Mtaji ni changamoto kubwa sana kwa
wajasiriamali wengi wadogo, utakuta mjasiriamali anayo mawazo mengi makubwa
lakini anaishia kuzeeka nayo shauri ya kukosa mtaji wa kutosha kuweza kuyageuza
kuwa biashara halisi.
Ni wajasiriamali wachache ambao huwa na bahati
ya kupigana kiume, wazungu hupenda kuita, bootstrapping, mpaka wanapata mitaji
mikubwa, kwa kudunduliza faida kidogokidogo inayotokana na biashara ndogo
wanazozifanya.
Kutumia rasilimali chache zilizomo ndiyo chaguo
la mwisho kwa mjasiriamali anayefanya biashara kwa kutumia mtaji kidogo huku akiwa hana dhamana za
uhakika au sifa za kutosha kukopesheka na taasisi za fedha, mabenki nk.
Hata ikiwa mjasiriamali atakuwa na sifa za
kukopa bado wengi hawana elimu sahihi ya mikopo jambo linalosababisha waogope
kwenda kukopa kwa kuhofia kuja kufilisiwa mali zao kidogo walizokuwa nazo.
SOMA : Biashara ndogondogo 7 unazoweza kuanza bila mtaji
SOMA : Biashara ndogondogo 7 unazoweza kuanza bila mtaji
Una mawazo makubwa na mazuri ya biashara,
lakini huna mtaji, umejaribu njia zote za kupata mtaji wa kutosha kama vile kukopa,
kuingia ubia na mtu, kuuza mali zako ulizokuwa nazo, kupata mfadhili, lakini
imeshindika, umekutana na vikwazo vingi. Njia pekee unayoweza kuitumia ili
kuweza kujenga hali yako kifedha na hatimaye angalao uweze kuaminika ni kwa
njia ya kuanza chini kabisa, na katika kuanza huko chini kabisa itakubidi
utafute njia za kukuingizia kipato zilizokuwa rahisi na ambazo hazita kugharimu
mtaji au fedha nyingi.
Unaweza ukaamua kutumia njia moja maarufu na
ambayo ndiyo iliyozoeleka na watu wengi zaidi ya kutafuta ajira au kibarua na
baadaye sasa utakapokuwa umelipwa mshahara ukaanza kuangalia ni kwa namna gani
unaweza ukaanza taratibu kuwekeza katika biashara ndogondogo.
Njia ya pili unaweza ukatafuta kwa njia
yeyote halali na utakayoona inafaa mtaji mdogo kabisa hata kuanzia shilingi elfu tano au mbili na kuanza
biashara ndogo sana ambayo ndiyo hasa ninayotaka kuzungumzia katika makala
yangu hii ya leo. Lengo langu ni kutaka kukupa moyo wewe mjasiriamali uliyekata
tamaa na kufikiri kwamba hakuna tena njia ya kutokea baada ya kuona kwamba
karibu kila njia unayojaribu kupata mtaji wa kuanzisha biashara ya ndoto yako
imefungwa.
Mtaji ni kati ya vitu vigumu mno duniani
kupatikana ikiwa hautakuwa mvumilivu na kukubali kufanya kazi kwa juhudi na
maarifa huku ukianzia chini kabisa. Haijalishi wewe una umri gani wewe anza
chini kisha jifanye ndio kwanza unaanza kushika hela kwa mara ya kwanza, hapa
namaanisha tumia pesa unazopata kwa uangalifu mkubwa ukitoa pesa kwa ajili ya
vitu muhimu tu, achana na matumizi yasiyoingiza faida. Ni bora ukatembea na
kiatu kilichotoboka ukachekwa lakini ukijua unatengeneza mtaji kwanza.
Watakaokucheka iko siku watakusalimia kwa heshima.
SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini.
SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini.
Ngoja tusiende sana nje ya mada ya leo, sasa
nitakutajia zile biashara 5 ambazo, kwa mtaji mdogo kabisa hata shilingi elfu
mbili 2, tano, elfu 10 mpaka laki moja(100,000) unaweza ukaanzisha na kwa
kutumia rasilimali kidogo kabisa ulizokuwa nazo mchanganyiko na kubana matumizi
kwa hali ya juu kabisa (bootstrapping)
basi unajikuta polepole unaanza kupata mtaji, biashara inakua, unafungua
biashara kubwa kidogo, na sasa wakopeshaji au wabia wakaanza kupigana vikumbo
wakikugombea wakukopeshe au kuingia ubia na wewe.
