Kila kitu Duniani kinabadilika kwa kasi ya ajabu sana
tangu mapinduzi mapya ya viwanda duniani(new industrial revoluton) yalipoanza
miongo kadhaa iliyopita. Na mabadiliko hayo yamesababisha biashara nayo
kubadilika kwa spidi hiyo hiyo kwani huwezi kutenganisha biashara na teknolojia
kwa urahisi.
Kwa kadri njia mpya au teknolojia mpya za kufanya mambo mbalimbali
duniani zinavyoibuka, basi unakuta na biashara nayo inafuata mkumbo huo huo.
Mapinduzi mapya ya kiviwanda yalianza tangia matumizi
ya kompyuta yalipoanza kushika kasi
katika miaka ya 50 na 60, tangu hapo dunia imeshuhudia kuporomoka kwa teknolojia
nyingi zilizokuwepo kabla sambasamba na kuzaliwa teknolojia nyinginezo mpya
kabisa. Na hali hiyo bado inaendelea na itaendelea kushuhudiwa kwa miaka mingi
inayokuja. Kila mabadiliko hayo yanapotokea duniani watu huwa na hofu, lakini
pia huwa kunakuwa na matumaini na vyote hivi viwili ni lazima vitokee kutokana
na sababu kwamba kunatokea uharibifu na ujenzi kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi moja kutoka Silicon
Valley nchini Marekani iitwayo, Singularity University(SU). Taasisi hii inafadhiliwa
na shirika la NASA na Kampuni ya Google na inalenga katika kutabiri maswala ya
maendeleo ya sayansi na teknolojia zinazobadilika kwa kasi zaidi duniani katika
kusaidia kubainisha ni kipi kifanyike wakati tuliokuwa nao sasa na kipi
kitafanyika katika wakati ujao unaokaribia kwa kasi.
Kwenye mlolongo wa makongamano ya taasisi hiyo wanalenga
zaidi kuzungumzia teknolojia zinazobadilika haraka kwa kasi na ambazo
huziathiri sekta za fedha, madawa, afya, elimu, viwanda, na chakula. Wanasema kwa
kiasi kile teknolojia inavyobadilika na kukua kwa kasi, kizazi kijacho cha
uongozi katika biashara kinatakiwa kiwe
na uwezo wa kuyasimamia hayo mabadiliko yanayojenga pamoja na yale mabadiliko hasi yanayobomoa
kwa haraka na kwa ufanisi kuliko muda wowote hapo kabla. Kubomoa
kunakojenga(creative destruction) katika
uchumi wa soko huria kunaongezeka kwa kiwango cha kipeo cha kumi.
Hivi karibuni, Udo Gollub kutoka Berlin nchini Ujerumani
baada ya kuhudhuria kongamano hilo aliandika
baadhi ya yale yaliyojadiliwa. Lakini ukumbuke kwamba mambo hayo
yaliyozungumzwa yote ni utabiri wa mwenendo wa teknolojia zinazobadilika kwa kasi uliofanyika na taasisi ya Singularity
University, hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kamilifu, kila kitu ni
mfululizo wa mabadiliko.
Utafiti huu ni kwa ajili tu ya kutia moyo na kusisimua
mawazo na umetumia baadhi ya dondoo muhimu kutoka katika kongamano hilo. Katika
ripoti hiyo pia mimi mwenyewe nitaongeza baadhi ya uchunguzi wangu binafsi
nilioufanya katika teknolojia mbalimbali na nyingine zilizowahi kuwa hapa
Tanzania lakini zikatoweka na kuja zingine.
RIPOTI
KAMILI.
Kampuni ya kutengeneza kamera na vifaa vya picha ya Kodak
iliyoanzishwa mwaka 1888 na George Eastman mpaka kufikia mwaka 1998 ilikuwa ni
kampuni inayoongoza katika sekta hiyo na hakuna mtu ambaye angeliweza kudhania
kama miaka michache tu mbele ingeliweza kuja kufilisika kabisa na mahali pake
kuchukuliwa na makampuni mengine yaliyokuja na teknolojia za kutoa picha za
dijitali. Kile kilichotokea kwa Kodak kitatokea katika sekta nyingine nyingi
ndani ya miaka 10 ijayo na watu wengi hawawezi kuliona hilo likija.
