Mpenzi msomaji wa blogu ya
jifunzeujasiriamali, blogu yako imeanzisha kipengele kidogo kitakachokuwa na
mfululizo wa zile aina za biashara ndogondogo ambazo tumezoea kuziona watu
wakizifanya mitaani lakini mara nyingi hatuzitilii maanani, tunadhani ni biashara
ambazo hazilipi au za watu wasiokuwa na mitaji, kumbe tunasahau ya kwamba ni
biashara kama zilivyokuwa biashara zingine zozote zile na huwaingizia faida ya
kutosha tu wale wanaoamua kuzifanya kwa malengo.
Unaweza ukakaa mahali huna cha kufanya
kutokana na kukosa pengine mtaji ama uao mtaji lakini ni kidogo sana na
unahofia ikiwa kama utaamua kuanzisha biashara kubwa kidogo au hata ya kati
basi mtaji wote utaishia hapohapo. Nataka nikutie moya kwamba unapojikuta kwa
bahati mbaya ukiwa katika hali kama hiyo, usikate tamaa bali angalia ni
biashara gani ndogo kabisa unayoweza ukaianzisha kwa mtaji kidogo kabisa
uliokuwa nao, haishindikani, na wala hamna kitu kisichouzika ilimradi tu,
umeangalia katika mazingira yako ni kitu gani wateja wanachohitaji kweli.
Ondoa aibu kwani yule utakayemuoonea aibu
hata ukimfuata kumuomba akupe mia mbili
ununulie kipande cha mhogo wa kukaanga atakuona mtu wa ajabu. Kwa leo
biashara ndogo ya mtaji kidogo niliyokuandalia si nyingine bali ni hii hapa
chini;
Biashara
ya kuuza supu.
Biashara ya supu inaonekana kuwa ni biashara
ya kawaida sana miongoni mwa biashara zinazofanyika katika mitaa yetu kila siku
hasa hasa mijini lakini biashara hii siri yake kubwa ni kwamba haihitaji
uwekezaji wa mtaji mkubwa sana kusudi mtu aweze kuanza, siri nyingine kubwa
katika biashara hii ni kwamba supu safi, halali na nzuri hupendwa sana na watu
wa kada mbalimbali, haijalishi mtu ni wa dini gani au kabila, karibu kila mtu
anapenda supu hasahasa nyakati za asubuhi au jioni.
Ni biashara endelevu kwani mtu anapokunywa
supu leo na kukuta ina ladha nzuri ya kupendeza na kesho yake atakuja tena na
tena na hivyo kukupa faida endelevu. Siri kubwa ya kuvuta wateja kwenye
biashara ya supu ni USAFI katika
vyombo, eneo lenyewe la biashara na mhusika anayewahudumia wateja.
Mtaji
wa biashara ya kuuza supu.
Unaju ni kwanini nimetangulia kusema biashara
ya supu haihitaji mtaji mkubwa? Hapa sasa nitaenda kukufafanulia. Ili biashara
nzuri ya supu iweze kukamilika vinahitaika vitu hivi vitatu;
1) Eneo
au mahali pa kuuzia supu
2) Vifaa
kama vile jiko, sufuria, sahani, bakuli, kisu na vijiko.
3) Nyama
na viungo vyake kama pilipili, ndimu, tangawizi, nk.
Ukitazama vitu hivi vikuu vitatu ambavyo
ndiyo mahitaji yetu makubwa kwa ajili ya kufungua biashara ya kuuza supu ni
mahitaji ambayo bila shaka yeyote ile kama mtu utaamua kikamilifu hayawezi
kukushinda. Ni kweli kabisa hata mimi nafahamu kuanzisha biashara yeyote ile
hata ikiwa mtaji ni mdogo kiasi gani lakini kama hauna pesa yeyote mfukoni hata
ungeambiwa zinahitajika shilingi elfu tano tu, inakuwa
mtihani.
Kwa hiyo pamoja na kusema kwamba ni biashara
isiyohitaji mtaji mkubwa bado kulingana na mazingira ya mtu mwingine anaweza
kuona bado mtaji kwake ni changamoto kubwa. Kwa hiyo nasema ni biashara isiyohitaji
mtaji mkubwa ukilinganisha ba biashara nyingine nyingi ndogondogo.
