Mtu kuanzisha na kuendesha biashara ndogo
toka mwanzo ni jukumu zito na linalogharimu kutokana na majukumu mengi
yanayokukabili wewe mwenyewe kama vile, kufikiria wazo la biashara itakayofaa, kutafuta
mtaji wa kuanza biashara, kuajiri wafanyakazi au mfanyakazi, kumfundisha
mfanyakazi/wafanyakazi nk.
Mambo hayo yote yanahitaji uangalizi wako kwa
wakati mmoja. Na tena isitoshe basi mambo hayo huhitaji muda na pesa,
rasilimali ambazo zote huwa adimu mno katika hatua za awali kabisa za biashara
inayoanza moja. Hata hivyo mbinu au njia zifuatazo zina uwezo wa kumuwezesha
mtu yeyote anayejikuta katika hatua za kuanzisha biashara kuweza kujibana
katika kila rasilimali aliyokuwa nayo kusudi mambo yaweze kwenda vizuri.
1.
Anza na kile ulichokuwa nacho kwanza.
Kabla hujaanza kufikiria utumie pesa kidogo
ulizokuwa nazo kwa ajili ya vitu mbalimbali vya kuanzia mfano sehemu ya
kufanyia biashara au chumba, fikiria njia zingine mbadala kwa mfano, kutumia chumba
cha ziada nyumbani au hata chumba chako mwenyewe cha kulala, sebule nk. badala
ya kupanga chumba cha gharama kubwa.
Hata ikibidi ni lazima upange chumba kwa
ajili ya biashara hiyo, basi kipambe kwa kutumia fenicha za ziada za nyumbani
na hata vitu kama kompyuta au simu tumia kwanza vile vyakwako binafsi. Elekeza
nguvu zako zaidi katika mauzo badala ya muonekano wa ofisi na fenicha, vitu
vinavyotakiwa kuja baadae.
SOMA: Soma vitabu hivi vya maisha na mafanikio.
SOMA: Soma vitabu hivi vya maisha na mafanikio.
2. Jiepushe
na utititiri wa njia za mawasiliano.
Mara nyingi biashara inayoanza huwa na mtu
mmoja au hata wakiongezeka sana labda ni wawili, sasa kitendo cha mtu mmoja
kuanza mara kusikiliza simu iliyopigwa, mara kuangalia meseji ya simu
iliyoingia, akigeuka huku email imeingia, huku simu imeita tena, facebook,
twitter, instagram, whatsapp nk. vyoote hivyo vitakupotezea muda wako mwingi na
hata pesa kwa ajili ya mabando ya kila mara. Badala yake waelekeze wateja wako
katika jukwaa moja tu la mawasiliano au mawili na utaokoa muda mwingi na fedha.
3.
Chukua wafanyakazi wa muda badala ya wale wa kudumu.
Unapoona majukumu yamekuwa mengi na unahitaji
mtu wa kukusaidia, tafuta mtu mwenye utaalamu husika lakini kwa mkataba wa muda
mfupi au kazi fulani tu, na akishaimaliza basi unamlipa mnaachana, badala ya
kuajiri mfanyakazi wa kudumu ambaye ni gharama kubwa kuwa naye kila mwezi.
4.
Nunua bidhaa/malighafi au vifaa vya ofisi kwa bei ya jumla.
Kitu chochote kile katika biashara yako
unachojua utakuja kuhitaji kukitumia mara kwa mara kwa mfano hata vitu kama
kalamu, karatasi nk. vinunue kwa bei ya jumla kusudi kupunguza gharama
utakayokuja kulipa ukinunua kimoja kimoja.
5. Tumia
teknolojia ya kisasa kama vile, intaneti, mashine za
kielectroniki za risiti na simu za kisasa kuokoa gharama za matumzi ya
makaratasi mengi. Katika matumizi ya teknolojia pia hakikisha vitu kama baadhi
ya programu ‘software’, unatumia zile zisizokuwa za gharama kubwa au
zinazopatikana bure(free) mitandaoni.
SOMA: Siri 10 za utajiri wa Aliko Dangote, tajiri namba 1 Afrika
SOMA: Siri 10 za utajiri wa Aliko Dangote, tajiri namba 1 Afrika
Na huo ndio mwisho wa makala yetu hii ya leo inayohusu jinsi ya kuanza biashara, au uanzishaji wa biashara mpya toka mwanzo(Startups). Kwa makala zaidi juu ya kipengele hicho angalia katika makundi ya makala pale pembeni mwa hii blog(tags) au chini(lebels) yenye jina “Kuanzisha biashara”
………………………………………………………………..
Ukihitaji Huduma zetu mbalimbali, bonyeza maandishi
hapo chini kupata maelezo zaidi.
0 Response to "NJIA 5 ZA KUKUZA MAPATO YA BIASHARA NDOGO KWENDA HATUA YA JUU"
Post a Comment