Hilo halina ubishi lakini ukweli unabakia palepale kwamba mafao hayo au pensheni hayawezi kumhakikisha mtu uhuru na usalama kifedha kwa kipindi kirefu. Fedha hizo za mafao zinahitajika zizae ndipo ziweze kumhakikishia mstaafu uhuru kifedha kwa maisha yake yote yaliyobakia.
Hali hii ndiyo husababisha watu wengi wanapokuwa bado
makazini au wawapo bado viongozi hata katika ngazi za juu kabisa wakati
mwingine hata maraisi wa baadhi ya nchi hapa duniani, hutamani au hata kuwa na
mawazo ya kuanzisha miradi ya kiuchumi kusudi watakapostaafu wawe na
vitegauchumi vya kuwafanya waendelee kuishi maisha mazuri na hapa ndipo ilipo hoja
yangu hii ninayotaka kuijenga ya kila binadamu katika nyakati fulani za maisha
yake ni lazima atafanya biashara hata mara moja taka asitake.
Yupo mzee mmoja rafiki yangu sana, siku moja nilipokuwa
napiga naye stori kuhusu masuala ya maisha, pesa, kazi na biashara kwa ujumla
akawa ananiasa sana juu ya kuzingatia kufanya biashara. Yeye anasema anapenda
sana kufanya biashara lakini anakiri katika maisha yake karibu yote hajawahi
kufanya biashara hata moja. Anasema alikuwa akifanya kazi ya kuajiriwa kama
afisa masoko kwenye taasisi moja ya serikali.
Lakini cha kushangaza akaniambia
baada ya kustaafu sasa analima mihogo huko Kiluvya kwa ajili ya kisamvu katika
shamba lake ambacho huwa anawauzia kina mama wajasiriamali ambao nao huenda kukiuza
kisamvu hicho maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Siyo hivyo tu mzee
yule wa kichagga alinieleza kwamba anao mradi wa kutotolesha vifaranga wa kuku
na kuku wachache kwa ajili ya mayai ya kuuza.
SOMA: Mchanganuo wa biashara ya kuku wa mayai 1000
SOMA: Mchanganuo wa biashara ya kuku wa mayai 1000
Ilibidi nimuulize, “Sasa mbona umesema hujui kufanya
biashara na miradi yote hiyo ni nini?” Mzee akachek sana na kusema, “afadhali
wewe unaelewa, sikupenda kukuambia nafanya biashara kwa sababu watu wengi
hawachukulii miradi kama hii kuwa ni biashara, kwenye akili za watu wengi
wamejenga taswira kuwa biashara ni zile kubwakubwa tu au zinazohusisha kuuza na
kununua peke yake wanasahau hata miradi kama hii ya ufugaji na kilimo pia ni
biashara ikifanywa kitaalamu.”
Mzee yule aliendelea kuniambia hata kuwa na
nyumba za kupangisha nayo ni biashara pia. Hivyo na mimi nikaja kutambua kwamba
hata mtu aliyestaafu kazi ya kuajiriwa lakini akawa alijenga nyumba zake za
kupangisha hilo lilikuwa ni wazo lake la biashara itakayomsaidia baada ya
kustaafu.
Hivyo ni sahihi kabisa kusema kwamba “Mwanadamu penda
asipende ni lazima katika muda fulani wa maisha yake atafanya biashara tu” Kama
ndiyo hivyo basi, ni nini cha kufanya?
Inafaa kila mtu kujifunza ABC kuhusiana na biashara na
ujasiriamali mapema iwezekanavyo bila kujali yupo katika ajira au karibu anaachana
na ajira au hata ameshastaau ajira. Uzuri ni kwamba siku hizi siyo kama zamani
mpaka uingie darasa la semina ndipo uweze kujifunza. Kuna mtandao wa Intaneti
ambao una njia nyingi za kujifunza kupitia simu yako au kompyuta. Kuna programu
mbalimbali unazoweza kufuatilia mwenyewe ukiwa popote pale. Vipo pia vitabu
kama vya SELF HELP BOOKS TANZANIA vilivyoandikwa kwa kiswahili vyenye kila kitu
ambacho mjasiriamali yeyote anahitaji ili kufanikisha biashara yake kwa ufanisi
wa hali ya juu.
Self Help books tuna kitabu kimoja, MICHANGANUO YABIASHARA NA UJASIRIAMALI, hiki ni kama alfa na Omega kwani kina kila kitu
ndani, kina kurasa 410 ambazo kila moja huwezi kuiruka kama wewe ni mroho wa
material za ujasiriamali na biashara. Tunacho pia MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRIWASIYOPENDA KUITOA, hiki nasema ndiyo baba wa vitabu vya hamasa Tanzania na
Afrika Mashariki kwa ujumla, sitii chumvi wala kuvuta kamba kwangu kama huamini
jaribu kudownload kurasa chache za KITABU HICHO HAPA usome.
Kitabu kingine cha malipo tuna MAFANIKIO YA BIASHARA. DUKA LA REJAREJA, nisingependa kukiongelea sana kitabu hiki kwani ni mimi nimekitunga mwenyewe kutokana na uzoefu wangu binafsi wa miaka 12 nikifanya biashara hiyo. Nathubutu kusema hakuna nisichojua kuhusiana na duka la rejareja, jipatie kitabu hicho uthibitishe mwenyewe.
Kitabu kingine cha malipo tuna MAFANIKIO YA BIASHARA. DUKA LA REJAREJA, nisingependa kukiongelea sana kitabu hiki kwani ni mimi nimekitunga mwenyewe kutokana na uzoefu wangu binafsi wa miaka 12 nikifanya biashara hiyo. Nathubutu kusema hakuna nisichojua kuhusiana na duka la rejareja, jipatie kitabu hicho uthibitishe mwenyewe.
Sipendi kukulazimisha kununua vitabu hivyo, kwanza sijui
mfuko wako ukoje na hali yenyewe sasa hivi inajulikana na kila mtu pesa ni
ngumu, basi walao nitakupa bure kitabu kingine hiki hapa, SIRI NA MBINU ZAKUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO, sitaki thumni yako, wewe bonyeza hayo
maandishi kisha ujaze email yako, jina na nambari ya simu kisha chukua kitabu
ujisomee free of charge..!
Kweli ksbisa
ReplyDelete