Eneo.
Eneo kwa ajili ya kuuzia supu, halina
usumbufu mkubwa sana kupatikana kutokana na biashara yenyewe kuwa ni ya muda
mchache maalumu. Supu inaweza ikauzwa kwa wastani wa masaa mawili mpaka matatu
tangu kuiva hivyo eneo litakalotumika linaweza likawa siyo la kudumu kama vile
barazani, stendi ya magari, mbele ya duka kabla wenyewe hawajafungua au baada
ya kufunga nk. Hivyo unaweza kuona ni kwa namna gani biashara hii inaweza ikawa
na urahisi katika sula zima la eneo la kuuzia.
Vifaa
mbalimbali.
Sufuria kubwa la kuchemshia supu, jiko la
mkaa au kuni, kisu, bakuli kadhaa na sahani zake, vijiko, meza pamoja na viti
au benchi ndiyo vifaa muhimu zaidi vitakavyohitajika. Hapa kidogo panaweza
pakawa na gharama lakini itategemea, wakati mwingine mtu unaweza hata kuazima
vyombo vyako mwenyewe kutoka nyumbani ukavitumia mpaka pale mambo yatakapokuwa “super”
basi ukanunua vya biashara.
Nyama
na viungo vyake.
Nyama yaweza kuwa ni ya ng’ombe, kuku, mbuzi,
au hata samaki, ngisi na pweza. Vilevile supu inaweza ikawa ni ya nyama ya
kawaida, supu ya kongoro au makongoro ambayo hujumuisha miguu ya mbuzi au ng’ombe
na baadhi ya sehemu za kichwani. Inaweza pia ikawa ni supu ya utumbo na nyama
zinazopatikana ndani ya mnyama kama vile, mapafu, figo na firigisi hasa kwa
supu ya kuku wa kienyeji na wale wa kisasa.
Viungo mbalimbali vinavyoambatana na supu
itategemea na mtayarishaji mwenyewe ataamua kuweka viungo gani. Wengine huweka
tangawizi na vitunguu, wengine karoti, pilipili hoho, kuna wengine pia hawaweki
chochote zaidi ya chumvi na mteja hujiwekea mwenyewe kwenye bakuli viungo
vingine kama vile ndimu na pilipili.
Mtaji wa kununulia vitu hivi siyo mkubwa sana
ukilinganisha na ununuzi wa bidhaa au malighafi katika biashara nyingine, na
uzuri wake ni kwamba biashara ya supu ni biashara inayofanyika na kuisha siku
moja hiyohiyo, unafahamu umepata fedha kiasi gani, unatenga kabisa pesa kwa
ajili ya kwenda kununulia malighafi kwa ajili ya siku inayofuata na faida
pembeni. Hata kama unakopa mtaji wa mtu kwa maana ya fedha taslimu au vifaa,
inakuwa rahisi sana jioni kumrudishia fedha zake zote ukabaki na faida yako
mkononi.
Kwa kawaida supu huendana na vitafunwa hasa chapati,
lakini pia vitafunio vingine huweza kutumika kama vile mandazi, mikate, skonzi,
mihogo, viazi, mkate wa kumimina, kababu, kachori nk. Vitafunwa hivi kama
huwezi kuviandaa mwenyewe unaweza ukamtafuta mtu atakayehakikisha kila siku
vinapatikana na katika ubora wa hali ya juu.
Utamu
wa supu ya kuku wa kienyeji!
Hakuna mtu yeyote yule labda awe “vegetarian” asiyeujua utamu wa supu ya
kuku wa kienyeji, ukipata eneo zuri la biashara hasa hasa stendi ya mabasi au
daladala ukaanza biashara polepole na
watu wakakuzoea, unaweza ukapata faida nzuri, kubwa na ya uhakika ndani ya kipindi
kifupi sana.
Supu
ya pweza na ngisi.