Biashara hizo ni kama vile hizi zifuatazo;
1.Biashara
ndogondogo za vitu vya kutafuna kama vile karanga, ubuyu, pipi na ice cream.
Biashara hizi unaweza ukazichukulia rahisi
rahisi na kusema, “nitazipanga wapi sina hata kibanda cha genge wala ninapoishi hamna
watu wengi”. Usikubali kushindwa kabla hujaanza, hakuna mahali watu
wasipopita, wewe unaishi wapi? Unatembea wapi? Hamna mtu hata mmoja?. Huna
majirani?
Kila mahali watu hawakosekani, walewale
unaokutana nao kila siku wanaweza kuwa wateja wako ilimradi tu wafahamu unacho
kitu wanachohitaji. Fikiria ni kitu gani watakachokuwa na mahitaji nacho na
uhakikishe kila siku hakikosekani katika yale mazingira wanayoishi au kufanya
kazi.
Kuwa mbunifu siyo lazima uwe na duka ndipo
uuze bidhaa. Baraza ya nyumba unamoishi au hata ulipopanga panatosha kuweka
stuli na ukapanga biashara yako watu wakanunua kama kawaida.
Kwanini nasema mtaji hata wa shilingi elfu
mbili (2,000) mtu unaweza ukaanza biashara? Tuchukulie kwa mfano karanga,
ukinunua kilo moja unaweza ukazikaanga na kuanza kuuza kwa kutembeza na bakuli
au ukazifunga vizuri katika paketi za nailoni.
2. Biashara unazoweza kufanyia nyumbani kama
vile kuuza mkaa, mafuta ya taa, kuni na pumba za kulishia mifugo.
Mahitaji niliyoyataja hapo juu yote ni
nishati ya kupikia chakula kasoro tu pumba za mifugo kwa sababu hakuna ubishi
wowote ule watu wengi Tanzania ni watu wa vipato vya wastani na vipato vya
chini, na nishati hizi zote ndizo wanazozitumia kila siku. Hata uwe unaishi
wapi vitu hivi vitanunuliwa tu na amini ninachokuambia haviwezi kukaa muda
mrefu bila kwisha.
Hali kadhalika pumba nimeitaja makusudi kwani
nafahamu watu wengi hufuga kuku, bata na baadhi ya wanyama na ndege wengine
wafugwao lakini uwezo wa kununua vyakula maalumu(special food) kwa wanyamana
ndege hao ni mdogo, hukimbilia pumba kutokana na urahisi, hivyo piga ua ni
lazima uuze.
Uzuri wa vitu vyote hivyo nilivyovitaja hapo
juu, unaweza ukavifunga(ukavipack) katika mifuko, chupa kwa upande wa mafuta ya
taa ukafahamu kabisa faida yake ni shilingi ngapi kabla hata hujaanza kuviuza.
3.
Kuuza matunda na mboga mboga.
Unaweza ukatumia staili ya kutembeza
barabarani au ukaweka meza mbele ya mahali unapoishi ukavipanga vizuri pale.
Unaweza pia ukatumia kakabati kadogo ka vioo ukaweka matunda safi yaliyomenywa
kabisa kwa ajili ya wateja wanaopita njia. Mtaji wake ni kidogo na vinatoka
harakaharaka.
SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara.
SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara.
4.
Uuzaji wa samaki na dagaa mchele.
Kila siku watu hutafuta vitoweo, watu wa hali
za chini hupenda sana dagaa wabichi waliokaangwa maarufu kama dagaa mchele kwa
Dar es salaam. Na hata mikoa mingine nako kuna dagaa wa aina nyinginezo nao
watu pia hupenda kununua kwa ajili ya kitoweo.
