JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUSHAWISHI WATU(HOW TO WIN FRIENDS & INFLUENCE PEOPLE)-CARNEGIE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUSHAWISHI WATU(HOW TO WIN FRIENDS & INFLUENCE PEOPLE)-CARNEGIE

Kama kilivyokuwa kitabu cha Think& Grow Rich, kitabu hiki nacho ni miongoni mwa vitabu vikongwe sana vya wakati wote, kimeandikwa mwaka 1936 na mwandishi Dale Carnegie lakini umuhimu wa mafundisho yake utadhani kimeandikwa jana tu. Dale ameuza nakala za kitabu hiki zipatazo milioni 15 na zaidi.

Mwandishi wa kitabu hiki kama umewahi kukisoma pamoja na hata maudhui yake vinashabihiana kwa kiasi fulani na yale yaliyokuwemo katika Think & Grow Rich na hata unaweza kudhania labda waandishi au baadhi ya wahusika katika vitabu hivi wana uhusiano wa damu.

Kwa mfano jina Carnegie, katika Think & Grow Rich tunamuona Andrew Carnegie ndiye mhamasishaji mkubwa wa Napoleon Hill. Wakati katika kitabu hiki cha How to win friends…..., tunamuona mwandishi wake kuwa anaitwa Dale Carnegie, sasa unaweza ukajiuliza, Andrew Carnegie na Dale Carnegie wana uhusiano gani?

Jibu la swali hilo litakuja mwishoni mwa makala hii, hebu kwanza tuangalie kitabu “Jinsi ya kushinda marafiki na kushawishi watu” au “how to win friends and influence people” kinazungumzia kitu gani.

Kwa ufupi kabisa kitabu hiki Jinsi ya kupata marafiki…kinazungumzia namna tabia za mtu zinavyoweza zikamfanya akapata mafanikio kimaisha hasa jinsi mtu unavyohusiana na watu wengine, mnavyowasiliana, jinsi unavyoweza kuwafanya watu wengine kuvutiwa na mwelekeo wako au kufuata kile unachoamini wewe.

Mwandishi amejitahidi sana kuonyesha kwamba mtu unaweza kuwashawishi watu jambo lolote pasipo kukwaruzana nao hata kidogo na binadamu, taka usitake ni lazima katika maisha utategemea watu wengine na kutegemewa pia na watu wengine.Hivyo ni muhimu sana kujifunza mbinu za kuishi na watu vizuri kwa kuwafanya wakuone wewe kama sumaku na siyo wakuone kama kaa la moto, uwe asali kwao na siyo pilipili.

Je Andrew Carnegie na Dale Carnegie mwandishi wa kitabu hiki ni ndugu?

Kwanza kuwafahamu watu hawa wawili itabidi kujua historia zao kwa ufupi.

Andrew Carnegie aliyetajwa sana katika kitabu cha Think & Grow Rich alikuwa tajiri, Bilionea mkubwa sana enzi hizo huko Marekani, ingelikuwa ni nyakati hizi tungemfananisha na kina Bill Gates au Warren Buffet, ndiye aliyemhamasisha  na kumfadhili mwandishi wa kitabu Think and Grow Rich, Napoleon Hill kuandika kitabu kile. Alizaliwa mwaka 1835 na kufariki mwaka 1919. Aliacha utajiri mkubwa majumba ya kifahari na mashamba.

Bilionea Andrew Carnegie
Dale Carnegie yeye alikuwa mwandishi wa vitabu na kitabu chake maarufu sana ni hiki cha “How to winFriends & Infuence peple” Alizaliwa mwaka 1888 na kufariki mwaka 1955. Alianza kama Mhamasishaji, na mtu wa mauzo, akafungua darasa la semina za kufundisha watu jinsi ya kuzungumza mbeleza watu(public speaking) na baadae kuweza kuandika kitabu hiki maarufu.
 
Mwandishi Dale Carnegie

Kusema ukweli watu hawa hawana uhusiano wowote uyle wa damu, na kama unavyoweza kuona kila mmoja alizaliwa kipindi tofauti na mwenzake. Kufanana kwao majina kunatokana na umaarufu wa huyu tajiri Andrew Carnegie, watu wengi kipindi hicho walivutiwa na kuiga jina lake, ikawa na huyu mwandishi wa kitabu hiki naye aliamua kuchukua jina lake ambapo hapo kabla alikuwa akitumia jina jingine. Dale Carnegie alikuwa na ofisi katika jengo moja mali ya huyu bilionea Andrew lililokuwa na jina hilohilo kama uonavyo jengo la Trump leo hii kule Marekani na hapo ndipo Dale naye alipoamua kuchukua jina hilo maarufu na akaitwa Dale Carnegie mpaka leo.








1 Response to "JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUSHAWISHI WATU(HOW TO WIN FRIENDS & INFLUENCE PEOPLE)-CARNEGIE"