Jijini Dar es salaam katika mitaa mbalimbali
hasa nyakati za jioni supu hizi ni maarufu sana, pweza na ngisi hupatikana feri
na waauzaji wa supu hii huhitaji mtaji kwa ajili ya kununulia pweza wenyewe na
ngisi tu, huweka kijimeza kidogo na bakuli kadhaa, kisha wateja humiminika kuja
kula ngisi na pweza, wachache hupenda kunywa na supu yake ambayo huwekewa
katika vibakuli vidogo.
Pembeni utakuta wanaweka pilipili iliyoungwa vizuri na
wakati mwingine kachori au kababu Ukitaka upate wateja wengi na wa uhakika kila
siku kuwa mbunifu katika suala la usafi kwani watu wengi supu hii wanaipenda
sana lakini huogopa mazingira ya uchafu na kushea vyombo.
Usimamizi
mzuri wa biashara ya supu.
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kwamba
biashara ya kuuza supu iwe ni ya kuku, ngombe, mbuzi, bata, samaki, ngisi,
pweza au hata sungura, mara nyingi sana hufanyika masaa machache aidha ya asubuhi au ya jioni. Ikiwa utaamua
kumuachia majukumu msaidizi katika biashara hii au utaamua kufungua maeneo
zaidi kwa ajili ya kuuza supu tuseme labda mtaji umekua ukaamua uwe na ‘goli’
Tabata, Mbezi, Kariakoo, Mwenge na lingine labda Manzese, basi huna budi
kuajiri wasaidizi.
Uzuri uliopo katika biashara hii ni kwamba
bidhaa yake inaweza kupimika na ukafahamu ndani ya siku hiyo moja yamepatikana
mauzo kiasi gani. Unaweza kumuachia msaidizi idadi ya kilo za nyama unayojua
ikimalizika hutoa kiasi gani cha fedha au hata mkahesabiana idadi ya vipande
vya nyama ni vingapi ili muda wa kufunga hesabu kusijekuwa na sintofahamu.
Halikadhalika na vitafunwa navyo idadi yake
hujulikana kirahisi hivyo kuifanya biashara hii ya kuuza supu kuwa ni biashara
nzuri sana katika upande wa usimamiaji. Mapato yako hayawezi yakapotea
kiurahisi.
Hitimisho.
Ndugu msomaji
wa makala hii, tutaendelea kukuletea biashara hizi zilizosahaulika au
zinazochukuliwa ‘poa’ na watu wengi wakati zina uwezo mkubwa wa kumtoa kimaisha
mtu yeyote yule anayeamua kuzifanya kwa nia. Wakati ukisema ni biashara kichaa,
wapo “wanaopiga hela si mchezo”.
Kama utapenda
kujifunza zaidi biashara na ujasiriamali kwa kina kabisa, usisite kupata moja
ya vitabu vyetu hivi hapa chini,
Vitabu vyote 3 kwa pamoja ni shilingi 18,000/=
Kwa vitabu
zaidi katika lugha ya kiswahili tembelea, SMARTBOOKS TANZANIA
Ikiwa pia unapenda kuandika mwenyewe tunaweza kukupatia course nzima, templates na samples za michanganuo ya kiswahili na kiingereza vitakavyokusaidia kuandika kwa wepesi
Wasiliana na sisi kwa namba zifuatazo;
Whatsapp/call: 0765553030
SMS/Call: 0712202244
Business Planning
Tunaandika Mpango wowote ule wa Biashara(Business plan) kwa mahitaji yeyote, benki, wabia, wawekezaji au hata kuendeshea tu biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi. Ikiwa pia unapenda kuandika mwenyewe tunaweza kukupatia course nzima, templates na samples za michanganuo ya kiswahili na kiingereza vitakavyokusaidia kuandika kwa wepesi
Wasiliana na sisi kwa namba zifuatazo;
Whatsapp/call: 0765553030
SMS/Call: 0712202244
Your blog is real educatable with alots of different ways on how one can achieve his or her goals in bussines by use a low capital_!
ReplyDeleteTHANK YOU A LOT!
DeleteThanks, this is helpful. keep it up
ReplyDeleteBe blessed too!
Deletethanks alot i got a good message
ReplyDeleteThank you too brother Jackson!
DeleteThank you for the education
ReplyDeleteThank you Guy!
DeleteGreat
ReplyDeleteBe blessed!
Deletebe blessed champ
ReplyDelete