Ungeweza kufikiria kwamba miaka 3 tu baada ya 1998
usingeliweza tena kupiga picha katika mikanda ya kamera ya film? Hata hivyo si
kama kamera za digitali ziligunduliwa juzijuzi tu hapana, ni tangu mwaka 1975
lakini teknolojia yake haikuwa bado ikiweza kutoa picha zenye ubora wa hali ya
juu na hata hivyo watu kama kawaida kinapoanza kitu kipya hawakuichangamkia
sana na ilichukua muda mrefu kukubalika sokoni. Mgunduzi wake Steven Sasson a kiwa ni
mfanyakazi katika kampuni hiyo ya Kodak, wala viongozi wa Kodak hawakuweza
kuona fursa hiyo, wangelijua wakamtumia pengine leo hii wasingelikuwa
wamefilisika.
Kilichotokea kwa Kodak pia kitatokea katika sekta za
afya, usafirishaji, nishati, elimu, kilimo, ajira, mashine zinazofanya kazi
kama binadamu na hata katika ufyatuaji wa maumbo mbalimbali(3D Printing).
Zitakuwa ni zama mpya za Mapinduzi mapya ya kiviwanda ya teknolojia
inayobadilika kwa kasi.
Unaweza
kuona hata hapa Tanzania mabadiliko hayo yanavyotokea, kwa mfano miaka michache
nyuma kulikuwa na teknolojia zilizotamba hapa kama vile mikanda ya redio za
kassetti, mikanda ya video(VHS) na redio kaseti zenyewe leo hii hata watoto
waliozaliwa miaka kumi tu iliyopita hawawezi kujua kama kulikua na vitu vya
namna hiyo. Teknolojia zingine zimechukua mahali pake kwa kasi, DVD, DVD players,
CD, Memory card, Flash disks, Hard disks, Kompyuta na Simu za mikononi ndiyo
zinazotamba sasa.
Nakumbuka
miaka ya 90 kuingia 2000 wakati naandaa jarida(gazeti) letu nililokuwa likitoka
kwa mwezi, lilikuwa mfano wa majarida yale ya Sani ya zamani lakini tulikuwa
tukiandika stori za kawaida. Tulikuwa tunatumia kompyuta moja, nadhani ilikuwa
Pentium, 66 MHZ wakati huo hakukuwa na mitandao ya kijamii, njia pekee za watu
kujieleza na hata kutoa maoni yao kupitia vyombo vya habari ilikuwa zaidi ni
kwa kupitia magazeti, majarida na kidogo redio. Teknolojia haikuwa imekua kama
ilivyokuwa sasa hivi, kuandaa gazeti mpaka ukalifikishe kwa mchapaji ilikuwa ni
shughuli pevu kwelikweli kwa mtu ambaye hukuwa na uwezo mkubwa wa pesa.
Tukiwa
hatuna kifaa chochote cha kubebea kazi kama flash za siku hizi, kupeleka jarida
lile kwa mchapaji ambaye alikuwa ni kampuni ya Business Printers wakati huo
ilitubidi tubebe kompyuta nzimanzima mpaka pale Kariakoo gerezani, wafanyakazi
wa Business Printers acha watucheke, “nyie vipi si mngetumia CD au email”. Sawa
CD zilikuwepo lakini kompyuta yetu haikuwa na CD ROM ya kuweza kuburn cd, na
pia email hatukuwa na moderm ya kuunganisha intaneti ambazo wakati huo zilipatikana
kwa tabu tena mpaka uwe na line ya simu ya TTCL.
Vifaa
pekee wakati huo vilivyopatikana kwa urahisi kwa ajili ya kusevu au kubeba faili
za kompyuta zilikuwa ni Floppy disk au 3.5
inch diskette, hizi zilikuwa zinafanya kazi sawa na flash disks au memory card lakini
tatizo lilikuwa, havikuwa na uwezo wa kubeba mafaili makubwa kama gazeti,
vilikuwa na ukubwa wa 1.44MB pekee.
Toleo
lililofuata tukaamua kuchomoa hard disk tukaipeleka, wao kule kiwanda cha
kuchapa wakaiunganisha na kompyuta zao ili kuweza kukopi kazi yetu kwa ajili ya
mchakato wa kuichapa. Baadae sasa tukaja kuwapata jamaa fulani pale Kariakoo
waliokuwa wakitengeneza kompyuta ikawa tunawapelekea hard disk wanatoa kazi na
kuiburn kwenye CD ndipo sasa tunakwenda na CD kule kiwandani.
