Teknolojia sasa mahali ilipofikia, huna haja tena ya
kuhangaika huku na kule kutafuta kitabu, gazeti ama jarida zuri ulipendalo kwa
ajili ya kusoma, kuna njia nyingi sasa hivi ambazo unaweza ukavipata vitu hivyo
moja kwa moja katika chombo chako cha mawasiliano unachotumia, kwa lugha ya
siku hizi huitwa MUBASHARA.
Maana yake unapata kitu iwe ni kitabu, taarifa, picha au
video moja kwa moja. Ingawa neno hilo ‘mubashara’ linaweza likamaanisha ‘live’
, kitu kikifanyika muda huo huo kama tukio, lakini pia kiswahili kinaruhusu
kubadilisha maana ya maneno yake pale neno linapoleta mantiki nzuri, mubashara
imetumika hata kumaanisha mapenzi ya kweli(mapenzi yasiyokuwa na chenga).
Moja tu ya njia hizo ni hii tunayoitumia sisi Self help
books Tanzania kuwafikia wateja wa vitabu tunavyochapisha. Tunaposema “vitabu
mubashara” tunamaanisha, Kitabu kinamfikia mteja moja kwa moja pale alipo, bila
kikwazo cha aina eyote ile, kwa gharama nafuu kuliko kama vile angelinunua
kitabu cha karatasi cha kawaida, mteja pia anakuwa na uwezo wa kukisoma kitabu
hicho muda huohuo au muda wowote awapo na nafasi na inaweza ikawa hata ni ndani ya usafiri
kwani kifaa kama simu ya mkononi mahali popote pale inawezekana mtu kufungua.
Mteja anahitaji kufanya vitu vifuatavyo ili kupata
kitabu/vitabu mubashara katika kifaa chake cha mawasiliano, kumbuka kifaa hicho
chaweza kuwa ni simu ya kisasa ya mkononi(SMARTPHONE), kompyuta ya
mezani(desktop), kompyuta mpakato(laptop) au tablet.
1) Kutuma
anuani yake ya email kwa njia ya meseji katika namba, 0712202244 au
0765553030
2) Kulipia
kitabu/vitabu kupitia namba za simu, 0712202244
au 0765553030(Peter Augustino
Tarimo)
3) Tuma
meseji ni kitabu kipi unachohitaji.
Baada ya kukamilsha hatua hizo 3, mteja atatumiwa kitabu
kikiwa katika mfumo wa softcopy(PDF) ndani ya dakika 5-10 kupitia email yake na
ataweza kukidownload(kukipakua) muda huohuo na kuanza kusoma au kukisave katika kifaa
chake cha mawasiliano.
Vitabu vilivyoko sokoni kwa sasa hivi ni hivi vifuatavyo;
Tsh. 10,000/=
Tsh. 5,000/=
Tsh. 3,000/=
Kwa vitabu zaidi, tembelea, SMART BOOKS TANZANIA
0 Response to "VITABU MUBASHARA KWENYE SIMU YAKO YA MKONONI, KOMPYUTA AU TABLET"
Post a Comment