Kama kuna kitabu kilichoelezea maana halisi
ya neno UJASIRIAMALI kwa lugha ya kiswahili, basi kitabu cha MICHANGANUO YABIASHARA NAUJASIRIAMALI kitashika nambari ya kwanza hapa Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla.
Hii dhana ya ujasiriamali kwa mtazamo wa juu juu mtu
unaweza ukadhani labda imeibuka juzijuzi tu kumbe ukikutana na mchambuzi
aliyebobea unaweza usiamini kile atakachokusimulia kuhusiana na Ujasiriamali
kama vile kitabu hicho kinavyokwenda kukupa hapa sasa hivi historia na maana ya
ujasiriamali kwa ufupi kabisa.
Ujasiriamali umepitia karibu katika kila ustaarabu
uliowahi kuwepo hapa duniani, tokea enzi na enzi ukikua taratibu kadiri jamii
mbalimbali nazo zilivyokuwa zikikua. Kufahamu historia hii na mabadiliko yake
katika kipindi kirefu kilichopita ni msingi muhimu kwa mjasiriamali yeyote
katika kumfanya aweze kuwa mjasiriamali mzuri zaidi na mfanyabiashara katika
karne hii ya sasa ya 21.
Ujasiriamali hauhusishwi tu na mazuri kama vile watu
kuutumia katika kupata mali, utajiri na mafanikio makubwa katika maisha yao,
bali pia ujasiriamali umekuwa ukihusishwa na mambo kadhaa mabaya kama vile
unyanganyi, utumwa, biashara ya ngono, wizi na hata uuzaji wa madawa ya
kulevya. Ndiyo maana nikatangulia kudokeza kwamba ukipata masimulizi mazuri
kuhusiana na ujasiriamali unaweza usiamini masikio yako.
Maana
ya neno Ujasiriamali ni nini?
Neno Ujasiriamali, “entrepreneurship”
kwa mujibu wa kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali linatokana na neno la Kifaransa “entrepende”
likimaanisha “kuanzisha” na
kuanzisha hapa linamaanisha ni kuingia katika safari au shughuli ya kiuchumi
kwa malengo ya kusaka faida.
Lakini hivi karibuni karne iliyopita wataalamu wa uchumi
akiwemo Joseph Schumpter raia ya Austria ndiye aliyekamilisha kutoa maana pana
zaidi ya neno ujasiriamali kwa kusema hivi,
“Ujasiriamali maana
yake ni Utaratibu na Uendeshaji wa
shughuli za kibiashara kwa Ubunifu kwa
lengo la kupata Faida na utayari wa
kukabiliana na Hasara yeyote ile
itakayojitokeza.”
Unaweza kuona katika maana hapo juu maneno yaliyowekewa
msisitizo ni Utaratibu, uemdeshaji,
ubunifu, faida, na hasara. Kwa hiyo ili ujasiriamali ukamilike mtu anapaswa
atimize vigezo hivyo vyote vilivyotajwa katika maana hiyo ya ujasiriamali.
Ujasiriamali
ulianza toka zama za mawe miaka 20,000 mpaka 30,000 iliyopita.
Unaweza kudhani kwamba ujasiriamali umeanza hivi
karibuni, lakini siyo kweli, ulianza tokea binadamu alipokuwa akitumia zana
duni za mawe (Paleolithic era),
wakati huo kuna makabila yaliyokuwa tayari yamekwishaanza kufanya biashara kwa
kubadilishana mali kwa mali mtindo unaoitwa kwa kimombo “barter trade”.
Halafu kikaja kipindi cha utawala wa Mesopotamia, kipindi na mahali panaposadikika kuwa ndipo ustaarabu
ulipoanza kumea kwa mara ya kwanza kabisa duniani kutokana na kuwa watu wa
kwanza kutumia maandishi na kujenga miji.
Matokeo yake liliibuka daraja la
wafanyibiashara(wajasiriamali) kwa mara ya kwanza kabisa. Kulikuwa na watu
ambao wao kimsingi hawakujishughulisha na kazi ya kuzalisha bidhaa walizouza
bali walijifanya watu wa kati(madalali) waliojihusisha na kazi ya kuuza tu, ni
katika kipindi na mahali hapa ndipo kulishuhudiwa kwa mara ya kwanza mfumo wa
fedha ukitumika sambamba na dhana ya kukopa.
Siyo
kila ustaarabu ulikumbatia ujasiriamali.
Ujasiriamali unaendeshwa na mtu mmoja mmoja, Dola au
serikali haiwezi kuundesha, bali serikali au dola kazi yake ni kuweka mazingira
mazuri kwa ajili ya ustawi wa ujasiriamali. Dola la Mesopotamia na dola jingine
la kale “Phoenicians” lililokuwa mwambao wa bahari ya Mediterranean katika nchi
zinazojulikana leo kama Syria, Lebanon na Israel, madola haya mawili yaliweka
mazingira mazuri sana kwa wajasiriamali, lakini kuna madola mengine kama vile
Warumi wao walitengeneza utajiri wao kupitia kuteka na vita kuliko
ujasiriamali. Hawakuweza kuzalisha kitu chochote kile kipya.