Changamoto
nyingine tuliyoipata ilikuwa ni katika picha, ilikuwa ili uweze kuingiza picha
katika kompyuta ni lazima kwanza picha hiyo iwe katika mfumo wa dijitali na kwa
kipindi hicho kamera pekee zilizotumika kupiga picha ni zile za film, ambazo
picha zilitoka kwenye karatasi hivyo ili uweze kuitumia katika kompyuta ni
lazima kwanza ukaiscan na scaner, uiweke kwenye diskette ndipo uje uihamishie
katika kompyuta yako kwa ajili ya kuitumia katika gazeti au jarida. Picha
zilizopigwa na kamera za digital zilikuwa bado hazijasambaa sana ingawa
zilishaanza kuwepo na simu za kamera ndio kwanza zilikuwa wala hazipo.
Kwa
ujumla program za kudizaini vitu kama majarida, vitabu na magazeti hazikuwa
zimeboreshwa sana kama siku hizi, ‘Desk
Top Publishing’ ilikuwa ndiyo ipo katika hatua zake za mwanzo kabisa ingawa
ilikuwa imekwishaanza kufanya kazi, Software za kutengeneza kurasa kama vile
Quark express, Indesign na Adobe Photoshop zilikuwepo lakini zilikuwa ghali, haikuwa
rahisi sana kwa kampuni ndogo kuwa nazo. Badala yake tulitegemea zaidi programu
moja iliyoitwa Page maker kwa ajili
ya shughuli za uandaaji jarida.
Lakini
kipindi hicho mambo yalibadilika kwa kasi sana, ndani ya miaka miwili tu au
mitatu kila kitu kilibadilika, tukaanza kushuhudia mitandao ya kijamii
iliyoanza taratibu kuondoa ule ukiritimba wa vyombo vya habari mama kama
magazeti, vijarida na redio, kukaanza kuingia kompyuta zenye nguvu na spidi
kubwa zaidi, Pentium 1 mpaka Pentium 4, zikaingia Flash disk, memory card, card
reades, simu za mkononi, external hard disks na teknolojia nyinginezo kibao
ambazo miaka mitatu nyuma usingeliweza kudhania kabisa kama zingekuja kuwepo.
Kasi ya mabadiliko hasa katika teknolojia ya mawasiliano
siyo ya kawaida kama tuliyozoea katika mabadiliko ya vitu vingine duniani,
wakati mabadiliko ya kawaida yakifuata utaratibu wa hesabu, 1, 2, 3, 4,…………mpaka
10, mabadiliko ya kasi ya teknolojia, yenyewe huhesabu 2, 4, 8, 16,………mpaka
1024 kwa mfano ukipiga hatua 30 tu za kawaida ni sawa na umbali kwenda mwezini
na kurudi wa mabadiliko hayo ya kasi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Katika kizazi cha kompyuta za mwazo miaka ya 50,
wanafunzi waliweza kutumia kompyuta moja kubwa iliyojaza chumba kizima lakini
leo hii kompyuta unayotumia kwenye simu yako ya mkononi, ni ndogo zaidi mara
elfu na iliyokuwa na nguvu mara elfu moja zaidi na bado miaka mingine 25 ijayo
itazidi kupungua ukubwa na gharama. Kipimo cha kasi ya mabadiliko katika
teknolojia ya habari na mawasiliano ni kanuni iitwayo “Gordons Moors Law”
isemayo, “Namba ya transistors katika saketi ya IC(intergrated circuit)
huongezeka mara mbili karibu kila baada ya miaka 2”
Lakini ni nini kitatokea baada ya kanuni hiyo kufikia
ukomo?, maana itafika mahali hizo transistors zitashindikana kuongeza kama
ilivyokuwa miaka hiyo ya 50, vacuum tubes(diodes) zilivyoshindwa kupunguzwa
ukubwa ndipo zikagunduliwa transistors. Na wakati huo, SU wanatabiri kuwa ni kuanzia
mwaka 2020 lakini habari njema ni kuwa wanasema kitakuja tena kizazi kingine
cha kompyuta kilichokuwa na nguvu zaidi(sixth
paradigm) au (three-dimensional, self-organizing molecular circuits.) kama ilivyokuwa kutoka vacuum tubes, transistors mpaka
Intergrated Circuit(IC)
Software ndizo zitakazokuwa zikitawala katika
sekta nyingi kwa miaka 5 – 10 itakayofuata kama tunavyoshuhudia sasa hivi,
kampuni mpya ya teksi ya Uber
inatumia software tu na wala hawamiliki hata gari moja lakini ndiyo wanaomiliki
biashara ya tax dunia nzima kwa sasa. Halikadhalika pia kwa Airbnb katika sekta
ya hoteli, ingawa hawana jengo lolote. Kwa hiyo mabadiliko haya ingawa kwa
upande mmoja yanabomoa au kuharibu zile fursa zilizokuwepo zamani lakini pia
yanatengeneza fursa nyingine nyingi mpya. Hivyo jiandae kwa vyote viwili, fursa
lakini pia hatari au maanguko.
