Wiki end hii tutakuwa
na semina ya kuandika mpango wa biashara itakayoanza siku ya jumapili mpaka
jumanne na itahusu Mchanganuo wa saloon ya kike iitwayo, Rose Hair and Beauty Saloon.
Semina hii itaendeshwa kwa mfumo wa blogu maalumu(private,
ambayo hufunguka kwa yule aliyealikwa tu) pamoja na email.
·
Mshiriki
atajifunza namna ya kuandika mchanganuo mzima wa biashara kuanzia mwanzo mpaka
mwisho kwa kutumia mchanganuo wa biashara ya saluni ya kike.
·
Mshiriki
atapata pia fursa ya kusoma masomo ya awamu nyingine zote zilizopita,awamu ya 1
& 2 ambazo zipo kwenye blogu hiyo.
·
Masomo
yapo katika mifumo ya post za kawaida, mp3 na PDF na hutumwa katika email ya
mshiriki pamoja na kuwekwa katika BLOGU HII MAALUMU YA SEMINA.
·
Mshiriki
atapewa bure kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA softcopy.
·
Mshiriki
anaweza kuuliza maswali kwa jambo linalomtatiza muda wowote na kujibiwa na
wakufunzi ambao muda wote wa semina wapo online.
ADA NA JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA
Kujiunga na semina hii, lipa shilingi elfu 10 kupitia namba za simu,
0712202244 au 0765553030
jina litokee, Peter Augustino Tarimo, tuma pia kwa njia ya meseji anuani
yako ya email(GMAIL), siyo yahoo wala aina nyingine yeyote kwani BLOGU HII YAMASOMO inasapoti gmail peke yake ili kujiunga.
Baada ya hapo utatumiwa email yenye baadhi ya masomo pamoja na link
itakayokuwezesha kuingia katika BLOGU YA SEMINA.
Hapa chini ni muhtasari wa mchanganuo huo tutakaojifunza,
SALUNI YA KIKE.
Rose Hair and Beauty Saloon.
Muhtasari.
Rose Hair and
Beauty Saloon ni saluni ya kike
itakayotoa huduma bora za utengenezaji
wa nywele pamoja na bidhaa mbalimbali za urembo. Rose Hair pia patakuwa ni mahali pa wasichana na kina mama kubadilishana mawazo juu ya maswala mbalimbali ya kimaendeleo badala ya majungu
na umbea kama ilivyokuwa kwa saluni nyingi.
Rose Hair and Beauty
Saloon itasajiliwa kwa msajili wa Makampuni na mmiliki wake ni Rosemary Michael
ambaye atatoa kiasi cha Sh. 3,200,000/=
kama mtaji utakaoongezewa na
mkopo kutoka Benki ya Wanawake kiasi cha
shilingi 5,000,000/=.
Mkakati wao mkubwa
utalenga katika kuhakikisha wateja wao
wanapata kitu cha ziada kama ushauri na
stadi mbalimbali za kimaisha zitakazojadiliwa
saluni. Pia watajitangaza kwenye face book na Twiter.
Kutakuwa na jumla ya wafanyakazi wanne akiwemo
Rosemary mwenyewe.Wafanyakazi wa Rose Saloon wakiongozwa na mkurugenzi wao
watakuwa ni watu wenye ujuzi na
ubunifu wa hali ya juu, siyo tu katika maswala ya urembo bali
pia katika maswala ya kijamii, kisaikolojia na ujasiriamali.
Mauzo yataongezeka kwa
wastani wa asilimia 22% kwa mwaka
huku Mauzo mengi yakitokana na huduma
mbalimbali kuliko bidhaa watakazouza. Faida itaanza kuonekana mara baada ya mwezi wa kwanza kupita
kutokana na eneo lenyewe kuwa ni lenye
watu wengi na linaonekana pande zote magari na watu wanakotokea.
...............................................................................................
Ndugu msomaji, Vitabu vyetu vitatu, Michanganuo na ujasiriamali, Biashara ya duka, na Miferei 7 ya pesa , vyote sasa vinapatikana katika mifumo yote miwili hrdcopy na softcopy.
Ukihitaji hardcopy bei yake na shilingi elfu 20, tupo Mbezi kwa Msuguri stendi ya daladala karibu na Bochi hospital kama upo Dar es salaam, na kama upo mikoani, tuma pamoja na usafiri shilingi elfu 8 jumla ziwe elfu 28. Unaweza pia kumuagiza mtu anayekuja Dar akuchulie.
mimi sijaunganishwa kwenye hiyo private blog ila nilikwisha lipia na nikatumiwa kitabu cha michanganuo ya biashara na ujasiriamali
ReplyDelete