Makala hii ya sauti ni kutoka Idhaa ya kiswahili ya Redio DW, kipindi cha Vijana tugutuke kilichorushwa hewani jioni ya tarehe 21 0ctoba 2017 na mtangazaji Silvanus Karemera. Kipindi kilihusiana na matatizo ya vijana katika masuala mazima ya miradi mbalimbali ya kibiashara ambapo vijana wamekuwa wakilalamika kwamba ukosefu wa mitaji, ukosefu wa usaidizi wa karibu au kushikwa mkono na wale waliokwishafanikiwa ni moja kati ya changamoto zinazowakwamisha licha ya serikali mbalimbali hususani za hapa Afrika Mashariki kudai kwamba zinaweka vipaumbele kwa vijana ambao ndio rasilimali kubwa na nguvukazi kwa nchi hizo.
Kijana wa leo katika biashara na ujasirriamali.
|
Mahojiano hayo yalihusisha vijana watatu, Paul, Johnson
na Tausi ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu nchini Rwanda. Mazingira kote Afrika
Mashariki yanafanana hivyo matatizo ya vijana sehemu moja ni yaleyale kote
Afrika Mashariki Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi. Endelea kusikiliza hapo
chini kujua vijana wanakabiliana vipi na changamoto hizo…………
0 Response to "CHANGAMOTO ZA MITAJI KWA VIJANA KUANZISHA BIASHARA, MTAJI KIDOGO NA SULUHISHO LAKE(MP3)"
Post a Comment