Katika masuala yote yanayohusiana na kazi, biashara
na ajira, wanawake ndiyo wanaopata madhara makubwa zaidi yanayotokana na
ukosefu wa vitu hivyo hasa katika uchumi wa siku hizi usioweza kutabirika kwa
urahisi tofauti na zamani ambapo mtu aliweza kuishi maisha mazuri tu akiwa na
ajira yake ya kawaida au biashara yake moja.
Siku hizi haiwezekani tena hata baada ya mtu
kustaafu kazi aishi kwa kutegemea mafao yake ya uzeeni, ni lazima kila mtu
wakiwemo wanawake kutafuta njia mbadala za kutokuwa tegemezi katika chanzo
kimoja tu cha mapato iwe ni kazi, biashara, mafao ya uzeeni au fedha anazopewa
na mumewe. Wanawake wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanawapunguzia waume zao
mzigo katika kulea familia kwa kuhakikisha wanakuwa na vyanzo mbalimbali vya
mapato.
Katika kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI
MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA, kitabu hicho kimezungumzia kwa undani sana mifereji
saba au vyanzo mbadala 7 vya pesa ambavyo mtu yeyote yule awe mwanamke au
mwanaume anaweza akaitumia mifereji hiyo na kujihakikishia uhuru kamili wa
kifedha katika maisha yake yote.
Wanawake kwa asili ni watu wanaopenda kuwa na
vyanzo vingi vya mapao na hii inatokana na mahitaji yao makubwa hasa
ukizingatia kwamba wao ndio watunzaji
wakuu wa familia. Tatizo kubwa linalosababisha mapato yao hayo yasiweze
kuonekana kama ya wenzao wanaume ni wingi wa matumizi. Mwanamke haiwezekani
mtoto akose penseli wakati ana pesa kidogo kwenye pochi yake, ataitoa hata
ikiwa pesa hiyo ni mtaji kwa ajili ya biashara yake.
Faida
za mwanamke kuwa na vyanzo vingi vya pesa(mifereji mingi ya mapato)
· Humwezesha mwanamke kuwa na uhuru mkubwa
zaidi na urahisi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku
anapojua kwamba hategemei kwa asilimia 100% kazi yake ya msingi au biashara.
· Humwezesha mwanamke kukaa nyumbani na
familia yake-kuwa huru kifedha maana yake ni kwamba
halazimiki tena kuiacha familia yake kutwa akiwa kazini, anao uwezo wa kufanya
shughuli zake akiwa nyumbani na kila kitu kikaenda sawa sawa.
· Ikiwa atafukuzwa au kuacha kazi; kitakachomtokea
baada ya kuachana na ajira ni mapato yake kupungua tu na wala siyo kukatika
kabisa kama vile angekuwa na chanzo kimoja tu cha mapato. Vyanzo vingine
vitakuwa vikimuingizia fedha kama kawaida.
· Uharaka katika kutimiza malengo yake. Mwanamke
hatasubiri tena kwa muda mrefu ndipo aweze kupata fedha kwa ajili ya kutimiza
malengo yake. Badala ya kuambiwa na mumewe, “subiri mwisho wa mwezi” anakuwa na
urahisi wa kuamua muda wowote ule.
Jinsi
mwanamke anavyoweza kujiwekea vyanzo vingi vya mapato.
Kuwa na mifereji mingi ya mapato maana yake
ni kuanzisha miradi mbalimbali tofauti na ule mradi wako mkuu au kazi yako ya
msingi. Ingawa jambo hili siyo rahisi sana kulitekeleza kama vile unavyoweza
kutamka lakini kupitia mbinu na mikakati mbalimbalia kama ilivyoainishwa katika
kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA, jambo hili linawezekana bila matatizo.
Hutakiwi kuanza mara moja kujijengea vyanzo
vingi vya mapato, kinachotakiwa ni kuanza na kimoja baada ya kingine taratibu.
Vile vile siyo kila mradi tu unafaa kuanzisha kama chanzo mbadala cha mapato,
kuna miradi rahisi zaidi na inayofaa zaidi ya mingine. Baadhi tu ya vyanzo vya
mapato au miradi mwanamke anayoweza akaanzisha kama mbadala ni hivi hapa;
1) Biashara
ndogondogo, zipo za aina nyingi kama zilivyoelezwa ndani ya kitabu chako cha
MIFEREJI 7 YA PESA.
2) Uwekezaji
katika majengo na ardhi
3) Biashara
katika mtandao wa intaneti
4) Kutumia
kipaji ulichokuwa nacho katika kutatua matatizo ya watu wengine.
5) Biashara
za mtandao(Network marketing)
6) Kutumia
muda wako wa ziada baada ya kazi
7) Kuweka
akaunti ya benki inayokupa riba kila mwezi
8) Kukodisha
vitu vyako kama vile gar ink.
9) Uandishi
wa kujitegemea
10)
Kuwa na hisa katika makampuni au biashara
zingine.nk.
Orodha ya vyanzo mbadala vya mapato haina mwisho, unaweza
ukawa na mlolongo mkubwa sana, ni wewe mwenyewe unayeweza kuamua utumie chanzo
kipi kulingana na mazingira na uwezo uliokuwa nao. Kama nilivyotangulia kusema,
vyanzo vingi vya mapato siyo rahisi sana kuanzisha kama unavyoweza kufikiria
lakini ni jambo linalowezekana ikiwa utakuwa tayari kufanya hivyo. Wanawake
wengi wameweza na wewe pia unaweza kufanya hivyo.
.................................................................................................
Kwa elimu zaidi ya kina kuhusiana na biashara na ujasiriamali, unaweza ukajipatia vitabu vifuatavyo kutoka Self Help Books Tanzania kupitia njia za Email au vitabu vya karatasi (hardcopy).
SIMU: 0712202244 au 0765553030
Peter Augustino Tarimo.
au tembelea SMART BOOKS TANZANAIA kwa vitabu zaidi
0 Response to "KWANINI KILA MWANAMKE ANASTAHILI KUMILIKI VYANZO VINGI VYA MAPATO?"
Post a Comment