Mwishoni mwa juma lililopita mpaka juzi jumanne, katika
blogu yako ya jifunzeujasiriamali tulitangaza kuendesha semina juu ya jinsi
ya kuandika mchanganuo wa biashara, semina ambayo ni mfululizo wa semina za
mara kwa mara na hii ilikuwa ni awamu ya tatu ya mfululizo huo ambapo
tulichanganua mpango wa biashara ya saluni ya kike.Tunashukuru, washiriki
walijitokeza wengi na semina ilikuwa ya kufana.
Kwanini
tumeiita HAICHACHI SEMINA?
Ni semina isiyochacha kwa maana kwamba, tofauti na semina
nyingine zilizozoeleka, hii hata kama ikiwa kwa bahati mbaya hukuweza kushiriki lakini ulikuwa nayo nia ya kushiriki,
basi fursa hiyo bado inakuwepo, masomo ya awamu zote za semina zilizokwisha
pita huhifadhiwa katika blogu maalumu wanayoingia washiriki tu peke yao.
Vilevile ukishalipia awamu moja ya semina unapata fursa ya kusoma awamu zote za
nyuma na zile zitakazofuata, unapata tiketi ya kudumu.
Pamoja na kwamba semina hii haiwezi kuchacha, lakini
utafika wakati itamalizika hivyo haitadumu milele, ni vyema basi kama
unaihitaji ukapata tiketi yako mapema kabla semina haijamalizika na kufungwa
rasmi kwa ajili ya kuanza semina mpya yenye maudhui tofauti na michanganuo ya
biashara.
Kitu kingine kikubwa katika semina hii, ni fursa ya
kipekee ya kupata kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali (softcopy)
bila malipo, kitabu hiki ni ofa kwa anayelipia semina lakini ofa yenyewe nayo
ni ya muda mfupi tu, muda ukimalizika kitabu kitaendelea kuuzwa peke yake na
semina peke yake, hivyo wahi sasa badala ya kulipa shilingi elfu 20 kitabu
pamoja na semina utalipa shilingi elfu 10 tu kwa vyote viwili.
………………………………………………………………………
Kwa
mahitaji yako ya vitabu mbalimbali hardcopy na Softcopy kutoka self help books
Tanzania, tembelea ukurasa huu, SMARTBOOKS RANZANIA.
0 Response to "HAICHACHI, SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA, TUNAWASHUKURU WALE WOTE WALIOSHIRIKI"
Post a Comment