Upangaji wa bei ni jambo muhimu sana katika kufaulu au kuanguka kwa biashara.Baada ya kufanya utafiti na kufahamu wateja wako watarajiwa ni akina nani, sasa ni wakati wa kujua kiasi cha fedha utakazowatoza kwa jili ya bidhaa au huduma utakayowauzia.
Bei ya bidhaa
au huduma hupangwa kutegemeana na moja kati ya vigezo vifuatavyo;
·
Gharama za bidhaa au
huduma inayotolewa.
·
Thamani ya bidhaa au
huduma kwa mteja.
·
Bei za washindani
wengine katika soko.
·
Idadi ya wateja
wanaohitaji huduma na hali ya
soko kwa ujumla.
(1). Gharama za
bidhaa /huduma .
Kigezo hiki
mfanyabiashara hujumlisha gharama zote
zilizotumika kuzalisha bidhaa/huduma
moja halafu huongeza kiasi anachoona kitampatia faida . Kwa mfano umenunua embe kwa sh. 50/=, ukaliuza sh. 100/= ongezeko la sh. 50/= ndiyo
faida na bei ya embe itakuwa sh.100/=
Wakati mwingine inakubidi pia uweke na gharama za uendeshaji au gharama za kudumu, kama vile mishahara ya wafanyakazi, kodi ya pango pamoja na uchakavu. Kwa hiyo bidhaa kama hilo embe badala ya kuliuza sh. 100/=, pengine litafikia hata shilingi 150/= kutokana na hizo gharama za kudumu (za uendeshaji) zilizoongezeka.
(2). Thamani ya bidhaa.
Unapanga bei ya
bidhaa au huduma kwa kuangalia thamani wateja
wanayoipata kutokana na huduma au bidhaa unayotoa. Mathalani, wewe ni fundi kompyuta, kutokana na mteja
kutojua namna ya kutengeneza kompyuta, unaweza ukamchaji bei kubwa na akaona
ni sawa, ingawa wewe hukutumia gharama kubwa sana kuitengeneza.
(3). Kuangalia washindani wengine sokoni.
Baada ya kufahamau
washindani wako bei zao zikoje, ni vizuri
ukapanga bei zako zisiwe juu sana wala chini sana pasipokuwa na sababu
yeyote ile ya msingi. utakapoweka
bei zako kuwa chini sana
kushinda washindani wako ni hatari kwako
kwani unaweza usipate faida na
mwishowe biashara ikafa. Pia ukiweka bei
za juu sana unaweza ukawakimbiza wateja
wakahamia kwa washindani wako na mwishowe biashara ikafa pia.
(4) Idadi ya
wateja wanaohitaji huduma na hali ya soko kwa ujumla.
Kigezo kingine
wakati wa kupanga bei, unaweza ukazingatia idadi ya wateja walio tayari kununua bidhaa/huduma
pamoja na mazingira ya soko kwa ujumla jinsi ilivyo. Njia hii huweza kuchukua sura tofauti tofauti kama
vile;
SOMA: Namna bora ya kufanya utafiti wa soko la biashara yako.
SOMA: Namna bora ya kufanya utafiti wa soko la biashara yako.
Mitindo; Watu wengine hununua nguo au viatu kwa bei ya juu bila kujali thamani
yake ilimradi tu ni mtindo unaochukuliwa ni wa kisasa na unawika kwa wakati huo.
Jina; Vitu vyenye majina makubwa kama
vile, ADIDAS, PUMA SONY, NOKIA Nk. Huuzwa kwa bei ya juu na watu huwa tayari
kununua bila wasiwasi kutokana na umaarufu wake.
Upatikanaji; Usiku muuzaji wa sigara katika kioski mjini anaweza
akauza sigara moja, sh.300/= badala ya bei ya kawaida ya sh. 150/=, na watu wakanunua
kwani hawawezi kupata mahali pengine kwa urahisi usiku huo.
Ukiritimba; Ikiwa
biashara haina mpinzani, mmiliki
anaweza akauza bei aitakayo, hata kama gharama zake siyo kubwa sana.
Ugavi na Mahitaji; Bidhaa au huduma zinapokuwa chache sokoni wauzaji
hupandisha bei kuliko bei za kawaida. Zikiwa nyingi bei hushusha bei.
Kumbuka unapopanga
bei, lenga bei ya juu, kwani baadaye ni rahisi zaidi uja kushusha kuliko kuanza
na bei ya chini halafu baadaye ukapandisha, wateja watakuchukulia kama mtu mwenye tamaa
na hatimaye kukuhama.Vilevile hatari ya kuuza
bei ya chini sana ni wateja kudhani kwamba bidhaa au huduma zako hazijapitia ukaguzi wa viwango vinavyotakiwa kama vile TBS nk.
Kwa biashara mpya
inayoanza, kupunguza sana bei ni kosa kubwa, ni bora ukaweka bei ya juu kidogo
na kisha wateja ukawapoza kwa kuwaahidi faida nyinginezo kama vile upatikanaji wa
uhakika wa bidhaa/huduma, huduma bora na za haraka, huduma za kitaalamu baada
ya mauzo nk. Wape sababu toufauti na bei
itakayowafanya wanunue kutoka kwako.
……………………………………………………………………
Kwa elimu ya
kutosha na ya uhakika kuhusiana na ujasiriamali na biashara, jipatie vitabu
mbalimbali hapa kwenye ukurasa wa SMART BOOKS TZ.
Pata hapa SEMINA KAMILI JUU YA UANDAAJI WA MICHANGANUO YA BIASHARA kwa shilingi elfu 10 tu
pamoja na kitabu cha michanganuo free bila malipo.
Kwa HUDUMA
nyinginezo bonyeza maandishi hayo.
0 Response to "NJIA RAHISI YA KUPANGA BEI YA BIDHAA AU HUDUMA UNAYOUZA"
Post a Comment