Maroboti(Artificial
Intelligence)
Singularity
University(SU) wanatabiri kuwa ifikapo mwaka 2030 kompyuta itakuwa na akili
kumshinda binadamu. Chip mpya ijulikanayo kama “Virtual Processing Unit” (VPU)
iliyo na uwezo wa kukokotoa mpaka mara
trilioni 8 kwa sekunde moja itakuwa na
kasi kubwa sana kushinda hata kasi ya mawazo ya binadamu.
Kwa mfano
huko Marekani sasa hivi wanasheria wanaomaliza vyuo wameshaanza kupata ugumu wa
kupata ajira kutokana na kampuni moja iitwayo IBM Watson inayotumia software
kutoa huduma za kisheria kwa haraka
zaidi na katika usahihi mkubwa asilimia 90% kulinganisha na asilimia 70% unapopata
ushauri kutoka mwanasheria wa kawaida( binadamu). Hapo baadae ni wanasheria
wale waliobobea tu ndiyo watakaopata ajira kiurahisi.
Siyo
hivyo tu Kampuni hiyo pia ina “madaktari
wa bandia” waliokuwa na uwezo wa kupima na kugundua kansa kwa usahihi mara
4 zaidi kushinda daktari binadamu na wanaweza pia wakatengeneza roboti
itakayokuwa mshauri katika maswala ya kifedha. Face book nao wametengeneza software iliyo na
uwezo wa kugundua sura ya mtu vizuri zaidi kushinda binadamu.
Magari yanayojiendesha yenyewe bila dereva
Ifikapo mwaka 2018 magari
yasiyokuwa na dereva yataanza kuonekana mitaani na kuanzia 2020 kwenda mbele
teknolojia ya zamani ya magari haya ya kawaida tuliyoyazoea itaanza kukumbwa na
mparaganyiko. Watu hawatakuwa tena na sababu ya kumiliki magari, utaita gari
kwa simu yako ya mkononi, litakuja na kukubeba mpaka unakotaka kwenda, hutakuwa
na haja ya parking wewe kazi yako ni kulipa na gari kuondoka zake. Tena
isitoshe watu watakuwa na uwezo wa kufanya shughuli zao wakati wakisafiri ndani
ya magari hayo.
Ajali zitapungua sana, hakutakuwa
na bima tena au zitakuwepo chache, vyuo vya udereva vitakufa, maeneo ya parking
yatageuzwa ya shughuli zingine, na hata watu hawatakuwa na sababu tena ya
kupanga maeneo karibu na miji kutokana na usafiri kuwa ni wa haraka na salama,
mtu anaweza akaishi morogoro kazi akafanyia Dar. Kelele zitapungua kutokana na
magari mengi kutumia umeme(Tesla).
Kama
ilivyokuwa kwa sekta za teknolojia ya habari na mawasiliano katika maswala ya
vingamuzi, (analojia kwenda dijitali), hapa Tanzania sekta ya usafirishaji na
miundo mbinu kwa ujumla inabadilika kwa kasi kubwa, tumeshuhudia mabadiliko
mengi ngani ya kipindi kifupi sana. Miaka mitatu tu nyuma hakuna mtu ambaye
angeweza kuamini kama leo hii
kusingekuwa tena na daladala au hice(vipanya) vinavyokwenda kariakoo kutoka
Ubungo na Mbezi.
