Ndugu msomaji wangu najua leo hii inawezekana kabisa
nikawakwaza baadhi ya wasomaji na wapenzi wa mtandao huu, lakini natanguliza
kuomba radhi, sijakusudia kuvunja maadili bali kuelezea hali halisi kwani pia
wasomaji hapa ni watu wa aina mbalimbali na waliokuwa na imani tofauti tofauti.
Kimsingi sishabikii vileo wala biashara yeyote ile haramu kwa baadhi ya makundi
ya watu.
Unapotaja biashara zilizokuwa na faida kubwa na ya haraka
haraka, huwezi ukaziacha biashara zifuatazo;
1. Biashara
ya vifaa vya ujenzi, hardware.
Mpenzi msomaji, hakuna ubishi wowote ule kwamba, kila
binadamu anayezaliwa baada ya kuwa na akili timamu kitu cha kwanza kufikiria
akilini kama ni mvulana ni, “Nikiwa mkubwa nitajenga nyumba yangu nzuri
ya kuishi mimi, mke wangu na watoto”. Hapo pengine hata hajaanza darasa
la kwanza. Kwa upande wa watoto wa kike nao, huanza kuwaza akilini kuja kuwa na
maisha bora ya familia ndani ya mjengo mzuri. Hii ni kumaanisha kwamba kwa
asili binadamu wote ni wapenzi wa kumiliki nyumba nzuri au majengo
yanayopendeza.
Cha ajabu hapa ni kwamba kila mtu anapenda jengo alimiliki yeye mwenyewe ndiyo maana utakuta mtu hata ikiwa wazazi wake wana mali nyingi, ni matajiri lakini bado atatamani kujenga nyumba yake nzuri kwa pesa zake mwenyewe.
Maajabu mengine ni kwamba majengo yote hata yale ya
serikali, madaraja, nyumba za ibada, Makanisa na Msikiti, reli, barabara na
hata viwanja vya michezo kama soka, baada ya miaka kadhaa huhitaji matengenezo
makubwa au kubomolewa na kujengwa tena upya kisasa jambo linalosababisha vifaa
vya kujengea kuendelea kuhitajika kila mara miaka yote.
Nyumba aliyojenga babu enzi hizo kwa gharama kubwa leo
hii mjukuu utatamani kuibomoa na kujenga jumba la kisasa zaidi. Reli aliyojenga
Mjerumani leo hii Mheshimiwa Rais Magu anaweza kuamua ibomolewe na kujengwa
upya, Barabara ya Morogoro aliyojenga Hayati Mwalimu Nyerere unaweza kuona leo
hii kuna watu wanaobomolewa nyumba zao kupisha ujenzi upya wa barabara hiyo.
Kwa kifupi tu nataka kuonyesha jinsi ambavyo suala la
ujenzi na vifaa vya ujenzi lilivyokuwa nyeti na endelevu na ambalo huwezi hata
siku moja ukadai eti itapitwa na wakati. Watu watapita lakini ujenzi utakuwa
palepale miaka yoye pengine mpaka mwisho wa dunia. Toka kujengwa Mapiramidi ya
Misri na Mafarao kule Misri ya Kale, Mfereji wa Suez, Kuta kuu za China na Berlin
na sasa Jengo refu kupita yote duniani kule Dubay, ujenzi haujakoma, ndiyo
kwanza unashika kasi duniani kote.
Kwanini
nimeitia biashara ya vifaa vya ujenzi kwenye kundi la biashara ndogondogo?
Kimsingi kabisa ungetegemea makala hii kukutana na biashara
zile ndogondogo kabisa lakini bila shaka unaweza kushangaa kwanini nimeamua
kuiweka biashara ya vifaa vya ujenzi. Vifaa vya ujenzi mtu anao uwezo wa kuanza
na kiasi chochote kile cha mtaji na wakati mwingine bila ya mtaji kabisa.
Kivipi?
Kuna jamaa mmoja namfahamu yeye alianza biashara hii kama
dalali, akaweka sampuli za baadhi ya vifaa hivyo kama vile tofali, baluster,
nguzo za fence, paving blocks nk. katika ukuta wa nyumba yake iliyokuwa
kandokando ya barabara ya Morogoro maeneo fulani pale Kimara, akaweka na
mawasiliano yake ya simu pale. Wateja walipompigia simu wakihitaji vifaa vile,
aliwapa bei na kwenda kuwachukulia kutoka kwa watengenezaji wengine waliokuwa
na site zao.
Unaweza pia kuanzisha uuzajiwa vifaa vya ujenzi
vilivyokwisha tumika au “used”. Unanunua kwa bei ya chini kutoka kwa watu
wanaobomoa majumba yao na kwenda kuuza kwa beiya juu kidogo lakini isiyofika
sawa na ya vifaa vipya. Vitu hivyo used vyaweza kuwa nondo, mabati, mabomba,
misumari, mbao, tofali, nk. Vile vile unaweza kuanza na kitu kimoja tu, mfano
kuuza sementi, ukaanza hata na mfuko mmoja kwa kupima kwa kilo kisha
kidogokidogo ukaweka vitu vingine. Mchanga na kokoto unaweza pia ukanunua kiasi
kidogokidogo na kuuza kwa kupima na ndoo au viroba. Kwa Tanzania inasemekana
bado ujenzi umefikia asilimia ndogo sana mpaka sasa hivi.
Biashara
ya vileo(pombe), bia, viroba, wine, spirit, sigara na tumbaku.
