SURA
YA 6
UBUNIFU
Karakana
ya akili
Hatua
ya tano kuelekea utajiri
Ubunifu maana yake ni karakana ambamo mipango
yote inayopangwa na watu hutengenezwa. Msukumo, shauku hupewa umbo au vitendo
kupitia msaada wa kitengo cha ubunifu wa akili.
Imesemekana kwamba tuna uwezo wa kuumba
chochote kile tunachoweza kufikiria. Katika zama zote za ustaarabu, hizi ndiyo
zama zinazofaa zaidi kwa ajili ya ukuzaji wa ubunifu kwa sababu ndiyo zama za
mabadiliko ya haraka. Kila mahali tunakutana na vichocheo vinavyokuza ubunifu.
Kupitia msaada wa kitivo cha ubunifu,
binadamu amegundua na kuvuna nguvu za asili nyingi katika kipindi cha miaka 50
iliyopita kuliko kipindi cha historia nzima ya mwanadamu huko nyuma. Tumelishinda
anga kwa ukamilifu kiasi kwamba ndege hawawezi kulingana na sisi katika kuruka.
Tumelitumia anga, na kulifanya kama njia ya haraka ya mawasiliano na sehemu
yeyote ya dunia. Tumelitathmini na kulipima jua katika umbali wa mamilioni ya
maili na kugundua kupitia msaada wa ubunifu,
viasili vilivyoliumba.
Tumegundua kwamba ubongo wetu wenyewe ni kama
kituo cha kurusha na kupokea mawimbi ya fikra, na tunaanza sasa kujifunza jinsi
ya kuuweka ugunduzi huu katika vitendo. Tumeongeza kasi ya vyombo vya usafiri
mpaka sasa unaweza kusafiri mpaka kasi ya zaidi ya maili 600 kwa saa. Kikwazo
pekee kwetu kipo katika kukuza na kutumia ubunifu wetu. Hatujafikia bado kilele
cha ukuaji katika matumizi ya kitivo chetu cha ubunifu. Tumegundua tu kwamba
tunao ubunifu na tumeanza kuutumia katika hatua ya mwanzo kabisa.
Aina
Mbili za Ubunifu
Kitivo cha ubunifu hufanya kazi katika hali
mbili. Moja hujulikana kama “Ubunifu sanisi”(synthetic imagination) na nyingine
kama “Ubunifu wa kujenga”(creative imagination)
UBUNIFU
SANISI: Kupitia kitivo hiki mtu anaweza akapanga fikra za
zamani, mawazo au mipango katika mchanganyiko mpya. Kitivo hiki hakiumbi kitu
chochote. Hufanya tu kazi na vitu kama uzoefu, elimu na ushuhuda ambavyo kinalishwa. Ni kitivo kinachotumika
zaidi na wagunduzi, ukiacha watu wenye akili nyingi sana(genius) ambao hutumia
Ubunifu wa kujenga wanaposhindwa kutatua tatizo kupitia ubunifu sanisi.
UBUNIFU
WA KUJENGA(Creative Imagination)
Kupitia kitivo cha Ubunifu wa kujenga, akili ya kawaida ya
binadamu ina mawasiliano ya moja kwa moja na nguvu ya uumbaji( chanzo cha vitu vyote
ulimwenguni). Ni kitivo ambacho kupitia hicho, hisia na ufunuo hupokelewa. Ni
kwa kupitia kitivo hiki kwamba mawimbi ya fikra kutoka kwenye akili za wengine
hupokelewa. Na ni kwa kupitia kitivo hiki kwamba mtu anaweza kufungulia au
kuwasiliana na akili za ndani za watu wengine.
Ubunifu wa kujenga hufanya kazi wenyewe,
katika namna iliyoelezwa kwenye kurasa zinazofuata. Kitio hiki hufanya kazi tu wakati akili ya nje ya kawaida
inapotetema katika kiwango cha kasi iliyopitiliza kama kwa mfano, wakati akili ya
nje ya kawaida inaposisimka kupitia mhemko wa hamu kubwa.
Kitivo cha kujenga (uumbaji) huwa makini
zaidi kupokea mawimbi na kwa wingi zaidi kutoka vyanzo vilivyotajwa, katika
uwiano na ukuaji wake kwa kadiri kinavyotumika. Kwa kweli vitivo vyote, kitivo
sanisi na kitivo cha kujenga huwa vinakuwa makini zaidi wakati vinapotumika
sawa tu na msuli wowote au ogani ya mwili inavyokua kutokana na kutumika.
