Unajua katika shughuli zozote zile zinazohusiana na
taarifa mfano wa makala kama hii unayoisoma hapa sasa hivi, suala la mrejesho “feedback”
ni kitu muhimu sana na ndiyo kichocheo kikubwa kinachoweza kusababisha mchakato
mzima wa shughuli yenyewe ya ubadilishanaji taarifa kuwa endelevu. Naandika
haya, kwani sikutegemea kile nilichopata kama mrejesho kutoka kwa
Mchungaji huyu kutoka Mtwara.
Wawezeshaji, viongozi wa dini na kijamii. |
“Ninashukuru sana kwa masomo mazuri yaliyokuwa ndani
ya kitabu hiki, tangu mchana nimekuwa nikipitia baadhi ya sura za kitabu, kwa
kweli ni kizuri. Kesho nafundisha watu hapa Mtwara kanisa la(sijataja kanisa lenyewe)
katika semina ya ujasiriamali ambayo itahusisha Wachungaji na Wainjilisti.
Kitabu hiki naamini kitakuwa msaada mkubwa sana kwangu.
Ubarikiwe sana na Bwana,
Mchungaji (Jina sijalitaja pia)”
Kwa kweli wakati nauza kitabu hicho sikuwa na wazo kabisa
kama mteja ninayemuuzia anaweza akawa ni mchungaji, kiongozi wa dini mpaka pale
nilipoona mrejesho huo na yeye kujitambulisha kuwa ni mchungaji. Binafsi
nilifarijika sana kuona hata viongozi wa dini, asasi ama vikundi mbalimbali vya
kijamii wakitumia vitabu vyetu kwa aili ya kufundishia semina mbalimbali za
ujasiriamali, biashara na maisha kwa ujumla kwani moja ya malengo yetu makuu
ni kuona jamii na hasa wananchi wengi wa kawaida wakipata ujuzi wa kufanya
biashara kusudi waweze kuboresha maisha yao zaidi.
SOMA: Gharama za kutuma vitabu vya 'Self Help Books' Mikoani ni shilingi ngapi?
SOMA: Gharama za kutuma vitabu vya 'Self Help Books' Mikoani ni shilingi ngapi?
Vitabu vyetu vyote vitatu, kile cha Michanganuo na
Ujasiriamali, Mafanikio Biashara ya Duka La Rejareja, na hata Mifereji 7 ya
Pesa, vyote ni vitabu ambavyo mkufunzi yeyote yule wa semina za ujasiriamali au
mwezeshaji katika vikundi mbalimbali vya kijamii anaweza akavitumia katika
kuandaa mada zake. Hatuzuii kufanya hivyo ikiwa mtu anafanya kwa lengo la
kuelimisha jamii.
0 Response to "JE WEWE NI KIONGOZI WA DINI, ASASI, SACCOS, AU KIKUNDI CHA KIJAMII?"
Post a Comment