Usimamizi wa biashara nyingi umekuwa ni changamoto na
sababu kubwa inayochangia kuanguka kwa asilimia kubwa ya biashara hizo hata
kabla ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake. Kusimamia vizuri biashara kunajumuisha
mambo mengi yakiwemo, udhibiti wa mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa au huduma
kwenye biashara, udhibiti wa mali na
rasilimali za biashara ukiwemo muda pamoja na udhibiti wa manunuzi na bajeti.
Waanzilishi wengi wa biashara hujikuta katika mtihani mgumu
hasa pale wanapofikiri kwamba wakishakuwa mabosi basi kila kitu wanawaachia
wasaidizi au wafanyakazi kwenye biashara zao kuanzia meneja mpaka mtunza stoo,
kumbe siyo hivyo inabidi uhakikishe unafanya usimamizi wa karibu kabisa na hata
ikiwezekana wewe jukumu la umeneja ujivike mwenyewe kusudi biashara yako iweze
kuvuka kirahisi katika ngazi hii ngumu ya kuanza kwa biashara.
Unapofanya kosa la kuajiri wafanyakazi na kuwaachia kila
kitu wasimamie wao wenyewe, maana yake umewaambia wajitafutie na wao mitaji yao
kusudi wakafungue biashara zao. Kumbuka hakuna mtu anayependa kuajiriwa, kila
mtu angependa kuanzisha na kusimamia biashara yake mwenyewe kikamilifu hata
ikiwa ndogo ili aweze kupata faida kubwa na nono zaidi, sasa anapokuja kwako
kuomba ajira ujue siyo mjinga, kama angekuwa na mtaji pengine hata wewe
ungeweza kuwa mfanyakazi wake. Ndiyo maana kukawekwa mifumo mbalimbali ya
usimamizi wa biashara au miradi kuzuia wanaofanya kazi katika miradi au
biashara hizo wasije wakazihujumu kwa namna yeyoe ile.
Kwa bahati mbaya katika biashara ndogo ndogo, udhibiti ni
suala tete kidogo kutokana na udogo wa mtaji. Mfanyakazi akidokoa pesa kidogo
tu, athari yake ni kubwa ajabu!. Kwa mfano unaweza kuajiri kijana wa kukaa dukani
kwako au biashara nyingine yeyote ile, yaweza hata ikawa ni saluni au mgahawa,
au hata mradi wa kuku wa mayai, usipojitahidi kufanya stoku mara kwa mara au
kuhesabu mali za dukani kwako, kijana huyo anaweza akawa kila siku anajiwekea
kiasi fulani cha fedha na pindi lengo lake litakapotimia, humuoni tena.
Atasingizia vitu kibao, mara “oo.. mimi naumwa…nataka
kupumzika…nimefiwa kijijini” nk. Ilimradi tu aache kazi na siku mbili tatu
unamkuta keshafungua biashara yake. Sasa kwa kuwa huna ushahidi wala kumbukumbu
nzuri za mahesabu ya duka lako(biashara yako), basi na wewe unaishia kumuacha
tu aende zake hivi hivi. Lakini kama siku ya kwanza unamuajiri mlipigiana
mahesabu, mkaorodhesha kila kitu kwenye daftari, ukamwambia “nakukabidhi
kiasi hiki cha mtaji” na kila siku manunuzi ya vitu ukarekodi mahali
ili kuja kubaini faida itakayopatikana dukani kila siku mpaka siku ya mwisho
mtakapokuja kufanya stock nyingine, basi kijana huyo itamuwia vigumu kwelikweli
kudokoa.
Na isitoshe mnasaini mahali kwa masharti kwamba akiingiza
hasara(shoti), basi atawajibika kulipa kwa fedha zake za mshahara. Hapo sasa
wewe usiwe mzembe hakikisha mnafanya mahesabu kikamilifu na kwa wakati, siyo
mara umefanya leo kesho umeacha. Ujue wafanyakazi ni wajanja sana, huwa wanawasoma
matajiri zao kujua udhaifu wao upo wapi. Wengi wakishajua huwa hawafanyi ajizi.
