Kama kilivyokuwa kitabu cha Think& Grow Rich, kitabu hiki nacho ni miongoni mwa vitabu vikongwe sana vya
wakati wote, kimeandikwa mwaka 1936 na mwandishi Dale Carnegie lakini umuhimu
wa mafundisho yake utadhani kimeandikwa jana tu. Dale ameuza nakala za kitabu
hiki zipatazo milioni 15 na zaidi.
Mwandishi wa kitabu hiki kama
umewahi kukisoma pamoja na hata maudhui yake vinashabihiana kwa kiasi fulani na
yale yaliyokuwemo katika Think & Grow Rich na hata unaweza kudhania labda
waandishi au baadhi ya wahusika katika vitabu hivi wana uhusiano wa damu.
Kwa mfano jina Carnegie, katika Think & Grow Rich
tunamuona Andrew Carnegie ndiye mhamasishaji mkubwa wa Napoleon Hill. Wakati katika
kitabu hiki cha How to win friends…..., tunamuona mwandishi wake kuwa anaitwa
Dale Carnegie, sasa unaweza ukajiuliza, Andrew
Carnegie na Dale Carnegie wana uhusiano gani?
Jibu la swali hilo litakuja
mwishoni mwa makala hii, hebu kwanza tuangalie kitabu “Jinsi ya kushinda
marafiki na kushawishi watu” au “how to win friends and influence people”
kinazungumzia kitu gani.
Kwa ufupi kabisa kitabu hiki Jinsi
ya kupata marafiki…kinazungumzia namna tabia za mtu zinavyoweza zikamfanya akapata
mafanikio kimaisha hasa jinsi mtu unavyohusiana na watu wengine,
mnavyowasiliana, jinsi unavyoweza kuwafanya watu wengine kuvutiwa na mwelekeo
wako au kufuata kile unachoamini wewe.
Mwandishi amejitahidi sana
kuonyesha kwamba mtu unaweza kuwashawishi watu jambo lolote pasipo kukwaruzana
nao hata kidogo na binadamu, taka usitake ni lazima katika maisha utategemea
watu wengine na kutegemewa pia na watu wengine.Hivyo ni muhimu sana kujifunza
mbinu za kuishi na watu vizuri kwa kuwafanya wakuone wewe kama sumaku na siyo
wakuone kama kaa la moto, uwe asali kwao na siyo pilipili.
Je Andrew Carnegie na Dale Carnegie mwandishi wa kitabu
hiki ni ndugu?
Kwanza kuwafahamu watu hawa
wawili itabidi kujua historia zao kwa ufupi.
Andrew Carnegie aliyetajwa sana
katika kitabu cha Think & Grow Rich alikuwa tajiri, Bilionea mkubwa sana
enzi hizo huko Marekani, ingelikuwa ni nyakati hizi tungemfananisha na kina
Bill Gates au Warren Buffet, ndiye aliyemhamasisha na kumfadhili mwandishi wa kitabu Think and
Grow Rich, Napoleon Hill kuandika kitabu kile. Alizaliwa mwaka 1835 na kufariki
mwaka 1919. Aliacha utajiri mkubwa majumba ya kifahari na mashamba.
Bilionea Andrew Carnegie |
Dale Carnegie yeye alikuwa
mwandishi wa vitabu na kitabu chake maarufu sana ni hiki cha “How to winFriends & Infuence peple” Alizaliwa mwaka 1888 na kufariki mwaka 1955.
Alianza kama Mhamasishaji, na mtu wa mauzo, akafungua darasa la semina za
kufundisha watu jinsi ya kuzungumza mbeleza watu(public speaking) na baadae
kuweza kuandika kitabu hiki maarufu.
Kusema ukweli watu hawa hawana
uhusiano wowote uyle wa damu, na kama unavyoweza kuona kila mmoja alizaliwa
kipindi tofauti na mwenzake. Kufanana kwao majina kunatokana na umaarufu wa
huyu tajiri Andrew Carnegie, watu wengi kipindi hicho walivutiwa na kuiga jina
lake, ikawa na huyu mwandishi wa kitabu hiki naye aliamua kuchukua jina lake
ambapo hapo kabla alikuwa akitumia jina jingine. Dale Carnegie alikuwa na ofisi
katika jengo moja mali ya huyu bilionea Andrew lililokuwa na jina hilohilo kama
uonavyo jengo la Trump leo hii kule Marekani na hapo ndipo Dale naye alipoamua
kuchukua jina hilo maarufu na akaitwa Dale Carnegie mpaka leo.
nishida
ReplyDelete