Hatimaye ulikuja ustaarabu wa Kiislamu, wahamasishaji wakubwa wa ujasiriamali. Ilikuwa ni katika
eneo na nyakati hizo mambo mengi sana yaliyokuwa muhimu katika kuufanya
ujasiriamali usitawi yaliibuka, vitu kama biashara ya Hariri iliyounganisha
mataifa mbalimbali kuanzia Ulaya, uarabuni, uchina, Korea, India hadi bahari ya
Mediterranean, matumizi ya karatasi
kuandikia pamoja na namba za kiarabu ikiwemo sifuri.
Ujasiriamali
na ubunifu ni sawa na watoto wawili mapacha.
Kila panapokuwa na ujasiriamali ujue na ubunifu ni lazima
uwepo, Ujasiriamali maana yake ni mwendelezo wa kubuniwa kwa mambo mapya na
unafikia upeo wake pale ambapo jamii husika inakumbatia ugunduzi, ubunifu au
ugunduzi waweza kuwa ni wa kiteknolojia kama intaneti, mapinduzi ya viwanda
kama yaliyotokea Uingereza karne ya 20 na kushuhudiwa wagunduzi-wajasiriamali
kama vile kina Alexander Graham Bell na Thomas Edison.
Siyo
kila kitu kinachohusiana na ujasiriamali ni kizuri.
Ukweli mchungu ni kwamba, kama ilivyokuwa kwa shilingi
kuwa na pande mbili, kichwa na mwenge, ujasiriamali nao unayo mambo yake
yasiyopendeza. Katika historia nzima ya ujasiriamali toka ulipoanza zama hizo
za mawe mpaka hivi leo, umepitia mambo mengi mabaya kama vile, Utumwa,
uharamia, uvamizi, vita, ukiritimba na ulaghai katika kujipatia faida isiyokuwa
halali.
Hitimisho.
Unaweza ukajiuliza, sasa ujasiriamali unaelekea wapi? Ni
nini kitatokea baada ya miaka tuseme 50 au 100 ijayo?. Tushuhudie mabadiliko
makubwa zaidi yatakayoletwa na ujasiriamali kama vile mapinduzi kakubwa zaidi
katika teknolojia kama ya intaneti, urukaji wa anga za mbali zaidi na pengine
binadamu kugundua hata sayari nyingine au mahali nje ya mfumo wetu huu wa
sayari(solar system) ambapo kutakuwa na makazi mapya.
Vizazi vijavyo vitakuja kusoma historia jinsi wavumbuzi
walivyoanza kufika sehemu hizo nje ya dunia hii tunayoishi mithili ya vile
tusomavyo leo jinsi kina Columbus walivyovumbua Amerika, India na Afrika.
........................................................................................................
Mpenzi Msomaji wa makala hii, blogu yako ya jifunzeujasiriamali inathamini sana muda wako na kuheshimu uamuzi wako wa kuacha mambo yako mengi ukasoma hapa, ndiyo maana inajitahidi pia kuhakikisha kila inachokiweka hapa kinakuwa ni kitu kilichokuwa na thamani.
Mbali na makala hizi za kueleimisha kila siku pia vipo vitabu vya biashara na ujasiriamali unavyoviona hapa chini;
1. BEI NI TSH. 20,000/=
2. BEI NI TSH. 10,000/=
3. BEI NI TSH. 5,000/=
Kama utapendezwa na kimojawapo, viwili au hata vyote vitatu basi usisite kuchukua. simu 0712202244 au 0765553030
Kwa vitabu halisi(Real books) au hardcopy njoo mbezi kwa msuguri, tunatazamana na Malori makubwa ya mikoani yanakosimama, au njia ya kuingia hospitali ya BOCHI, fuata njia kulia mwa kibao cha hospitali utakuta hardware ofisi ipo hapo.
Ukitaka uletewe ulipo, tuwasiliane lakini gharama ya nauli itaongezeka sh.1500/=
Kwa wateja wa mikoani, ghaarama ya kutuma kitabu/vitabu vikubwa ni shilingi elfu nane 8 (8,000/=)
Ukitaka utumiwe kitabu kama softcopy(pdf) kwa email, bei zake hupungua kidogo, kitabu cha 1 ni sh. 10,000, kitabu cha 2 ni sh. 5,000/= na cha tatu 3 ni sh, 3,000/= Lipa fedha kupitia namba zetu za simu, tuma na anuani yako ya email na utatumiwa kitabu nara moja bila kuchelea.
SIMU:
0712202244 au 0765553030 Jina: Peter Augustino Tarimo
Kwa vitabu zaidi tembelea, SMART BOOKS TANZANIA
0 Response to "MAANA KAMILI YA UJASIRIAMALI: ULIKOTOKA, ULIPO NA UNAKOELEKEA DUNIANI"
Post a Comment