Kitivo chako cha ubunifu kinaweza kuwa dhaifu kutokana na kutokutumika.
Kinaweza kuhuishwa na kufanywa kuwa tayari tena kupitia matumizi. Kitivo hiki
huwa hakifi ingawa kinaweza kikasinyaa kutokana na kuto kutumika. Kauli hii ni
muhimu! Fikiria juu yake kabla hujaendelea.
Kumbuka akilini wakati unafuata kanuni hizi
kwamba habari nzima ya jinsi mtu anavyoweza kubadilisha shauku kuwa pesa haiwezi ikaelezwa katika kauli moja. Habari
itakamilika tu wakati mtu anapokuwa amezielewa vizuri, kuzizoea na kuanza
kuzitumia kanuni zote. Viongozi wakubwa wa biashara, viwanda, fedha na wasanii
wakubwa, wanamuziki, wanamashairi na waandishi walikuwa wakubwa kwasababu
walikuza kitivo cha Ubunifu wa Kujenga
Shauku ni wazo tu, msukumo. Ni kama nyota ya
mbali sana au wingu la muda mfupi sana. Ni kitu kisichoshikika na kisichokuwa
na thamani mpaka kimegeuzwa kuwa katika kitu(mwenzake) kinachoshikika. Wakati
ubunifu sanisi ndio unaotumika mara nyingi zaidi katika mchakato wa kubadilisha
msukumo wa shauku
Kuwa pesa, ni lazima ukumbuke kwamba unaweza
ukakabiliwa na mazingira yanayohitaji matumizi ya ubunifu wa kujenga pia.
Kwa sasa elekeza umakini wako katika ukuzaji
wa ubunifu sanisi. Mageuzi ya msukumo usioshikika wa shauku kuwa katika ukweli unaoweza kushikika wa pesa huhitaji
matumizi ya mpango au mipango. Mipango hii ni lazima itengenezwe kwa msaada wa
ubunifu, na zaidi kwa kitivo sanisi.
Soma kitabu chote, kisha rudi kwenye hii sura
na uanze mara moja kuweka ubunifu wako katika kazi ya kutengeneza mpango au
mipango kwa ajili ya mageuzi ya shauku
yako kuwa pesa. Maelezo ya kina ya kutengeneza mpango yametolewa karibu katika
kila sura. Tekeleza maelekezo yaendane zaidi na mahitaji yako. Weka mipango
yako katika maandishi, ikiwa bado hukuwa umefanya hivyo.
Dakika unayomalizia kufanya hivyo utakuwa
moja kwa moja umepewa fomu ya shauku
isiyoshikika. Soma sentensi iliyotangulia kwa mara nyingine tena. Isome kwa
sauti, taratibu sana. Utakapokua ukifanya hivyo, kumbuka kwamba muda
unapoandika kauli ya shauku yako na mpango kwa ajili ya kuifanikisha, unakuwa
kweli umechukua hatua ya kwanza ya
mfululizo wa hatua zitakazokuwezesha kubadilisha wazo kuwa katika kitu chake
halisi kinachoshikika.
Dunia ambayo unaishi juu yake, wewe mwenyewe
na kila kitu ni matokeo ya mabadiliko ya taratibu ambayo kupitia hayo
chembechembe ndogo sana zimekusanywa na kupangiliwa katika mfumo maalumu. Zaidi
ya hapo na kauli hii ni ya umuhimu mkubwa – dunia hii, kila moja ya mamilioni
ya seli moja moja ya mwili wako na kila atomu ya maada ilianza
kama mfumo wa nguvu isiyoshikika.
Shauku ni msukumo(mawimbi) wa fikra! Mawimbi
ya fikra ni aina ya nguvu. Unapoanza na shauku ya msukumo wa mawazo
kujikusanyia pesa, unavuta katika upande wako ‘uwezo’ ambao asili ilitumia
kuumba hii dunia na kila aina ya kitu kilichokuwemo ulimwenguni vikiwemo mwili
na ubongo ambamo misukumo ya fikra hufanya kazi.
Kwa kiasi ambacho sayansi imeweza kugundua,
Ulimwengu mzima una viasili viwili, maada na nguvu. Kupitia muunganiko wa maada
na nguvu, kila kitu kinachoonekana kimeumbwa, kuanzia nyota kubwa kabisa
zinazoelea angani kuelekea chini na binadamu akiwemo.