Kwahiyo biashara ni USIMAMIZI
asikudanganye mtu bwana, ndiyo maana katika kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA.DUKA LA REJAREJA, mwandishi kwa kutumia uzoefu wake mkubwa katika biashara hiyo
kwa muda wa miaka 12, ameweza kuainisha mifumo mbalimbali inayomuwezesha
mmiliki wa duka hasa la rejareja au biashara nyingine yeyote ile ya rejareja
kusimamia na kudhibiti hesabu za biashara yake kikamilifu, jambo
linalomuwezesha kusimamia hata maduka zaidi ya sita kwa wakati mmoja bila ya
kupoteza mapato yake ovyo.
Si hivyo tu katika kitabu hicho pia mbinu mbalimbali za
uendeshaji wa biashara ya rejareja zimeelezwa kwa kina ikiwa ni pamoja na
mchanganuo mzima wa biashara hiyo wenye kila kitu, makosa mbali mbali
yanayoweza kukufanya uhisi umelogwa, jinsi ya kuzuia chuma ulete dukani au
kwenye biashara yako, siri nzito wenye maduka makubwa hawatakueleza hata uwape
pesa nk.
Mbinu hizo zimezingatia makundi mbalimbali ya jamii na
makundi ya wakongwe wa biashara hizi za rejareja kuanzia Wahindi, Wachagga,
Wapemba, Wakinga na hata jamii moja ya kabila linalopatikana huko China balaa
kwa biashara hizi, hujifanya wajingawajinga kumbe ni moto wa kuotea mbali, anapokuuzia
kitu utanunua tu hata akuambie bei kubwa vipi, wana tekiniki balaa!.
Kwa hiyo ndugu msomaji wa makala hii, nakusihi kama wewe
ni mmiliki wa biashara ndogo, una lengo la kuanzisha biashara ndogondogo au
hata una mpango wa kumuajiri mtu kazi ya kukaa kwenye biashara yako ndogo, hakikisha suala la usimamizi unalipa
kipaumbele cha kwanza, lifanye kuwa ndiyo sirikuu ya mafanikio ya biashara
yako.
Ni bora hata mfanyakazi mwenye tabia ya kukimbiza wateja
kwa kauli zake mbovu, unaweza ukamrekebiasha, lakini ndugu yangu, huyu aliye na
tabia ya kuhamisha mtaji wako utarekebisha tatizo hilo saa ngapi wakati
ukijakuchukua hatua yeye keshafungua biashara yake? So be carefull, usije vuna
mabua bure.
………………………………………………………………………………..
Vitabu 3 vya Self Help Books Tanzania kikiwemo kile
cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA
REJAREJA, unaweza ukavipata kwa urahisi na ukiwa mahali popote pale nje na
ndani ya Tanzania kupitia E-mail yako kama PDF
file au softcopy.
Cha kufanya tu ni kutuma pesa ya kitabu husika kwenye
namba za simu 0712202244 au
0765553030 jina Peter Augustino Tarimo, pamoja na anuani yako ya
E-mail kwa njia ya meseji, kisha na sisi tunakutumia kitabu/vitabu muda huohuo.
Hatujawahi kamwe kumsumbua au kumcheleweshea mteja
anayetuma fedha yake kununua kitabu.
Vitabu vya karatasi(Hardcopy) pia vinapatikana na kwa Dar es salaam tunakuletea mpaka pale
ulipo au unafika Mbezi stendi kwa Msuguru tunakopatikana. Piga pia, 0712202244
au 0765553030 au sms
kufahamu zaidi.
SOFTCOPY SH. 5,000/=
HARDCOPY SH. 10,000/=
SOFTCOPY SH. 10,000/=
HARDCOPY SH. 20,000/=
SOFTCOPY SH. 3,000/=
HARDCOPY SH. 5,000/=
0 Response to "KUSIMAMIA BIASHARA YAKO NDOGO UNAONA NI KAZI NGUMU? BORA UIACHE, UTAVUNA MABUA"
Post a Comment