Ikiwa kama bidhaa ya lile birika la shaba
ingeliweza kuzungumza, ingeliweza kusimulia hadithi ya kusisimua ya mapenzi, ya
wanataaluma wanaume kwa wanawake ambao kila siku huburudishwa nayo.
Mwandishi ana uhakika wa angalao moja ya
hadithi hizo, kwani alikuwa sehemu ya hadidhi hiyo, na yote yalianza siyo mbali
kutoka eneo lilelile ambalo muuza dawa(karani wa duka la dawa) aliponunua
birika la zamani. Ilikuwa ni hapa Mwandishi alipokutana na mke wake, na alikuwa
ni mke wake aliyekuwa wa kwanza kumuelezea juu ya birika la ajabu. Ilikuwa ni
bidhaa ya lile birika waliyokuwa wakinywa wakati alipomuomba kumkubalia “kwa
shida na raha”
Sasa, kwamba unafahamu kilichokuwemo ndani ya
birika la ajabu ni kinywaji maarufu duniani, inapendeza kwamba mwandishi
anakiri kuwa, mji wa nyumbani wa kinywaji hicho ulimpa mke, pia kwamba kinywaji
chenyewe kilimpa msisimko wa mawazo bila sumu, na hivyo kutoa burudisho la
akili lililomwezesha mwandishi kufanya kazi yake nzuri.
Yeyote awaye, popote pale unapoweza kuwa
unaishi, kazi yeyote ile unayoweza kuwa unafanya, kumbuka tu wakati ujao, kila
wakati utakapoona jina “Coca cola” kwamba
ni miliki kubwa sana ya utajiri na ushawishi iliyotokana na wazo moja, na
kwamba kiambata cha ajabu, karani wa dawa – Asa Candler – alichochanganya na
kanuni ya siri kilikuwa ni……Ubunifu !
Simama na ufikirie kuhusiana na hilo kwa muda
kidogo.
Kumbuka, pia kwamba hatua 13 kuelekea utajiri
zilizoelezwa katika kitabu hiki zilikuwa ni chombo, kupitia hicho, ushawishi wa
coca cola umeenezwa kwa kila jiji, mji, kijiji na katika njia panda za dunia .
Wazo lolote unaloweza kubuni lililokuwa zuri na lenye kustahili kama coca cola,
lina uwezekano wa kuiga(kukopi) rekodi kubwa ya kinywaji hiki cha dunia nzima.
Ukweli mawazo ni vitu, na upeo wake wa kufanya kazi ni dunia yenyewe.
Ningefanya
Kitu Gani Kama Ningepata Dolla Millioni Moja
Simulizi hii inathibitisha ukweli wa ule
usemi wa zamani, ‘Penye nia pana njia’ Nilisimuliwa na yule mpendwa mwalimu na
mchungaji, Frank W. Gunsaulus, ambaye alianza kazi yake ya kuhubiri katika eneo
la Stockyards la Kusini mwa Chicago.
Wakati Dr. Gunsaulus alipokuwa chuoni,
aligundua mapungufu mengi katika mfumo wetu wa elimu, mapungufu ambayo aliamini
angeliweza kuyarkebisha ikiwa kama angelikuwa Mkuu wa Chuo. Shauku yake kubwa
kabisa ilikuwa ni kuwa kiongozi mkuu wa chuo cha elimu ambacho vijana wadogo wa
kiume na wa kike wangeweza kufundishwa “kujifunza
kwa vitendo”
Alifanya uamuzi wa kuanzisha chuo kipya
ambacho angeweza kutekeleza wazo lake jipya pasipo kulemazwa na njia za jadi za
utoaji elimu. Alihitaji Dolla Milioni moja ili kutekeleza mradi ! Ni wapi
angelaza mikono yake kwa kiasi kikubwa hivyo cha pesa? Hilo lilikuwa ni swali
lililotawala sehemu kubwa ya mawzo ya mhubiri huyu kijana aliyekuwa na malengo
makubwa.
Lakini hakuweza kuonekana kupiga hatua
yeyote.
Kila siku aliingia kitandani na lile wazo.
Aliamka nalo asubuhi. Alitembea nalo kila mahali alipokwenda. Aliligeuza tena
na tena katika akili yake mpaka likageuka kuwa shauku isiyotulizika. Dolla
Millioni moja ni fedha nyingi. Alitambua ukweli huo lakini pia aligundua ukweli
kwamba kikwazo pekee ni kile ambacho mtu hujiwekea katika akili yake mwenyewe
Alikuwa mwanafilosofia na pia mhubiri,
Dr.Gunsaulus alitambua, kama wafanyavyo wale
wote wanaofanikiwa maishani kuwa, udhahiri
wa lengo ndiyo kituo ambapo mtu ni lazima aanzie. Alitambua pia kwamba
udhahiri wa lengo huchukua umbo, uhai na nguvu unaposaidiwa na Shauku kubwa kulibadilisha lengo hilo kuwa
katika kitu kinacholingana nalo.
