SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA AWAMU YA 3: SALUNI YA KIKE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA AWAMU YA 3: SALUNI YA KIKE

Wiki end hii tutakuwa na semina ya kuandika mpango wa biashara itakayoanza siku ya jumapili mpaka jumanne na itahusu Mchanganuo wa saloon ya kike iitwayo, Rose Hair and Beauty Saloon.

Semina hii itaendeshwa kwa mfumo wa blogu maalumu(private, ambayo hufunguka kwa yule aliyealikwa tu) pamoja na email.

·       Mshiriki atajifunza namna ya kuandika mchanganuo mzima wa biashara kuanzia mwanzo mpaka mwisho kwa kutumia mchanganuo wa biashara ya saluni ya kike.

·       Mshiriki atapata pia fursa ya kusoma masomo ya awamu nyingine zote zilizopita,awamu ya 1 & 2 ambazo zipo kwenye blogu hiyo.

·       Masomo yapo katika mifumo ya post za kawaida, mp3 na PDF na hutumwa katika email ya mshiriki pamoja na kuwekwa katika BLOGU HII MAALUMU YA SEMINA.

·       Mshiriki atapewa bure kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA softcopy.

·       Mshiriki anaweza kuuliza maswali kwa jambo linalomtatiza muda wowote na kujibiwa na wakufunzi ambao muda wote wa semina wapo online.

ADA NA JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA
Kujiunga na semina hii, lipa shilingi elfu 10 kupitia namba za simu, 0712202244  au  0765553030  jina litokee, Peter Augustino Tarimo, tuma pia kwa njia ya meseji anuani yako ya email(GMAIL), siyo yahoo wala aina nyingine yeyote kwani BLOGU HII YAMASOMO inasapoti gmail peke yake ili kujiunga.

Baada ya hapo utatumiwa email yenye baadhi ya masomo pamoja na link itakayokuwezesha kuingia katika BLOGU YA SEMINA.

Hapa chini ni muhtasari wa mchanganuo huo tutakaojifunza,

SALUNI YA KIKE.
Rose Hair and Beauty Saloon.

Muhtasari.
Rose  Hair and Beauty Saloon ni saluni  ya kike itakayotoa huduma  bora za utengenezaji wa nywele pamoja na bidhaa mbalimbali za urembo. Rose Hair pia  patakuwa ni mahali pa wasichana  na kina mama kubadilishana mawazo  juu ya maswala  mbalimbali ya kimaendeleo badala ya majungu na umbea kama ilivyokuwa kwa saluni nyingi.

Rose Hair and Beauty Saloon itasajiliwa kwa msajili wa Makampuni na mmiliki wake ni Rosemary Michael ambaye atatoa kiasi cha Sh. 3,200,000/= kama mtaji utakaoongezewa na mkopo  kutoka Benki ya Wanawake kiasi cha shilingi 5,000,000/=.

Mkakati wao mkubwa utalenga  katika kuhakikisha wateja wao wanapata kitu cha ziada  kama ushauri na stadi mbalimbali za kimaisha  zitakazojadiliwa saluni. Pia watajitangaza kwenye face book na Twiter.

Kutakuwa na jumla ya wafanyakazi wanne akiwemo Rosemary mwenyewe.Wafanyakazi wa Rose Saloon wakiongozwa na mkurugenzi wao watakuwa  ni watu wenye ujuzi na ubunifu  wa hali ya  juu, siyo tu katika maswala ya urembo bali pia katika maswala ya kijamii, kisaikolojia na ujasiriamali.

Mauzo yataongezeka kwa  wastani wa asilimia 22% kwa  mwaka huku Mauzo mengi  yakitokana na huduma mbalimbali kuliko bidhaa watakazouza. Faida itaanza kuonekana  mara baada ya mwezi wa kwanza kupita kutokana  na eneo lenyewe kuwa ni lenye watu wengi na linaonekana pande zote magari na watu wanakotokea.

...............................................................................................
Ndugu msomaji, Vitabu vyetu vitatu, Michanganuo na ujasiriamali, Biashara ya duka, na Miferei 7 ya pesa , vyote sasa vinapatikana katika mifumo yote miwili hrdcopy na softcopy.

Ukihitaji hardcopy bei yake na shilingi elfu 20, tupo Mbezi kwa Msuguri stendi ya daladala karibu na Bochi hospital kama upo Dar es salaam, na kama upo mikoani, tuma pamoja na usafiri shilingi elfu 8 jumla ziwe elfu 28. Unaweza pia kumuagiza mtu anayekuja Dar akuchulie.





1 Response to "SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA AWAMU YA 3: SALUNI YA KIKE"

  1. mimi sijaunganishwa kwenye hiyo private blog ila nilikwisha lipia na nikatumiwa kitabu cha michanganuo ya biashara na ujasiriamali

    ReplyDelete