Semina yetu ya namna ya kuandaa mpango wa biashara au mchanganuo wa biashara katika blogu maalumu ya kiingilio iitwayo DARASA LASEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA, leo hii ndiyo inafika mwisho wake lakini habari njema ni kuwa Semina hii jinsi mfumo wake ulivyotengenezwa ni kwamba HAICHACHI.
Ikiwa hujajiunga na una nia ya kupata semina hizo basi
unaweza ukajiunga hata baada ya muda wa mwisho. Masomo yote toka awamu za nyuma
yamehifadhiwa katika blogu hiyo maalumu. Unachopaswa tu kufanya ni kulipa
kiingilio chako shilingi elfu 10 kupitia namba za simu 0712202244 au
0765553030, jina litokee Peter
Augustino Tarimo, unatuma na anuani yako ya e-mail kwa meseji kisha utatumiwa
email yenye link ya kuingia katika BLOGU HII.
Siku ya tatu ya awamu hii ya 3 ya semina tutamalizia na
vipengele vya Muhtasari, Biashara, Mikakati na Utekelezaji vya mchanganuo wa
biashara ya saluni ya kike, Rse Hair & Beauty Saloon iliyopo maeneo ya
Mwenge jijini Dar es salaam. Utaona toka mwazo hatukufuata mlolongo rsami wa
vipengele kama unavyotakiwa kuwa nah ii ni kuonyesha kwamba unapoandika
mchanganuo wa biashara siyo sheria au lazima kwamba ufuate mlolongo sawasawa
kama ulivyo, unaweza ukaanza na kipengekle chochote kile.
Nachukua pia nafasi hii kuwashukuru sana washiriki wote
tuliokuwa wote katika semina hii na awamu nyingine zote zilizopita, nawaahidi
tutakuwa na semina nyingine nyingi hapo baadae zilizokuwa na manufaa makubwa
kwa wote mtakaoshiriki na wale watakaojiunga baada ya hapa.
Mwisho nawatakia kheri wale wote waliofunga, Mfungo
Mtukufu wa Ramadhani.
0 Response to "NI SIKU YA MWISHO YA SEMINA AWAMU YA 3 LEO LAKINI BADO HAIJACHACHA, NAFASI IPO"
Post a Comment