Hapo ndipo naomba radhi kwa wale ambao imani au maadili
yao hayawaruhusu kutumia wala kuuza. Kwa kweli nimetaja tu pombe aina ya viroba
nikimaanisha spirit au wine iliyokuwa ikifungashwa katika paketi za nailoni
lakini kila mtu anafahamu kuwa kwa sasa paketi hizo hazipo tena baada ya
serikali kuzipiga marufuku.
Vitu hivi vinapouzwa licha ya kuwa na wateja wengi faida
yake pia ni kubwa sana ukilinganisha pengine na bidhaa za aina nyingine kama
soda au maji. Watu wengi wanaofungua biashara hizi mitaji yao hukua haraka huku
wakifungua matawi ya biashara hizo. Unaweza kupata ushahidi wa kile
ninachokizungumza kama siku chache zilizopita kabla viroba havijapigwa marufuku
ulikuwa ukitembea maeneo mbalimbali ya stendi na kujionea jinsi wenye vioski na
meza za kuuza bidhaa ndogondogo walivyokuwa wakiuza pombe hizo.
Sigara nazo, halikadhalika ni biashara ambayo japo faida
yake ni ndogondogo, lakini kutokana na wingi wa wavutaji na uvutaji wao wa mara
kwa mara katika siku moja, utakuta muuzaji wa sigara akiuza paketi nyingi na kutengeneza
faida kubwa kwa siku. Kuna wanaouza pia Tumbaku yenyewe iliyosagwa au ugoro,
tumbaku zinazoletwa kutoka Asia nk.ijapokuwa nazo nyingi zimekwishapigwa
marufuku hapa Tanzania baada ya kuonekana ni baa kubwa kwa vijana wa Kitanzania
hasa wanafunzi walioanza kuzitumia kwa wingi, jambo ambalo lingeweza
kuwasababishia maradhi mbalimbali ikiwemo kansa ya koo, mapafu na nyinginezo.
3.
Biashara zote ndogo ndogo za vitu vya kula na kunywa.
Tunapozungumzia biashara hizi, si suala tu la kuuza
biashara ndogondogo za vitu vya kula na vinywaji, bali pia ili kuweza kupata
faida ya haraka na kubwa, basi ubunifu unahitajika. Kwa kuwa biashara hizi ni
rahisi kuanzisha na kila mtu anao uwezo wa kuanzisha, wale wanaoweza kuiona
faida kubwa ya haraka ni wale tu wanaofanya ubunifu na kuwa wavumilivu.
Nimefurahishwa na jamaa fulani pale Mbezi, wao
wameanzisha biashara ya kuuza juisi ya
miwa lakini staili yao ilinivutia. Wanatumia pikipiki iliyofanyiwa ‘modification’,
ijnini yake hiyohiyo huzungusha kinu cha kukamulia miwa wakati ikiwa imesimama
stendi na wateja huja kunuua juisi.
Kiduka hicho cha aina yake kimejengewa juu ya hiyo
pikipiki, huku pakiwa na sehemu ya kuwekea vitafunwa mbalimbali, vyombo na
sehemu ya kukaa dereva na muuzaji wakati wanapofunga biashara kurudi nyumbani.
Ni kama vile kiwanda kidogo kinachotembea. Wana uwezo wa kwenda eneo au stendi
yeyote ile hasa hasa nyakati za jioni palipo na wateja wengi.
4.
Biashara zote ndogo ndogo za utoaji wa huduma.
Tofauti ya hizi na zile nilizozitaja katika makala
nyingine ya biashara zilizokuwa na faida kubwa na ya haraka mara mbili ya faida
utakayowekeza ni kwamba, hizi zipo katika kundi la biashara ndogondogo tu
wakati hizo nyingine zinajumuisha biashara zote kwa ujumla.
Biashara ndogo za utoaji wa huduma ni kama vile, ususi wa
nywele majumbani kwa wakina mama na kina dada, Uzibuaji wa mitaro ya maji
machafu, usafi wa majumbani(fumigation), biashara za kwenye mitandao(blogging)
kama hii ninayofanya, Kufundisha masomo ya ziada kwa wanafunzi wa shule za
msingi au sekondari, kufundisha semina mbalimbali kama ujasiriamali, muziki,
nk. kwa watu au makundi ya watu walio na mapenzi na kile unachofundisha.
Ndugu msomaji, kwa leo makala hii imeishia hapa, siku
zijazo nitaendelea kukuletea makala zaidi juu ya uanzishaji na uendelezaji wa
biashara ndogondogo zilizosahaulika au biashara ambazo watu wengi
wanazichukulia poa(kuzipauzito mdogo)
Kama ulikuwa hujasoma kitabu hiki tulichokupa bure kabisa
usome, basi JIUNGE NA BLOGU HII HAPA KUKIPAKUA au bonyeza picha ya jalada
unayoiona hapo chini.
Ni free hutachajiwa senti tano! Pamoja na vitabu vingine
zaidi ya 20 katika lugha ya kiingereza.
Kwa vitabu zaidi vya Biashara na Ujasiriamali katika lughaya kiswahili fungua, SMART BOOKS TANZANIA.
Asante kwa somo nafatilia vizuri makala zako
ReplyDeleteAsante sana Johnson ubarikiwe!
DeleteNaelimika vyakutosha na makala hii.
ReplyDeleteBarikiwa nawewe pia Mr. Ndaki!
DeleteGreat job.
ReplyDeleteThanks
ReplyDeleteVery good ideas
ReplyDeletenice
ReplyDeleteBe blessed
DeleteMm ninayo laki 3 naweza fanya biashara gani na mm
ReplyDelete