MEN ARE FROM MARS, WOMEN ARE FROM VENUS ni kitabu kinachohusu mahusiano baina ya mwanamke na mwanamume maarufu sana na kilichowahi kuuza nakala zaidi ya milioni 50, kiliandikwa na kuchaposhwa na John Gray hapo mwaka 1992. Maudhui ya kitabu hiki ni utofauti mkubwa ulioko baina ya wanaume na wanawake kiasi kwamba tofauti hiyo inalinganishwa na viumbe hawa wawili kutokea sayari mbili tofauti yaani Mars na Venus.
Mwandishi wa kitabu hiki haishii tu hapo bali anazidi
kubainishakwamba, matatizo na sintofahamu nyingi kwenye mahusiano ya mwanamke na mwanaume
hutokana na wahusika kutokuzifahamu tofauti hizo zilizopo na kuzifanyia kazi
ipasavyo.
Na
kunapokuwa na mikwaruzano kati ya watu wawili
mume na mke au baina ya marafiki wawili wa jinsia tofauti ujue na
ufanisi katika kazi au biashara nao hupungua kwa kiasi kikubwa. Ili kuweze kuwa
na maendeleo wanawake na wanaume inafaa waishi kwa masikilizano.
0 Response to "WANAUME NI KUTOKA SAYARI YA MARS , WANAWAKE VENUS"
Post a Comment