SIRI HII NDIYO CHANZO CHA MAFANIKIO MAKUBWA NA UTAJIRI MWINGI DUNIANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SIRI HII NDIYO CHANZO CHA MAFANIKIO MAKUBWA NA UTAJIRI MWINGI DUNIANI

SURA YA 6
UBUNIFU
Karakana ya akili
Hatua ya tano kuelekea utajiri

Ubunifu maana yake ni karakana ambamo mipango yote inayopangwa na watu hutengenezwa. Msukumo, shauku hupewa umbo au vitendo kupitia msaada wa kitengo cha ubunifu wa akili.

Imesemekana kwamba tuna uwezo wa kuumba chochote kile tunachoweza kufikiria. Katika zama zote za ustaarabu, hizi ndiyo zama zinazofaa zaidi kwa ajili ya ukuzaji wa ubunifu kwa sababu ndiyo zama za mabadiliko ya haraka. Kila mahali tunakutana na vichocheo vinavyokuza ubunifu.

Kupitia msaada wa kitivo cha ubunifu, binadamu amegundua na kuvuna nguvu za asili nyingi katika kipindi cha miaka 50 iliyopita kuliko kipindi cha historia nzima ya mwanadamu huko nyuma. Tumelishinda anga kwa ukamilifu kiasi kwamba ndege hawawezi kulingana na sisi katika kuruka. Tumelitumia anga, na kulifanya kama njia ya haraka ya mawasiliano na sehemu yeyote ya dunia. Tumelitathmini na kulipima jua katika umbali wa mamilioni ya maili na kugundua kupitia msaada wa ubunifu, viasili vilivyoliumba.

Tumegundua kwamba ubongo wetu wenyewe ni kama kituo cha kurusha na kupokea mawimbi ya fikra, na tunaanza sasa kujifunza jinsi ya kuuweka ugunduzi huu katika vitendo. Tumeongeza kasi ya vyombo vya usafiri mpaka sasa unaweza kusafiri mpaka kasi ya zaidi ya maili 600 kwa saa. Kikwazo pekee kwetu kipo katika kukuza na kutumia ubunifu wetu. Hatujafikia bado kilele cha ukuaji katika matumizi ya kitivo chetu cha ubunifu. Tumegundua tu kwamba tunao ubunifu na tumeanza kuutumia katika hatua ya mwanzo kabisa.

Aina Mbili za Ubunifu
Kitivo cha ubunifu hufanya kazi katika hali mbili. Moja hujulikana kama “Ubunifu sanisi”(synthetic imagination) na nyingine kama “Ubunifu wa kujenga”(creative imagination)

UBUNIFU SANISI: Kupitia kitivo hiki mtu anaweza akapanga fikra za zamani, mawazo au mipango katika mchanganyiko mpya. Kitivo hiki hakiumbi kitu chochote. Hufanya tu kazi na vitu kama uzoefu, elimu na ushuhuda  ambavyo kinalishwa. Ni kitivo kinachotumika zaidi na wagunduzi, ukiacha watu wenye akili nyingi sana(genius) ambao hutumia Ubunifu wa kujenga wanaposhindwa kutatua tatizo kupitia ubunifu sanisi.

UBUNIFU WA KUJENGA(Creative Imagination)
Kupitia kitivo cha  Ubunifu wa kujenga, akili ya kawaida ya binadamu ina mawasiliano ya moja kwa moja na nguvu ya uumbaji( chanzo cha vitu vyote ulimwenguni). Ni kitivo ambacho kupitia hicho, hisia na ufunuo hupokelewa. Ni kwa kupitia kitivo hiki kwamba mawimbi ya fikra kutoka kwenye akili za wengine hupokelewa. Na ni kwa kupitia kitivo hiki kwamba mtu anaweza kufungulia au kuwasiliana na akili za ndani za watu wengine.

Ubunifu wa kujenga hufanya kazi wenyewe, katika namna iliyoelezwa kwenye kurasa zinazofuata. Kitio hiki hufanya kazi tu wakati akili ya nje ya kawaida inapotetema katika kiwango cha kasi iliyopitiliza kama kwa mfano, wakati akili ya nje ya kawaida inaposisimka kupitia mhemko wa hamu kubwa.

