
kuifanya. Unaanza tu kuifanya, tayari unakuwa umeshaweka mpango wako kwamba
wewe baada ya kuacha biashara hiyo au pengine hata baada ya kufa, ni nani
utakayemuachia aendelee kuiongoza hiyo biashara. Kwa mtindo huo unaweza kuona
biashara itaweza hata kudumu baada ya wewe kuondoka hapa duniani.
Katika mpango wa biashara yako usipange
kufaulu tu peke yake, tambua pia kuna kuanguka na majanga mbalimbali. Hakikisha
vyote unavizungumzia na kuweka mpango mbadala ikiwa vitatokea ufanyeje ili
kupunguza hatari zake. Mpango wa Biashara unakuwa na vipengele muhimu
vifuatavyo lakini siyo lazima uwe navyo vyote kulingana na aina na malengo ya
mpango wako.
Jalada
la nje
Yaliyomo
1.Dhamira
kuu
2.Maelezo
kuhusu biashara
3.Maelezo
kuhusu bidhaa
4.Maelezo
ya soko
5.Mikakati
na utekelezaji
6.Utawala
na wafanyakazi
7.Maswala
ya fedha
Vielelezo.
Kumbuka mpango wa biashara siyo lazima
uandike kwenye karatasi, unaweza tu kupanga kichwani kwako kama walivyokwisha
kufanya watu wengi hapo kabla, sasa na hata baadaye. Lakini ni jambo la faida
zaidi kwako ikiwa utaelewa japo kwa kusoma tu ni jinsi gani mpango wa biashara
unavyokuwa.
Ni jambo zuri pia kuhakikisha mpango wa
biashara yako ikiwa utataka ukupe matokeo mazuri, basi uhakikishe unauandaa
mwenyewe au ikiwa atakuandalia mtu mwingine au mtaalamu, fahamu kila hatua ni
kitu gani kinatakiwa kufanyika, kifupi utafiti wa vipengele mbalimbali
unatakiwa uufanye mwenyewe kwani wewe mwenyewe ndiye utakayeifanya hiyo
biashara na wala si yule atakayekuandikia au mtaalamu. Kwa hiyo ni muhimu sana
mtu kufahamu ni kitu gani huwa ndani ya mpango wa biashara.
SOMA: Kwanini mpango wa biashara wa kuandikiwa siyo mzuri kwako?
SOMA: Kwanini mpango wa biashara wa kuandikiwa siyo mzuri kwako?
Sisi
Self Help Books Tanzania, tuna kila kitu unachohitaji kufahamu
namna mpango wa biashara unavyokuwa, unavyoandikwa na hata mipango/michanganuo
yenyewe halisi iliyokwisha andikwa ya biashara mbalimbali zinazofanywa hapa
Tanzania.
Tuna Kitabu, MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pamoja na SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA
inayoendeshwa kupitia blogu maalumu ya kulipia. Unaweza kupata vitu vyote hivi,
kitabu na semina kwa gharama ndogo tu ya shilingi Elfu 10, badala ya shilingi elfu
20 bei halisi kupitia email yako.
Lipa kupitia namba za simu; 0712202244
au 0765553030, jina litokee
Peter Augustino Tarimo, pamoja na kutuma anani yako ya email, utatumiwa kitabu
ndani ya dakika chache. Ukihitaji kitabu cha karatasi wasiliana na sisi, tupo
Mbezi kwa Msuguri stendi.
0 Response to "JINSI YA KUANZISHA BIASHARA ITAKAYODUMU MIAKA 100 NA ZAIDI IJAYO"
Post a Comment