Unapoandika
mpango wa biashara au hata ikiwa wewe ni mfanyabiashara tu unayetaka kufanikiwa
katika biashara unayofanya, huna budi kugawa soko lako katika vipande vipande. Kuligawa soko katika
vipande tofauti maana yake ni kuwapanga wateja wako watarajiwa katika makundi
tofauti tofauiti kulingana na vigezo
kama vile, umri, kipato, aina ya bidhaa wanazopendelea, maeneo (kijiografia),
mahitaji ya wateja, ama mgawanyo mwingine wowote ule utakaochagua.
Kuligawa
soko kutakuwezesha kulifahamu vizuri
zaidi soko lako na kukuwezesha kuelekeza
nguvu zako za matangazo na promosheni
katika lengo moja au mawili
badala ya malengo mengi tofauti
tofauti yatakayo sababisha mafanikio yawe kidogo. ‘Kumbuka mkimbia na kuku wengi
hatimaye huwakosa wote’.
Pia
kutakuwezesha kuwafahamu washindani pamoja na bidhaa wanazozalisha zinazofanana
na za kwako hivyo utaweza kujua ni hatua zipi uchukue kuimarisha zaidi shughuli
zako za kutafuta masoko na mauzo.
Kwa mfano mtu
mwenye mgahawa eneo fulani anaweza akawagawa wateja wake
muhimu kama ifuatavyo;
1)
Wenye kipato cha chini.
2)
Wenye
kipato cha kati na
3)
Wenye kipato cha juu.
Mwenye biashara ya kusambaza vifaa vya ujenzi
anaweza akaligawa soko/ wateja wale katika makundi kama ifuatavyo;
1) Taasisi za serikali.
2) Makampuni binafsi.
3) Watu binafsi.
Mgawanyo
wa soko unasaidia biashara /kampuni
kupanga malengo yake katika makundi
tofauiti ya wateja
ukizingatia unakuwa umefahamu
vizuri ni kundi lipi lenye wateja wengi au ni lipi linalolipa zaidi. Katika kuchagua ni
kipande/kundi gani utazingatia zaidi faida za kundi husika.Unaweza ukachagua
kundi moja, mawili au zaidi. Lakini inashauriwa “kudili” na makundi machache
kadiri inavyowezekana hata ikibidi kundi moja tu kwani unapoamua kulenga
makundi mengi zaidi unapunguza ufanisi.
Hakikisha
kama unatengeneza mpango wa biashara, unaelezea kwa chati na jedwali kila kipande katika mgawanyo wako kwani ndio msingi wa mikakati
yako. Eleza kwa mfano ni kitu gani kinachotofautisha Taasisi za serikali na
makampuni binafsi, je ni mauzo?, ni idadi ya wafanyikazi?, ni wingi wa
bidhaa wanazonunua ama kuna kigezo kingine chochete kile?.
Pia
mgawanyo wa soko unakuwezesha kufahamu kwa uhakika zaidi washindani wako
wanaolenga soko lile lile unalolenga wewe. Utapangilia vizuri kampeni zako za matangazo, promosheni na programu za mauzo.
Katika kugawa soko zingatia vigezo vinavyoleta tofauti katika watu kununua, kuchagua vyombo
vya habari utakavyotumia kutangaza na hadhi ya wateja walengwa, jiulize ikiwa
vitu kama umri , elimu aina ya chakula kipato na mitindo kama vina athari yeyote kwa wateja unaotaka
kuwalenga.
Jibu
litategemea aina ya biashara unayofanya,
kwa mfano nguo za mtindo fulani zitapendwa na
vijana zaidi kuliko makundi ya
watu wengine,na kuna baadhi ya migahawa huwavutia zaidi watu wenye elimu ya
juu, Ni mara chache utakuta watu wenye elimu ama vipato vya chini
wakiingia sehemu kama Mlimani City, Movenpick
au migahawa mingine mikubwa mjini.
Kipande cha soko
lengwa.
Kipande
cha soko lengwa maana yake ni kwamba katika makundi ya watu au soko uliyogawa, chagua
ni kipande au kundi gani unaloona linafaa zaidi au linaendana na mikakati yako
uliyojiwekea.Kundi/kipande hiki ndicho utakachozingatia zaidi kukihudumia ili
kikuingizie faida zaidi.
Elezea
ni kwa nini biashara yako inalenga kundi/makundi
hayo ya wateja (soko), ni kitu gani
kinachoyafanya yakuvutie kushinda makundi mengineyo?. Unapogawanya soko lako katika
vipande vipande unatakiwa ufanye
hivyo ki-mkakati, kwa mfano, muuza nguo
za fasheni anaweza kulenga kundi la
wenye kipato cha juu kwani anajua wanapenda vitu vyenye majina makubwa na vya
bei ya juu.
………………………………………………………….........
Mpenzi
msomaji wa makala hii, ikiwa unataka kujua kwa kina jinsi ya kuandaa mpango wa
biashara yeyote ile jiunge na semina inayoendelea sasa katika BLOGU YA MICHANGANUO,
ni blogu (private) unayoingia tu kama umeshalipa kiingilio chako sh. elfu 10.
Ndani ya semina hiyo utapata mambo mengi yakiwamo,
·
Masomo 11 ya jinsi ya kuandaa mpango wa biashara katika fomati za
PDF na MP3
·
Templates au vielezo kwa ajili ya kurahisisha kazi ya kuandika
mpango wa biashara kwa lugha za kiswahili na kiingereza.
·
Mpango wa biashara ukurasa mmoja, hii ni staili au mtindo wa
kuandika mpango wa biashara mfupi na uliokuwa rahisi sana ikiwa huna muda wa
kutosha kuandika mpango mrefu.
·
Mifano halisi ya michanganuo ya biashara kwa kiswahili na kwa
kiingereza.
·
Michanganuo halisi mbalimbali ukiwemo wa kuku wa mayai, saluni ya
kiume na mingineyo.
·
Vitabu 2 vya jinsi ya kuandika mpango wa biashara, vya kiswahili
na kiingereza(The very best books on business
planning ever)
Jiunge sasa
kwa kulipa kiingilio chako sh. elfu 10 tu kupitia namba za simu 0712202244 au
0765553030, jina ni Peter Augustino, tuma na anuani yako ya e-mail(GMAIL
lakini) kwa meseji, kisha utapata email yenye masomo pamoja na link ya BLOGU YAMASOMO YA SEMINA hiyo.
0 Response to "UMUHIMU WA KULIGAWA SOKO LA BIASHARA YAKO KATIKA MAKUNDI/VIPANDE TOFAUTI"
Post a Comment