Kama
ilivyokuwa kawaida kwa kipengele hiki cha Zungumza na mshauri, huwa baadhi ya
majibu ya maswali wanayouliza wasomaji wa blogu hii tunayaweka moja kwa moja
kwenye blogu kama makala za kawaida, kuna maswali mengine mengi ambayo huwa
tunawajibu wasomaji moja kwa moja kwenye inbox zao. Katika majibu tunayoyaweka
hapa kama haya ya leo tunafanya hivyo lakini bila ya kutaja kabisa jina la
muuliza swali wala kutaja utambulisho wake wowote ule, tunatumia jina
lisilokuwa halisi kwa mfanao katika majibu ya leo tumetumia jina la Salma
ambalo ni la kubuni siyo jina halisi la aliyeuliza swali.
Muuliza
swali la leo aliuliza kama ifuatavyo;
Asante sana kaka
Peter kwa kunifumbua macho kuhusiana na ujasiriamali, kitu ambacho nakipenda
sana lakini bado ninazo changamoto. Makala zako hasa hii ya Biashara
zilizosahaulika hususani biashara ya kuuza supu ya kuku wa kienyeji kwa kweli
imenihamasisha mno. Nimepata wazo jipya ambalo naomba tu Mungu anisaidie niweze
kulitimiza kutokana na kwamba mtaji wangu ni mdogo sana. Ninao kuku wa kienyeji
kama mia hivi na hapo kabla sikuwa nawaza kabisa juu ya biashara
zilizosahaulika kama hii ya supu ya kuku. Natamani sana kuifanya lakini
changamoto yangu kubwa na ambayo ningehitaji ushauri kutoka kwako ni jinsi ya
kuweka mpangilio wa biashara hii. Naomba sana mawazo yako nahisi biashara hii
itaweza kunitoa na kuondokana na hali ngumu ya kiuchumi.
AHSANTE SANA.
Hellow
Dada “Salma”,
Kwanza kabisa
nashukuru sana kwa kuwa msomaji wa makala katika blogu ya jifunzeujasiriamali,
tena pia nimefurahi kwa kuniambia makala hizo mfano wa hii ya biashara
zilizosahaulika imekuhamasisha kwa kiasi kikubwa.
Umeniambia tayari unao
mradi wa kuku wa kienyeji 100 na nadhani hilo ni jambo zuri, hiyo kijasiriamali
siyo hatua ndogo hata kidogo, tayari wewe unao mtaji mkubwa tu ambao kama
utajitahidi zaidi kutega vyanzo vingine vya mapato unaweza kutoka na kuwa mtu
mwingine tofauti kabisa baada ya kipindi kifupi.
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa nasoma, nipeni ushauri nina wakati mgumu.
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa nasoma, nipeni ushauri nina wakati mgumu.
Salma tayari wewe ni
mjasiriamali wala usiwe na shaka kuhusiana na hilo, unachohitaji zaidi ni
uthubutu tu, hebu zidisha ujasiri wako uweze kupiga hatua zaidi ya pale
ulipokuwa na kulingana na swali lako nadhani hiyo ndiyo shida yako kubwa kwani
tayari mtaji unao kitu ambacho kwa kiasi kikubwa ndicho kinachowasumbua
wajasiriamali wengi wadogo na wala siyo maarifa kama wengi wanavyodai, mimi kwa
maoni yangu kuna wakati maarifa nalazimika kuyaweka nafasi ya pili.
Kuhusiana na
mchanganuo wa biashara, umetoa mfano wa biashara kama za supu nk. mbona siyo
kitu kigumu? Maana ya mpango wa biashara au mchanganuo siyo kitu cha ajabu
sana, mtu yeyote yule anayeanzisha biashara au aliyewahi kufanya biashara
yeyote ile basi na ujue moja kwa moja ameshafanya mchanganuo wa biashara
kichwani mwake, ni vile tu huwa hatujui kama tunafanya michanganuo ya biashara
vichwani mwetu.
Kitendo cha kufikiri ni mtaji kiasi gani unahitaji, biashara yako
utaifanyia eneo gani, utaweka mfanyakazi au utakaa mwenyewe kwenye biashara,
utanunua wapi bidhaa zako au malighafi, utauza bei shilingi ngapi, faida
utapata kiasi gani nk. huo ndiyo mchanganuo wenyewe wa biashara, "so,
almost every person do a business plan at a certain time in his/her
lifetime" Tatizo huja pale mtu unapomwambia juu ya mpango wa
biashara wa kuandika katika makaratasi, watu wengi hawapendi lakini ni kwa vile
tu hawaelewi faida zake.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanijio ya biashara yako.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanijio ya biashara yako.
Hivyo dada Salma
nisingependa kukuchosha sana na mlolongo wa maelezo wakati wewe shida yako ni
mchanganuo wa biashara ya supu ya kuku wa kienyeji. Kwa kuwa tayari unafanya
biashara, suala la mchanganuo wa biashara haliwezi likawa gumu kwako hata
kidogo, unaweza kama nilivyokutajia hapo juu ukafikiria tu kichwani masuala
yote yanayohitajika kutekeleza biashara ya supu na ukawa ndiyo mpango wako wa
biashara, au pia unaweza ukaamua kutafuta mchanganuo wowote ule ulioandikwa
ukaupitia na ukapata picha mchanganuo wa biashara unakuwaje na kisha ukaandaa
wa kwako.
Sisi tunacho kitabu
kiitwacho MICHANGANUO YA BIASHARA NAUJASIRIAMALI, ndani yake kuna michanganuo ya biashara mbalimbali
iliyoandikwa kwa lugha ya kiswahili ambayo mtu yeyote yule mwenye nia ya
kujifunza michanganuo ya biashara kwa lengo la kuendesha biashara yake kwa
ufanisi basi michanganuo iliyopo katika kitabu hiki inaweza ikawa msaada muhimu
sana kwake. Vile vile tuna kakitabu kengine kazuri sana na nafikifi kama
hukuwahi kukisoma kitakufaa sana mtu ambaye una nia ya kutengeneza vyanzo
mbadala vya mapato, kinaitwa MIFEREJI 7YA PESA.
Mwisho nikutakie
shughuli njema na mafanikio katika mradi wako wa kuku na naamini kwa ushauri
huu basi hutasita kuanzisha moja kati ya biashara zilizosahaulika kama hii ya
kuuza supu ya kuku wa kienyeji, tena kwa bahati njema basi wala
hutahangaika kutafuta mtaji, kuku unao mwenyewe, labda utauza hapo wawili au
watatu tu upate hela kidogo kwa ajili ya mahitaji mengine kama eneo, vyombo na
viungo kama pilipili, ndimu au limao.
0 Response to "BIASHARA HII ILIYOSAHAULIKA NATAMANI KUIFANYA LAKINI SIFAHAMU MCHANGANUO WAKE (USHAURI)"
Post a Comment