Ujio
wa Mabasi ya Mwendo kasi umeharibu ajira za madereva wengi wa daladala,
makondakta na wapiga debe lakini wakati huo huo umeibua ajira mpya kwa watu
wengi kupitia ujenzi wa vituo vya mabasi hayo(UDART), madereva wa Mabasi ya
mwendokasi, wahudumu katika vituo, wakatishaji tiketi, walinzi pamoja na
wanaofanya usafi katika vituo na ofisi zao.
Bado
tutegemee mabadiliko mengine ya kasi na ya haraka katika kipindi kifupi sana
kijacho. Yanakuja mabadiliko makubwa katika usafiri wa barabara, barabara za
juu(flyovers), treni za umeme, na mabasi yaendayo kasi kuzunguka jiji zima la
Dares salaam. Magari yaendayo kwa nguvu za umeme nayo yanategemewa kuingia muda
siyo mrefu.
Sekta
ya Maji.
Kutokana na umeme wa jua kuzidi
kuwa rahisi maji safi nayo yatapatikana kwa urahisi zaidi kwani maji ya chumvi
yataweza kuondolewa chumvi(desalination) kwa urahisi zaidi. Kuondoa chumvi kwa
mita moja ya ujazo ya maji zinahitajika Kilowatt 2 tu za umeme huo, Kumbuka Dunia
haina uhaba wa maji bali maji mengi ni ya chumvi yasiyofaa kwa matumizi ya
kawaida ya binadamu.
Afya.
Kampuni moja iitwayo, Qualcomm
inadhamini mashindano ya dola milini 10 kuleta huduma za afya kiganjani na
tayari kuna makampuni 312 katika nchi 38 yanayoshindana kuunda kifaa cha
matibabu kinachoitwa TRICORDER ambacho kitafanya kazi na simu za mkononi
kugundua aina yeyote ile ya ugonjwa uliokuwa ndani ya mwili wa binadamu baada
ya mtu huyo kukipumulia, kuweka sampuli ya damu pamojana kuscan macho.
Ufyatuaji
wa maumbo ya vitu(3D Printing)
Kama vile unavyotoa fotokopi ya
maandishi ya kitu, zipo printa maalumu ambazo unaweza kukitoa kitu chochote
kile kama kilivyo. Kwa mfano unataka kiatu cha namna fulani, unakipiga picha(scan)
kile kitu na kisha unakiprint(kukiunda) kama kilivyo. Halikadhalika unaweza
kutoa spea za aina mbalimbali za mashine kama magari, ndege, pikipiki nk. Huko
nchini china wameanza hata ku3D majengo ya ofisi na inakisiwa ifikapo mwaka
2027 karibu asilimia 10% ya vitu vyote vinavyozalishwa viwandani vitakuwa
vinaweza kufyatuliwa.
Fursa za biashara.
Ikiwa unafikiria kuingia katika
biashara fulani, hebu jiulize kwanza kama biashara hiyo itakuwepo miaka kadhaa
ijayo au haitakuwepo, na kama jibu ni itakuwepo basi jiulize tena ni kwa namna
gani utakavyoweza kuitekeleza biashara hiyo haraka iwezekanavyo. Na kama
biashara hiyo haiwezi kufanyika kupitia simu yako, sahau kabisa kuhusiana na
wazo la biashara hiyo. Biashara yeyote ile iliyokuwa ikionekana ni yenye faida
katika karne ya 20 itakuwa haina faida tena katika karne ya 21.
Tayari kuna application iitwayo, “moodies”
inayoweza kukueleza kama upo katika mudi gani. Ifikapo 2020 kutakuwa na app
itakayokuwa na uwezo wa kutafsiri hali ya uso wa mtu ikiwa kama anachozungumza
ni ukweli au uwongo. Hebu fikiria itakuwaje wakati wanasiasa watakapokuwa
wakinadi sera zao majukwaani wakati wa kampeni huku ukiwa na simu yako yenye
uwezo wa kutambua ikiwa anatoa sera za uwongo au za kweli.
Ajira.