Alifahamu ukweli wote huu mkubwa, lakini bado
hakujua ni wapi au ni jinsi gani angeweza kuweka mikono yake kwenye dola milioni
moja. Utaratibu wa asili ingeliweza kuwa ni kukata tamaa na kuacha, akisema ,
‘Ah sawa, wazo langu ni zuri lakini siwezi kufanya nalo chochote kwa sababu
kamwe siwezi kupata dolla millioni moja zinazohitajika’. Hivyo ndivyo hasa
ambavyo watu wengi wangeliweza kusema, lakini sivyo Dr. Gunsaulus alivyosema.
Alichosema yeye, na alichokifanya, ni muhimu
kiasi kwamba sasa namtambulisha na kumuacha azungumze, mwenyewe.
‘Siku moja Jumamosi mchana nilikuwa chumbani
kwangu nikifikiria njia na namna ya kupata fedha ili kutekeleza mipango yangu.
Kwa karibu miaka niwili nilikuwa nikifikiria, lakini sikuwa nimefanya chochote
zaidi ya kufikiria.
Muda ulikuwa umewadia wa kuchukua hatua !
Niliamua mara moja kwamba ningeweza kupata
dolla milioni moja zilizohitajika, ndani ya wiki moja. Ki vipi? Sikujali
kuhusiana na hilo. Jambo kubwa na la muhimu lilikuwa ni uamuzi wa kuzipata
fedha ndani ya muda uliopangwa. Dakika niliyofikiria uamuzi huo, hisia ya ajabu
ya kujiamini ilinijia kwa namna ambayo kamwe sikuwahi kuhisi hapo kabla. Kitu
ndani yangu kilionekana kusema, “Kwanini
hukufikia uamuzi huo muda mrefu? Pesa
zilikuwa zikikusubiri muda wote !”
‘Mambo yalianza kutokea kwa haraka. Niliita
magazeti na kutangaza kuwa ningeweza kutoa mahubiri(hotuba) asubuhi ya siku
iliyofuata yanayohusu, “Ningefanya nini
kama ningepata Dola million moja”
‘Nilikwenda kuifanyia kazi hotuba ile mara
moja. Ni lazima nikueleze, ukweli haikuwa kazi ngumu kwasababu nilikuwa
nikiiandaa hotuba hiyo kwa karibu miaka miwili. Roho yake ilikuwa sehemu yangu
!
‘muda kabla ya usiku wa manane nilikuwa
nimemaliza kuandika hotuba. Niliingia kitandani na kulala na hisia za kujiamini
kwani niliweza kuona mwenyewe kama tayari
nilikuwa nazo dolla milioni moja.
‘Asubuhi iliyofuata niliamka mapema, nikaenda
bafuni, nikasoma hotuba, kisha nikapiga magoti na kusali ili hotuba yangu iweze
kusikika na mtu ambaye angeliweza kutoa pesa zilizohitajika.
‘Wakati nikiwa nasali, tena nilijiwa na zile
hisia za kujiamini, kwamba pesa zingeliweza kupatikana haraka. Kwa taharuki
niliondoka bila kuchukua hotuba yangu, na sikugundua kosa hilo mpaka nilipokuwa
kwenye mimbari yangu na karibu kuanza kuhutubia.
‘Muda ulishakwenda mno kurudi tena kuchukua
karatasi, baraka lioje, badala yake akili yangu ya ndani mwenyewe ilizalisha
vitu nilivyohitaji. Niliposimama kuanza hotuba yangu, nilifumba macho yangu na
kuzungumza kwa moyo wangu wote na roho kuhusu ndoto zangu. Sikuzungumza na wasikilizaji
wangu tu, bali pia niliigiza kama nazungumza na Mungu. Nilieleza ningeliweza
kufanya kitu gani na dola milioni moja ikiwa kiasi hicho kingewekwa mikononi
mwangu. Nilielezea mpango niliokuwa nao akilini mwangu kwa kuanzisha taasisi
kubwa ya kielimu ambapo vijana wadogo wangeliweza kujifunza kufanya vitu kwa
vitendo, na wakati huohuo wakikuza akili zao.