Sasa unajiingiza katika jukumu la kujaribu
kupata faida kwa kutumia Njia za asili. Tunatumaini kwa uaminifu na kwa moyo
unajaribu kujitengeneza mwenyewe uendane na Sheria za asili kwa kufanya
jitihada kubadilisha shauku kuwa
katika kitu chake halisi na thamani ya pesa inayolingna nayo. UNAWEZA KUFANYA
HIVYO! IMEWAHI KUFANYIKA KABLA!
Unaweza ukatengeneza utajiri kupitia msaada
wa sheria zisizobadilika. Lakini kwanza ni lazima uzifahamu sheria hizi na
ujifunze kuzitumia. Kupitia
kuzirudiarudia, na kwa kufanya maelezo ya kanuni hizi kutoka kila kona
inayoweza kudhaniwa, mwandishi anatumaini kukupa siri ambayo kupitia hiyo
utajiri mkubwa umeweza kulimbikizwa. Kama inavyoweza kuonekana ya ajabu na
iliyofichika, “siri hiyo siyo siri”.
Asili yenyewe huitangaza juu ya dunia tunayoishi, nyota, sayari
zilizoninginizwa ndani ya upeo wetu, katika vitu vilivyomo juu na
vinavyotuzunguka, katika kila ubapa wa jani na katika kila aina ya uhai ndani
ya upeo wetu.
Asili huitangaza “siri” hii kupitia
baiolojia, katika mabadiliko ya seli ndogo sana, (ndogo kiasi kwamba inaweza
ikapotea katika ncha ya sindano) kuwa binadamu
anayesoma sentensi hii sasa. Mabadiliko ya Shauku kuwa katika kitu chake halisi
bila shaka siyo maajabu tena!
Usivunjike moyo ikiwa haujaelewa kikamilifu
vile vyote vilivyoelezwa. Labda uwe umejifunza kwa muda mrefu maswala
yanayohusiana na akili(fikra), haitegemewi kwamba utayazoea yote yaliyokuwepo
kwenye hii sura kwa kusoma mara moja tu. Lakini kwa kadiri muda utakavyosogea
utapiga hatua nzuri.
Kanuni zinazofuata zitafungua njia kwa ajili
ya uelewa wa ubunifu. Jizoeshe kile unachoelewa, wakati ukisoma filosofia hii
kwa mara ya kwanza, kisha wakati utakaporudia kuisoma na kujifunza, utagundua
kwamba kitu fulani kimetokea kuifafanua, na kuipa uelewa mpana wa kanuni nzima.
Juu ya yote usiache wala kusita katika kujifunza hizi kanuni mpaka umesoma
kitabu angalao mara tatu, kwa wakati
huo hautataka kuacha tena.
Jinsi
ya Kutumia Ubunifu kwa Vitendo
Mawazo ndiyo hatua za mwanzo za kila utajiri!
Mawawazo ni mazao ya ubunifu. Hebu tutazame mawazo machache yanayojulikana
vizuri ambayo yamezaa utajiri mkubwa, kwa matumaini kwamba maelezo haya yatatoa
taarifa halisi kuhusiana na njia ambayo ubunifu unaweza kutumika katika
kulimbikiza utajiri.
Birika La Kushangaza
Miaka mingi iliyopita, daktari mmoja mzee wa
kijijini aliendesha farasi kuelekea njini, akimvuta farasi wake, taratibu
alipenyeza kwenye duka la dawa kupitia mlango wa nyuma na kuanza “kupatana bei”
na kijana karani muuza dawa. Hatima ya dhamira yake hii ingekuja kuzaa utajiri
mkubwa kwa watu wengi. Ingekuja kuleta katika eneo la kusini, faida kubwa tangu
vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa zaidi ya saa moja, nyuma ya dirisha la
kutolea dawa, daktari mzee na muuza dawa walizungumza kwa sauti za chini. Kisha
daktari aliondoka. Alitoka nje kwenda kwenye kigari cha farasi na kurudi na
birika kubwa la zamani na mwiko mkubwa wa mbao (uliotumika kukorogea
vilivyokuwemo kwenye birika), na kuviweka nyuma ya duka.
Karani muuza dawa alilikagua birika, akaingia
ndani ya mfuko wake wa ndani, akatoa bunda la pesa na kumkabidhi daktari. Bunda
lilikuwa na $500 kamili – akiba yote ya karani(muuza dawa). Daktari alimpa
kipande kidogo cha karatasi ambacho juu yake kiliandikwa kanuni ya siri. Maneno
juu ya kile kipande kidogo cha karatasi yalikuwa na thamani kubwa sana! Lakini siyo kwa daktari! Maneno hayo ya maajabu yalihitajika
kuanzisha birika lichemke, lakini siyo daktari wala kijana muuza dawa
aliyefahamu utajiri mkubwa ambao ungekuja kumiminika kutoka lile birika.