Wanaomudu kununua samaki nao hununua kila
mara, unapomuuzia mtu leo akikuta samaki wako ni wazuri, haitapita wiki, ni
lazima akutafuta tena kwa ajili ya samaki wengine. Mtaji wake siyo mkubwa na unaweza
kuchagua kuwauzia mazingira ya nyumbani au ukawatembeza majumbani mwa watu kila
siku.
5. Biashara
za utoaji wa huduma mbalimbali zisizohitaji mtaji mkubwa kama vile udobi,
ubebaji wa maji kwa ndoo na madumu na utengenezaji wa bustani za maua(gardening)
Biashara hizi kama kufua na kunyosha nguo “udobi”, mtaji wako ni maji na kipande
cha sabuni tu, eneo laweza kuwa ni nyumbani kwako au nyumbani kwa mteja.
Kuwabebea watu maji kwa madumu au kwa ndoo utahitaji kuwa na mtaji wa kununulia
mkokoteni kiasi kisichozidi shilingi laki moja pamoja na madumu yenyewe, mtaji
wa kununulia maji bombani unaweza hata kuteka kwa mkopo ukaja kulipa baada yaw
ewe kulipwa.
SOMA: Biashara zinazolipa zaidi duniani.
SOMA: Biashara zinazolipa zaidi duniani.
Kwa ufupi tu nimejaribu kuonyesha biashara
ambazo mtaji wake ni mdogo kuanzia shilingi elfu mbili 2 mpaka shilingi laki
moja ambazo mtu yeyote anayetaka kuingia kwenye ujasiriamali anaweza akaanza,
biashara nilizozitaja hapa zinawakilisha biashara kama hizo nyingi, hivyo siyo
lazima mtu anayetaka kuanza chini kabisa basi aanze na zile nilizotaja bali
anaweza kuanza hata na biashara nyingine yeyote lakini yenye sifa hiyo ya
kuhitaji mtaji mdogo.
……………………………………………………………………….
Ndugu
msomaji wa blogu hii, kama kama makala unazosoma humu zinakuvutia, basi ujue na
vitabu kutoka self help books Tanzania
vitakuvutia na kukunufaisha mara dufu. Vitabu vitatu 3 hapo chini kutoka kwetu
hakuna mtu aliyewahi kununua hata mmoja akajutia pesa yake aliyotoa.
1. SHILINGI 20,000/=
2. SHILINGI 10,000/=
3. SHILINGI 5,000/=
1. Dar es salaam ukihitaji kimoja, viwili
au hata vyote 3, Unaweza kuja moja kwa moja ilipo ofisi yetu, Mbezi kwa Msuguri
stendi, ukifika tazama kibao cha hospitali ya Bochi kilipo mkono wako wa kulia
pana njia, au ni mkabala opp. na yanakosimama Malori makubwa yaendayo mikoani,
vuka barabara pana hardware nje.
2. Ukitaka uletewe ulipo kwa Dar es salaam
wasiliana na sisi upate utaratibu. 0712202244 au 0765553030
3. Wateja wa Mikoani, tunatuma kwa njia ya
mabasi na gharama ya kutuma kifurushi ni shilingi elfu 10, hivyo kama utapenda
tukutumie kitabu/vitabu tuma fedha kwa ajili ya kitabu/vitabu pamoja na sh.
10,000/= ya usafirishaji wa basi linalofika ulipo.
4. Kama utapenda kutumiwa vitabu kwa njia
ya email(softcopy) popote pale ulipo, bei za vitabu hupungua, cha kwanza ni
elfu 10, cha pili elfu 5 na cha tatu elfu 3. Tuma pesa na anuani yako ya email tutakutumia
kitabu /vitabu muda huohuo. Namba zetu ni 0765553030 au 0712202244, watsapp: 0765553030
MICHANGANUO YA BIASHARA / BUSINESS PLANS
Unahitaji kuandikiwa mpango wa biashara yako kwa gharama nafuu?
AU
Unahitaji mafunzo kwa ajili ya kuandika mwenyewe mpango wa biashara yako kwa njia rahisi?
Basi wasiliana na sisi bei zetu ni rafiki mno
Simu/whatsapp: 0765553030
Simu/sms: 0712202244
Asante
ReplyDeleteThanks too!
DeleteAsante sana Mahumbimedia!
ReplyDelete