Kitivo cha kujenga (uumbaji) huwa makini zaidi kupokea mawimbi na kwa wingi zaidi kutoka vyanzo vilivyotajwa, katika uwiano na ukuaji wake kwa kadiri kinavyotumika. Kwa kweli vitivo vyote, kitivo sanisi na kitivo cha kujenga huwa vinakuwa makini zaidi wakati vinapotumika sawa tu na msuli wowote au ogani ya mwili inavyokua kutokana na kutumika. Kitivo chako cha ubunifu kinaweza kuwa dhaifu kutokana na kutokutumika. Kinaweza kuhuishwa na kufanywa kuwa tayari tena kupitia matumizi. Kitivo hiki huwa hakifi ingawa kinaweza kikasinyaa kutokana na kuto kutumika. Kauli hii ni muhimu! Fikiria juu yake kabla hujaendelea.

Kumbuka akilini wakati unafuata kanuni hizi kwamba habari nzima ya jinsi mtu anavyoweza kubadilisha shauku kuwa pesa haiwezi ikaelezwa katika kauli moja. Habari itakamilika tu wakati mtu anapokuwa amezielewa vizuri, kuzizoea na kuanza kuzitumia kanuni zote. Viongozi wakubwa wa biashara, viwanda, fedha na wasanii wakubwa, wanamuziki, wanamashairi na waandishi walikuwa wakubwa kwasababu walikuza kitivo cha Ubunifu wa Kujenga

Shauku ni wazo tu, msukumo. Ni kama nyota ya mbali sana au wingu la muda mfupi sana. Ni kitu kisichoshikika na kisichokuwa na thamani mpaka kimegeuzwa kuwa katika kitu(mwenzake) kinachoshikika. Wakati ubunifu sanisi ndio unaotumika mara nyingi zaidi katika mchakato wa kubadilisha msukumo wa shauku
Kuwa pesa, ni lazima ukumbuke kwamba unaweza ukakabiliwa na mazingira yanayohitaji matumizi ya ubunifu wa kujenga pia.

Kwa sasa elekeza umakini wako katika ukuzaji wa ubunifu sanisi. Mageuzi ya msukumo usioshikika wa shauku kuwa katika ukweli unaoweza kushikika wa pesa huhitaji matumizi ya mpango au mipango. Mipango hii ni lazima itengenezwe kwa msaada wa ubunifu, na zaidi kwa kitivo sanisi.

Soma kitabu chote, kisha rudi kwenye hii sura na uanze mara moja kuweka ubunifu wako katika kazi ya kutengeneza mpango au mipango kwa ajili ya mageuzi ya shauku yako kuwa pesa. Maelezo ya kina ya kutengeneza mpango yametolewa karibu katika kila sura.  Tekeleza maelekezo  yaendane zaidi na mahitaji yako. Weka mipango yako katika maandishi, ikiwa bado hukuwa umefanya hivyo.

Dakika unayomalizia kufanya hivyo utakuwa moja kwa moja umepewa fomu  ya shauku isiyoshikika. Soma sentensi iliyotangulia kwa mara nyingine tena. Isome kwa sauti, taratibu sana. Utakapokua ukifanya hivyo, kumbuka kwamba muda unapoandika kauli ya shauku yako na mpango kwa ajili ya kuifanikisha, unakuwa kweli umechukua hatua ya kwanza ya mfululizo wa hatua zitakazokuwezesha kubadilisha wazo kuwa katika kitu chake halisi kinachoshikika.

Dunia ambayo unaishi juu yake, wewe mwenyewe na kila kitu ni matokeo ya mabadiliko ya taratibu ambayo kupitia hayo chembechembe ndogo sana zimekusanywa na kupangiliwa katika mfumo maalumu. Zaidi ya hapo na kauli hii ni ya umuhimu mkubwa – dunia hii, kila moja ya mamilioni ya seli moja moja ya mwili wako na kila atomu ya maada  ilianza kama mfumo wa nguvu isiyoshikika.

Shauku ni msukumo(mawimbi) wa fikra! Mawimbi ya fikra ni aina ya nguvu. Unapoanza na shauku ya msukumo wa mawazo kujikusanyia pesa, unavuta katika upande wako ‘uwezo’ ambao asili ilitumia kuumba hii dunia na kila aina ya kitu kilichokuwemo ulimwenguni vikiwemo mwili na ubongo ambamo misukumo ya fikra hufanya kazi.

Kwa kiasi ambacho sayansi imeweza kugundua, Ulimwengu mzima una viasili viwili, maada na nguvu. Kupitia muunganiko wa maada na nguvu, kila kitu kinachoonekana kimeumbwa, kuanzia nyota kubwa kabisa zinazoelea angani kuelekea chini na binadamu akiwemo.