Miaka 20 ijayo asilimia 70 – 80%
ya kazi zitatoweka na kutakuwa na kazi mpya nyingine ila haijulikani ikiwa kutakuwa
na kazi mpya za kutosha katika kipindi kifupi namna hiyo. Wahitimu wa vyuo
watatakiwa kufundishwa kwamba baada ya mahafali huwezi tena kwenda kutafuta ajira
na badala yake unakwenda kutengeneza ajira.
Kilimo.
Siku zijazo kutakuwa na maroboti
ya bei rahisi mpaka kufikia dola $100. Wakulima katika nchi za Dunia ya 3 sasa
watageuka kuwa mameneja katika mashamba yao wenyewe badala ya kufanya kazi siku
nzima katika mashamba hayo. Uoteshaji wa mazao bila kutumia udongo (Aeroponic) unahitaji maji kidogo zaidi.
Nyama iliyotengenezwa maabara sasa ipo na itakuwa bei rahisi kushinda nyama ya
kawaida ya ng’ombe ifikapo mwaka 2018.
Kuna makampuni mengi mapya
yatakayoleta protini ya wadudu sokoni hivi karibuni, ina protini nyingi
kushinda ile iliyokuwepo katika nyama na itaandikwa “Chanzo
mbadakla cha protini” (kwasababu watu wengi bado hawakubaliani na
wazo la kula wadudu)
Mfumo
mpya wa fedha (Fiat Currency)
Badala ya
kutumia sarafu na noti za kawaida, utatumika mfumo mpya wa sarafu za
kielektroniki(BITCOIN) ambao hautakuwa na mipaka ya nchi kama ilivyokuwa sasa
hivi kila nchi na sarafu yake.
Umri wa kuishi binadamu.
Wastani
wa umri wa binadamu kuishi umeongezeka miezi mitatu 3 kwa mwaka. Miaka 4
iliyopita wastani ulikuwa ni miaka 79 na sasa hivi umepanda mpaka wastani wa
miaka 80. Inakisiwa ifikapo mwaka 2036 watu wengi zaidi watakuwa na uwezo wa
kuishi miaka zaidi ya 100
Elimu.
Simu ya
kisasa “Smartphone” ya bei rahisi kabisa tayari inauzwa katika masoko ya Afrika
na Asia kwa bei ya Dolla za Kimarekani , $10, ifikapo 2020 asilimia 70% ya binadamu
wote duniani watakuwa wanamiliki simu za kisasa za mkononi ‘smartphones’ Hiyo inamaanisha kwamba
kila mtu atakuwa na uwezekano sawa wa kupata elimu bora inayopatikana nchi
nyingine zilizoendelea. Kila mwanafunzi katika nchi zinazoendelea ataweza
kutumia masomo yote yanayotolewa katika mtandao kwa wanafunzi katika nchi
zilizoendelea hivyo ndani tu ya mwaka mmoja mwanafunzi katika nchi masikini atakuwa
na uwezi wa kuongea kiingereza fasaha.
Ni dunia
inayokwenda kwa kasi na inazidi kukimbia, kutakuwa na fursa pamoja na majanga njiani.
Viongozi wajao kwenye biashara
wanatakiwa wawe na uwezo mkubwa wa kusimamia haya mabadiliko chanya pamoja na
mabadiliko hasi haraka na kwa ufanisi zaidi kushinda wakati wowote nyakati
zilizopita.
Je, ndugu msomaji, upo katika nafasi ipi katika kujiandaa na mabadiliko haya makubwa ya dunia yanayozigusa sehemu muhimu zaidi za maisha yetu?. Usisubiri kusombwa na mafuriko yatakayosababishwa na dhoruba la mabadiliko haya fanya maamuzi sasa kuona ni jinsi gani utakavyoweza kukabiliana nayo pindi yanapojitokeza.
Je, ndugu msomaji, upo katika nafasi ipi katika kujiandaa na mabadiliko haya makubwa ya dunia yanayozigusa sehemu muhimu zaidi za maisha yetu?. Usisubiri kusombwa na mafuriko yatakayosababishwa na dhoruba la mabadiliko haya fanya maamuzi sasa kuona ni jinsi gani utakavyoweza kukabiliana nayo pindi yanapojitokeza.