‘Nilipomaliza na kuketi chini, mwanaume mmoja
taratibu alisimama kwenye kiti chake, mistari mitatu kutoka mstari wa mbele na
kuja kuelekea ilipo mimbari(jukwaa). Nilishangaa alikuwa anakuja kufanya kitu
gani. Alikuja mimbarini akanyoosha mkono wake, na kusema, “Mheshimiwa,
nimependa hotuba yako. Ninaamini unaweza kufanya kila kitu ulichosema unaweza
kufanya kama ungekuwa na dola milioni moja. Kuthibitisha hilo nakuamini pamoja
na hotuba yako, kama utakuja kwenye ofisi yangu kesho asubuhi nitakupa dolla
million moja. Jina langu ni Philip D. Armour”
Kijana Gunsaulus alikwenda ofisini kwa bwana
Armour na kupewa Dola Millioni moja. Kwa kutumia fedha zile alianzisha Taasisi
ya teknolojia ya Armour. Hizo ni fedha nyingi kushinda fedha wengi wa wahubiri
walizowahi kuona katika maisha yao yote, bado msukumo wa mawazo nyuma ya pesa
hizo ulianza katika akili ya mhubiri kijana katika nukta ya dakika.
Dolla Milioni moja zilizohitajika
zilipatikana kama matunda ya wazo . Nyuma ya wazo kulikuwa na Shauku ambayo kijana Gunsaulus alikuwa
ameilea katika akili yake kwa takribani miaka miwili.
Chunguza
ukweli huu muhimu:
ALIZIPATA FEDHA NDANI YA MASAA 36 BAADA YA
KUFIKIA UAMUZI NDANI YA AKILI YAKE MWENYEWE WA KUZIPATA NA KUAMUA JUU YA MPANGO
KAMILI(DHAHIRI) WA KUZIPATA !
Kulikuwa hakuna kitu kipya au cha ajabu juu
ya mawazo yasiyokuwa na uhakika ya kijana Gunsaulus kuhusiana na dola millioni
moja na kuziwekea matumaini hafifu. Wengi kabla yake, na wengi tangu wakati
wake, wamekuwa na mawazo yanayofanana na yakwake. Lakini kulikuwa na kitu
fulani cha kipekee na tofauti kuhusiana na uamuzi alioufikia katika jumamosi
ile ya kukumbukwa, wakati alipoyatupa nyuma mawazo yasiyokuwa na uhakika na
kutamka waziwazi, “Nitazipata pesa ndani ya wiki moja !”
Mungu inaonekana hujitupa mwenyewe upande wa
watu wanaofahamu kwa uhakika kile kitu wanachokitaka, ikiwa wana nia thabiti ya
kukipata kitu hicho !
Zaidi ya hapo kanuni ambayo Dr. Gunsaulus
aliitumia kupata dola milioni moja bado inaishi ! Inapatikana kwako ! Sheria hii ya wote
inafanya kazi leo kama ilivyokuwa wakati kijana mhubiri alipoitumia kwa
mafanikio. Kitabu hiki kinaelezea hatua kwa hatua, vipengele 13 vya sheria hii
kubwa na kupendekeza jinsi zinavyoweza kuwekwa katika matumizi.
Ona kwamba Asa Candler na Dr. Frank Gunsaulus
walikuwa na tabia moja inayofanana . Wote waliujua ukweli unaoshangaza kwamba,
MAWAZO YANAWEZA YAKAGEUZWA KUWA PESA KUPITIA NGUVU YA LENGO LILILOKUWA DHAHIRI,
PAMOJA NA MIPANGO KAMILI(DHAHIRI)
Kama wewe ni mmoja kati ya wale wanaoamini
kwamba kufanya kazi kwa bidii na uaminifu tu peke yake vitaleta utajiri, achana
na wazo hilo ! Siyo kweli ! Utajiri unapokuja kwa kiasi kikubwa kamwe siyo
matokeo ya kazi ngumu! Utajiri huja, kama utakuja, kutokana na matakwa
yaliyokuwa thahiri, chini ya matumizi ya kanuni zilizokuwa wazi, na siyo kwa
kubahatisha au bahati njema.