Sasa unajiingiza katika jukumu la kujaribu kupata faida kwa kutumia Njia za asili. Tunatumaini kwa uaminifu na kwa moyo unajaribu kujitengeneza mwenyewe uendane na Sheria za asili kwa kufanya jitihada kubadilisha shauku kuwa katika kitu chake halisi na thamani ya pesa inayolingna nayo. UNAWEZA KUFANYA HIVYO! IMEWAHI KUFANYIKA KABLA!

Unaweza ukatengeneza utajiri kupitia msaada wa sheria zisizobadilika. Lakini kwanza ni lazima uzifahamu sheria hizi na ujifunze kuzitumia. Kupitia kuzirudiarudia, na kwa kufanya maelezo ya kanuni hizi kutoka kila kona inayoweza kudhaniwa, mwandishi anatumaini kukupa siri ambayo kupitia hiyo utajiri mkubwa umeweza kulimbikizwa. Kama inavyoweza kuonekana ya ajabu na iliyofichika, “siri hiyo siyo siri”. Asili yenyewe huitangaza juu ya dunia tunayoishi, nyota, sayari zilizoninginizwa ndani ya upeo wetu, katika vitu vilivyomo juu na vinavyotuzunguka, katika kila ubapa wa jani na katika kila aina ya uhai ndani ya upeo wetu.

Asili huitangaza “siri” hii kupitia baiolojia, katika mabadiliko ya seli ndogo sana, (ndogo kiasi kwamba inaweza ikapotea katika ncha ya sindano) kuwa binadamu anayesoma sentensi hii sasa. Mabadiliko ya Shauku kuwa katika kitu chake halisi bila shaka siyo maajabu tena!

Usivunjike moyo ikiwa haujaelewa kikamilifu vile vyote vilivyoelezwa. Labda uwe umejifunza kwa muda mrefu maswala yanayohusiana na akili(fikra), haitegemewi kwamba utayazoea yote yaliyokuwepo kwenye hii sura kwa kusoma mara moja tu. Lakini kwa kadiri muda utakavyosogea utapiga hatua nzuri.

Kanuni zinazofuata zitafungua njia kwa ajili ya uelewa wa ubunifu. Jizoeshe kile unachoelewa, wakati ukisoma filosofia hii kwa mara ya kwanza, kisha wakati utakaporudia kuisoma na kujifunza, utagundua kwamba kitu fulani kimetokea kuifafanua, na kuipa uelewa mpana wa kanuni nzima. Juu ya yote usiache wala kusita katika kujifunza hizi kanuni mpaka umesoma kitabu angalao mara tatu, kwa wakati huo   hautataka kuacha tena.

Jinsi ya Kutumia Ubunifu kwa Vitendo
Mawazo ndiyo hatua za mwanzo za kila utajiri! Mawawazo ni mazao ya ubunifu. Hebu tutazame mawazo machache yanayojulikana vizuri ambayo yamezaa utajiri mkubwa, kwa matumaini kwamba maelezo haya yatatoa taarifa halisi kuhusiana na njia ambayo ubunifu unaweza kutumika katika kulimbikiza utajiri.

Birika La Kushangaza
Miaka mingi iliyopita, daktari mmoja mzee wa kijijini aliendesha farasi kuelekea njini, akimvuta farasi wake, taratibu alipenyeza kwenye duka la dawa kupitia mlango wa nyuma na kuanza “kupatana bei” na kijana karani muuza dawa. Hatima ya dhamira yake hii ingekuja kuzaa utajiri mkubwa kwa watu wengi. Ingekuja kuleta katika eneo la kusini, faida kubwa tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa zaidi ya saa moja, nyuma ya dirisha la kutolea dawa, daktari mzee na muuza dawa walizungumza kwa sauti za chini. Kisha daktari aliondoka. Alitoka nje kwenda kwenye kigari cha farasi na kurudi na birika kubwa la zamani na mwiko mkubwa wa mbao (uliotumika kukorogea vilivyokuwemo kwenye birika), na kuviweka nyuma ya duka.