Narudia tena ndugu msomaji kwamba, ripoti hii
lengo lake kubwa ni kuhamasisha na kusisimua mawazo. Yote yaliyoandikwa hapa yalikuwa
ni makisio tu ya muelekeo wa mabadiliko ya kasi ya teknolojia yaliyofanywa na
taasisi ya Singularity University ya
jijini California Marekani pamoja na makisio au mtazamo wangu mwenyewe binafsi
juu ya teknolojia mbalimbali zilizowahi kutumika hapa nyumbani Tanzania.
Makisio hayo hayawezi kuwakilisha uhalisia wa mambo utakavyokuwa kwa asilimia
100% miaka kadhaa ijayo.
*Shukrani kwa tovuti ya EQUITAS
*Shukrani kwa tovuti ya EQUITAS
………………………………………………………………………
FURSA MPYA YA BIASHARA!
Self
Help Books Publishers
Inatangaza fursa ya kipekee kwa
yule mwenye mapenzi na biashara ya uandishi wa vitabu. Ikiwa una wazo la kuandika
kitabu chochote kile au tayari unao mswada wa kitabu uliokwisha andikwa, njoo
kwetu tukuonyeshe njia rahisi ya kuugeuza mswada huo kuwa kitabu kamili ndani
ya muda mfupi.
·
Ikiwa tayari mswada umekwisha andikwa katika kompyuta, kitabu kitachukua
siku tatu tu kukamilika na kuingia sokoni.
·
Utawezeshwa kuchapisha vitabu vya kawaida vya karatasi(Hardcopy) sambamba
na vile vya kwenye mtandao(Softcopy)
·
Utatengenezewa blogu nzuri yenye kila kitu muhimu kwa ajili ya kupromoti
kitabu chako ikiwemo e-mail listing, mitandao ya kijamii pamoja na kufundishwa
namna ya kuihudumia blogu yako hiyo kama hujui ikiweo uandishi wa makala za
kuvutia wateja wa kitabu chako.
·
Utafundishwa pia njia za kukitangaza na kukisambaza kitabu chako nje ya
mtandao(offline marketing)
· Gharama ya mafunzo na huduma zote ni shilingi elfu 50 kwa kitabu cha
kurasa zisizozidi 100. Kuanzia kurasa 100 na kuendelea ni shilingi laki moja.
·
Gharama za kuchapa vitabu itategemea ni idadi gani ya vitabu unayotaka.
Unaweza ukatoa idadi yeyote ile ya vitabu uitakayo ilimradi isipungue vitabu
10. Pia gharama hizo za kutoa vitabu hazihusiani na gharama(ada) ya mafunzo.
·
Ukiamua kwa mfano kuanza na vitabu10
- 15 vya kurasa chini ya 100, gharama zote, mafunzo pamoja na kuchapa
vitabu hivyo hazitazidi wastani wa shilingi laki moja. Hivyo unakuwa umemiliki
kampuni yako ndogo kwa mtaji wa shilingi 100,000/= tu kuanzia hatua za wazo
mpaka mauzo, online na offline
·
Mafunzo ni kwa vitendo kwenye kompyuta pamoja na kwenda field maeneo
mbalimbali jijini wakati wa maandalizi ya kitabu na mshiriki anafundishwa peke
yake mmojammoja na mtaalamu mwenye uzoefu wa muda mrefu katika fani ya uandishi
na uchapishaji.
· Kitu cha pekee katika mpango huu ni kwamba mtu anawezeshwa kuchapisha
kitabu chake kwa gharama ndogo kabisa iwezekanavyo, kitu ambacho
kisingewezekana kabisa katika uchapishaji wa kawaida uliozoeleka. Pia haichukui
muda mrefu, ni siku 3 tu au nne kama mswada umeshakamilika mtu unaingia sokoni.
·
Tunapatikana MBEZI KWA MSUGURI karibu na stendi au unaweza
kuwasiliana nasi kwa namba zifuatazo,
0712
202244 au 0765
553030
KARINBU SANA UJE TUKUONYESHE NJIA MPYA NA RAHISI ZA KUFANYA MAMBO!
Kwa vitabu mbalimbali, kutoka
Self Help Books tembelea,
Kujiunga na BLOGU YA MASOMO YA SEMINA, lipa kiingilio shilingi elfu 10 kisha ubonyeze hayo maandishi.
0 Response to "NJIA MPYA ZA KUFANYA MAMBO: DUNIA, BIASHARA, AJIRA VINABADILIKA KWA KASI YA AJABU"
Post a Comment