Katika kitabu chake hiki cha Kanuni za mafanikio(The
Success Principles) Canfield anakupa kanuni 65 zitakazoyabadilisha kabisa
maisha yako. Kanuni hizi zinaweza zisiwe mpya au ngeni kwako, pengine
ulishawahi kuzisoma au kuzisikia mahali pengine lakini kwasababu ni vitu
unavyohitaji kujikumbusha na kuvirudia mara kwa mara kusudi uweze kuyatimiza
malengo yako uliyojiwekea maishani, sidhani kama zitakuchosha kuzisoma.
Kanuni hizi, Jack Canfield alijifunza wakati akiwa kwenye
safari yake kuelekea kuwa mjasiriamali aliyefanikiwa, mwandishi mashuhuri wa
vitabu, kocha na mzungumzaji mahiri. Sehemu 6 za kitabu hicho zitabadilisha
kabisa mtazamo wako wa maisha uliokuwa nao na kuwa mtu wa kuchukua usukani wa maisha
yako mwenyewe, hivyo kuweza kutoka pale ulipokuwa sasa kwenda pale unapotaka
uwe.
Jack anakuamba hivi; “Kile watu wengine wanachofikiri
kuhusiana na wewe hakikhusu kabisa”
Mwisho anakupa masomo haya matatu muhimu sana;
1. Acha
kulalamika
2. Jitengee
wiki-endi moja kumalizia viporo vyako vyote vya kazi ulizokuwa hujamalizia.
3. Unaweza
kufa kwa mawazo hasi, hivyo jitahidi kufikiri chanya.
0 Response to "KANUNI ZA MAFANIKIO(THE SUCCESS PRINCIPLES) BY JACK CANFIELD"
Post a Comment