Karani muuza dawa alilikagua birika, akaingia ndani ya mfuko wake wa ndani, akatoa bunda la pesa na kumkabidhi daktari. Bunda lilikuwa na $500 kamili – akiba yote ya karani(muuza dawa). Daktari alimpa kipande kidogo cha karatasi ambacho juu yake kiliandikwa kanuni ya siri. Maneno juu ya kile kipande kidogo cha karatasi yalikuwa na thamani kubwa sana! Lakini siyo kwa daktari!   Maneno hayo ya maajabu yalihitajika kuanzisha birika lichemke, lakini siyo daktari wala kijana muuza dawa aliyefahamu utajiri mkubwa ambao ungekuja kumiminika kutoka lile birika.

Daktari mzee alikuwa na furaha kuuza vitu vyake  kwa $500. Pesa zingeweza kulipa madeni yake na kumpa uhuru wa mawazo. Muuza dawa alikuwa anabahatisha bahati yake kwa kuhatarisha akiba yake yote ya maisha katika kipande cha karatasi na birika la zamani! Kamwe hakuota uwekezaji wake huo ungeweza kuanzisha birika kufurika dhahabu ambayo ingeweza kuzidi utendaji wa kimiujiza wa taa ya Aladdin.

Ukweli kitu muuza dawa alichonunua ilikuwa ni wazo!

Birika la zamani na mwiko wa mbao na ujumbe wa siri juu ya kipande cha karatasi vilikuwa ni tukio la kawaida. Utendaji wa ajabu wa birika lile ulianza kutokea baada ya mmiliki mpya kuchanganyika na maelekezo ya siri, kiambato ambacho daktari hakuwa anafahamu chochote.

Soma habari hii kwa umakini, na upe ubunifu wako jaribio! Angalia kama unaweza ukagundua ilikuwa ni kitu gani kijana alichoongeza kwenye ujumbe wa siri kilichosababisha birika kufurika dhahabu. Kumbuka  wakati ukisoma kwamba, hii siyo hadithi kutoka Arabian Nights. Hapa una simulizi ya ukweli, inayosisimua kushinda riwaya, ukweli ulioanza katika hali ya wazo

Hebu tuutazame utajiri mkubwa wa dhahabu, wazo hili lililouleta. Limelipa na bado hulipa utajiri mkubwa kwa wanaume na wanawake duniani kote ambao husambaza kilichokuwemo ndani ya birika kwa mamilioni ya watu.

Birika la zamani sasa ni moja kati ya watumiaji wakubwa zaidi wa sukari, hivyo kutoa ajira za kudumu kwa maelfu ya wanaume na wanawake wanaojihusisha katika kilimo cha miwa na katika kusindika na kuuza sukari.

Birika kuukuu kwa mwaka hutumia mamilioni ya chupa za kioo, likitoa ajira kwa idadi kubwa ya wafanyakazi wa viwanda vya vioo. Birika la zamani hutoa ajira kwa ‘jeshi’ la makarani, waandishi na wataalamu wa matangazo nchi nzima. Limeleta umaarufu na utajiri kwa kundi la wasanii waliotengeneza picha nzuri kabisa zinazoelezea bidhaa hiyo. Birika la zamani limebadilisha mji mdogo wa Kusini kuwa jiji la kibiashara la Kusini, ambalo sasa huzinufaisha kila biashara na karibu kila mkaazi wa jiji kwa njia ya moja kwa moja au isiyokuwa ya moja kwa moja. Ushawishi wa wazo hili sasa hunufaisha kila nchi iliyostaarabika duniani, likitiririsha mfereji usiokauka wa dhahabu kwa kila anayeligusa.

Dhahabu kutoka kwenye birika ilijenga na kuendeleza moja kati ya vyuo maarufu zaidi Kusini ambapo maelfu ya vijana wadogo hupata mafunzo muhimu kwa ajili ya mafanikio.

Birika la zamani limefanya vitu vingine vya ajabu!


Kipindi chote cha mdororo wa kiuchumi cha miaka ya 1930, wakati viwanda, mabenki na nyumba za biashara zilikuwa zinafunga na kusitisha biashara kwa maelfu, mmiliki wa hili birika la ajabu yeye aliendelea kupiga gwaride, akiendeleza ajira kwa jeshi la wanaume na wanawake dunia nzima, na kulipa sehemu ya ziada ya dhahabu kwa wale ambao tangu muda mrefu walikuwa na imani katika lile wazo.


Usikose sehemu ya 2 ya Sura hii ya 6 hapo kesho Jumapili 30th Apr. 2017 jioni.







0 Response to "SIRI HII NDIYO CHANZO CHA MAFANIKIO MAKUBWA NA UTAJIRI MWINGI DUNIANI "

Post a Comment