Hamasa binafsi ndani ya mtu ni jambo la
msingi sana katika kuleta mafanikio na maendeleo binafsi. Ikiwa mtu atakosa ama
kupoteza hamasa inakuwa rahisi kujikuta akishindwa kuutumia vizuri muda wake kitu ambacho ndicho chenye
thamani kubwa kushinda kila kitu. Ukishashindwa kutumia muda wako kikamilifu ni
dhahiri kabisa kuwa utashindwa pia kutimiza malengo yako binafsi pamoja na yale
ya kibiashara au kazi.
Kuna nyakati binadamu huwa tunajikuta katika
wakati mgumu wa kupoteza hamasa(lose attitude) na hutokea siyo kwa kundi moja
tu la watu bali kwa kila mtu hata na wale watu wanaodhaniwa kuwa ni wenye hamasa
kubwa, waliofanikiwa au walio na malengo makubwa maishani, lakini hutumia mbinu
mbalimbali zinazowawezesha kurudi tena kwenye mstari kwa kupandisha viwango
vyao vya hamasa kuwa juu mbinu kama hizi tunazokwenda kuziona hapa chini sasa
hivi;
1. Jikumbushe
malengo uliyojiwekea mara kwa mara.
Kitu cha kwanza kabisa wakati unapokuwa ukijiwekea malengo yako yawe ni ya
muda mfupi ama ni ya muda mrefu, hakikisha malengo hayo ni halisi kusudi usije
ukavunjika moyo pindi pale malengo yako kwa bahati mbaya yatakapokataa kutimia
kama ulivyoyapanga. Kila wakati pima ni kiasi gani umetimiza malengo yako na
hakikisha malengo yako yanakupa changamoto, ikiwa hayakupi changamoto yeyote
basi ujue hayo siyo malengo. Kupima, malengo yako kila mara na kuona maendeleo
yake kutaifanya hamasa yako kubakia kuwa juu muda wote kwa kipindi kirefu. Pima
malengo yako kwa siku, wiki nk.
2.Hakikisha
unajipa zawadi.
Unapotimiza malengo yako, tuseme uliyojiwekea
labda kwa siku, wiki au hata kwa mwezi, jipe motisha au zawadi na zawadi
inaweza ikawa ni kitu chochote kile mfano kinywaji, kusikiliza muziki mzuri au
hata kula chakula kizuri unachokipenda.
3. Jipe
mapumziko.
Baada ya kufanya kazi muda mrefu na kwa nguvu
zako zote, jitengee muda wa mapumziko na hili litasaidia sana kurudisha hamasa
yako upya kama ilikuwa imeshuka chini.
4. Unapoanguka,
amka, jifunze na kusonga mbele.
Badala ya kuanza kuwaza jinsi ulivyoshindwa
kutimiza malengo uliyojiwekea, chukua kushindwa kwako huko kama funzo na
uhakikishe lengo au jukumu linalofuata
unalifanya kwa umakini zaidi, likamilishe kabla ya muda uliopanga kusudi muda
wa ziada urekebishe lile uliloshindwa kutimiza. Kumbuka kuwa kila binadamu
hukosea na kuanguka katika safari yake ya maisha.
5.
Pendelea kusoma na kutazama habari na hotuba zinazohamasisha.
Tafuta vipindi kwenye redio au televisheni
vinavyohamasisha au DVD na vitabu vya namna hiyo, unaweza pia ukasoma historia
za watu mashuhuri wanaokugusa na kukupa hamasa ya maisha katika vitabu, kwenye
mitandao au kwingineko kokote kule.
6.
Jiepushe kabisa na mambo yanayoingilia ratiba zako(vidakizi).
Baini vidakizi vyote na uviondoe mara moja au
kuviweka mbali na wewe. Unaweza kuuza, kuhifadhi au hata kukitupa kitu chochote
unachohisi kinaingilia ratiba zako na kukufanya ushindwe kutimiza malengo yako
kwa wakati. Vitu kwa mfano redio, tv, simu, magazeti nk.
7.
Jiwajibishe mwenyewe kwa kukosa kutimiza yale unayojipangia kufanya.
Unaweza ukajiwekea adhabu mbalimbali kama
vile, kujinyima vitu unavyopendelea, kuwajulisha ndugu jamaa na marafiki juu ya
mambo unayopanga kuyafanya, kusudi usipokuja kutimiza wakuchekeau kukusema na hii
itakupa motisha wa kutokushindwa tena.
SOMA: Uamuzi mgumu kwako kuchukua ili biashara yako iweze kupenya wakati huu mgumu kiuchumi.
SOMA: Uamuzi mgumu kwako kuchukua ili biashara yako iweze kupenya wakati huu mgumu kiuchumi.
8. Pata
kikombe cha kahawa au chai.
Viburudisho ni muhimu lakini chunga sana
usije ukageuka mraibu wa caffeineau pombe, tumia kiasi kidogo sana kwa ajili tu
ya kukuchangamsha.
9.
Fanya mazoezi ya mwili.
Mazoezi hata kwa kiasi kidogo tu
yamethibitika kupandisha hamasa ya mtu, kuondoa msongo wa mawazo na kuongeza
fikra chanya vitu vinavyochangia kuongeza hamasa .
10. Yagawanye
majukumu yako katika vipande vidogovidogo vinavyotekelezeka kiurahisi.
Iwe ni kazi au hata ni tatizo linalohitaji
suluhisho, kisaikolojia kuligawa katika mafungu wakati unapolishughulikia
kunakufanya uone ni rahisi zaidi kulitekeleza au kulitatua kuliko ungelitekeleza
likiwa zima kama lilivyo.
………………………………………………………………………........
Mpenzi msomaji wa makala hii, hakikisha hukosi
makala hata moja zinazowekwa katika blogu yako hii, tunajitahidi kukuletea kile
kilichokuwa bora kabisa kwa lengo la kubadilisha fikra na mitazamo kutoka ile
isiyokuwa na hamasa kubwa kwenda katika ile iliyojaa hamasa na mtazamo chanya
wenye tija katika biashara au kazi yeyote ile mtu aifanyayo.
Kwa matokeo bora zaidi ya programu yetu hii,
tunashauri pia mtu kusoma vitabu mbalimbali tulivyokuandalia, na siyo lazima
usome vile vinavyouzwa kama hali yako kipesa haiko vizuri sana, tunafahamu watu
wengi “tunastruggle” shilingi elfu 3, 5 au 10 kwa kweli wakati
mwingine ni mtihani kuipata.
Wengi wetu tunapitia huko na wengine tayari
walishapitia huko, ndiyo maana tuna vitabu pia bila malipo kama hiki cha SIRINA KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA BIASHARA, au hata hiki kingine, MSAHAFU WAMAFANIKIO(Think & Grow Rich) unachoweza ukakisoma bila kulipa chochote
ndani ya blogu yako hii.
Ikiwa bajeti yako itaruhusu basi siyo vibaya pia
ukajipatia moja kati ya vitabu hivi vitatu vifuatavyo, viwili au hata vyote kwa
pamoja kama utapenda;
BEI
Tsh. 20,000/= hardcopy na 10,000/=
softcopy kwa email
BEI: Tsh. 10,000/= hardcopy na 5,000/= softcopy kwa email
BEI: Tsh. 5,000/= hardcopy na 3,000/= softcopy kwa email
Kuona vitabu zaidi na maelezo yake tembelea SMARTBOOKS TANZANIA
Nazidi kubadilishwa na mafundisho yako
ReplyDelete