Daktari mzee alikuwa na furaha kuuza vitu
vyake kwa $500. Pesa zingeweza kulipa
madeni yake na kumpa uhuru wa mawazo. Muuza dawa alikuwa anabahatisha bahati
yake kwa kuhatarisha akiba yake yote ya maisha katika kipande cha karatasi na
birika la zamani! Kamwe hakuota uwekezaji wake huo ungeweza kuanzisha birika
kufurika dhahabu ambayo ingeweza kuzidi utendaji wa kimiujiza wa taa ya
Aladdin.
Ukweli kitu muuza dawa alichonunua ilikuwa ni
wazo!
Birika la zamani na mwiko wa mbao na ujumbe
wa siri juu ya kipande cha karatasi vilikuwa ni tukio la kawaida. Utendaji wa
ajabu wa birika lile ulianza kutokea baada ya mmiliki mpya kuchanganyika na
maelekezo ya siri, kiambato ambacho daktari hakuwa anafahamu chochote.
Soma habari hii kwa umakini, na upe ubunifu
wako jaribio! Angalia kama unaweza ukagundua ilikuwa ni kitu gani kijana
alichoongeza kwenye ujumbe wa siri kilichosababisha birika kufurika dhahabu.
Kumbuka wakati ukisoma kwamba, hii siyo
hadithi kutoka Arabian Nights. Hapa una simulizi ya ukweli, inayosisimua
kushinda riwaya, ukweli ulioanza katika hali ya wazo
Hebu tuutazame utajiri mkubwa wa dhahabu,
wazo hili lililouleta. Limelipa na bado hulipa utajiri mkubwa kwa wanaume na
wanawake duniani kote ambao husambaza kilichokuwemo ndani ya birika kwa mamilioni
ya watu.
Birika la zamani sasa ni moja kati ya
watumiaji wakubwa zaidi wa sukari, hivyo kutoa ajira za kudumu kwa maelfu ya
wanaume na wanawake wanaojihusisha katika kilimo cha miwa na katika kusindika
na kuuza sukari.
Birika kuukuu kwa mwaka hutumia mamilioni ya
chupa za kioo, likitoa ajira kwa idadi kubwa ya wafanyakazi wa viwanda vya
vioo. Birika la zamani hutoa ajira kwa ‘jeshi’ la makarani, waandishi na
wataalamu wa matangazo nchi nzima. Limeleta umaarufu na utajiri kwa kundi la
wasanii waliotengeneza picha nzuri kabisa zinazoelezea bidhaa hiyo. Birika la
zamani limebadilisha mji mdogo wa Kusini kuwa jiji la kibiashara la Kusini,
ambalo sasa huzinufaisha kila biashara na karibu kila mkaazi wa jiji kwa njia
ya moja kwa moja au isiyokuwa ya moja kwa moja. Ushawishi wa wazo hili sasa
hunufaisha kila nchi iliyostaarabika duniani, likitiririsha mfereji usiokauka
wa dhahabu kwa kila anayeligusa.
Dhahabu kutoka kwenye birika ilijenga na
kuendeleza moja kati ya vyuo maarufu zaidi Kusini ambapo maelfu ya vijana
wadogo hupata mafunzo muhimu kwa ajili ya mafanikio.
Birika la zamani limefanya vitu vingine vya
ajabu!
Kipindi chote cha mdororo wa kiuchumi cha
miaka ya 1930, wakati viwanda, mabenki na nyumba za biashara zilikuwa zinafunga
na kusitisha biashara kwa maelfu, mmiliki wa hili birika la ajabu yeye
aliendelea kupiga gwaride, akiendeleza ajira kwa jeshi la wanaume na wanawake
dunia nzima, na kulipa sehemu ya ziada ya dhahabu kwa wale ambao tangu muda
mrefu walikuwa na imani katika lile
wazo.
Usikose sehemu ya 2 ya Sura hii
ya 6 hapo kesho Jumapili 30th Apr. 2017 jioni.
0 Response to "SIRI HII NDIYO CHANZO CHA MAFANIKIO MAKUBWA NA UTAJIRI MWINGI DUNIANI "
Post a Comment