MCHANGANUO WA BIASHARA SALOON YA KIUME: MAELEZO NA HESABU ZAKE KAMILI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MCHANGANUO WA BIASHARA SALOON YA KIUME: MAELEZO NA HESABU ZAKE KAMILI

Karibu tena ndugu msomaji wa blogu hii ya jifunzeujasiriamali katika awamu ya pili ya SEMINA yetu ya jinsi ya kuandika mpango au mchanganuo wa biashara. Kama makala hii iliyotangulia  iliyokuwa na kichwa cha habari, “BAADA YA MASOMO 11 YA SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA, SASA INAINGIA AWAMU YA PILI” ilivyosema, awamu hii ya pili tutaweka msisitizo zaidi katika maeneo ya kuandika kwa vitendo pamoja na hesabu za michanganuo mbalimbali ya biashara kwa undani.

Kwa kuanza leo tutajadili fungu la kwanza la vipengele vya mchanganuo wa Saluni ya kiume ambavyo kwa mujibu wa post hiyo ya utangulizi vipengele vitakavyoanza kujadiliwa katika mchanganuo huo wa saloon ya kiume ni hivi 4;

1. Maelezo ya biashara au kampuni,
2. Maelezo ya huduma,
3. Mikakati na utekelezaji pamoja na
4. Uongozi na Utawala

Katika fungu la vipengele hivi tutatazama hatua kwa hatua namna unavyoanza kukusanya taarifa mbalimbali zinazohusiana na vipengele hivyo, ni taarifa zipi za kuweka na zipi za kuacha kulingana na malengo na mikakati uliyojiwekea, kisha tutaona unaandika vipi aya za kila kipengele.

Mchanganuo wa Saluni inayochanganuliwa inaitwa BOYS TO MEN BARBER SHOP iliyopo mtaa wa Agrey Kariakoo jijini Dar es salaam. Siku ya kwanza leo tutachanganuo vipengele hivyo vinne, siku ya pili kesho tutachanganua sehemu ya Soko na siku ya tatu keshokutwa tutachanganuo kipengele cha fedha. Hivyo nakuomba ndugu msomaji usikose hata siku moja kwani ratiba itazingatiwa na wakufunzi wako tupo muda wote kwenye kompyuta tukisubiri mirejesho na maswali mbalimbali toka kwa washiriki kama awamu iliyopita ya semina hii. 


Kwa washiriki wapya wanaojiunga sasa watapata kuyasoma, (full access) masomo yote ya awamu iliyopita sawasawa na wale waliotangulia, kupitia blogu yetu maalumu na email.

Kwa wale washiriki waliokwishajiunga katika awamu ya kwanza ya semina hii hawatalipa tena kiingilio mara ya pili, bali wataendelea kujifunza masomo kama kawaida. Kumbuka lengo kubwa ni kila mshiriki kuweza kuandika mpango wa biashara mwenyewe bila matatizo.


Ili uweze kuyasoma masomo haya yote pamoja na ya awamu iliyopita, lipa ada ya semina Shilingi elfu 10 kupitia namba za simu 0712 202244  au  0765 553030  jina ni Peter Augustino Tarimo. Tuma pia na email yako ya GMAIL katika moja ya namba hizo kwa ajili ya kuunganishwa katika blogu hii yenye MASOMO YA SEMINA, kitabu cha bure softcopy cha michanganuo, pamoja na kutumiwa masomo moja kwa moja kwenye email hiyo kwa njia za pdf na mp3 kwa tahadhari ya blogu kutokufunguka kwa sababu mbalimbali zikiwemo za network kuwa chini. Lakini pia masomo hayo yote yatakuwa katika blogu yako hii MAALUMU.

KARIBU SANA UJIUNGE LEO MASOMO YANAANZA!

0 Response to "MCHANGANUO WA BIASHARA SALOON YA KIUME: MAELEZO NA HESABU ZAKE KAMILI"

Post a Comment