Kwa ujumla, wazo ni msukumo wa mawazo unaohimiza
kitendo kwa kuvutia ubunifu. Wawakilishi wote wakubwa wa mauzo hufahamu kwamba
mawazo yanaweza kuuzwa mahali ambapo bidhaa haiwezi. Wawakilishi wa mauzo wa
kawaida hawaelewi hili – hii ndiyo sababu wao ni wa “kawaida”
Mchapishaji wa vitabu alifanya ugunduzi wemye thamani kubwa kwa
wachapishaji kwa ujumla. Alijifunza kwamba watu wengi hununua majina ya vitabu
na wala siyo yaliyokuwemo kwenye vitabu. Kwa kubadilisha tu jina la kitabu
kimoja kilichokuwa hakinunuliwi haraka, mauzo yake kwenye kile kitabu yalipanda
juu zaidi ya nakala milioni moja. Ndani ya kitabu hakukubadilishwa kwa namna
yeyote ile. Aliondoa tu jalada lililokuwa na jina ambalo halikuwa likiuza, na
kuweka jalada jingine jipya lenye jina lililokuwa na thamani ya “mauzo ya
filamu”
Hivyo, rahisi kama inavyoweza kuonekana,
ilikuwa ni wazo! Ulikuwa ubunifu!
Hakuna bei moja maalumu ya mawazo. Waanzilishi wa mawazo huweka bei
zao wenyewe, na ikiwa ni wajanja, hulipwa kiwango hicho.
Tasnia ya picha zinazotembea(filamu)
ilitengeneza kundi zima la mamilionea . Wengi wao walikuwa wanaume ambao
hawakuweza kubuni mawazo – lakini walikuwa na ubunifu wa kutambua mawazo
walipoyaona.
Andrew Carnegie alifahamu kidogo sana juu ya
namna ya kutengeneza chuma cha pua(steel) – nina maneno yake mwenyewe Carnegie
kwa hili – lakini alitekeleza kwa vitendo matumizi ya kanuni mbili kati ya
kanuni zilizoelezwa kwenye kitabu hiki na kuifanya biashara ya chuma cha pua
kumpa utajiri.
Habari za karibu kila utajiri mkubwa huanzia
siku ambayo muanzilishi wa mawazo na muuzaji wa mawazo wanapokutana na kufanya
kazi kwa masikilizano. Carnegie yeye mwenyewe alizungukwa na wataalamu
walioweza kufanya vitu vyote ambavyo hakuweza kuvifanya , watu walioanzisha
mawazo na watu walioyaweka mawazo katika vitendo na kuwafanya wao wenyewe na
wengine kuwa matajiri wakubwa.
Mamilioni ya watu huishi wakitumaini mazingira
yanayofaa(bahati). Pengine mazingirayanayofaa yanaweza yakampa mtu
fursa, lakini mpango salama zaidi siyo wa kutegemea bahati. Ilikuwa ni bahati
iliyonipa fursa kubwa zaidi ya
maisha yangu – lakini miaka 25 ya juhudi thabiti ilihitajika kwenye fursa ile
kabla haijageuka kuwa rasilimali.
Mazingira yalijumuisha bahati yangu nzuri ya
kukutana na kupata ushirikiano wa Andrew Carnegie. Alipanda ndani ya akili
yangu wazo la kuziunganisha kanuni za kutimiza malengo kuwa filosofia ya
mafanikio. Maelfu ya watu wamenufaika na ugunduzi uliofanyika katika miaka 25
ya utafiti, na utajiri mkubwa umelimbikizwa kupitia matumizi ya filosofia hii.
Mwanzo ulikuwa rahisi. Ilikuwa ni wazo ambalo mtu yeyote angeliweza kulibuni.
Mazingira mazuri yalikuja kupitia Carnegie
lakini vipi kuhusiana na kukata shauri, uthahiri wa lengo, shauku ya
kulifikia lengo na juhudi zisizokoma kwa miaka 25? Haikuwa Shauku ya kawaida iliyoweza
kuhimili hali ya kuvunja matumaini, kukatisha tamaa, anguko la muda,
kukosolewa, na tuhuma zisizoisha, juu ya “kupoteza muda”. Ilikuwa ni Shauku
kuu, isiyotulizika !
Mwanzoni wakati Bwana Carnegie alipopanda
wazo katika akili yangu, lilibembelezwa, kutunzwa, na kushawishika kubakia hai.
Taratibu, wazo liligeuka kuwa kubwa chini ya nguvu zake lenyewe, na
lilinibembeleza, kunilea na kuniendesha. Mawazo yako hivyo. Kwanza unatoa uhai,
kitendo na ulinzi kwa mawazo, na halafu yanapata nguvu yao yenyewe na kusukumiza
kando upinzani wote
Mpenzi msomaji na huo ndio mwisho wa
sehemu yetu hii ya 6, usikose sehemu ya 7, "MIPANGO MATHUBUTI"
0 Response to "KANUNI YA SIRI YA COCA COLA, BIRIKA LA AJABU NA WAZO LA DOLA MILIONI 1"
Post a Comment